Lambardi
Platinum Member
- Feb 7, 2008
- 20,226
- 24,577
Unguja na Pemba.....!!!kabla ya Tanganyika Zanzibar ipo
Unguja na Pemba.....!!!kabla ya Tanganyika Zanzibar ipo
Basi tui assimilate Zanzibar iwe mikoa ya Tanzania....Kama tulichanganya udongo na majina ni kwanini tusichanganye raia na mifumo yake?
Sema hii issue ya muungano ipo esoterically mno, hata mashuleni kinachofundishwa ni tarehe ya kuundwa huo muungano...no more than that.
Tushaingiliana Sana.Ili iweje?Tukivunja Muungano kuna hasara gani?
Ni kweli kabisa, movement ya watu imesaidia kuimarisha muungano, lakini kuna hatari ya vyama viwili tofauti kushika dola Zanzibar na kwenye serikali ya Muungano, jaribu kupata picha mwaka 84 kama Jumbe asingekua mwanachama wa CCM.muungano hauwezi kuvunjika kwasababu, wazanzibari wengi eidha wanaishi, wameishi bara, ama wana ndugu zao bara, ama wamewekeza bara, ama wamesoma bara. kwa hilo tu muungano unanguvu kijamii.
ila pia wazanzibari wanahofu ya kumezwa na kufutwa na huu muungano hasa ukizingatia idadi yao ambayo jiji moja tu la dar ni kubwa kuliko wao wote,
hivyo wazanzibari wanahofu yenye mashiko ya kuogopa kufutwa, hivyo lazima wasimamie maslahi yao kama wazanzibari
na hilo ni lazima lifanyike, na ndio mbinu ya kudumu ya kuuweka muungano
muungano hautadumu kama wazazibari watajiona wamefutwa nafasi yao duniani kama watu
lazima wawe na mamlaka yao na kujisimamia hasa kwa mambo yanayowagusa wao moja kwa moja
hivyo mtoa mada ondoa hofu. muungano hauwezi kuvunjika maana tayari una mizizi iliyozama. ila la muhimu pia ni hayo mamlaka ya kizanzibari lazima yawepo.
maamuzi ya wengi ni lzm yaheshimiwe.wanachi ndo wenye maamuzi ni aina gani ya muungano wautakao.Kwanini atake dhuluma ilihali anao uhakika wa kushinda?
Muungano ni lazima kwa msitakabari wa uchumi wa Tanganyika.Tatizo ni Tanganyika hapo sasa harasa zote kwanini bado mtaitaka zanzibar na wao hawakutakeni?????????/
hapa umewasingizia wakoloni hawakuhusiki,muungano ulikuwa ni kwa faida ya mwalimu na karume ambao waliangalia suala la ulinzi kw awakati ule ili kudhibiti tishio la sultani wa oman kuweza kurudi kuitawala zanzibar,ambavyo hizi hoja ni mfu kwa karne hii ya kisasa.Muungano ni jinamizi linaloitafuna tanganyika na zanzibar, muungano huu wa shinikizo la wakoloni wa kutekeleza mpango wa udhibiti wa nchi za afrika. Mpaka leo hii hakuna anaejua umuhimu wa muungano na sababu za muungano,sababu zinazotolewa na viongozi ambao wote wanakaririshwa sababu hizo juu ya umuhimu wa muungano ni ulinzi na usalama,sababu ambazo ni za uongo wala hazina mashiko yeyote,umbali wa Kenya na tanganyika ni kama mita moja tu na hakuna tishio la aina yeyote wala hakukuhitajika muungano wa hofu kama ulivyo wa Zanzibar na tanganyika
-Mambo yalitakiwa kudhibitiwa barani afrika ni historia
Nchi ambazo zilikuwa na utawala wenye historia ndefu zote zimepinduliwa na historia zao kuuliwa kabisa Kama ethiopia, Zanzibar na nchi nyengine za afrika
wakoloni walitaka historia ya nchi zote za afrika ianze kwenye kupata uhuru na sherehe za uhuru ziwe jiwe la msingi kwa nchi za afrika,kwa hio ikitokea kama kuna nchi ambao ina historia,utawala na serikali inayopita tarehe za uhuru lazima waiangamize,na Zanzibar ni moja ya hizo nchi ambazo historia yake ya utawala ni mrefu ulianzia na waraabu mpaka masultani wakawa Wazanzibari ambao ni machotara walochanganya kama wazanzibari wa sasa
Ethiopia pia ilipitiwa na kimbunga hiki cha wakoloni wanaodhibiti historia za afrika,utawala wa Ethiopia ulikuwa na zaidi ya miaka 3000 ya ufalme, wakoloni walihakikisha unakufa na historia yake pia,na kuanzisha utawala wa dunia mpya
kwahio muungano wetu hapa ni jinamizi ambalo mpaka viongozi wetu wanachezeshwa ngoma wasioujua mdundo wake,wanageuzwa kuwa maagent wa kuliteketeza bara la afrika,
kwa maana kama watoto wetu hawana kiio cha historia watakuwa hawana morality ya kujielewa na kufanya chochote cha maana
Hata Tanganyika tunapata hasara na huu Muungano..
Wabunge wa Zanzibar hawako active na mambo mengi ya huku bars
Wabunge wao zaidi ya 40 wanawakilisha watu
Sawa na mbunge wa Mbagala..
Hii inafanya wananchi wengi kukosa sauti
Uwakilishi bungeni hauendani na idadi ya watu majimboni only kisiasa tu..
Tunalazimika kuwa na makamu kutoka Zanzibar
Na kufanya zoezi la transition kwetu kuwa
Unpredictable ....imagine makamu angetoka bara..
Waziri mkuu hatambuliki Zanzibar wakati hata wizara za Muungano yeye ndo msimamizi
Tuvunje Muungano Kwa faida zetu wote
Hapo kwenye muungano kukosa sababu za msingi (at least tunazozijua) naungana na wewe kabisa. Nimepekua sana, sababu kubwa ninayokutana nayo ni 'undugu wetu'.Muungano ni jinamizi linaloitafuna tanganyika na zanzibar, muungano huu wa shinikizo la wakoloni wa kutekeleza mpango wa udhibiti wa nchi za afrika. Mpaka leo hii hakuna anaejua umuhimu wa muungano na sababu za muungano,sababu zinazotolewa na viongozi ambao wote wanakaririshwa sababu hizo juu ya umuhimu wa muungano ni ulinzi na usalama,sababu ambazo ni za uongo wala hazina mashiko yeyote,umbali wa Kenya na tanganyika ni kama mita moja tu na hakuna tishio la aina yeyote wala hakukuhitajika muungano wa hofu kama ulivyo wa Zanzibar na tanganyika
-Mambo yalitakiwa kudhibitiwa barani afrika ni historia
Nchi ambazo zilikuwa na utawala wenye historia ndefu zote zimepinduliwa na historia zao kuuliwa kabisa Kama ethiopia, Zanzibar na nchi nyengine za afrika
wakoloni walitaka historia ya nchi zote za afrika ianze kwenye kupata uhuru na sherehe za uhuru ziwe jiwe la msingi kwa nchi za afrika,kwa hio ikitokea kama kuna nchi ambao ina historia,utawala na serikali inayopita tarehe za uhuru lazima waiangamize,na Zanzibar ni moja ya hizo nchi ambazo historia yake ya utawala ni mrefu ulianzia na waraabu mpaka masultani wakawa Wazanzibari ambao ni machotara walochanganya kama wazanzibari wa sasa
Ethiopia pia ilipitiwa na kimbunga hiki cha wakoloni wanaodhibiti historia za afrika,utawala wa Ethiopia ulikuwa na zaidi ya miaka 3000 ya ufalme, wakoloni walihakikisha unakufa na historia yake pia,na kuanzisha utawala wa dunia mpya
kwahio muungano wetu hapa ni jinamizi ambalo mpaka viongozi wetu wanachezeshwa ngoma wasioujua mdundo wake,wanageuzwa kuwa maagent wa kuliteketeza bara la afrika,
kwa maana kama watoto wetu hawana kiio cha historia watakuwa hawana morality ya kujielewa na kufanya chochote cha maana
Watalii wanapoenda mahali wanafuata vivutio vya utalii sio majina ya nchi. Pia Zanzibar kama sikosei ina bodi yake ya utalii na pia utalii sio jambo la muungano.Muungano unaificha Zanzibar kwenye sura ya kimataifa. Ukienda sehemu nyingi duniani jina Zanzibar ni maarufu kuliko Tanzania.
Mkuu umenikosha kwa bandiko lako lililoenda Shule, hii ndo ilikuwa JF ya zamani,Tangu kuasisiwa kwake mwaka 1964, mauungano wa Tanganyika na Zanzibar umeonekana wazi kugubikwa na ujanja ujanja mwingi.
Ni jambo lililo wazi kabisa kuwa waasisi wa muungano walikua na malengo yasiyofanana, mwalimu Nyerere alidhamiria kuwepo na muungano kamili chini ya serikali moja huku mzee Karume yeye alitaka kuutumia muungano kuhodhi mamlaka kule Zanzibar baada ya mapinduzi kisha auvue kama koti linalobana mambo yakikaa sawa.
Inaonekana mwalimu alimzidi kete Karume kwasababu tokea mwaka 1964 hadi 1984 kulikowepo na juhudi za wazi za kimkakati za kudhoofisha mamlaka ya Zanzibar huku akizidi kuiunganisha nchi.
Baada tu ya muungano, nchi yetu mpya iliitwa 'The united republic of Tanganyika and Zanzibar'. Na kwenye hati za muungano kulikua na mambo 11 (sio 9 kama baadhi ya watu wanavyo dai) yakiyo ainishwa kuwa ni mambo ya muungano ambayo ni;
Baada ya muungano, mwalimu alianza kutekeleza 'master plan' yake, pamoja na kubadili jina la nchi kuwa 'The united republic of Tanzania' aliendelea kuongeza mambo mengine kwenye orodha ya mambo ya muungano (kwa makubaliano ya pande zote mbili of course) kadri fursa zilipo jitokeza.
- Katiba na serikali ya Jamuhuri ya Muungano
- Mambo ya nchi za nje
- Ulinzi
- Polisi
- Mamlaka juu ya mambo ya hali ya hatari
- Uraia
- Uhamiaji
- Mikopo na biashara ya nchi za nje
- Utumishi katika serikali ya jamuhuri ya muungano
- Kodi (income, cooperate, customs and exercise)
- Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa anga, posta na simu
Kuvunjika kwa taasisi za EAC kama bank na mahakama ya rufani pamoja na kuvunjika kwa jumuiya yenyewe kulitoa nafasi adimu sana ya kuongeza mambo yaliyokuwa EAC kuwa ya muungano. Kwa mujibu wa katiba ya JMT ya sasa, orodha ya mambo ya muungano ina mambo yafuatayo ya ziada;
Kwa hakika tunaweza kusema hili la vyama vya siasa likitanguliwa na kuungana kwa ASP na TANU kuunda CCM lilikua kama msumari wa mwisho kwenye jeneza la Zanzibar huru.
- Sarafu, fedha, mabenki na fedha za kigeni
- Leseni za viwanda na takwimu
- Elimu ya juu
- Makiasili ya mafuta na gesi asilia
- Baraza la taifa la mitihani
- Usafiri na usafirishaji wa anga
- Utafiti
- hali ya hewa
- Takwimu
- Mahakama ya rufani ya JMT
- Uandikishaji wa vyama vya siasa
Ukizingatia kwamba tulikuwa kwenye mfumo wa chama kimoja, basi kwa mara ya kwanza ilipatikana 'mechanism' madhubuti ya kumdhibiti rais wa Zanzibar na serikali yake kupitia vikao vya chama.
Umuhimu wa kete hii ulionekana kipindi cha mchafuko wa hali ya hewa Zanzibar mwaka 1983/1984 ambapo rais wa Zanzibar wa wakati huo ndugu Aboud Jumbe 'alifukuzwa kazi' na CCM. Yaani rais wa Zanzibar anaweza akaitwa Dodoma kwenye vikao vya kawaida kisha akavuliwa uanachama wake na kupotesa sifa ya kuwa rais, akarudi nyumbani akiwa mwananchi wa kawaida tu.
Baada ya mwalimu kung'atuka, na baadaye kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, tumejikuta tunakumbana na changamoto ambazo hatukuwahi kuzitegemea hapo awali.
Kwa mfano, nini kitatokea iwapo vyama viwili tofauti vitashinda uchaguzi wa Zanzibar na ule wa Jamhuri ya Muungano? Tutaweza vipi kumfunga speed governor rais wa Zanzibar na serikali yake kupitia mgongo wa chama ikiwa rais wa JMT anatoka chama tofauti?
Nikiri kuwa nimeona jitihada kupitia ACT kwa kumuweka Maalim Seif katikati ya wadau wa dola lakini mkakati wa namna hii unaweza kufanya kazi as long as CCM imeshikilia madaraka ya JMT. Pia hili sio suluhisho la kudumu.
Lakini kikubwa zaidi, ni wazi kuwa ule mkakati wa mwalimu uliishia 1985 alipo ng'atuka, kuanzia hapo hadi leo Zanzibar wamekua wajanja zaidi, na inaonekana kama sasa ni wao wenye mkakati wa kulivua koti la muungano.
Mifano michache ya jinsi Zanzibar ilivyo anza kujiimarisha ni kama;
1. Kuimarisha taasisi zake, ni trend inayoendele sasa huko viziwani. Japo tunaweza kusema hili linafanyika ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa SMZ, lakini ndivyo inavyopunguza utegemezi wa SMZ kwa SJMT.
2. Wimbo wa taifa na bendera ya tifa la Zanzibar, mwaka 2005 Zanzibar ilipitisha sheria iliyorejesha bendera yake na wimbo wake wa taifa. Kwa maana hiyo wazanzibari wanafundishwa utii, heshima na uzalendo kwa Zanzibar.
3. Maboresho ya vikosi maalum huko Zanzibar mf. KMKM na JKU. Japokuwa baadhi ya vikosi hivi vina historia ndefu kutokea idara ya usalama Zanzibar hadi jeshi la wanamaji Zanzibar, lakini uwepo wake kwa sasa na jinsi vinavyozidi kuboreshwa ni wazi kuwa wanajiandaa siku wakiwa huru wawe na majeshi yaliyo kamilika. Ukisoma majukumu ya KMKM yako wazi kabisa kuwa ni kulinda mipaka ya Zanzibar.
4. Maboresho ya katiba ya Zanzibar. Pengine hili ndio kubwa kuliko yote, Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ilikua inasema 'Zanzibar ni sehemu ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania', lakini baada ya marekebisho makubwa kwa sasa inafungua kwa kusema 'Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar'.
Tena katiba hii inamtambua Rais wa Zanzibar kama amiri jeshi mkuu wa vikosi maalum vya Zanzibar na kumpa mamlaka ya kuanzisha vikosi vipya kulingana na mahitaji.
Sasa basi, kwa maslahi mapana ya uhai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani tutalazimika kuyajadili haya siku moja kwa ukweli na uwazi hata kama ni mambo yenye ukakasi.
Kinyume na hapo basi wanamikakati inabidi mkazitafute plan za mwalimu kisha mumshauri mwenyekiti aendelee pale alipokua ameishia mwalimu. Walau kufikia 2064 tuwe na serikali moja.
Kinyume na hapo tutajikuta tunakwama njia panda hususani kwenye hili la vyama vingi, hauwezi kuiba uchaguzi kila siku, kuna siku watu watachoka itakua patashika na unaweza kuwa mwisho wa muungano.
Ikitokea vyama viwili tofauti vikashinda Bara na Visiwani, je Tanzania itabadili jina?Hizi mada hua kuna watu hawazitaki.
Fuatilia kwa undani kwa waasisi wa ASP kule Zanzibar ujuwe yaliyo moyoni mwao.
Tafakari haya.
1. Nini sababu za kifo cha hayati Karume mwaka 1972 mwaka wa 9 kuelekkea muda wa Mwisho uliokusudiwa Muungano uvunjike baada ya miaka 10? fuatilia upate simulizi za kusisimua. Siri ya kifo cha Karume anaijua Mwenyezi Mungu lakini........... Lakini siasa za Muungano zinatajwa.
2. Fitina ya Zanzibar na ubaguzi unaoendelea imesukwa vyema kwa malengo yaliyojificha ya kuimeza Zanzibar. CCM imebeba bango hilo kutoka serikali mbili kuelekea moja.
3. Wazanzibari asili na wana Mapinduzi asili wanacheza karata ya URAIS ya kutaka kupewa MTU wao ili walau wajifariji lakini imekuwa pata potea maana sasa CCM ina utamaduni wa kumpitisha mtu wao kutoka Dodoma. ( CCM asili wanaugulia machungu ya kujitakia) walisahau ajenda ya bara ni kuimeza Zanzibar sasa wamenasa.
4. Ndio huwa tunawashangaa wasiojua Historia ya Zanzibar kumsifu Marehemu Mzee Jumbe. Huyu ndie aliyefanikisha Kuivunja ASP na Kuiunganisha na TANU kuwa CCM. Lakini fitina ilianza miaka ya nyuma ya kuunganishwa Shirazi Association na African Association kupatikana ASP. Mawindo ya Tanganyika kuuwa uzalendo wa Zanzibar yalianzia mbali. Historia ni ndefu lakini Mzee Jumbe alikosana na Mwalimu Nyerere ndio akafukuzwa lakini alikuwa mwana mikakati wa kuidhoofisha Zanzibar.
5. Kuunganishwa kwa ASP na TANU na kupatikana CCM, fuatilia siku hiyo Wazanzibari wazalendo waliokuwemo kwenye ASP namna walivyolia kuuliwa kilichoitwa " AFRO MAMA" ukipata simulizi machozi yatakutoka.
Kwa ufupi Zanzibar tokea wakati wa Mzee Karume hawajawahi kufurahia Muungano huu na wala usibabaishwe na utofauti wa vyama.
Kuna jambo moja hulijui. CCM sasa kwa upande wa Zanzibar iko kwenye mkakati wa kuongozwa na watu waliopandikizwa kutoka Bara na wala sio hao akina Pandu na Jecha tena. Mkakati ni kuondowa vikwazo zaidi ili njia ya kuihodhi SMZ na kisha kuipoteza Zanzibar iendelee.
Hata Tanganyika tunapata hasara na huu Muungano..
Wabunge wa Zanzibar hawako active na mambo mengi ya huku bars
Wabunge wao zaidi ya 40 wanawakilisha watu
Sawa na mbunge wa Mbagala..
Hii inafanya wananchi wengi kukosa sauti
Uwakilishi bungeni hauendani na idadi ya watu majimboni only kisiasa tu..
Tunalazimika kuwa na makamu kutoka Zanzibar
Na kufanya zoezi la transition kwetu kuwa
Unpredictable ....imagine makamu angetoka bara..
Waziri mkuu hatambuliki Zanzibar wakati hata wizara za Muungano yeye ndo msimamizi
Tuvunje Muungano Kwa faida zetu wote
Naam shukrani mkuu kwa nondo hizi.Hizi mada hua kuna watu hawazitaki.
Fuatilia kwa undani kwa waasisi wa ASP kule Zanzibar ujuwe yaliyo moyoni mwao.
Tafakari haya.
1. Nini sababu za kifo cha hayati Karume mwaka 1972 mwaka wa 9 kuelekkea muda wa Mwisho uliokusudiwa Muungano uvunjike baada ya miaka 10? fuatilia upate simulizi za kusisimua. Siri ya kifo cha Karume anaijua Mwenyezi Mungu lakini........... Lakini siasa za Muungano zinatajwa.
2. Fitina ya Zanzibar na ubaguzi unaoendelea imesukwa vyema kwa malengo yaliyojificha ya kuimeza Zanzibar. CCM imebeba bango hilo kutoka serikali mbili kuelekea moja.
3. Wazanzibari asili na wana Mapinduzi asili wanacheza karata ya URAIS ya kutaka kupewa MTU wao ili walau wajifariji lakini imekuwa pata potea maana sasa CCM ina utamaduni wa kumpitisha mtu wao kutoka Dodoma. ( CCM asili wanaugulia machungu ya kujitakia) walisahau ajenda ya bara ni kuimeza Zanzibar sasa wamenasa.
4. Ndio huwa tunawashangaa wasiojua Historia ya Zanzibar kumsifu Marehemu Mzee Jumbe. Huyu ndie aliyefanikisha Kuivunja ASP na Kuiunganisha na TANU kuwa CCM. Lakini fitina ilianza miaka ya nyuma ya kuunganishwa Shirazi Association na African Association kupatikana ASP. Mawindo ya Tanganyika kuuwa uzalendo wa Zanzibar yalianzia mbali. Historia ni ndefu lakini Mzee Jumbe alikosana na Mwalimu Nyerere ndio akafukuzwa lakini alikuwa mwana mikakati wa kuidhoofisha Zanzibar.
5. Kuunganishwa kwa ASP na TANU na kupatikana CCM, fuatilia siku hiyo Wazanzibari wazalendo waliokuwemo kwenye ASP namna walivyolia kuuliwa kilichoitwa " AFRO MAMA" ukipata simulizi machozi yatakutoka.
Kwa ufupi Zanzibar tokea wakati wa Mzee Karume hawajawahi kufurahia Muungano huu na wala usibabaishwe na utofauti wa vyama.
Kuna jambo moja hulijui. CCM sasa kwa upande wa Zanzibar iko kwenye mkakati wa kuongozwa na watu waliopandikizwa kutoka Bara na wala sio hao akina Pandu na Jecha tena. Mkakati ni kuondowa vikwazo zaidi ili njia ya kuihodhi SMZ na kisha kuipoteza Zanzibar iendelee.
Yaa! Ni kweli, nyerere alipoteza fursa adhimu, aliogopa kuonekana mkoloni mpya kwa zanzibar, kwani wakati ule kulikuwa na vuguvugu la ukombozi afrika, na yeye alikuwa msitari wa mbele,Umesoma historia potofu ktk hili suala la muungano, ukweli ni kwamba Karume ndo alipenda kuwe na serikali/nchi moja ila Nyerere ndo akakomalia serikali mbili tukiri tu hapa nyerere alipotoka alishindwa kuona ya mbele!
Naam, ni hatari ambayo kila mtu anaiona lakini wanasita kuitaftia ufumbuzi wa kudumu. wakisha iba uchaguzi wanasahau kabisa, baada ya miaka mitano ndio matumbo yanapata joto tena.Mkuu umenikosha kwa bandiko lako lililoenda Shule, hii ndo ilikuwa JF ya zamani,
Wenye maono tulitaka Katiba mpya ili kuridhiana ili tuwe na mfumo thabiti wa Muungano. Wakatokea wabinafsi wachache wasioona mbali wakavirunga mchakato wa Katiba mpya.
Ukweli Ni kuwa kwa Sasa hatuna Katiba ya kuulinda Muungano ndani ya mfumo huu wa vyama vingi, kilichopo Ni Bora liende tu.
Mkakati ni Kwa kuibara kura kufuta matokeo, na ubabe wa kutangaza mshindi mtu wao
Ipo siku yaja haiko mbali, watafeli na Muungano itakuwa Basi tena itabaki majuto Ni mjukuu
kivipi.Muungano ni lazima kwa msitakabari wa uchumi wa Tanganyika.