Je, Zanzibar inajiandaa kujitwalia uhuru kamili?

Je, Zanzibar inajiandaa kujitwalia uhuru kamili?

Zanzibar ikiwa huru itapaa kiuchumi,kutakuwepo na free port kubwa sana kwa east na central africa hivo nchi za jirani na tz hazitolazimika kwenda dubai au china kununua bidhaa.
 
Nimelipenda andiko lako. Ila kiukweli ukiangalia kwa sasa Zanzibar wamejidhatiti na wameweka components zote za kujitosheleza kama Taifa.
 
Naam shukrani mkuu kwa nondo hizi.
Wahafidhina wasioona mbali walidiriki hadi kuifuta nafasi ya Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais wa JMT automatic, eti walihofu Maalim Seif angekuwa rais Zanzibar na hivyo kuuweka Muungano kwenye sintofahamu hapo mwaka 1995.

Baada ya miaka 15 tu, Mwaka 2009, CCm walishaona madhara na janja ya wazi ya kupotezwa Zanzibar, Wakalazimika kutumia Upenyo wa Muafaka walau kuirejesha Zanzibar Kikatiba na kuitambua kama nchi. Its too late, CCM Zanzibar hawana tena nguvu za maamuzi za kichama huko dodoma kutokana na katiba ya chama chao. Majuto ni Mjukuu.

Fursa ndogo iliyopo ni kutumia uchaguzi wa vyama vya upinzani. Navyo vinabanwa kuliko, kwa kufanywa khilba za kufuta matokeo kila upinzani wenye uchungu na Zanzibar kila ukishinda.

CCM Zanzibar ndio wachawi halisi wa Zanzibar tokea kwenye ASP huko na kuendelea.

wameshindwa kuitetea Zanzibar, wamenyanganywa sauti na nguvu za kuitetea Zanzibar kwa kujitakia na sasa wanashirikiana na CCM Tanganyika kuvunja maamuzi ya wazanzibari ambao kwa umoja wao wameamua kuchagua upinzani ili kutetea Hadhi ya Zanzibar kwa kupumbazwa kupewa vijivyeo uchwara na kuuza nchi yao.

Sasa katikati ya mapambano ya kimkakati kati ya wazanzibari wanaotaka kurejeshwa Zanzibar na kati ya wanaotaka kuipoteza Zanzibar, kumeibua mgongano wa katiba ya Zanzibar na ile ya JMT kila moja ikijinasibu kuwa nchi.

Fursa ya kutatua changamoto na mkwamo huo ikapotea baada ya wabinafsi kuvuruga mchakato wa Katiba mpya, Sasa imebaki hio RISK ya kufuta matokeo ya Upinzani na kutishana kwa mizinga na masilaha ya kijeshi.
 
zanzibar ikiwa huru itapaa kiuchumi,kutakuwepo na free port kubwa sana kwa east na central africa hivo nchi za jirani na tz hazitolazimika kwenda dubai au china kununua bidhaa

Eneo kubwa la bahari linamilikiwa na Zanzibar kwa hiyo Zanzibar kuwa huru ni hatari kwa usalama wetu na uchumi
Mkuu mipaka ya bahari ipo kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Japo ni kweli tutapoteza eneo nyeti la bahari tena lenye potential ya mafuta na gesi.

Tena ukizingatia mafuta na gesi ni mambo ya muungano.
 
Mkuu mipaka ya bahari ipo kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Japo ni kweli tutapoteza eneo nyeti la bahari tena lenye potential ya mafuta na gesi.

Tena ukizingatia mafuta na gesi ni mambo ya muungano.
Mabavu huwa na ukomo,muhimu huwa ni reform ya maridhiano ubabe wa Mkapa ausaidii,kumbuka kila kizazi huwa ni tofauti na kizazi kilichopita
 
Eneo kubwa la bahari linamilikiwa na Zanzibar kwa hiyo Zanzibar kuwa huru ni hatari kwa usalama wetu na uchumi
Hatari ipi hio kwa ulimwengu wa sasa tunaojitegemea kwa kiuchumi,
upo ulinzi shirikishi wa nchi mbili kwa manufaa ya nchi hizo
 
Mkuu mipaka ya bahari ipo kwa mujibu wa sheria za kimataifa. Japo ni kweli tutapoteza eneo nyeti la bahari tena lenye potential ya mafuta na gesi.

Tena ukizingatia mafuta na gesi ni mambo ya muungano.
Ndiyo maana hatupo tayari kupoteza muungano pia muungano unaosaidia Zanzibar maana kila uchwao Zanzibar eneo linapungua kumezwa na maji na watu wanaongezeka hivyo muungano utasaidia wa Zanzibar kuishi Tanganyika maana miaka 100 ijayo population ya Zanzibar itakuwa million 15 hawawezi kupata nafasi za kuishi
Zanzibar inaweza ku cover raia million tano tu
 
Hili nalo neno.
 
4. Ndio huwa tunawashangaa wasiojua Historia ya Zanzibar kumsifu Marehemu Mzee Jumbe. Huyu ndie aliyefanikisha Kuivunja ASP na Kuiunganisha na TANU kuwa CCM. Lakini fitina ilianza miaka ya nyuma ya kuunganishwa Shirazi Association na African Association kupatikana ASP. Mawindo ya Tanganyika kuuwa uzalendo wa Zanzibar yalianzia mbali. Historia ni ndefu lakini Mzee Jumbe alikosana na Mwalimu Nyerere ndio akafukuzwa lakini alikuwa mwana mikakati wa kuidhoofisha Zanzibar.
Pamoja na udhaifu wake na makosa yake lakini alikuja gundua kuwa kaingia pabaya na alidiriki kutafuta njia ya kuirudisha Zanzibar (hata kama ni kwa maslahi yake binafsi). Na yaliyotokea Dodoma yalithibitisha kwa wengi jinsi Tanganyika inavyo iburuza Zanzibar. Kila uchaguzi CCM zanzibar na hasa Dodoma wamepindua matokeo ya kura ilipobidi.

Nafikiri kama sikosei Dr Bilali alikuwa mfano mzuri, mwisho alipewa umakamu ili asiwe raisi wa Zanzibar. Safari hii wamepewa mbunge wa zamani wa Mkuranga (Bara).

Kuna jambo moja hulijui. CCM sasa kwa upande wa Zanzibar iko kwenye mkakati wa kuongozwa na watu waliopandikizwa kutoka Bara na wala sio hao akina Pandu na Jecha tena. Mkakati ni kuondowa vikwazo zaidi ili njia ya kuihodhi SMZ na kisha kuipoteza Zanzibar iendelee.
Wakifanikiwa hili basi itasemekana "wanatimiza yale wazanzibari wayatakayo". Wazanzibari wakiacha uchama hapa wanaweza kubadilisha hali ya hewa kwa kupigia kura upinzani na kulinda kura zao. Si rahisi lakini yawezekana hasa uchaguzi huu unaokuja.
 
Back
Top Bottom