Je, Zanzibar inajiandaa kujitwalia uhuru kamili?

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
3,702
11,635
Tangu kuasisiwa kwake mwaka 1964, mauungano wa Tanganyika na Zanzibar umeonekana wazi kugubikwa na ujanja ujanja mwingi.

Ni jambo lililo wazi kabisa kuwa waasisi wa muungano walikua na malengo yasiyofanana, mwalimu Nyerere alidhamiria kuwepo na muungano kamili chini ya serikali moja huku mzee Karume yeye alitaka kuutumia muungano kuhodhi mamlaka kule Zanzibar baada ya mapinduzi kisha auvue kama koti linalobana mambo yakikaa sawa.

Inaonekana mwalimu alimzidi kete Karume kwasababu tokea mwaka 1964 hadi 1984 kulikowepo na juhudi za wazi za kimkakati za kudhoofisha mamlaka ya Zanzibar huku akizidi kuiunganisha nchi.

Baada tu ya muungano, nchi yetu mpya iliitwa 'The united republic of Tanganyika and Zanzibar'. Na kwenye hati za muungano kulikua na mambo 11 (sio 9 kama baadhi ya watu wanavyo dai) yakiyo ainishwa kuwa ni mambo ya muungano ambayo ni;

  1. Katiba na serikali ya Jamuhuri ya Muungano
  2. Mambo ya nchi za nje
  3. Ulinzi
  4. Polisi
  5. Mamlaka juu ya mambo ya hali ya hatari
  6. Uraia
  7. Uhamiaji
  8. Mikopo na biashara ya nchi za nje
  9. Utumishi katika serikali ya jamuhuri ya muungano
  10. Kodi (income, cooperate, customs and exercise)
  11. Bandari, mambo yanayohusu usafiri wa anga, posta na simu
Baada ya muungano, mwalimu alianza kutekeleza 'master plan' yake, pamoja na kubadili jina la nchi kuwa 'The united republic of Tanzania' aliendelea kuongeza mambo mengine kwenye orodha ya mambo ya muungano (kwa makubaliano ya pande zote mbili of course) kadri fursa zilipo jitokeza.

Kuvunjika kwa taasisi za EAC kama bank na mahakama ya rufani pamoja na kuvunjika kwa jumuiya yenyewe kulitoa nafasi adimu sana ya kuongeza mambo yaliyokuwa EAC kuwa ya muungano. Kwa mujibu wa katiba ya JMT ya sasa, orodha ya mambo ya muungano ina mambo yafuatayo ya ziada;

  1. Sarafu, fedha, mabenki na fedha za kigeni
  2. Leseni za viwanda na takwimu
  3. Elimu ya juu
  4. Maliasili ya mafuta na gesi asilia
  5. Baraza la taifa la mitihani
  6. Usafiri na usafirishaji wa anga
  7. Utafiti
  8. hali ya hewa
  9. Takwimu
  10. Mahakama ya rufani ya JMT
  11. Uandikishaji wa vyama vya siasa
  12. Usalama (imeongezwa kwenye ulinzi)
Kwa hakika tunaweza kusema hili la vyama vya siasa likitanguliwa na kuungana kwa ASP na TANU kuunda CCM lilikua kama msumari wa mwisho kwenye jeneza la Zanzibar huru.

Ukizingatia kwamba tulikuwa kwenye mfumo wa chama kimoja, basi kwa mara ya kwanza ilipatikana 'mechanism' madhubuti ya kumdhibiti rais wa Zanzibar na serikali yake kupitia vikao vya chama.

Umuhimu wa kete hii ulionekana kipindi cha mchafuko wa hali ya hewa Zanzibar mwaka 1983/1984 ambapo rais wa Zanzibar wa wakati huo ndugu Aboud Jumbe 'alifukuzwa kazi' na CCM. Yaani rais wa Zanzibar anaweza akaitwa Dodoma kwenye vikao vya kawaida kisha akavuliwa uanachama wake na kupotesa sifa ya kuwa rais, akarudi nyumbani akiwa mwananchi wa kawaida tu.

Baada ya mwalimu kung'atuka, na baadaye kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi, tumejikuta tunakumbana na changamoto ambazo hatukuwahi kuzitegemea hapo awali.

Kwa mfano, nini kitatokea iwapo vyama viwili tofauti vitashinda uchaguzi wa Zanzibar na ule wa Jamhuri ya Muungano? Tutaweza vipi kumfunga speed governor rais wa Zanzibar na serikali yake kupitia mgongo wa chama ikiwa rais wa JMT anatoka chama tofauti?

Nikiri kuwa nimeona jitihada kupitia ACT kwa kumuweka Maalim Seif katikati ya wadau wa dola lakini mkakati wa namna hii unaweza kufanya kazi as long as CCM imeshikilia madaraka ya JMT. Pia hili sio suluhisho la kudumu.

Lakini kikubwa zaidi, ni wazi kuwa ule mkakati wa mwalimu uliishia 1985 alipo ng'atuka, kuanzia hapo hadi leo Zanzibar wamekua wajanja zaidi, na inaonekana kama sasa ni wao wenye mkakati wa kulivua koti la muungano.

Mifano michache ya jinsi Zanzibar ilivyo anza kujiimarisha ni kama;

1. Kuimarisha taasisi zake, ni trend inayoendele sasa huko viziwani. Japo tunaweza kusema hili linafanyika ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa SMZ, lakini ndivyo inavyopunguza utegemezi wa SMZ kwa SJMT.

2. Wimbo wa taifa na bendera ya tifa la Zanzibar, mwaka 2005 Zanzibar ilipitisha sheria iliyorejesha bendera yake na wimbo wake wa taifa. Kwa maana hiyo wazanzibari wanafundishwa utii, heshima na uzalendo kwa Zanzibar.

3. Maboresho ya vikosi maalum huko Zanzibar mf. KMKM na JKU. Japokuwa baadhi ya vikosi hivi vina historia ndefu kutokea idara ya usalama Zanzibar hadi jeshi la wanamaji Zanzibar, lakini uwepo wake kwa sasa na jinsi vinavyozidi kuboreshwa ni wazi kuwa wanajiandaa siku wakiwa huru wawe na majeshi yaliyo kamilika. Ukisoma majukumu ya KMKM yako wazi kabisa kuwa ni kulinda mipaka ya Zanzibar.

4. Maboresho ya katiba ya Zanzibar. Pengine hili ndio kubwa kuliko yote, Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ilikua inasema 'Zanzibar ni sehemu ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania', lakini baada ya marekebisho makubwa kwa sasa inafungua kwa kusema 'Zanzibar ni Nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la Visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Visiwa vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar'.

Tena katiba hii inamtambua Rais wa Zanzibar kama amiri jeshi mkuu wa vikosi maalum vya Zanzibar na kumpa mamlaka ya kuanzisha vikosi vipya kulingana na mahitaji.

Sasa basi, kwa maslahi mapana ya uhai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani tutalazimika kuyajadili haya siku moja kwa ukweli na uwazi hata kama ni mambo yenye ukakasi.

Kinyume na hapo basi wanamikakati inabidi mkazitafute plan za mwalimu kisha mumshauri mwenyekiti aendelee pale alipokua ameishia mwalimu. Walau kufikia 2064 tuwe na serikali moja.

Kinyume na hapo tutajikuta tunakwama njia panda hususani kwenye hili la vyama vingi, hauwezi kuiba uchaguzi kila siku, kuna siku watu watachoka itakua patashika na unaweza kuwa mwisho wa muungano.
 
Hata Tanganyika tunapata hasara na huu Muungano..
Wabunge wa Zanzibar hawako active na mambo mengi ya huku bars

Wabunge wao zaidi ya 40 wanawakilisha watu
Sawa na mbunge wa Mbagala..

Hii inafanya wananchi wengi kukosa sauti
Uwakilishi bungeni hauendani na idadi ya watu majimboni only kisiasa tu..

Tunalazimika kuwa na makamu kutoka Zanzibar
Na kufanya zoezi la transition kwetu kuwa
Unpredictable ....imagine makamu angetoka bara..

Waziri mkuu hatambuliki Zanzibar wakati hata wizara za Muungano yeye ndo msimamizi


Tuvunje Muungano Kwa faida zetu wote
 
Hata Tanganyika tunapata hasara na huu Muungano..
Wabunge wa Zanzibar hawako active na mambo mengi ya huku bars

Wabunge wao zaidi ya 40 wanawakilisha watu
Sawa na mbunge wa Mbagala..

Hii inafanya wananchi wengi kukosa sauti
Uwakilishi bungeni hauendani na idadi ya watu majimboni only kisiasa tu..

Tunalazimika kuwa na makamu kutoka Zanzibar
Na kufanya zoezi la transition kwetu kuwa
Unpredictable ....imagine makamu angetoka bara..

Waziri mkuu hatambuliki Zanzibar wakati hata wizara za Muungano yeye ndo msimamizi


Tuvunje Muungano Kwa faida zetu wote

Tatizo ni Tanganyika hapo sasa harasa zote kwanini bado mtaitaka zanzibar na wao hawakutakeni?????????/
 
muungano hauwezi kuvunjika kwasababu, wazanzibari wengi eidha wanaishi, wameishi bara, ama wana ndugu zao bara, ama wamewekeza bara, ama wamesoma bara. kwa hilo tu muungano unanguvu kijamii.

ila pia wazanzibari wanahofu ya kumezwa na kufutwa na huu muungano hasa ukizingatia idadi yao ambayo jiji moja tu la dar ni kubwa kuliko wao wote,

hivyo wazanzibari wanahofu yenye mashiko ya kuogopa kufutwa, hivyo lazima wasimamie maslahi yao kama wazanzibari

na hilo ni lazima lifanyike, na ndio mbinu ya kudumu ya kuuweka muungano

muungano hautadumu kama wazazibari watajiona wamefutwa nafasi yao duniani kama watu

lazima wawe na mamlaka yao na kujisimamia hasa kwa mambo yanayowagusa wao moja kwa moja

hivyo mtoa mada ondoa hofu. muungano hauwezi kuvunjika maana tayari una mizizi iliyozama. ila la muhimu pia ni hayo mamlaka ya kizanzibari lazima yawepo.
 
Umesoma historia potofu ktk hili suala la muungano, ukweli ni kwamba Karume ndo alipenda kuwe na serikali/nchi moja ila Nyerere ndo akakomalia serikali mbili tukiri tu hapa nyerere alipotoka alishindwa kuona ya mbele!
Hii sio kweli kabisa ndugu, karume aliuhitaji muungano kwa ajili tu ya temporary stability kule visiwani kufuatia mapinduzi.

Kama unamfahamu mtu yeyeto aliyewahi kuziona hati za muungano basi muulize, karume alizi saini au la? Ukipata jibu utaelewa nilichokiandika.
 
Hili lina ukweli, utalii peke yake unatosha kabisa kuendesha uchumi wa Zanzibar. wangekua na platform kwenye jumuiya za kimataifa bila shaka wangekua mbali.
Kwani muungano unazuia watalii kwenda Zanzibar? Au umesikia mapato ya utalii yanayopatikana Zanzibar ni mali ya muungano?
 
Hata Tanganyika tunapata hasara na huu Muungano..
Wabunge wa Zanzibar hawako active na mambo mengi ya huku bars

Wabunge wao zaidi ya 40 wanawakilisha watu
Sawa na mbunge wa Mbagala..

Hii inafanya wananchi wengi kukosa sauti
Uwakilishi bungeni hauendani na idadi ya watu majimboni only kisiasa tu..

Tunalazimika kuwa na makamu kutoka Zanzibar
Na kufanya zoezi la transition kwetu kuwa
Unpredictable ....imagine makamu angetoka bara..

Waziri mkuu hatambuliki Zanzibar wakati hata wizara za Muungano yeye ndo msimamizi


Tuvunje Muungano Kwa faida zetu wote
Basi tui assimilate Zanzibar iwe mikoa ya Tanzania....Kama tulichanganya udongo na majina ni kwanini tusichanganye raia na mifumo yake?

Sema hii issue ya muungano ipo esoterically mno, hata mashuleni kinachofundishwa ni tarehe ya kuundwa huo muungano...no more than that.
 
Back
Top Bottom