Je, wewe ni mtoto wa kwanza katika familia: Fahamu jinsi Potential yako inavyowindwa ili uharibike

Nimeona.

Ni mchango mzuri na kuna neno.

Japo umetumia nasaha za kujinasibu na vyanzo vya 'kidini' na 'imani' -- maudhui yako kwa ujumla yana kusudi jema.

Umeleta kisa cha Musa na maisha ya Waisraeli wakati mmoja, kulingana na simulizi zinazopatikana kwenye vitabu vya Biblia -- japo mimi kama mtu si 'muumini', lakini ninapenda kusoma chochote na kujifunza kutoka popote na ninaona kuna neno la kutilia maanani kuhusiana na kisa cha Musa na Waisraeli kwa mujibu wa simulizi na muktadha wa somo lako.

Musa alikuwa ni Kiongozi wa Jamii ya watu; alikuwa akipata msaada kutoka kwa 'Mungu' -- mungu wa Waisraeli... Ukiwa ni mtu wa visomo, hili litakuja kuwa bayana, kila jamii hapa duniani imepata kuwa na 'misingi ya imani' na 'taratibu' zenye kushikiza mila, tamaduni, desturi na stawi zao. Ukija kuwa na bidii ya visomo utakuja kubaini si kweli hasa kudai 'sura ya mungu' katika jamii moja ni sawa sawa na jamii ingine... Kwanza kabisa, kwa kadri kabisa ya sayansi ya kijamii, mapokeo na 'harakati za jamii kutafuta ufunuo' si lazima 'imani' ya jamii, kabila, watu fulani wa makazi ya pamoja iwe ya namna moja, kufanana kwa hapa na pale kunaweza kuwepo -- lakini si lazima kwa kila kitu. Na hapana shaka, gurudumu la 'harakati za jamii kutafuta ufunuo' ni endelevu. Kama vile stawi na staarabu huinuka na kuanguka, ndivyo hivyo hata imani na mapokeo yanaweza kuja na kwenda... Kwa maana tunachodhania kukifahamu kwa misingi ya kufaa kheri na utangamano wa leo, kesho tunaweza kuja kujua ilivyo bora zaidi na basi kuja kuchukua sura ya ustawi na ustaarabu bora zaidi. Utamaduni wa mtu, makundi ya watu na hata Taifa hauko kusimama tu -- ni wenye kutembea kwenda mbele panapo mazingira bora ya kustawi na maendeleo. Kwa hivyo, si tu kawaida ya leo -- kwa kesho inaweza kuwa ni batili ama bure tu, hata sheria za leo -- kwa esho inaweza kuwa ni batili... Tunaishi kutafuta muafaka kati ya 'upeo na vina vya tafsiri kwa mambo yetu' na 'mapana ya elimu, ujuzi na kujua ilivyo bora' -- kama mtu mmoja mmoja, tunaofanya makundi ya watu, makundi ya watu yanayo zifanya taasisi , na basi tuseme -- kadiri ya 'Taifa' kwa ujumla...

Sisi kama taifa, tunahistoria, nasibu na mustakabari inayoweza kutohitaji kufananishwa na Kisa cha Musa -- tuseme Musa na Waisraeli siku za zamani. Kwa mfano, Tanzania, kama taifa changa, ni jamii inayofanyika kutokana na muunganiko na mchanganyiko wa watu wanatokea katika mila, desturi, tamaduni na imani tofauti tofauti; hili linaleta changamoto nyingi katika mbinu za kileo -- za kuunganisha 'sauti' na 'nguvu' za watu kwa misingi ya taasisi za kidemokrasia -- ili kuwanasibu watu na maendeleo, ustawi na ustaarabu... Je, Unakumbuka usemi, unaotokana na mawaidha ya Uyunani ya Zamani, siku za Plato, kukadirisha kudai 'Ili Nchi Iendelee, inahitaji Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi Bora' (?)

Umoja wa Kinchi katika siku za leo, unasigana na harakati za makundi ya watu kupendelea kujipambanua kwa misingi ya udini, ukabila, ukanda na mengine mengi ya namna hii. Tunapenda kujivunia mazuri na makuu ya waliotutangulia na kurithishwa kwetu; lakini haya yanaweza kuwa vikwazo katika utekelezaji wa demokrasia, uhuru, ustawi na maendeleo. Hali kadhalika, huwezi kusema 'watu ni wamoja' na kumbe hao hao 'kila mtu anaamini chake' mintarafu 'jaala ya maisha yake' na 'hatma ya harakati/pilika zake'. Hili ndilo linaleta swali makini kwa wanazuoni wa kwa mfano siasa na maendeleo... Je, demokrasia ni jambo linaloweza kusanifika na kutekelezwa duniani? Kwa sasa na dunia nzima, kuna ukomo wa utumikivu wa dhana, nadharia na tafsiri za 'demokrasia' -- jambo linalojidhihirisha kwa migogoro mingi ya harakati na 'siasa za uwakilishi' katika mataifa na nchi -- ugumu katika utekelezaji wa demokrasia za kiliberali...

Haya, yawekwe hapa ili kutusaidia kubaini kuwa kila kizazi katika nyakati kinachangaoto zake. Ni wajibu wa jamii husika kutafuta muafaka wa ustawi na maendeleo kwa misingi ya mbinu kama elimu za visomo... Tukifanya mbinu na visomo juu ya hatma za maendeleo na ustawi wetu basi tutajinasibu na hata kuweza kuona, zamani ilikuwa ni rahisi 'kushikilizisha' dola, jamii ama kabila ukiweza kutaasisha imani iliyomoja kwa wote -- juu ya mambo kama vile 'mungu', 'miungu', 'Mizimu','Mababu', 'Wahenga' n.k... Katika ulimwengu wa leo, makundi mengi kwa ujumla yanajinasibu 'kujiondoa' na 'usadikifu pofu wa kimakundi' -- hili si la kushangaza, kwa kuwa haya pia ni matokeo ya kuongezeka kwa maarifa na elimu... Lakini, kwa mtu yoyote wa kisomo na visomo hasa -- si rahisi kukwepa kuchunguza na kumulika kila kitu...Hata muafaka wa 'Pengo la Mungu' katika kubayanisha ukweli 'uliowazi' ama 'kujificha' -- kule kuliko ni nyuma ya hatma za watu, ustawi na mamendeleo. Huu 'uko pale pale kutafutwa'.... Kushuku, labda 'maarifa' na' visomo' vyetu vya leo bado 'si kamili hasa'...

Mbadala wa siasa na harakati zake kwa maisha ya leo upo katika jitahada za 'Mipango na Ushirikishwaji' kwa maendeleo ya jamii na kujichagulia. Kwa Tanzania kwa mfano, kama taifa tumekuwa tukijifunza na tunaendelea kujifunza ni namna gani tutapata muafaka wa kukabiliana na maadui wakuu watatu --- Umaskini, Maradhi na Ujinga. Kutoka katika uwanja siasa na sera, tumejipambanua kutoka kwenye 'Siasa za Ujamaa na Kujitegemea' hadi kuwa 'Wanabidii katika Ulimwengu wa Leo wa Utandawazi'--kupitia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025... Katikati ya haya mawili, kuanzia mnamo miaka ya 80, Tulitekeleza maboresho ya kimfumo na taasisi, kutoka 'Ukati' wa Serikali Kuu hadi 'Ugatuzi' wa Mamlaka kwa Serikali Ndogo Ndogo za eneo moja hadi jingine. Kutoka ngazi moja ya mipango, maamuzi na utekelezaji hadi ingine -- kuanzia vitongoji/Mitaa, Kata, Wilaya. Mkoa mpaka Taifa/Serikali Kuu. Azma kuu ya hili ikiwa ni kuongeza tija katika kuibua mahitaji, kusuka na kutekeleza mipango kwa mbinu shirikishi ili kusaidiana na serikali kuu katika kutekeleza makusudi makuu ya Kitaifa kama vile maendeleo kwa watu wote --- na sura ya maendeleo tunayoitafuta ni yale ya watu --- si vitu. Japo katika maendeleo ya watu kuna ya vitu humo humo, mambo yanasohusiana na ukuaji wa uchumi...

Aidha, kwa ujumla, matumizi bora ya Rasilmali, yanaweza kutatua kadhia zetu za umasikini na maradhi pale ambapo tunajitahidi misingi ya maendeleo endelevu kwa kuzingatia 'utawala bora', 'ukuaji wa Uchumi', 'Maboresho ya Huduma za Kijamii' na 'Uhifadhi wa Mazingira'. Na ikumbukwe, kuzungumzia 'utawala bora' ni kuzungumzia kujenga uwezo wa 'jamii ndogo ndogo kujitawala zenyewe' kwa kuhakikisha kuna uwazi katika mabadilishano ya taarifa, kuna uwakikilishi na Ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ya wenyeji na wadau katika kuandaa na kutathmini muktadha wowote wa mipango, mkakati na utekelezaji wake. Ukuaji wa Uchumi unaakisi ongozeko katika ufikiaji wa mahitaji ya karibu na mbali kuhusiana na riziki, fanaka, uzalishaji na huduma... Maboresho ya huduma yanabeba mambo kama vile miundobinu muhimu kama upatikaji wa umeme/maji, Upangaji wa Matumizi bora ya ardhi, ujenzi wa vituo vya Afya na Elimu na mengine mengi ya namna hii. Katika haya manne ya nguzo za maendeleo endelevu --- Suala la Mazingira ndilo Mama wa yote, kutunasibu wanadamu wa leo kung'amua 'Mungu' katika ulimwengu wa leo anaingia katika eneo gani la 'visomo, uweza, mstahiilisho wa yote'... JInsi gani, kutokujali, kukosa umakini, kufanya mambo kiholela kunaweza kuwa 'laana' na 'kukosa baraka' juu ya hatma ya matendo yetu. Jinsi gani sisi kama watu duniani tunaweza kujiangamiza wenyewe ikiwa tunakosa maarifa, busara na 'moyo wa mapenzi' mema kati yetu na viumbe vyote vilivyomo sayarini mwetu...

Kwa kueleza haya, ikidhi kuonesha hata leo hii tuna akina 'Musa'... Unaweza usiwaone ubayana wao kwa kuwa tunaishi nyakati tofauti na matendo yetu yanabeba sura mpya na tofauti na zamani. Unapokuwa na kiongozi na mwanataasisi kama Rais Magufuli John, anayekazana kusimamia na ujenzi wa miundombinu muhimu -- analolifanya lina mengi ya manufaa kuliko hasara katika jamii. Kujitahdi kuimarisha misingi ya utawala bora -- wengi labda wanadhani ile 'tafsiri ya kisiasa' itajapwo 'utawala bora' ina mapekeleo muhimu, lakini ukweli halisi ni kuwa: mapambano dhidi ya rushwa ndipo penye 'mzizi wa fitina' hasa-- silika ya makusudio yenye kuharibika upesi katika mtu, ni kati ya sumu mbaya kwa ustawi wa jamii...Ugatuzi wa mamlaka kwa mfano, huongeza uwanja wa mawezekano ya rushwa kubwa na ndogo katika kila nafasi na ngazi za maamuzi na utekelezaji wa haki -- na hili lina uwezekano wa madhara makubwa kuliko kuingilia kati mgawanyo wa matunda nchi ili kupendelea miradi yenye kunufaisha sura pana ya ustawi wa taifa... Kinyume na inavyodhaniwa na wengi, maendeleo kwa sehemu kubwa ni uimarishaji wa taasisi na 'si siasa' hasa.... Na hata ikibidi tumulikie siasa na umadhubuti wake katika 'kuwaunganisha' watu, Chama kama Chama Cha Mapinduzi kina mtaji bora wa kuweza kujisuka kimkakati na kujipanga ili kuithibiti siasa -- mpaka pale ulimwengu wa harakati za kisiasa utakapomaliza pumzi yake.... Hili linaweza jambo la kimtego sana kulibaini ukweli wake, lakini linaweza kudadavuliwa vile vile ukweli wake....

Sasa, naona mada inahusu 'Mtoto wa Kwanza' lakini, 'nimeteka nyara' maudhui na basi kulingania 'Maarifa ya Ujamhuri' wa leo. Nimefanya hivi, kumaliza nguvu mashauri ya 'Musa' na 'Israeli'... Lakini hii ni nusu ya kisa...

Mbali kupitiliza haya yote mpaka hapa, ni mchango wangu kama mtu, kunasibu maendeleo na stawi za watu ziachane na 'vikomo vya utumikivu' wa mifumo ya leo. Nikiwa ni mwenyekujua wazi yaliyopo, yanayoendelea na mawezekano ya kesho, nitafanya muingiliano muono wangu kama mwanataifa na visomo vya kitaasisi ili kunasibu maendeleo ya siku zijazo --- yenye kupitiliza 'usadikifu pofu wa kimakundi' -- kuelekea liberiti kamili. Sehemu ya maono na tafsiri ya haya unaweza kuyapitia katika uzi huu.

Kuna uwezekano, miaka michache inayofuatia kuanzia sasa, dunia yote itapitia kipindi kigumu... Uchumi wa dunia kwa sehemu kubwa unakwenda kuathirika na kadhia kama ya hili janga la ugonjwa wa virusi vya korona... SI kuwa mimi kama mtu ninakubaliana na yanayosemwa huko nje ya nchi kuhusiana na hili 'jangaa', la hasha. Mawaidha yangu kama mtu yapo katika uzi huu. Kuna mambo mengi nyuma ya pazia katika tawala za dunia. Sisi kama taifa tunaweza kuathirika na kukongoroka/kudorora kwa uchumi katika nchi za 'dunia ya kwanza' kunakonukia. Mfumo wa leo uchumi wa dunia na mategemeano ya 'biashara za kimataifa' ni 'si endelevu'. Tunavyoweza kujiandaa na kipindi hichi cha mpito, kuna uwezekano wa kuleta 'Uhandisi Kamili wa Kijamii'... Katika huo, usijekushangaa wazo lako la 'Mtoto wa Kwanza kuzaliwa' litachukua sura ipi...

Katika jamhuri iliyotaamulika ya watu wa kesho, mtoto wa kwanza atachukua majukuu muhimu sana ya 'kutunza' na 'kuendeleza' nasaba za wanajamii wake. Kwa mfano, kutakuwa na uhuru wa watoto wa kike kuchagua wazae na nani na wazae wakati upi. Lakini, tutapendelea ama tuliweke hivi -- watoto wa kike wataombwa na kusititizwa kwamba mtoto wa kwanza wa kuzaliwa awe wa jamii yake ya karibu... Tuseme, kama ni kabila, mtoto wa kwanza awe kazaa na mwanakabila mwenzake... Wanaofuatia, wanawake watakuwa na uhuru wa kuzaa hata nje ya mbari zao... Muafrika atapenda kuzaa na Mzungu, Mhindi, Mjapu, Mchina n.k Vivyo kwa hao. Lakini dunia haitapoteza 'vinasaba' watu kulingana na mchangamano wa watu na usasa, busara itatumika iliyo ni zaidi na nasibu za 'chuki na ubaguzi' wa sura zote. Ni ulimwengu shujaa sana wa kesho, lakini ukifungua moyo na akili yako -- utakirimika kuyajua haya hata leo na sasa... Ulimwengu wa kesho hakutakua na 'ndoa'... Watu watakuwa wanakaa pamoja na kutunza watoto na kaya zao kwa makundi kulingana na shughuli, mapenzi na mapendeleo yao... Wanawake katika ulimwengu wa kesho watakuwa ndiyo nguzo hasa ya 'utawala bora'; wanaume wanakuwa watu wa 'kuweka picha' kupitia visomo na vina vya upeo wa mambo, na wanawake watakuwa ndiyo wenye kubadili 'sura mbegu za kiustawi' kuwa 'stawi halisi.'.. Tendo la kujiaminana katika jamii litakuwa ni jambo linaloangaliwa kwa jicho bora na akili zaidi... Labda wakati mwingine, ningependa nishiriki hili kwa mapana ili kuelimisha...

Basi lije kuwa ni mwendelezo wa shauri la 'Mtoto wa Kwanza'.... Kwa kuwa unapenda mifano ya Israeli, tafiti 'Kibbutzi' --Je, ni jambo gani? Ulimwengu wa kesho utakuwa kama 'kibbutzi', lakini itakuwa bora zaidi... Si kama jaribio letu la 'vijiji vya ujamaa' lilvyobuma... Lakini Mwalimu Nyerere, alikuwa na 'magutu kwa mambo ya kesho'... Tutakuja kujua siku moja, undani wa maisha na wito wake katika kutumikia 'Taifa Changa' ulitokea wapi hasa...

Hmmm
Nje ya mada.
what's your profession.?
u so deep mate
 
FB_IMG_15776607151241080.jpg
 
Nje ya mada.
what's your profession.?
u so deep mate
Mkuu Da'Vinc: mtu anaandika story ndefu isiyo na mashiko. Nilichogundua nikwamba anajaribu kuwatoa watu kwenye mstari ili watu wamjadili yeye badala ya hoja.

Nafikiri hakuna mtu humu aliyemaliza kusoma alichoandika.

Usikwazike Mkuu kwani hata Mitume wako waliowapinga. Hivyo wewe songa mbele.
 
Mkuu Da'Vinc: mtu anaandika story ndefu isiyo na mashiko. Nilichogundua nikwamba anajaribu kuwatoa watu kwenye mstari ili watu wamjadili yeye badala ya hoja.

Nafikiri hakuna mtu humu aliyemaliza kusoma alichoandika.

Usikwazike Mkuu kwani hata Mitume wako waliowapinga. Hivyo wewe songa mbele.
Ahsante mkuu..
Bandiko lake refu mno
nitajitahidi kusonga hvyo hvyo japo waja wanakatishana tamaa
 
Mkuu as long as unajitambu kua wewe ndio mkubwa katika familia yenu basi hii inakuhusu. Haijalishi kwa mama au kwa baba.. Ilimradi una watu wanaokuita dada ua kaka.

Lakini kwa mujibu wa nukuu zangu za Holly Scriptures najua kwamba kipindi hicho Mussa anapewa agano hilo ilikua ni aghalabu ntu kuzalia nje. Bila ndoa.
so Ndio maana sheria ilikua specific mno kua mzawa wa kwanza wa familia ya ndoa kwakua walikua hawazai bila ndoa.

Mambo yanabadirika Mungu analegeza sometimes ili kuendana na wanawe
Ukiondoa sababu za kuza nje ya ndoa. Vipi kama kama mke wa kwanza wa mke amefariki mzee akaoa mke mwingine na kisha akapata watoto wengine....hapo kutakuwa na mtoto mwingine wa kwanza kwa mama yake.
 
Tatizo malezi tu!
Wanadekezwa sana
Hawakatazwi wakikosea
Hupewa cha uvunguni
Baadae mnadai wanazongwa na mapepo, huu ni uongo...... first born pambaneni sana la sivyo wazazi wengi wanaowadekeza wakishafariki hakuna rangi mtaacha kuona
 
Tatizo malezi tu!
Wanadekezwa sana
Hawakatazwi wakikosea
Hupewa cha uvunguni
Baadae mnadai wanazongwa na mapepo, huu ni uongo...... first born pambaneni sana la sivyo wazazi wengi wanaowadekeza wakishafariki hakuna rangi mtaacha kuona
Kuna watoto wanaodekezwa kama last born. ..?
 
Ukiondoa sababu za kuza nje ya ndoa. Vipi kama kama mke wa kwanza wa mke amefariki mzee akaoa mke mwingine na kisha akapata watoto wengine....hapo kutakuwa na mtoto mwingine wa kwanza kwa mama yake.
Ndio atakuwepo Ila bado kuna mtu kwenye familia ambae ni mkubwa kuliko hao wemgine. Swala dogo tu Unakumbuka yakobo/Israel alizaa na wake wangapi.? Ila mkubwa alikua mmoja tu!
 
Back
Top Bottom