Je, wenye elimu wa Postgraduate Diploma in Education hawana sifa ya kuajiriwa kama walimu?

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Mar 8, 2019
366
1,377
Kama mada inavyojieleza hapo

Kuna hiki kiwango cha elimu ya Stashahada ya Uzamili katika Elimu(Postgraduate Diploma in Education) ambacho mtu aliesomea degree ya fani tofauti na ya ualimu anasoma hii PGDE ili awe na sifa ya kuwa mwalimu na hatimaye aajiriwe as a teacher

Sasa ni miaka inakata kuna rafiki zangu walisoma hii PGDE ili wawe walimu ila cha ajabu kila wakiomba wanapigwa chini na wamemaliza miaka mingi.

Je, kwa ajira za TZ PGDE haina nafasi ya kuajiriwa kama mwalimu?

Najua hapa kuna wajuvi wa mambo jaribuni kufungua watu macho kwenye hili suala ili wapate kujua chochote kitu.
 
Ni sahihi kabisa, tangu 2021 wameacha ku iorodhesha hata kwenye tangazo la kutuma maombi, ukiforce kutuma wanakutema.!
 
Mfano, Iringa university inatoa pgde, mtu yeyote mwenye degree unawez kusoma pale kitu ambacho sio sahihi.

Kwa mfano, advance umesoma HGL na chuo ukasoma sheria, ukienda Iringa university wanakuuliza masoma yako ya kufundishia ni yepi? Kwa vyovyote utasema kati ya hayo matatu ulosoma advance.
Baada ya hapo watakufundisha kozi na misingi ya ualimu tu, badala yake wanapaswa wakufundishe pia content za masomo husika.

Kwa mfumo wa iringa un. Inawafaa waliosoma chuo soma husika mfano kuna jamaa yangu alisoma hesabu tu degree hivyo anahitaji misingi tu ya ufundishaji maana base ya hesabu anayo ya chuo na si advance.
 
Pamoja na hayo kuna mabadiriko yanapaswa kufanyika ili pgde itambulike na wahitimu waajirike bila tatizo.
 
Back
Top Bottom