Je Wazanzibar wana material presidential candidate 2015 ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Wazanzibar wana material presidential candidate 2015 ?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MNYISANZU, Jan 13, 2012.

 1. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Je Wazanzibar wana material candidate anayefaa kuwa rais wa URT?
   
 2. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Leo naona mzee umewaamkia jamaa zetu wa unguja naona umeamua kuja na nyingine kuonyesha msisitizo...basi bwana inatosha,itoshe tu tukubali this time na wao angalau watoe rais then baadae kiti kitarudi tena huku mbona easy tu!
   
 3. h

  hmzuyu Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  katiba yetu haifai kumpa mzanzibari uraisi wa muungano, Hata mhe mwinyi ilikuwa ni kosa,vipi atafanya maamuzi kwenye mambo ya watanganyika yasiyo ya muungano?
  Kwa wao kukubali muundo wa serikali mbili huku hii ya muungano ikitawala na mambo ya watanganyika kumehalalisha watanganyika kuongoza muungano maisha, kwa hiyo hata kama wana mtu anayeefaa kuwa raisi hatutakubali kama watanganyika eti mzanzibari afa maamuzi kwenye hata mambo yasiyo ya muungano.
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,288
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  sasa hivi ni zamu yao full stop. La sivyo fisadi lowasa atachukua nchi
   
 5. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,128
  Trophy Points: 280
  Sifa za "Material President" ni zipi, nje ya zile zinazotajwa kwenye katiba?
   
 6. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Shamuhuna
   
 7. k

  kicha JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 503
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 180
  pumzika kwanza tuache tushushe pumzi
   
 8. F

  FredKavishe Verified User

  #8
  Jan 13, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkipeleka nchi kizamu hivyo tutaharibu hahaa soon utasikia kaskazini watasema ni zamu yao na wao kuongoza nchi
  Nao wa magharibi watibuka na kusema na sisi pia.
  Mkitoka humu watakuja kwenye dini nao wakristo watasema ni zamu yao na waislamu watasema ni zamu yao.
  Kwenye wakristo kitaubuka wa anaglikan watasema ni zamu mbona mnawapendelea sana wakatoliki.
  Cha msingi ni kutafuta mtu makini haijalishi anatoka upande kwa hali ya nchi ya sasa we ned a strong leader kwa kwel na mwenye kufanya maamuz aliye tayar kukubali serikali yake ijifunge mikanda ikate cost zote za kijingA huyo ndo tunamuhitaji
  Awe muislamu sijui mkristo sijui mpagan sijui katoka zenji sijui katoka kaskazin kitu kimoja ajue majukumu yake kwamba sisi ndo tuliye mwajili
   
 9. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  acha ujanja,tuko kwenye muungano wa nchi mbili,hatuwezi kutawala pekeetu kila siku,lazima tuwe fair,zanzibar ni nchi wala huwezi kufananisha na arusha au mbeya ile ni nchi ndio maana haina mkuu wa mkoa ina rais na bendera,acheni hizo dharau na kejeli kwa wazanzibari ndio na wao kina jussa wanatutukana then tunakasirika...sisi tumeshatoa marais wawili wametuvumilia sasa inatosha,kuhusu material president sijaelewa jamaa alimaanisha nini,lakini wapo kina salim,yupo karume wawili kule mmoja kishakuwa mpaka rais huko atashindwa nini hapa?
   
 10. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160

  Mawazo ya kijinga kabisa kutoka kwa anayejiita great thinker!

  Hatutamchagua mtu kwa kuangalia alipotoka. Hatutamchagua mtu kwa kuangalia dini yake. Hatutamchagua mtu kwa kuangalia kabila lake. Ni upuuzi wa ccm kukimbia kivuli chake mambo yakishawawia magumu kwa hoja za kijinga kama hizi. Walipoona uchaguzi uvccm umewakamoto, wakaja na swala la sasa ni zamu ya z'bar. Wakaishia kumweka Masauni ambaye aliishia kufukuzwa kwa kudanganya umri. Ingawa ni makosa kisheria lakini akaachwa na kwenda kugombea ubunge kwao.
  Angalia uchaguzi wa spika. Mafisadi walipomkataa Sitta, wakamtanguliza Chenge kuchafua hali ya hewa na kumtuma Makinda kuchukua form. Wakaleta hoja ya "zamu ya mwanamke" na chama kikaona hapo ndio pa kutokea. Angalia bunge lilivyo sasahivi. Upuuzi mtupu!
  Sasa wamekuja na hoja ya "sasa ni zamu ya z'bar" kwenye urais baada ya kuona wanasigana na hakuna anayemwamini mwenzake. Wote wanaogopana. Wanaona bora aje wa mbali. Wameanza kuipigia debe hoja yao na kama kawaida wamewatuma vijana kwenye mitandao ya kijamii. Inasikitisha sana kuona na wewe umetumbukia humo!

  Amka ndugu yangu. Usiendeshwe na propaganda za magamba. Chama chao kinaelekea kufa. Ni bora ujitoe mapema usije ukazama nao!
   
 11. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  nyie mngekubali??????????au unasema tu kaka,hebu vivae viatu vya wazanzibari uone kama vitakutosha kwenye suala hili,acheni huo ubinafsi hii ni nchi yetu sote na lazima muelewe hii inazungumziwa kwa mgombea urais kupitia ccm kwani ndio wenye muungano wengine tuna pretend but kiukweli hatuutaki!
   
 12. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Alaska ni sehemu ya Marekani. Haijawahi kutoa rais wa Marekani. Tafakari!
   
 13. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hata hawaii ni sehemu ya marekani lakini imetoa rais wa marekani pia....acheni kujipenda kupita kiasi,zanzibar watu wapo wa kushika wadhifa huo wa juu kabisa,tuwe fair au kwa kuwa wao wako wachache ndio tunataka kuwaonea kwa kuwa tunajua kura zao hazitoshi pale chimwaga kulinganisha na za kwetu?tusijipendelee bwana
   
 14. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #14
  Jan 13, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,115
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna mkristo Zanzibar, kama yupo na anaweza kutawala wampe. La sivyo rais atoke bara tena awe mkristo mana safari hii ni ya wakristo.
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  wakristo wako wengi,sasa tuwape wakatoliki ama walutheri,hili nalo neno...!hakuna pa kutokea,tuache kuwaonea wazanzibari kwa sababu wako wachache!
   
 16. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #16
  Jan 13, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Material candidate ? Tumieni kiswahili, Kiingereza kigumu jamani.
   
 17. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2012
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Kwahiyo tuchague rais kwa kuwaonea wazanzibari huruma maana wao ni wachache? Sidhani kama hicho ni kigezo kizuri.
  Pili, nadhani Watanzania wanao uhuru wa kuhamua kwamba wanamtaka Mzanzibari ama la. Kwa jinsi mnavyojadili, ni kama vile mgombea atakaepitishwa na CCM tayari yeye ni rais! Kama CCM wanataka kuweka Mzanzibari sawa, waweke. Watanzania kama hawamtaki si watachagua mtu kutoka chama kingine?
   
 18. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #18
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145

  umenena!ndio mana nikasema hapo mwanzo muungano ni wa ccm,watu hawakunielewa..
   
 19. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #19
  Jan 13, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  2015-2025 Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni Mh.Edward Lowassa.

  wajuvi wote washajua,so jipange utadili na uongozi huo kivipi.
  Kiutendaji jamaa anaweza na ameonyesha uwezo wake,kiasi kwamba mshikaji wake aliona anafunikwa ndio maana kamtosa,nasi watanzania tusivyoweza kuchambua mambo kwa kina tukakubali kumuita Fisadi Papa Je unaweza ukaosha kidole cha kati ukaacha kidole gumba kwa kisingizio kuwa hakikutumika ktk tukio.

  Nasikitika na pia nakubali kiana kuwa Mh.EL ndio Raisi wa URT kipindi kijacho cha uchaguzi,labda tume na msimamizi wa uchaguzi iundwe kwa njia mpya.

  jamani msinituhumu hii ni ndoto tu,niliota jana

  Alamsiki :)
   
 20. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #20
  Jan 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  watowe rais aje atufanyie nini? zanzibar ni nchi ya nje na ina rais wake. hatutokubali mambo hayo yatokee tena. ilikuwa zamani.
   
Loading...