Je Wazanzibar wana material presidential candidate 2015 ?

Je Wazanzibar wana material presidential candidate 2015 ?

Enzi za chama kimoja zilisha isha. Maamuzi ya nani atakuwa Rais ni ya Watanzania wote. Kama ni kupokezana basi next time iwe zamu ya CDM, then CUF, NCCR n.k. maana CCM washa tawala miaka 50 sasa. Watanzania wana akili za kuchagua kiongozi bora kama hawatapandikiziwa kiongozi na wanasiasa. mwaka 2005 Salim alikuwa ni potential candidate ambaye angekubalika sana na Watanzania lakini Wanzibar wakamkataa.

Na kama ni mambo ya zamu kutoa mgombea huko CCM then that time ilikuwa ni zamu yao wakaamua JK achukue. Sasa zamu yao imekwishapita maana walimpa JK. Kwa ujumla ngoma CCM ni ngumu sana sasa wanataka kutumia huo mtaji kuendelea kutawala na sisi tunakuwa carried away as if we are not GTs na kubaki kudisscuss CCM candidates wakati tunajua kuna potential candidates from opposition kama Dr. Slaa ambao wako tayari kutuongoza kwa moyo wote kuliko hawa wa CCM ambao wako tayari kututawala kwa njia yeyote.
 
acha ujanja,tuko kwenye muungano wa nchi mbili,hatuwezi kutawala pekeetu kila siku,lazima tuwe fair,zanzibar ni nchi wala huwezi kufananisha na arusha au mbeya ile ni nchi ndio maana haina mkuu wa mkoa ina rais na bendera,acheni hizo dharau na kejeli kwa wazanzibari ndio na wao kina jussa wanatutukana then tunakasirika...sisi tumeshatoa marais wawili wametuvumilia sasa inatosha,kuhusu material president sijaelewa jamaa alimaanisha nini,lakini wapo kina salim,yupo karume wawili kule mmoja kishakuwa mpaka rais huko atashindwa nini hapa?

kama zanzibar ni nchi inakuwaje waje wazanzibar kutvawala watanganyika? hapa ndipo serikali tatu zinapohitajika.
 
nyie mngekubali??????????au unasema tu kaka,hebu vivae viatu vya wazanzibari uone kama vitakutosha kwenye suala hili,acheni huo ubinafsi hii ni nchi yetu sote na lazima muelewe hii inazungumziwa kwa mgombea urais kupitia ccm kwani ndio wenye muungano wengine tuna pretend but kiukweli hatuutaki!
Siasa za kipuuzi kama hizi ndizo ambazo zimeitumbukiza nchi yetu kwenye matatizo makubwa ya kiuchumi na kijamii tuliyo nayo sasa. Viongozi hawafikirii mambo ya maana ya kuwaondoa Watanzania kwenye matatizo lukuki yanayolisumbua Taifa letu kwa sasa kama mfumuko wa bei, kushuka kwa thamani ya shilingi, ukata serikalini na maslahi duni kwa Watumishi wa Umma. Siasa zinaingizwa kwenye mambo ambayo yanatakiwa kutumia utaalamu ndio maana nchi haiendi. Sasa kama Watanzania tunataka haya matatizo yaishe, tuzikatae hizi siasa za kupeana zamu katika kuliongoza Taifa letu. Hatupaswi kuchagua Rais kwa kigezo cha eneo analotoka. Tuchague Rais kwa kuangalia sifa na uwezo wake kiutendaji na kimaamuzi. Watanzania tusikubali kurudia tena makosa ambayo tumeshayafanya. Tunajionea wenyewe hali ya Nchi ilivyo kwa sasa.
 
Watanzania wenzangu tusikubaliane na hizi siasa za kipuuzi na zisizokuwa na maana kwetu. Nasikitika sana kwa sababu kwa sasa nchi ipo kwenye matatizo makubwa ya kiuchumi na kijamii kama vile mfumuko wa bei, kushuka kwa thamani ya shilingi, migomo vyuo vikuu, ukata serikalini na maslahi duni kwa watumishi wa umma. Lakini Viongozi tulio nao hawana wala hawafikirii hatua zozote za kitaalamu za kuliondoa Taifa katika matatizo haya, badala yake akili zao zinafikiria siasa za kipuuzi zisizokuwa na tija kwa watanzania. Watanzania hatuhitaji kuchagua Rais kwa kigezo cha eneo anakotoka.Tuchague Rais kwa kuangalia sifa za kiutendaji, uwezo wa kuthubutu na kufanya maamuzi sahihi pamoja na uadilifu. Watanzania tunajionea hali ya nchi yetu ilivyo mbaya kwa sasa. Tafadhali tusikubali kurudia tena makosa ambayo tumeshayafanya.
 
Je Wazanzibar wana material candidate anayefaa kuwa rais wa URT?

Mbona mnakuwa na wasiwasi na waZnz. Muda bado mpaka 2015. Kuweni na subra mtamuona.
Kwa sasa sumbueni vichwa vyenu kuinua uchumi wenu
 
Jenga hoja na sio kutoa visingizio visivyo na maana. Chama kinapotangaza kutafuta mgombea wa kiti cha urais, hakisemi tunatafuta mtu wa kutoka eneo fulani. Wenye sifa wanagombea na chama kinafanya mchujo kwa kuangalia sifa za mtu na umakini katika kuelewa matatizo ya watanzania na vipi atayatatua. Rais wa Tanzania ni lazima atatoka ama Zanzibar au Tanganyika na hatumchagui kwa sababu za uzanzibar wake ama utanganyika wake. Tuna vigezo vingine lakini si hivyo vya wapi mtu anakotoka ama anakoishi. Isitoshe, hii zamu unayoizungumzia wewe imeandikwa wapi? Hata kama kungekuwa na mkono wa Jk, kesho tukigundua kuwa kweli ameshiriki, atachukuliwa hatua za kinidhamu au za kisheria. Kutangaza zamu ni kutugawa watanzania kwa misingi tu ya uzanzibari na unzanzibara.
Nionavyo mimi, tatizo lipo katika mfumo wa kuteua mgombea, hii kazi ya kuiachia NEC ndiyo itutangazie mgombea kiti cha urais, si haki na mfumo huu unatakiwa ubadilishwe ili haki iende kwa wanachama kwa kupiga kura katika primaries. Hawa wajumbe wa NEC ambao hawafiki hata 1000, iweje wachukue haki za mamilioni ya wanachama? Ndiyo maana hapa wengi inakuwa ni kishinda kiti kwa nguvu ya pesa. Yametokea mwaka 2005 na wote mnaona wapi taifa lilipo. Tubadilishe mifumo yetu ya kupata mgombea kupitia NEC na badala yake, NEC iteue majina 3 ambayo yatapigiwa kura na wanachama kote nchini na atakayeibuka na wingi wa kura ndiye apeperushe bendera ya chama katika uchaguzi mkuu wa kumtafuta rais wa nchi yetu. Wazanzibari washindane kwa uwiano sawa na watanganyika. UKitokea ni msululu wa tanganyika hata katika miaka 100 hapana matatizo na ukitokea ni msululu wa wanzibar hapana matatizo. Lengo ni nini watawafanyia watanzania na Tanzania na sio Tanzania itawafanyia nini. Nadhani nimejibu hivyo visingizio vyako...
 
Alaska ni sehemu ya Marekani. Haijawahi kutoa rais wa Marekani. Tafakari!

znz ni sehemu ambayo haijawahi toa raisi wa muungano,mwinyi kwao mkuranga.mwanae alikua mbunge mkuranga atakuja kua raisi JMT
 
Sidhani kama ni busara kuendelea kuchangia mada hii kwa misingi ya ubaguzi wa kieneo, kidini nk. Kama ni lazima urais uwe unapatikana kwa zamu (za kidini, kikanda nk) basi ni vema tuweke huo utaratibu uwe wazi-hasa kwenye katiba. Vinginevyo kwa sasa mtu yeyote aliye na 'SIFA' anafaa kugombea na hata kuwa rais.
 
2015-2025 Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ni Mh.Edward Lowassa.

wajuvi wote washajua,so jipange utadili na uongozi huo kivipi.
Kiutendaji jamaa anaweza na ameonyesha uwezo wake,kiasi kwamba mshikaji wake aliona anafunikwa ndio maana kamtosa,nasi watanzania tusivyoweza kuchambua mambo kwa kina tukakubali kumuita Fisadi Papa Je unaweza ukaosha kidole cha kati ukaacha kidole gumba kwa kisingizio kuwa hakikutumika ktk tukio.

Nasikitika na pia nakubali kiana kuwa Mh.EL ndio Raisi wa URT kipindi kijacho cha uchaguzi,labda tume na msimamizi wa uchaguzi iundwe kwa njia mpya.

jamani msinituhumu hii ni ndoto tu,niliota jana

Alamsiki 🙂
We vipi tunajadili ya Unguja unaleta ya Lowasa, una nia gani na nchi yetu???????? Unataka tuibiwe hadi chupi, RICHIMOND kujilipa mabilion kwa siku 156m unaona haitoshi, kununua majumba ya kifahari kwa fedha zetu London hadi wazungu wanastuka unaona haitoshi, kuweka mabillion ya dola kwenye mabenki ulaya , Uswizz kwa fedha za watanzania unaona haitoshi!!!!!!!!!! Au unapiga chaka uone kitatoka nini, Watanzania hatutaki hatukubali uozo huo tumechoka na mafisadi, CCM mkimleta tutatoka na CHADEMA mkiiba kura safari hii zitapigwa kama Libya, massage sent!!!!!!!!!!!!

 
GTers hatupaswi kukubali simpletons waje na hoja dhaifu za ueneo, ukanda, udini, jinsia nk.
Kumbuka hoja ya CCMJ ya 'jinsia' ndiyo inalitesa Bunge letu la muungano.
Haijalishi kama watafuliza watanganyika kumi, au hata wazanzibar kumi.

Hii ya ueneo inanikumbusha kauli aliyoitoa Prof Lipumba wakati wa kuelekea uchaguzi wa 2005 kuwa baada ya BW Mkapa sasa Rais afuataye atoke Zanzibar. Kichekesho ni kuwa yeye mwenyewe (Lipumba) ambaye ni Mtanganyika alichukua fomu na kugombea urais. Mzanzibar aliyekuwa na nafasi kubwa (Dr Salim) alipigwa vita na kuzushiwa uzushi na wazanzibar wenzake. Je kama ingekuwa zamu mbona wajumbe wa Mkutano mkuu wa CCM ambao ni wazenji waliihujumu 'zamu' yao?

Katiba haina cha zamu, kila chama kitasimamisha mgombea wanayeona anafaa, awe Mtanganyika au Mzanzibar.

Mfano:
CCM- Sumaye, Lowassa, Dr Magufuli, Membe, na wengineo...
Chadema- Dr Slaa, Mbowe...
CUF- Prof Lipumba.

Au chukulia kuwa CCM imewaengua watanganyika wote (kinyume cha katiba of course) na kupachika wagombea wazanzibar watupu kwa CCM.
Sasa watu wakimchagua mfano Dr Slaa?

Rais anaweza hata akawa Mkara...
 
acha ujanja,tuko kwenye muungano wa nchi mbili,hatuwezi kutawala pekeetu kila siku,lazima tuwe fair,zanzibar ni nchi wala huwezi kufananisha na arusha au mbeya ile ni nchi ndio maana haina mkuu wa mkoa ina rais na bendera,acheni hizo dharau na kejeli kwa wazanzibari ndio na wao kina jussa wanatutukana then tunakasirika...sisi tumeshatoa marais wawili wametuvumilia sasa inatosha,kuhusu material president sijaelewa jamaa alimaanisha nini,lakini wapo kina salim,yupo karume wawili kule mmoja kishakuwa mpaka rais huko atashindwa nini hapa?

Good, kumbe unatambua kwamba zanzibar ni nchi.

Sasa huu mtazamo wa kutaka raisi wa JMT ambaye ndiye raisi wa Tanganyika atoke zanzibar unautoa wapi?

Marekebisho ya katiba ya zanzibar yaliyofanyika mwaka 2010 ndiyo yamewaondolea wazanzibari haki ya kuwa maraisi wa JMT kwa mtazamo wangu, maana tayari wamejitenga, wamerudi kwenye nchi yao ya asili.

Kama ni muhimu mzanzibari awe raisi wa JMT, inabidi katiba ibadilishwe na kumpa mamlaka kamili ya kuendesha serikali ya JMT waziri mkuu ambaye bila shaka atakuwa mtanganyika. Lakini kinyume na hivyo, hata mimi siungi mkono hoja ya mzanzibari kuwa raisi wa JMT. Tukikubali kuongozwa na raisi mzanzibari ni sawa na kukubali kuongozwa na raisi mkenya ama mganda.
 
Yeyote watakaye mteua lazima atakuwa na SECOND LADY.....gharama tupu

_DSC1019.JPG
 
nyie mngekubali??????????au unasema tu kaka,hebu vivae viatu vya wazanzibari uone kama vitakutosha kwenye suala hili,acheni huo ubinafsi hii ni nchi yetu sote na lazima muelewe hii inazungumziwa kwa mgombea urais kupitia ccm kwani ndio wenye muungano wengine tuna pretend but kiukweli hatuutaki!

mimi sipretend kwel siupend muungano, mana wazanzbar ndo wanafaid na huu muungano, mbona huzungumzii swala la wao kumilik aridh bara lkn ni ngumu sis kumilik aridh zanzbar, nasubir tutengane
 
mbona mnataka kugeuza urais wa hii nchi wa kupeana kama pipi?swala la muungano na zanzibar lenyewe ni kitendawili,bado mnataka wapewe urais,huu ni upumbavu, mbona mikoa ya kaskazin,kabila kama la wachaga lenyewe watu zaid ya milion mbili,mara mbili zaidi ya watu wote wa zanzibar hamtaki hata wajitokeze ku-contest urais, swala la uraisi wa hii tanganyika liachwe kwa watanganyika wenyewe,swala la kumleta mtu wa zanzibar hapa ni sawa na kututukana watanganyika wote, wazanzibar ni kina nani mpaka tuwafikirie kwenye maswala ya siasa za huku bara sizisowahusu?hata hizi wizara wanazoongoza ni zamu ya watanganyika sasa kuziongoza,uongozi wa hii nchi si wakupeana na watu wa zanzibar
 
Hata hawaii ni sehemu ya marekani lakini imetoa rais wa marekani pia....acheni kujipenda kupita kiasi,zanzibar watu wapo wa kushika wadhifa huo wa juu kabisa,tuwe fair au kwa kuwa wao wako wachache ndio tunataka kuwaonea kwa kuwa tunajua kura zao hazitoshi pale chimwaga kulinganisha na za kwetu?tusijipendelee bwana
Siungi mkono raisi kutoka Zenji na hii sio ubinafsi bali
ni aina ya muungano na katiba tuliyonayo. Unashangaza kufananisha muungano wetu na wa USA! ataamua nn juu ya mambo ya Tanganyika? itakuwa sawa na raia wa kigeni kuja kutawala nchi yetu na ninaamini hatutaweza kurisk nchi yetu kiac hicho.
 
Back
Top Bottom