Je, wasanii wa muziki wamekubaliana na uharamia (piracy) katika kazi zao?

Chief Mtangi

Member
May 11, 2020
74
125
Uharamia (piracy) sio jambo jipya katika sanaa nchini, lilichangia kuanguka kwa BONGO MOVIE hasa baada ya mapato kupungua leo wasanii wamebaki kulaumu foreign films, TV shows and series wakati ukweli wanaujua dhahiri.

Now jinamizi hili limeshika hatamu katika upande wa Bongo fleva, tangu digital era took the lead now piracy/uharamia umeshamiri mno, utitiri wa blogs na websites ambazo unofficially zimekuwa zikishusha kazi za wasanii bure, jambo ambalo limeleta kilio cha wasanii kulalamika mapato duni ya kazi, licha ya gharama kubwa katika kuandaa kazi zao ila zimekuwa zikiishia mikononi mwa mashabiki huku zikiwaacha wasanii mikono mitupu ama mapato kiduchu.

Japo kumekuwepo na digital platforms kadhaa kama YouTube, Spotify, Deezer, Amazon Music, iTunes music, BoomPlay, Audiomack, Mkito, Mziiki, Mdundo etc. lakini ni ukweli ni kwamba kazi nyingi zimekuwa zikiishia katika utitiri na nyomi la blogs na websites ambapo kazi zimekuwa zikishushwa (downloaded) bure, pia ni ukweli usiopingika kuwa blogs/websites hizi hazina makubaliano yeyote ya usambazaji wa kazi za wasanii, huku zile official platforms zikipokea watembeleaji wachache mno hivyo kufinya mapato ya wasanii.

Pamoja na hali hii bado wasanii, vyama vya wasanii, COSOTA, BASATA, TRA, TCRA na Wizara husika zimekaa kimya na kushindwa kuchukua hatua yeyote. Kwangu nimeshangaa kuona walengwa (wasanii) kuchukulia bila uzito wowote jambo hili huku wakilalamika mapato kiduchu. Ni kweli blogs/websites hizi zili/zimechangia kuwatambulisha wasanii baada ya kazi zao kusambaa, lakini katika dunia ya leo ambapo wasanii wapo kibiashara (music as business) sites hizo poses as parasites hazina faida yeyote hasa katika muktadha wa kibiashara

Wapo wasanii wakubwa lakini wamekuwa wakihemea mapato kiduchu ilhali ni maarufu mtaani. Swali ninalojiuliza je, wasanii wamekubaliana na uharamia huu wa kazi na jasho lao?
 

Asksr

Senior Member
Jun 12, 2019
142
250
So sad Leo hii diamond tungeweza msikie kwenye jarida la Forbes kama kungekuwa na utaratibu mzuri.halafu na korona hii sijui wanaishije maskini
Basata kazi yao ni kufungia nyimbo tu na wizara hakuna wanachofanya japo na wasanii wetu hawana umoja siku hizi
 

LwandaMagere

Member
Mar 15, 2020
84
150
Kwani ninapo-download kwa mfano tubidy msanii hapati kitu?,na kama hapati kitu nyimbo zao huko zinafikaje?

Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..
 

Chief Mtangi

Member
May 11, 2020
74
125
LwandaMagere,

Tubidy haina tofauti na YouTube converter websites or apps, msanii yeyote yule duniani halipwi na Tubidy, wao ni kama converting machines/websites wanachukua video YouTube na kuzibadilisha kwenda audio ama kushusha video!!
 

Chief Mtangi

Member
May 11, 2020
74
125
Asksr,

Ndo hivyo mkuu, BASATA wako kimya pia chama cha wasanii (TUMA) hakina umoja zaidi ya unafiki tu, wakati jambo muhimu kama hili wangekuwa very strictly kulishughulikia!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom