Nilijua hiyo itasababisha controversy,
actually binadamu ni worse than Punda, angalau Punda anaweza kusema ung'amuzi wake wa mambo ni mdogo.Binadamu hata baada ya ung'amuzi mkubwa wa mambo bado anakuwa fisadi by nature.Ndiyo maana ukomunisti umeshindwa Urusi, wakati wengine wakipanga foleni kupata mikate ya rationing, wakuu wa chama cha kikomunisti walikuwa wanajivinjari katika ma Dacha yaliyo kwenye posh suburbs za Muskva.Na hata maduka yao yalikuwa tofauti kwani walikuwa na Supermarket zao zina kila kitu kutoka west.
Lord Acton alisema power corrupt, absolute power corrupts absolutely.Binadamu is worse than Punda na hawezi kutegemewa ku act responsibly bila ya kuwekewa sheria, at least as far as the context of government is concerned ambako all sorts of weird groupthink and mob psychology zinatokea na kuwafanya hata watu rational waanze kufanya mambo ya ajabu within a group.
Hujasema lolote kuhusu usawa wa binadamu na punda inapokuja kwenye kujifanya mambo kwa hiari bila koboko.!
actually binadamu ni worse than Punda, angalau Punda anaweza kusema ung'amuzi wake wa mambo ni mdogo.Binadamu hata baada ya ung'amuzi mkubwa wa mambo bado anakuwa fisadi by nature!
Aya ya kwanza umeongelea Ufisadi wa ma apparatchiks wa Russia.
Aya ya pili umeleta msemo wa mja mmoja wa Kiiingereza ambao hausemi lolote kuhusu kufanana kwa asili ya binadamu na Punda.
Pointi ya mwisho kuhusu group thinking na mob psychology inasaidia kuudhoofia hoja yako kwamba Binadamu ni kama Punda kwa sababu umekubali kuna wakati binadamu anakuwa rational isipokuwa kwenye vikundi - ambavyo anajiunga kwa hiari.
Lakini hakuna punda ambae ana rationale ya kwenda bila kiboko! Bado hujanishawishi kwamba asili ya Binadamu ni kama asili ya Punda!
...
Simjui hata Punda mmoja aliye amass chakula cha wizi worth USD 25 M huku wenzake wanakufa na njaa.
Bin Maryam,
I feel you on this. Kuna watu wanasema "be careful what you wish for, you may receive it".Basically I am envisioning watu washaitoa CCM na tuna upinzani kwenye power bila institutional changes. Watakubali kuji clip wings in the interest of government efficiency and integrity au ndiyo tutaona kama mambo aliyoleta Kibaki alipochaguliwa mara ya kwanza?
My fear is that human nature is too unrealiable, that is why we need clear institutional changes at least simultaneously with regime change, if not before.
Pundit bado nasubiria kuona ukisema namna ambavyo institution zitabadilishwa kabla ya kuwapa wapinzani uongozi.
Unaweza vipi kubadili institutions bila kubadili fikra za watu?
Tulipowaondoa wakoloni tulifanya wakati huo huo kuingiza watu wapya. Tulifanya hivyo tukiamini kuwa wakoloni ndiyo kizuizi cha maendeleo yetu na hivyo wao wakiondoka tukishika sisi wenyewe basi mambo yatakuwa mazuri.
Matokeo yake ni yapi? Wale tuliowaingiza si walifanya vizuri mwanzo lakini baadaye wameanza kugeuka na kuitwa wakoloni weusi? Na kuna watu wamefikia kudiriki hadi kusema "bora mkoloni"!
Sasa, tunapotamania kuiondoa CCM na utawala wake huku tukitumaini kuwa wale watakaoingia watakuwa bora zaidi. Matumaini hayo yanajiandaa kufeli kama sheria ya pili ya thermodynamic (the law of entropy) of which my esteemed friend Pundit is very familiar with inavyotuhakikishia.
Kwa hiyo naamini tunapanga na kufikiria kuing'oa CCM ni lazima tuwe very focused kuwa hatuing'oi CCM ili tubadilishe tu (cosmetic change) bali tubadilishe kwa kilichobora. Lakini pia hatuna budi kutambua hata hicho kilichobora nacho kitavuruga (the law of entropy). Jukumu letu basi ni kuhakikisha hicho kilichobora kinazuiwa kuvuruka kwa kiasi kikubwa kama wale tuliowatoa.
To me the question is, tunajuaje kilichobora ambacho chapaswa kuchukua nafasi badala ya CCM na viongozi wake? Je tunatafuta chama au watu?
Pundit... that is where I'm going.. unaweza vipi kubadilisha taifa la watu ambao hawajiamini? Unaweza vipi kubadilisha Taifa la watu ambao wanaona hawawezi? Je Taifa la watu wanaojihisi ni duni kuwa walichonacho ndicho wanastahili linajengwaje?
Bila kubadilisha fikra unaweza vipi kufanya watu waamini wanaweza na hivyo wanapaswa kubadilisha wasichokitaka (CCM). Ndio maana binafsi siamini kuwa lengo la kuiondoa CCM madarakan in and in itself linatosha kufanya watu washabikie.
Unaweza vipi kubadili institutions bila kubadili fikra za watu?
Wait a minute....hivi debate hapa ni ipi?...kwamba wapinzani hawawezi kutuletea maendeleo wakipewa nchi/ wapinzani hawako tayari kuongoza au tunahitaji mabadiliko ya kikatiba kwanza kabla ya wapinzani kuwa tayari kushika madaraka au kwamba tunahitaji mabadiliko ya kikatiba na kisheria ili tuweze kupiga hatua mwenye maendeleo?
Bottom line inabidi kuwaelimisha na kuwa involve watu zaidi katika political process.
Nyani.. swali lenyewe lina makosa.. hakuna mtu "atakayewapa" wapinzani nchi; wapinzani wanaweza kuichukua nchi kwa kutuata taratibu za kidemokrasia... yaani hawatapewa kama zawadi; kupewa kwao nchi kutatokana na wao kustahili na kuonesha kuwa wanastahli kupewa kwa kupigiwa kura.
Ndipo hapo mjadala ulipogeuka; kwanini watu wawape nchi? Lazima kuwe na sababu. Kwanini wawape nchi wapinzani na wawape ili kiwe nini...?
Hilo la swali kukosewa hata mimi nililiona....
Ni kweli lazima kuwe na sababu na sababu yenyewe ni CCM wameshindwa kuongoza.
Umewahi kujiuliza hivi ni kwa nini CCM inaendelea kuwa madarakani huku taifa likibomoka badala ya kujengeka?
Hilo la swali kukosewa hata mimi nililiona....
Ni kweli lazima kuwe na sababu na sababu yenyewe ni CCM wameshindwa kuongoza.
Umewahi kujiuliza hivi ni kwa nini CCM inaendelea kuwa madarakani huku taifa likibomoka badala ya kujengeka?