Unaweza kweli kumgundua?

Unaweza kweli kumgundua?

papag

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
1,280
Reaction score
1,931
Tujifunze kwenye ujasusi

Kwenye nyanja ya ujasusi hapa duniani Kuna michezo mingi😃😃😃 😄

Kuna mbinu mmoja ambapo idara ya kijasusi inaweza kutengeneza mtu akawa mkosoaji mkubwa serikali hadharani lakini Kwa siri akawa anafanya kazi na vyombo vya usalama.,Ndio maana kuna msemo unasema kwenye harakati zozote usije ukamuamini mtu yeyote 😄😄

Wananchi wanakuwa wanaamini mtu huyo Kuwa ni adui wa serikali lakini ukweli ni kwamba ni rafiki wa serikali Kwa siri

Mtu huyo anaweza akafunguliwa kesi na serikali lakini kesi yake haiwezi kwenda popote wala haiwezi kuleta madhara kwake..

Mtu huyo anaweza kukamatwa na kupelekwa mahabusu na serikali kwa madai ametenda makosa ukweli ni kwamba mtu huyo hatakwenda mahabusu zaidi ataishi hotelini.

Mtu huyu akikamatwa na wenzake anatenganishwa wakati wa kupelekwa mahabusu ,wenzanke wanapelekwa mahabusu yeye anapelekwa hotelini kula kuku 🤣🤣

Mtu huyu mara nyingi hutumika kukusanya taarifa kutoka kwa wakosoaji wa serikali na kupeleka kwenye idara ya kijasusi .

Kwa upande wa Afrika watu hawa wanapelekwa sana kwenye vyama vya upinzani ambapo kazi yao inakuwa ni kukusanya taarifa kutoka upinzani na kuzipeleka kwenye vyombo vya usalama,Pia mtu huu upeleka mipango wanayopanga na wapinzani kwenda kwenye vyombo vya usalama

Kwenye nyanja ya ujasusi hapa duniani hakuna kosa Kwa idara ya kijasusi kupeleka watu wake kwenye vyama vya upinzani ila kosa linakuwa watu hao wanaopelekwa huko Kwenye vyama vya upinzani wanapelekwa kwa lengo gani ?? Zaidi wanakwenda Kwa lengo la kuvuruga vyama upinzani na kulinda maslahi ya Chama tawala,

Huko Ulaya au Marekani ya mashiriki ya kijasusi wanatuma watu wao kwenye vyama upinzani na vyama tawala kwa lengo la kusimamia maslahi ya nchi siyo kusimamia maslahi ya vyama tawala badala ya kuvuruga vyama vya upinzani,

Tofauti ni kwamba huko Ulaya na Merekani hawa watu wanaotumwa mashirika yao ya kijasusi kwenye vya upinzani ni Kwa ajili ya kulinda maslahi ya nchi lakin Afrika hawa watu wanatumwa na idara za kijasusi kwenda vyama vya upinzani kulinda maslahi ya vyama tawala na kuvuruga vyama vya upinzani.

Kwa lugha ya kijasusi hawa watu Wana majina mengi mfano.
1. Agent Provocateur: Huyu ni mtu ambaye anatumwa na idara za kijasusi kwenda vyama vya upinzani Kwa ajilli ya kuhamamisha wenzake wavunje sheria Ili waweze kukamatwa na vyombo vya usalama.

2. Double Agent: Huyu ni mtu ambaye anakuwa anatumikia mabwana mawili Kwa wakati Mmoja, yan anatumikia upinzani na idara za kijasusi , wakati mwingine huyu mtu anaweza kuwapelekea habari vyama vya upinzani kutoka serikalini ili aweze kuaminika lakini habari hizo zinakuwa hazina madhara Kwa serikali na wakati mwingine hizo habari zinaweza zikawa za uongo kijasusi zinaitwa
(Disinformation)

3.Controlled Opposition,(Upinzani Unaodhibitiwa) huyu ni Mtu au kikundi ambacho kwenye jamii kinaonekana kupinga na kukosoa serikali, ukweli kinakuwa kinaelekezwa cha kusema na kinafadhiliwa na serikali ,pia wakati mwingine kinatumiwa na serikali hiyo hiyo kufatilia upinzani halisi 😂😂😂

4. Covert agent.

5. Undercover.

6. Informer

7. Infiltration Agent ni

8. Mole Agent
 
***Kuna mbinu mmoja ambapo idara ya kijasusi inaweza kutengeneza mtu akawa mkosoaji mkubwa serikali hadharani lakini Kwa siri akawa anafanya kazi na vyombo vya usalama.,Ndio maana kuna msemo unasema kwenye harakati zozote usije ukamuamini mtu yeyote 😄😄
Na Huyo Mtu anakosoa Sana lakini hutaona Mamlaka zikimsumbua na hata zikimsumbua ni kama geresha tu haathiriki na chochote
 
Back
Top Bottom