Je wanadamu tuna FREE WILL??

Habari zenu wakuu,swali Hilo linanisumbua Sana,je Ni kweli tuna uwezo WA kuamua nini cha kufanya juu ya maisha yetu??je tuna uwezo WA kuchagua wema au ubaya??sio hatma yetu imeshaamriwa kabla??nimesoma thread ya member flani akizungumzia kisa cha Yuda na Yesu,je yuda alikua na free will au tayari ishapangwa aje amsaliti yesu???..karibuni..


!
!
Free will ..... Fate....Dedtiny
 
Free will inawezakana tena pasipo upinzani wowote inategemea na ukuaji wa mwanadamu katka ukuaji wake....


Kinachomaliza nguvu hii ya maauzi utakayo ni IMANI hasa hizi za dini na makabila,ila kuu zaidi ili la huu uongo wa dini unamaliza sana hii kitu FREE WILL..,


mtu anaamini kuwa hana makamilifu hashituki analifaam jema na baya,mtu anaamini ana dhambi ya asili hashituki ni wapi alithibitisha hilo zaidi ya kuletewa hizo hadithi....


Mtu anaamini kuna mungu ambaye ndiye mwenye power zaid ya chochote duniani,hashituki huyo mungu ni nani na ni nini yaani yupoje,anapewa neno la kumridhisha linaitwa UWEPO,tafakari nn maana ya uwepo...ina maana ww bakia tu au simama hapo hapo ila icho kitu kipo endelea kukingoja ama kukiamini....


Mimi kama mimi huu uwezo wa free will ninao na ninatumia katka maisha yangu ya kila siku siwez kupangwa ama kuendeshwa na imani za ajabu ajabu....
Kama unafuata Sheria za nchi.... Huna maamuzi huru
 
Free will ni uhuru wa mustakabali wako.. Ni nguvu isiyo na uwezo wa kuidhibiti kimwili.. Ni mtazamo wenye asili ya roho na kila mtu huwa nayo utotoni
Lakini kadiri makuzi yanavyoendelea nguvu hiyo huuliwa taratibu na mila desturi imani na elimu
. mila kuna limitations nyingi kwenye mila unaambiwa hairuhusiwi kufanya hili au lile..
. imani unaambiwa kutokana na imani yetu ukisema hivi unakosea
. elimu zetu ni za upande mmoja huku wengi sana wakinyimwa elimu za kiroho utambuzi na ugunduzi
karibu mshana,sikutegemea ungekuja na jibu zuri,fupi,na la kueleweka..so IMANI ndio ina hathiri free will
 
  • Thanks
Reactions: rbt
katika amri za mungu ya pili anasema "nami nawaptiliza wana na maovu ya Baba zao,hata kizazi cha tatu na cha nne wanichukiao...so kama mzee Wako alikosa,,utahukumiwa hadi wewe..
Mkuu ni vyema ungemalizia huo mstari maana umeutamka nusu tu.

Nusu iliyobaki yasema "nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kushika amri zangu"
Hivyo kama wewe utachagua kumtii Muumba basi haijalishi kama Babu zako walikuwa waovu uovu wao hautapitilizwa kwako.
 
Uhuru wa kuchagua upo ndio maana sisi tuko dhambini maana Wazazi wetu Adam na Hawa walichagua kuasi sheria ya Mungu, isingelikuwa hivyo basi dhambi isngeweza kuwepo maana viumbe vyote vingemtii Mungu bila ridhaa yao yoyote.
 
Uhuru wa kuchagua upo ndio maana sisi tuko dhambini maana Wazazi wetu Adam na Hawa walichagua kuasi sheria ya Mungu, isingelikuwa hivyo basi dhambi isngeweza kuwepo maana viumbe vyote vingemtii Mungu bila ridhaa yao yoyote.
Mi nadhani kuwa ni mipango endelevu ilishapangwa before! Adam kuasi tu hapo hapo ikaja kitu kurithi dhambi ya asili! Wakati hata hakuwahi ambiwa kama ukifanya kosa utarithisha vizazi!

..ipo kama ipo lakini hatuna matumizi nayo....
Kuanzia kwenye dini..tawala... Mifumo yote ....
...uhuru wa bendera!
 
Kosa lilifanyik kizazi cha ADM...alkn Mbona adhabu zinaendelea hadi Leo?
kama unasoma bible vizuri,sisi hatuna adhabu tena,Yesu katuokoa,,Kuna mstari unasema kwaajili ya mtu mmoja ulimwengu wote,umetenda dhambi,na kwa mtu mmoja wote tumeokolewa
 
kama unasoma bible vizuri,sisi hatuna adhabu tena,Yesu katuokoa,,Kuna mstari unasema kwaajili ya mtu mmoja ulimwengu wote,umetenda dhambi,na kwa mtu mmoja wote tumeokolewa
Adhabu alizopewa adam na hawa juu ya uasi wao zimeisha?
Kula kwa taabu
Kuzaa kwa uchungu
Kifo....na mengine....
 
Adhabu alizopewa adam na hawa juu ya uasi wao zimeisha?
Kula kwa taabu
Kuzaa kwa uchungu
Kifo....na mengine....
swali zuri,sijajua nikujibu kwa mujibu WA bible inavyofundisha ama laaah..coz mambo hayo kama yamenipitia kushoto
 
Kuna mahali nlisoma kwenye maandiko panasema
MUNGU ALIUMBA KILA JAMBO KWA MAKUSUDI YAKE HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA
Thank God kuna neema ya toba na Mungu ni Mungu wa huruma
 
Adhabu alizopewa adam na hawa juu ya uasi wao zimeisha?
Kula kwa taabu
Kuzaa kwa uchungu
Kifo....na mengine....
Zimeisha ukisimama kwenye mstari wako wala huwezi kuzitumikia izo adhabu...
 
Kuna mahali nlisoma kwenye maandiko panasema
MUNGU ALIUMBA KILA JAMBO KWA MAKUSUDI YAKE HATA WABAYA KWA SIKU YA UBAYA
Thank God kuna neema ya toba na Mungu ni Mungu wa huruma
Kwann kuumba wabaya?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom