Maneno ya mwanamke hana dini ni maneno ambayo yako kinyume na Uislam. Na mwanamke wa kiislam anapaswa kulelewa katika Dini yake na kushikamana na Dini yake kwa sababu ndio sababu ya kufaulu kwake duniani na akhera. Kwetu Waislam (ikiwemo wanawake) Dini ndio kila kitu.
Muislam usipoteze Dini kwa sababu ya ndoa, ni bora usioe/usiolewe kuliko kuritadi. Usipoteze Dini yako ya Uislam kwa sabab yoyote ile. Maisha ya Dunia ni mafupi na hayana thamani ya kuilinganisha na Dini ya Uislam.
Namuomba Allah anifishe katika Uislam. Allah atudumishe Waislam wote katika Dini hii tukufu na atufishe katika Tawheed na Sunnah. Aameen.