Uchaguzi 2020 Je, wajua kuna watu wazuri, waadilifu wenye uwezo, wanaotaka kuingia Bungeni kulisaidia Taifa, Bunge na kumsaidia JPM kwa dhati, lakini kwa vile...

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
51,514
116,607
Wanabodi,

Kila nipatapo fursa, huja na makala elimishi kuhamasisha uzalendo kwa taifa letu kupitia makala elimishi hizi za " Kwa Maslahi ya Taifa"

Swali katika mada yangu ya leo ni katika kuwapata wagombea wa CCM, Je, vikao vya uteuzi vya CCM, vitazingatia tuu matokeo ya kura za maoni, ambayo ndio maslahi ya CCM, au navyo vitangulize mbele maslahi ya taifa kwa kutupatia wagombea wazuri, watu safi, waadilifu na wenye uwezo wa uongozi hata kama kwenye kura za maoni, wamepa kura sifuri?

Vikao vya uteuzi vya CCM, vinakaa wiki hii, kuteua wagombea ubunge na udiwani, hivyo hili ni bandiko la ushauri, info pack kwa chama changu cha Mapinduzi, CCM, kwa kuwajulisha kuwa miongoni mwa watangaza nia kupitia CCM, kuna watu wazuri, watu safi, watu waadilifu na wenye uwezo wa uongozi waliogombea kupitia CCM na kutaka kuingia Bungeni kwa lengo la kwenda kulisaidia Taifa, Bunge, na kumsaidia JPM kwa dhati kabisa ya kusaidia kufuatia kubaini madhaifu mbalimbali ya Bunge na serikali, na kufuatia uadilifu wao, watu safi wazuri, waadilifu hawa, hawakutoa hata senti tano!, na kwa vile watu hawa hawakutoa hata senti 5!, na kufuatia ule msemo wa Waswahili usemao "Mkono mtupu haulabwi", wajumbe walifanya yao!, walitoa senti sifuri, na kwenye kura wakapata kura sifuri!.

Kama sasa na vikao vya uteuzi vya CCM, vitazingatia tuu kura za wajumbe na matokeo ya kura za maoni pekee, then CCM, itapoteza watu wengi safi, wazuri, waadilifu na wenye uwezo wa uongozi, lakini watakosa kuteuliwa kwasababu hawakutoa chochote na matokeo yake hawakupigiwa kura zozote na wajumbe.

Mimi ni miongoni mwa kundi hili ambaye nilitangaza nia kugombea kupitia CCM, sikutoa hata senti tano kwa yoyote, na katika kura za maoni, nikavuna nilichopanda!

Hizi ni baadhi ya agenda zangu zilizonivutia kwenda Bungeni.



Japo wajumbe walifanya yao, lakini kufuatia trends za siasa za Tanzania kwa sasa zinaonyesha Bunge lijalo linakwenda kuwa ni Bunge la CCM predominantly, bado naamini ili Bunge hili liwe na impact ya kuisaidia serikali, linahitaji baadhi ya mijitu bold na critical thinkers ambao watakuwa critical kule Bungeni, vinginevyo kama tutajaza wapiga meza tu kuunga mkono kila kitu, then kiukweli kabisa, Bunge lijalo lita.

Naomba nisimalizie.

Mungu waongoze wajumbe wa vikao vya uteuzi vya CCM, kutuchagulia watu wazuri, watu safi, watu waadilifu na wenye uwezo ambao sio tuu watawasaidia wananchi, watalisaidia Bunge na kuisaidia serikali ikiwa ni pamoja na kumsaidia Rais wa JMT.

Mungu Ibariki CCM iwatendee haki Watanzania.
Mungu Ibariki Tanzania
.

Paskali
 
Unalalamika au unatoa ushauri? au unajipigia debe? nyie ni walewale ambao mnaongea mkiwa nje ya system ya chama lakini mkishapata nafasi mkaingia huko mnashindwa kurekebisha mapungufu na kuziba mianya inayosababisha haki za wengine waliopo nje yabinywe zaidi kisa mnanyonya asali.

Siku mkitolewa nje ya nyonyo lenye asali mnaanza tena kupiga kelele mithili ya akina Nape na Membe.
 
Upendeleo utakuwa pale pale bila kusahau rushwa ya pesa na ngono, sioni kamati kuu ya CCM ikijitenga na uchafu huo. CCM na rushwa ni samaki na maji maana kila mgombea alitoa rushwa kwenye kura za maoni. Sasa hao wasafi wanatoka CCM ipi?
 
Tatizo sio kuingia bungeni na kusaidia shida hata uwe mzuri vipi lakini kama ufanyi kazi kwa maagizo ni lzm uchezee tumbuzi,wote ni wazuri ila wanakuwa na chaguzi mbili either utii maagizo ili usife njaa au utumie taaluma yako ufe njaa kwa kuchezea utumbuzi.

Ukileta professenalism imekula kwao ni lzm uwe type ya musiba ili usifie njaa.Mfano maagizo yamekuja nunua wapinzani we ukihoji haiwezi leta tija hapa ni lzm uchezee utumbuzi,au hakuna mpinzani kuruhusiwa kufanya siasa wwe ukawaruhusu as per katiba hapa imekula kwako.
 
unalalamika au unatoa ushauri? au unajipigia debe? nyie ni walewale ambao mnaongea mkiwa nje ya system ya chama lakini mkishapata nafasi mkaingia huko mnashindwa kurekebisha mapungufu na kuziba mianya inayosababisha haki za wengine waliopo nje yabinywe zaidi kisa mnanyonya asali.

Siku mkitolewa nje ya nyonyo lenye asali mnaanza tena kupiga kelele mithili ya akina Nape na Membe.
Au bashru na polepole
 
Jee Vikao vya uteuzi vya CCM, vitazingatia tuu matokeo ya kura za maoni, ambayo ndio maslahi ya CCM, au navyo vitangulize mbele maslahi ya taifa kwa kutupatia wagombea wazuri, watu safi, waadilifu na wenye uwezo wa uongozi hata kama kwenye kura za maoni, wamepa kura sifuri?.
Kura za maoni ni moja ya indicator ya mtu kukubalika na jamii anayo omba kuiwakilisha. Aliyepata sifuri hakubaliki, na Kuna sabb nyingi za kutokukubalika, siyo uadilifu peke yake.

na katika kura za maoni, nikavuna nilichopanda!.
Hapa umenichanganya. Kama unajjua hukupanda mbegu bora basi jipange ukapande upya.

vinginevyo kama tutajaza wapiga meza tuu kuunga mkono kila kitu, then kiukweli kabisa, Bunge lijalo lita...
Kwenye hili mkuu naomba nitofautiane na wewe. Kuna kitu kinaitwa "party caucus" huwa kinawa-fix watu wenye nguvu ya hoja kinzani ndani ya chama kilichompa ubunge. Ungetaka kuyatekeleza haya basi ungegombea kupitia vyama vya upinzani. Hapa ndipo ingeweza kulikosoa bunge linaloongozwa na wanaccm.
 
Sijasoma yote maana inamwelekeo wa kupotosha.

Nani kakuambia rais atakuwa John Magufuli? Mtajinyonga bure baada ya kujua kuwa 28/10 ndio mwisho wa Giza la nchi hii maana mwanga, furaha, amani na heshima vinarudi tena.
 
Mayala, kama ulikatwa na wajumbe usitegemee kamati kukubeba.

Kuisaidia nchi si lszima uende bungeni, fanya kazi nzuri na nchi utaisaidia sana tu!
Kwamba kwa kupata kura mbili na yeye anaweza kuisadia nchi kwa kuingia bungeni ili akawe wa ndioooo. Ameshindwa kuisaidia nchi kwa kutumia taaluma yake kwa kukemea mambo mengi ya hovyo amebaki kusifia.
 
Back
Top Bottom