Wanabodi nimeshawishika kuuliza hivi kutokana na maendeleo waliyonayo hawa mabwana pamoja na uwezo mkuu walionao katika kufanya mambo kwa usahihi kabisa, kwanza kitu chochote kilichotengenezwa na mjerumani ni kitu chenye thamani Kubwa sana, uwezo wake kijeshi na jinsi alivyojaribu kuitawala dunia mara mbili, jinsi anavyowabagua hata weupe wenzake na mambo mengine mengi yanayofanywa na mjerumani yanaonyesha yupo tofauti na watu wote duniani.