Je, wafanyakazi wa ndani husaidiwa na waajiri kufikia malengo yao?

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,163
2,000
Wafanyakazi wa ndani wamekuwa msaada mkubwa kwa familia nyingi hasa sisi wanawake maana tunakuwa maofisini tunawaachia watoto wetu.

Pamoja na kuwa na msaada pia wanamapungufu yao.

Je, waajiri wa wafanyakazi hao huwasaidia kufikia malengo yao?

Karibuni Tujadili

==========

Akisoma risala ya Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi, Hoteli, Nyumbani, Huduma za jamii na ushauri (CHODAWU), Mary Mwarabu, katika maadhimisho ya siku wafanyakazi wa majumbani iliyofanyika mjini Dodoma.

Alisema wafanyakazi hao wengi ni wanawake na wana mchango mkubwa katika familia na uchumi wa nchi.

Alisema ni vyema waajiri wakawapa fursa wafanyakazi hao kufanya kazi za uzalishaji katika sekta rasmi na isiyo rasmi ili waweze kujiinua kiuchumi kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine.

Aidha, alisema katika kazi zao wanakutana na changamoto nyingi kama kulea wagonjwa,watu wasiojiweza na watoto ambao wanashinda nao kwa muda mrefu kuliko wazazi wao.

Alisema wanakumbana na changamoto nyingine ikiwa ni pamoja na kunyimwa mishahara, kuzidi kwa saa za kazi, kupigwa, kubakwa na manyanyaso ya hali ya juu.

Alitoa rai kwa waajiri wao kuwapa likizo, kuwalipia huduma za afya,uzazi na kuwalipa muda wa ziada wa kazi kwa mujibu wa sheria za kazi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wanawake Chodawu kitaifa, Atupakisye Mtafya, aliwaomba waajiri kuzingatia Sheria ya Ajira na uhusiano kazini namba sita ya mwaka 2004 na Sheria ya Taasisi za kazi ya namba saba ya mwaka huo.

Aliiomba serikali kutunga sheria madhubuti kwa ajili ya wafanyakazi wa majumbani.

Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Rehema Shija, alisema wafanyakazi wa majumbani ni wafanyakazi kama wengine wana haki kupewa mikataba ya kazi kwa maandishi.

Shija alisema wanastahili haki ya kuchangiwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii kama wafanyakazi wengine ili kujiwekea akiba yao ya baadaye.

Chanzo: Nipashe
 
sumbai

JF-Expert Member
Jun 16, 2014
15,405
2,000
Mungu awabariki saana,.

Wanatukanwa na Mama mwenye nyumba, wanategwa na baba mwenye nyumba,

Vitoto vya kiume ndipo vinapatapo uzoefu kwao, Bado mangi gengeni nae anataka.

Mama akirudi anamuona mwanae wakike kavaa surual, house girl nae pia lakini haose girl tuu ndio anaonekana kavaa vibaya. Anaambiwq kavae kanga.
 
Akili 09 Nguvu 01

JF-Expert Member
Jun 23, 2015
591
1,000
Mim bint yang wa kaz kanambia yey anahitaj ajifunze cherehan awe fund wa kushona!
Nlimuuliza km anatak nimpeleke sekondar akasema "Shemeji(huna ananiita shemej) usijisumbue mi natak kushona tu. Basi nmemwambia mlee mtot zen akifikisha 2yrs nakununulia mashine nakupeleka kwa fund ukajifunze
kaz yako uipendayo
Anamlea vizur mtot wang na ana tabia njema
Tuishi nao vizur awa wabint tuwasaidie kutimiza ndoto zao tucwafanye michepuko ingawa wengine hua wanatutega sn
 
Ubarikiwe na Mungu
 
Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,163
2,000
Mungu awabariki saana,.

Wanatukanwa na Mama mwenye nyumba, wanategwa na baba mwenye nyumba,

Vitoto vya kiume ndipo vinapatapo uzoefu kwao, Bado mangi gengeni nae anataka.

Mama akirudi anamuona mwanae wakike kavaa surual, house girl nae pia lakini haose girl tuu ndio anaonekana kavaa vibaya. Anaambiwq kavae kanga.
Wanapitia vingi sana..tusiwaache tu tuwe tunawasaidia..
 
harder king

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
3,885
2,000
Kiukweli dada wa kazi wanamchango mkubwa sana ila changamoto wanazokutana nazo kwa mama mwenye nyumba/japo baba cyo sana Mungu ndio anajua cjui kwa nini wamama huwachukulia dada wa kazi kama cyo binadamu,inanikera yan!.
 
BADILI TABIA

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
31,378
2,000
Ndio.
Kama katulia.

Hg wangu mmoja alikuwa na ndoto z biashara.... pamoja na kufinya watoto baada ya mwaka na nusu alienda kkoo kitafuta mzigo sasa hivi anauza kwao.... ndio biasshara yake kwa sasa....

Same na hb....

Ila niliyenae sasa hata asipotimiza malengo yake atajiju...mvivuuuuuuuu.........mchafuuuuu...... yaani naona amenigeuza mie ndio hg sasa shurti niamke alfajiri nisafishe niandae menyu ya mchana ndio nisepe... (yeye kabaki kulinda nyumba)
 
Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,163
2,000
Ndio.
Kama katulia.

Hg wangu mmoja alikuwa na ndoto z biashara.... pamoja na kufinya watoto baada ya mwaka na nusu alienda kkoo kitafuta mzigo sasa hivi anauza kwao.... ndio biasshara yake kwa sasa....

Same na hb....

Ila niliyenae sasa hata asipotizima malengo yake atajiju...mvivuuuuuuuu.........mchafuuuuu...... yaani naona amenigeuza mie ndio hg sasa shurti niamke alfajiri nisafishe niandae menyu ya mchana ndio nisepe... (yeye kabaki kulinda nyumba)
Ulifanya vyema sana...
 
Mehek

JF-Expert Member
Feb 26, 2017
7,487
2,000
Mungu awabariki saana,.

Wanatukanwa na Mama mwenye nyumba, wanategwa na baba mwenye nyumba,

Vitoto vya kiume ndipo vinapatapo uzoefu kwao, Bado mangi gengeni nae anataka.

Mama akirudi anamuona mwanae wakike kavaa surual, house girl nae pia lakini haose girl tuu ndio anaonekana kavaa vibaya. Anaambiwq kavae kanga.
Nikweli mkuu mabosi wengi wanaroho ngumu mnoo, hasa hasa wachaga, wapare, wanyaqsa
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
38,828
2,000
Inategemea na akili yake, kuna wengine wanakuwa vizuri sana ila ukishawapeleka kusomea chochote wanakuona fala tokea hapo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom