Ushauri wa OSHA: Kampuni yenye wafanyakazi kufikia 50, waajiri nesi kufundisha na kuangalia mfumo wa huduma ya kwanza

Hassanjk

Senior Member
Feb 24, 2023
168
379
Niliwahi kuhudhuria mafunzo ya huduma ya kwanza ya osha nikapata wazo kuwa, wanaweza kuboresha zaidi tofauti na hivi sasa.

Fikiria mtu ahudhurie mafunzo ya siku nne au tano halafu awe certified kutoa huduma ya kwanza na hapo ujue wengine wanao hudhuria walipata sifuri somo la baiolojia.

Kama wapo serious nashauri hivi.

Kwa kampuni yenye wafanyakazi wa kufikia 50, waajiri nesi anaweza kuwa na Diploma au hata cheti kwa kadri ya uhatarishi wa kazi za taasisi husika. Nesi huyo ndiye atakuwa anafundisha na kuangalia mfumo mzima wa huduma ya kwanza na ndiye atarepoti kwa OSHA.

Naamini wakifanya hivyo, watakuza ajira kwa manesi lakini muhimu zaidi wafanyakazi watapata huduma bora zilizokusudiwa kwani manesi wamepikwa vizuri sana kwenye kutoa huduma ya kwanza.
 
Back
Top Bottom