Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,505
Wafanyakazi wa ndani wamekuwa msaada mkubwa kwa familia nyingi hasa sisi wanawake maana tunakuwa maofisini tunawaachia watoto wetu.
Pamoja na kuwa na msaada pia wanamapungufu yao.
Je, waajiri wa wafanyakazi hao huwasaidia kufikia malengo yao?
Karibuni Tujadili
==========
Akisoma risala ya Chama cha Wafanyakazi wa Hifadhi, Hoteli, Nyumbani, Huduma za jamii na ushauri (CHODAWU), Mary Mwarabu, katika maadhimisho ya siku wafanyakazi wa majumbani iliyofanyika mjini Dodoma.
Alisema wafanyakazi hao wengi ni wanawake na wana mchango mkubwa katika familia na uchumi wa nchi.
Alisema ni vyema waajiri wakawapa fursa wafanyakazi hao kufanya kazi za uzalishaji katika sekta rasmi na isiyo rasmi ili waweze kujiinua kiuchumi kama ilivyo kwa wafanyakazi wengine.
Aidha, alisema katika kazi zao wanakutana na changamoto nyingi kama kulea wagonjwa,watu wasiojiweza na watoto ambao wanashinda nao kwa muda mrefu kuliko wazazi wao.
Alisema wanakumbana na changamoto nyingine ikiwa ni pamoja na kunyimwa mishahara, kuzidi kwa saa za kazi, kupigwa, kubakwa na manyanyaso ya hali ya juu.
Alitoa rai kwa waajiri wao kuwapa likizo, kuwalipia huduma za afya,uzazi na kuwalipa muda wa ziada wa kazi kwa mujibu wa sheria za kazi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wanawake Chodawu kitaifa, Atupakisye Mtafya, aliwaomba waajiri kuzingatia Sheria ya Ajira na uhusiano kazini namba sita ya mwaka 2004 na Sheria ya Taasisi za kazi ya namba saba ya mwaka huo.
Aliiomba serikali kutunga sheria madhubuti kwa ajili ya wafanyakazi wa majumbani.
Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), Rehema Shija, alisema wafanyakazi wa majumbani ni wafanyakazi kama wengine wana haki kupewa mikataba ya kazi kwa maandishi.
Shija alisema wanastahili haki ya kuchangiwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii kama wafanyakazi wengine ili kujiwekea akiba yao ya baadaye.
Chanzo: Nipashe