Je, utachukua uamuzi gani?

Je, utachukua uamuzi gani?

rikiboy

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
22,163
Reaction score
43,988
Jamani habari wakuu,

Natumaini mpo poa kuna jambo nataka kujua kutoka kwenu hasa kwa wale wanaume wenzangu mliopatwa na jambo kama hili.

Hivi ikitokea umezaa na mwanamke flani mtoto na mmedumu kwa miaka kama mitatu hivi japo wewe hujajipanga bado kimaisha hata kazi official hujapata still una Hustle lakini mwanamke wako kila siku analalamika kuhusu Ndoa..kwamba anataka umuoe mpaka anafikia stage ya kusema kuachane japo kweli unampenda and she is wife material!

Je, uamuzi gani wa busara ulichukua au utachukua? Au inawezekana kuna mtu anamdanganya huko nje anataka kumuoa?

Ushauri jamani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo lenu wanaume mnajidanganya kuwa hamuwezi kuoa mkiwa bado mnahustle, ni kwa sababu mmeshajiwekea ile notion kwamba mwanamke ukimuoa huku bado unahustle atachoka kuvumilia atakukimbia.

Huyo mwanamke yeye anajua kuwa bado unatafuta pesa ila bado kataka umuoe hivyo hivyo kwa maana kwamba anajua kuwa ataweza kukuvumilia ukiwa bado unatafuta pesa, sasa wewe unachojishauri hapo ni nini.
 
Kama umejiridhisha pasipo na shaka ya kuwa unampenda na ni wife material, kwa nini msihalalishe mahusiano yenu? Unataka ujipange kwa kitu gani kwa miaka yote hiyo zaidi ya mitatu! Maana kama ni maisha mnaweza kuanzia hata kwenye nyumba ya kupanga.

Acha uoga mkuu! Oa wife material huyo mapema maana wako wachache sana! Ukikubali muachane kwa sababu tu hutaki kuhalalisha ndoa, utakuja ujute siku za baadae.
 
Ikiwa miaka mitatu upo nae na umemzalisha una maana unamhudimia so kinachokushinda wewe nini hapo si ukamishe tu suala la ndoa huenda mungu akafungua rizk ukimuoa changamka acha uzembe oa kijana
 
Umeweza kuishi naye miaka mitatu pamoja na mtoto ukihustle..ugumu wa kufunga ndoa unakuwa wapi na umemuona ni wife material ..ndoa sio lazima iwe shazi ya watu mkuu ,Fanya taratibu za mahari ufunge ndoa ya kiuchumi

Analazimisha ndoa kwa sababu ameshaona uwezo wa ndoa upo ila wewe unakuwa mzito..pia anajua vijana hamtabiriki muda wowote unaweza ukapotea ukamuacha solemba...ikawa amepoteza muda bure angali kuna mabaharia huko nje wanatangaza ndoa

Ukishindwa huu ushauri muache binti akaangalie ustaarabu mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeweza kuishi naye miaka mitatu pamoja na mtoto ukihustle..ugumu wa kufunga ndoa unakuwa wapi na umemuona ni wife material ..ndoa sio lazima iwe shazi ya watu mkuu ,Fanya taratibu za mahari ufunge ndoa ya kiuchumi

Analazimisha ndoa kwa sababu ameshaona uwezo wa ndoa upo ila wewe unakuwa mzito..pia anajua vijana hamtabiriki muda wowote unaweza ukapotea ukamuacha solemba...ikawa amepoteza muda bure angali kuna mabaharia huko nje wanatangaza ndoa

Ukishindwa huu ushauri muache binti akaangalie ustaarabu mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Mpak hapo sio wife material
 
Je huyo mwanamke ana kujua vizuri? Kama umejiridhisha kuwa ana kujua vizuri na wewe anampenda na unaona anakufaa muoe jua kuna sababu za msingi na hataki kukupoteza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
weka ndani hilo zigo mlale njaa wote huku mnajipanga, anakukomalia hvo asijekupoteza mda bure kumbe huna nia nae mkuu
 
Jibu:
Mwanamke analazimisha ambacho tayari kipo. Ninyi ni mke na mume ila anataka uthibitisho tu.

Mwanamume hayuko tayari kufanya uthibitisho wa kumuoa mwanamke huyu kwa sababu anazozijua mwenyewe (ameficha). Lakini kiuhalisia ni mke kamili.

Hizi hadithi za wife material huku mnaendelea kumegana hadi mtoto ni upuuzi mkubwa zaidi katika kizazi hiki cha nyoka. Kama kweli ungemhesabu kuwa wife material wala usingehangaika kuja hapa kuomba ushauri kama umwoe, bali jamii ndio ingehangehangaika kujaribu kukuzuia usioe kwa sababu hauko tayari.

Acha kukwepa majukumu mkuu, unataka nikushauri umwache mkeo?

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Oa mengine utajua mbele ya safari
Tena oa sasa wakati wa Corona.
Watu 10 Tu ..done
 
Back
Top Bottom