Je, ungekuwa wewe ungefanyaje?

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,248
2,000
Nusura sherehe ya harusi ivunjike ghafla bi harusi alipoduwaa na kushindwa kutia sahihi cheti cha ndoa alipomwona mpenzi wake wa zamani kanisani.Bi harusi alionekana kuchanganyikiwa alipomwona jamaa huyo akiingia kanisani alipokuwa akijiandaa kutia sahihi cheti hicho na kwa dakika mbili akasimama kama sanamu.
Ilisemekana kuwa, jamaa alikuwa amepanga kumuoa kidosho huyo lakini akahama mji na mwasiliano kati yao yakakatika.

Ndipo kipusa akaamua kuolewa na bwana huyu wa sasa alipokosa matumaini ya kumpata jamaa huyo tena. Mpenzi wake wa zamani alitokea wakati bwana harusi alipokuwa akitia sahihi cheti cha harusi. Alipomaliza alitaka kumkabidhi bi harusi kalamu lakini akashangaa kuona akiduwaa huku akikaza macho yake kwa jamaa aliyeingia kanisani na ikabidi Pastor amshawishi mwanadada atie sahihi cheti hicho.
Kisa hiki kimetokea huko BUNGOMA, mashariki mwa Kenya.

Je, ungekuwa wewe ndiye bwana harusi ungefanyaje?
 

Blue G

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
5,236
2,000
nimgemruhusu aendelee na jamaaa na wafunge naye ndoa kama hivyo ndivyo anavyotaka na mimi kutafuta ustaarabu mwingine,coz kulazimisha ni sawa na kuandaa usaliti kimakusudi,ni bora maumivu ya kuachwa kuliko maumivu ya kusalitiwa yanauma mara 100 ya kuachwa.
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Umenikumbusha wimbo fulani wakati nikiwa kijana ulikuwa unaimba

"Nimemuona Sigalame..
Anaishi BUNGOMA
Na huko BUNGOMA..
Anafanya biashara...
Na hiyo biashara...
Anaijua mwenyewe"...

Ulibamba sana enzi za miaka ya 80 mwanzoni...
 

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,248
2,000
Inaonekana huyu demu alikubali kuolewa na mume mwingine as a last resort ila hakuwa akimpenda kivile. Sasa kipenzy chake cha moyoni kilipoingia kanisani moyo wake ukawa kama vile umepigwa ganzi. Hapa hata kama jamaa alilazimisha kuoa lakini nina hakika kwamba jamaa wa zamani lazima atakuwa anamgongea kwa sana tu--tena anaweza hata kupelekea ndoa kuvunjika--kwa mke kunogewa na penzi la zamani.

Ingekuwa mimi ni mwanaume muoaji ningeachana na hiyo ndoa nitafute ustaarabu mwingine. Haiwezekani nioe mke ambaye penzy lake halipo kwangu. Ushahidi mwingine wa kimazingira ni kwamba jamaa wa zamani alikuwa vizuri sana kunako 6 by 6--atakuwa alikuwa akimpiga mipini sawasawa. Ndio maana alipomuona tu akakumbuka mapigo yake na kushikwa na butwaa! Huyo muoaji mwingine atabakia kuwa boya tu. Itakuwa kuna wambeya walimtonya jamaa kwamba mpenzy wake anaolewa na boya mwingine--akaamua kufuatilia hadi kanisani na kufuatilia afahamu maskanini kwa boya ili awe anaenda kujimegea ngoma yake bila wasiwasi. Kaaaaaaaaazi kwelikweli!!!!
 

byb sac

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
909
500
mhhhh aibu kinoma yaan...
hapo bola angemwacha tu..maana niwazi kwamba mapenzi ya mdada yapo kwa mchiz mwengine na ukizingatia wala hawakugombana...inauma kuwana mtu ambaye hakupendi.nakaonyesha mbele ya kadamnasi.
 

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,248
2,000
huyu bwana asipoutua huu mzigo haraka, ataendelea kugongewa na x wa mkewe mpaka basi!
 

Asamwa

JF-Expert Member
Apr 13, 2012
2,981
2,000
Watu wengi huoa wanawake waliopaswa kuwa wake wa watu wengine kabisa...

Ni kweli mkuu...hii inahusu pia wanawake!

Kuna wanawake kadhaa nimeshaongea nao wakakiri kuwa waume waliokuja kuwaoa hawakuwavutia ile mara ya kwanza walipoonana!
 

mgeni10

JF-Expert Member
Nov 29, 2010
1,109
1,195
Umenikumbusha wimbo fulani wakati nikiwa kijana ulikuwa unaimba

"Nimemuona Sigalame..
Anaishi BUNGOMA
Na huko BUNGOMA..
Anafanya biashara...
Na hiyo biashara...
Anaijua mwenyewe"...

Ulibamba sana enzi za miaka ya 80 mwanzoni...
Tuko, kumbe siku hizi umeshazeeka ?????, Hongera mpo wachache sana Mpe Mungu Sifa Na Utukufu kwa Umri Wako
 
Last edited by a moderator:

mbota

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
834
500
Huwezii kuusemea moyo
Siku zote moyo hauwezi ukapenda Sehemu mbili equally
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom