Ndugu zanguni, ukipewa lift usitoe tena changamoto kwa aliyekupa mpaka akajuta

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,471
23,744
Jana nimetoka zangu mkoa kurudi Jijini nikiwa na jamaa yangu katika mizunguko ya maisha.

Kufika Chalinze tukakuta watu kadhaa wakisubiri usafiri wa kuja Dar. Nlimwona dada mmoja mzuri amependeza na amekaa kwa unyonge sana, zaidi alikuwa na kabag tu kadogo.

Akasimamisha gari, nikasimama mbele yake akaja anakimbia. Akauliza tsh ngapi mpaka Dar. Nilimwambia apande tu nampa lift akasita kidogo but akapanda.

Tukatambuana kwa majina na nikamwuliza anaelekea Dar wapi akajibu Kijitonyama. Akasema alikuja Chalinze juzi kusalimia ndugu na shamba lake.

Huyu dada baadaye alianza kuwa anatoa sana gesi mara ya kwanza nilimtizama rafiki yangu naye akanitizama tukiulizana kwa macho kuwa ni wewe. Jamaa akakataa, na kweli namfahamu jamaa asingeweza fanya hivyo.

Basi njiani tuliendelea kuwa na wakati mgumu sana. Sielewi dada mrembo alikula nini huko Chalinze.

Na bahati mbaya tulikuwa tumefunga vioo tumewasha AC ikawa inabidi sometimes tufungue madirisha.

Kuna kipindi nikawa nahisi au amekunya mle ndani! Maana si kwa changamoto ile na mateso ambayo aliamua kutupatia.

Mbaya zaidi akawa analala sometimes anakoroma kinyama. Hapo sasa ndo akawa anajamba tu kwa sauti.

Tukaamua kushusha madirisha maana tulianza kufikia hatua ya kulewa kutokana na gesi ile ya ukaa.

Tumekuja mshusha Ubungo amechoka sana utadhani yeye alikuwa anasukuma gari badala ya kuendeshwa. Akaomba tubadilishane namba za simu na haraka akatoa biznez card yake.

Tumeachana ila ilibidi gari nilipitishe car wash maana sikuwa naona kama tumebaki salama mle ndani. Nikawaza hali hii mdau unapopewa lift ni muhimu kuzingatia. Usije kuwa kero kwa aliyekupa lift. Kuna wale wengine akipewa lift anabadilisha na nyimbo, radio stations, anaongeza au punguza sauti.

Wengine kama walikuta umewasha AC kiasi fulani wanaongeza au punguza. Yaani ujuaji unakuwa mwingi kwenye lift. Kama haitoshi anaweza hata kukuelekeza upite njia gani.

Ukipewa lift tulia. Weka mikono yako kama unataka kupokea sacrament au unafanya maombi kisha elekeza macho yako mbele ukiwa umefunga mkanda.

Usipende kudakia maongezi. Wewe sikiliza na ujibu ukiulizwa tu. But pia kuwa makini ujue aliyekupa lift anashabikia team gani au chama gani.usije kuwa chana pinzani au team pinzani na aliyekupa lift.

Pia epuka kuwa msemaji mkuu. Naweza kukushusha kama unakuwa mjuvi sana.
 
Sio mbaya mkuu hata mgeni ukimkaribisha kwako kauli ya kwanza inayotoka 'jisikie uko nyumbani"

Cha muhimu umemsaidia inatosha hayo mengine ni ya kuachana nayo
 
Kuna jamaa yangu yeye ukimpa lifti mkikaribia viwanja vya bata au sehemu ina mademu zake basi atahakikisha anakutoa ili aendeshe yeye, na kiumri ni mkubwa kuliko mimi maana ningesema ni utoto.

Kwakua nilishamjua huwa namuachia nakaa nyuma.
 
Kuna jamaa yangu yeye ukimpa lifti mkikaribia viwanja vya bata au sehemu ina mademu zake basi atahakikisha anakutoa ili aendeshe yeye, na kiumri ni mkubwa kuliko mimi maana ningesema ni utoto.

Kwakua nilishamjua huwa namuachia nakaa nyuma.
Ana umri Mkubwa ila ana akili za kitoto. Unamvumilia sana. Mi ningempa siku ya kwanza kwa kuwa nsingejua kama ni tabia yake.baada ya hapo ngempiga chini na kumtaka aache ujinga wake.
 
Kumbe na watoto wazuri huwa wanajamba jamani?
255788363637_status_3db06ab39ce34996a4242f528e7a20c7.jpeg
 
Nafikiria sana kumkwepa ila nashindwa, na sitaki nionekane kama mtu mwenye majigambo au kumkwaza mtu, hii ndio inani cost. Japo nimemchoka sana huyu mwamba na mambo yake ya kishamba
Usiwe na rafiki mzigo. Ukiona rafiki yako ana makwazo achana naye.mwache afikirie anachotaka. Mwanzoni mwambie aamue kubadilika au vipi.kama hayupo tayari kubadilika achana naye
 
Back
Top Bottom