Je unasikiliza redio kwa siku ngapi kwa wiki? Unasikiliza vipindi gani?

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,882
155,860
Binafsi nasikiliza radio mara mbili tu kwa wiki. Nasikiliza siku ya Ijumaa Asubuhi na Jumamosi asubuhi.

Radio ninayosikiliza ni Radio One. Na siku ya Ijumaa nasikiliza kuanzia saa nne na robo asubuhi, kipindi cha nyimbo za zamani. Na sìku ya Jumamosi nasikiliza kipindi cha Kiswahili. Baaaaaaas
 
According to my routine
Nasikiliza radio daily

Nasikiliza sana vipindi vya michezo

Ila my favorite radio ni

East africa radio
Radio free africa
Clouds
 
J3 - Ijumaa

Vipindi vyangu pendwa ni
1. Power Breakfast Clouds Fm
2. Good Morning Wasafi Fm
3. Sports Arena Wasafi Fm.

Hapo nimemaliza siku na huwa asubh vyote
 
According to my routine
Nasikiliza radio daily

Nasikiliza sana vipindi vya michezo

Ila my favorite radio ni

East africa radio
Radio free africa
Clouds
 
Nasikiliza amka na BBC kupitia RFA kila asubuhi baada ya hapo wana kipindi cha kusoma magazeti nacho nakisikiliza
 
Hivi n redio gan apa bongo inatangaza kwa kiingereza tu..Mimi napenda kusikiliza home Boyz redio ya Nairobi tatizo Ni kustream online hivyo network wakat mwingine nashindwa kuinjoy inakua inagoma goma..hivyo naitaji mbadala kwa hapa tz nipate redio gani?

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Hayo mambo tuwaachie ma legend kizazi Cha 60s-80s sisi 90s ni TikTok na social networks
Tena sisi ndio unatuonea manake vipindi vya siku hizi vimebadilika sana, Mimi hata kwenye gari tu siwashi redio naona Bora nikae kimya kuliko kusikiliza makelele na matangazo ya kubet
 
Sikumbuki ni lini nimesikiliza ila ukiacha ile ya saloon wakati wa kunyoa........kusilkiliza ile yangu mimi inaweza ikawa imepita hata miaka 4 bila kusikiliza
Lakn hata simu yangu pia haina redio
 
1. Matangazo ya DW Asubuhi na jioni, jtatu mpaka ijumaa

2. Jmos na jpili ni BBC world service muda wote
.
IMG_20230120_102545_105736.jpg
 
Back
Top Bottom