CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,304
- 12,999
Soma kisa hiki kisha utajibu kama unampenda mama yako au la!
Siku moja dada fulani alianza kumwambia mama yake,
"Mama mie sikupendi, uso umekunjamana, sura yako mbaya, wewe sio mzuri kama wamama wa rafiki zangu. Mikono yako ina makovu. Hakika sikupendi hata kidogo. Ninakuchukia sana"
Yule mama alilia kwa uchungu sana kisha akamwambia,
"Mwanangu, baba yako alifariki wakati ukiwa mdogo sana. Alituacha tukiwa tunaishi kwenye kijumba cha nyasi nje kabisa ya mji, tulikuwa fukara sana. Siku moja niliondoka na kukuacha ndani ukiwa umelala nikaenda shamba jirani na kijumba tulichokuwa tunaishi. Ghafla nilisikia watu wakipiga yowe MOTOOO MOTOOO..... Nikarudi ili nitizame wapi kunawaka moto. Ndipo nikaona ni kijumba chetu ndicho kinawaka moto ilhali wewe ukiwa ndani yake umelala.
Nilipofik wanakijiji walinizuia nisiingie ndani kwani moto ulikuwa mkubwa, lakini nilipambana nao nikafanikiwa kuingia na kukuta moto haujafika mahali ulipolala. Nilikuchukua nikakukumbatia vyema ili moto usikupate. Nilifanikiwa kutoka ndani bila mwale wowote wa moto kukupata wewe.
Na haya majeraha uyaonayo niliungua na moto ili wewe upone"
Alipomaliza kumsimulia ile habari, yule dada alilia saaaanaaaa na kumuomba mama yake msamaha na tangu siku hiyo alimpenda mama yake....
Hebu turudi katika maisha yetu, kuna watu wanaowachukia wazazi wao kwa sababu mbalimbali.... Ni kweli wakati mwingine wanakosea kwani hata wao ni binadamu, ila hatuna budi kuwasamehe kwa wamepitia mengi ili kutufikisha hapa tulipo.
Wazazi wetu wengine waliteseka wakati wa ujauzito lakini hawakukata tamaa, wengine walifukuzwa na wazazi wao lakini walivumilia mateso hayo na kutuzaa, wengine walitelekezwa na baba zetu lakini hawakuthubutu kutuua, Wengine hata kupata ulemavu kwa ajili yetu... Na mengine meeengi sana.
HEBU TUWAPENDE MAMA ZETU KULIKO KITU CHOCHOTE.... MAKE KUNA WANAOTAMANI KUWAONA MAMA ZAO LAKINI WALISHALALA MAUTI NA HATA WENGINE HAWAKUWAHI KUWAONA. LAKINI MIMI NA WEWE TUNAWACHUKIA..
TUBADILIKE WAPENDWA