Je, unajua? Ubatizo wa maji mengi ni ishara ya mtu kufa na kufufuka na Yesu Kristo

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
5,527
Reaction score
7,121
Ubatizo wa maji mengi ni ishara yenye maana sana kiroho. Mtu anapozamishwa ndani ya maji mengi, wakati wa kubatizwa, anaonyesha kuwa utu wake wa kale uliojaa dhambi, umekufa na kuzikwa pamoja na Kristo. Na anapotoka majini, ni ishara ya kufufuka pamoja na Yesu na kuanza maisha mapya ya utakatifu.

Mtume Paulo anasema katika
Warumi 6:4
"Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.”

Ubatizo wa maji mengi ni kitendo cha kuonyesha hadharani kwamba mtu ameacha maisha ya kale, amekubali Yesu Kristo awe Mwokozi wake, na sasa anaishi maisha mapya ya wokovu.
 
Kwanini katika Warumi 6:4 ubatizo wa maji mengi unafananishwa na kuzikwa na Kristo? Mtu akizikwa, anazikwa mwili mzima(mwili wote). Mtu hazikwi kichwa tu. Ndio sababu mtu akibatizwa anazamishwa katika maji mengi.
Ubatizo ndani ya maji mengi.jpg
Ubatizo ndani ya maji tele.jpg
 
Je, ni lazima mtu abatizwe katika maji mengi?
Ukisoma Biblia kwa makini utagundua kuwa ubatizo ulifanyika mahali penye maji mengi, kuthibitisha kuwa mtu anatakiwa kuzamishwa majini anapobatizwa.

Haya ni baadhi ya Maandiko yanayoonyesha kuwa ubatizo ulifanyika katika maji mengi
Yohana 3:23
"Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa."

Mdo 8:36-38
"Walipokuwa bado wanaendelea na safari, walifika mahali penye maji, na huyo ofisa akasema, Mahali hapa pana maji; je, kuna chochote cha kunizuia nisibatizwe? Filipo akasema, Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa. Naye akajibu, Naam, ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu. Basi, huyo ofisa akaamuru lile gari lisimame; na wote wawili, Filipo na huyo towashi wakashuka majini, naye Filipo akambatiza."

Wakashuka majini maana yake, maji yalikuwa mengi.
 
Hata Yesu Kristo alibatizwa katika maji mengi, akasema imetupasa kuitimiza haki yote. Yesu alituachia kielelezo tufuate nyayo zake.
Mathayo 3:13-17
"Wakati huo Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka Yordani kwa Yohana ili abatizwe. Lakini Yohana alitaka kumzuia, akisema, Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu? Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa; kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Ndipo akakubali. Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara aliibuka kutoka majini na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, na kutua juu yake; na tazama, sauti kutoka mbinguni ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye."

Yesu alibatizwa ndani ya mto Yordani, mto wenye maji mengi. Kwa kuwa Yesu mwenyewe alikubali kubatizwa kwa maji mengi, ni wazi kwamba ubatizo wa maji mengi sio chaguo la hiari kwa waumini, bali ni hatua muhimu ya utii na imani.

Tunaposherehekea Pasaka tukumbuke uhusiano huo kati ya ubatizo wa maji mengi na kufa na kufufuka kwa Yesu.
 
Aise nakumbuka mara ya mwisho natoka ndani ya maji baada
ya ubatizo nikafunikwa na blanket zito
tukapiga picha na ndugu na familia wakifurah kweli

Ndo ilikuwa mara yangu ya mwisho kukanyaga kanisani mpaka leo na siji kurudia tena ujinga ule!
Nimeokoka nipo huru.
 
bila shaka ndio umetoka shule, kwahiyo bado una joto kali la homa ya dini uliyolishwa.ila kadri unavyokaa na jamii, utagundua dini ni upendo,kutenda mema na haki ili kupata amani ya moyo na jamii.

Ila omba mungu,shetani asijaze roho ya chuki na ubaguzi kifuani mwako.maana utakua tofauti na unayoyahubiri!
 
Je, ni lazima mtu abatizwe katika maji mengi?
Ukisoma Biblia kwa makini utagundua kuwa ubatizo ulifanyika mahali penye maji mengi, kuthibitisha kuwa mtu anatakiwa kuzamishwa majini anapobatizwa.

Haya ni baadhi ya Maandiko yanayoonyesha kuwa ubatizo ulifanyika katika maji mengi
Yohana 3:23
"Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa."

Mdo 8:36-38
"Walipokuwa bado wanaendelea na safari, walifika mahali penye maji, na huyo ofisa akasema, Mahali hapa pana maji; je, kuna chochote cha kunizuia nisibatizwe? Filipo akasema, Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa. Naye akajibu, Naam, ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu. Basi, huyo ofisa akaamuru lile gari lisimame; na wote wawili, Filipo na huyo towashi wakashuka majini, naye Filipo akambatiza."

Wakashuka majini maana yake, maji yalikuwa mengi.
Inaonekana wewe umeingia katika hizi dini juzi juzi. Punguza speed dada yangu.
 
Sikosoi wanaobatizwa kwa maji mengi wala wale wanaobatizwa kwa maji kidogo mradi tu wanaamini.Jambo la mhimu ni kwamini kwamba Yesu kristo ni Bwana na mwokozi wako.Maji ni ishara tu.
 
Aise nakumbuka mara ya mwisho natoka ndani ya maji baada
ya ubatizo nikafunikwa na blanket zito
tukapiga picha na ndugu na familia wakifurah kweli
Duh, pole sana BLACKTIGER . Familia walifurahi kweli sasa wanasikitika umerudi nyuma.
Huna tofauti na mwana mpotevu katika Luka 15:11-32.
Nakuombea urudi tena kwa Baba..
 
Ivi na yule ambaye Yohana alisema Mimi nawabatiza Kwa maji lakini yeye atawabatiza Kwa moto na Roho mtakatifu si ndio ubatizo watu Bado wanaangaika na maji maji mengi mala maji machache watu mtaoga sana lakini uchawi hautoki, uzinzi autoki na mengine mengi cha msingi mkili Yesu kuwa ni bwana Mambo ya maji ilisha Baki utambuliwo wa madhehebu iwe maji mengi au machache japo maji AYANA uwingi. Note nakubali kukosolewa pia na ushauri
 
Sikosoi wanaobatizwa kwa maji mengi wala wale wanaobatizwa kwa maji kidogo mradi tu wanaamini.Jambo la mhimu ni kwamini kwamba Yesu kristo ni Bwana na mwokozi wako.Maji ni ishara tu.
Hata mimi nilikuwa mbishi kama wewe tungatagaga kabla sijabatizwa katika maji mengi. Ila nilipoujua ukweli, nikakubali kubatizwa kwa kuzamishwa ndani ya mto, kama Yesu alivyobatizwa.
Umefanya vema sana kuchukua hatua hiyo ya kwanza ya kuamini kwamba Yesu Kristo ni Bwana na Mwokozi wako. Hatua ya pili ni kubatizwa(kuzamishwa).

Nafikiri hujaielewa maana ya ubatizo.
Neno "ubatizo" limetokana na neno la Kigiriki "baptizo" linalomaanisha kuzamishwa kabisa. Wengine hawajui hili, hivyo wanatumia maji machache wakidhani inatosha. Lakini kama tulivyoona, Maandiko yanaonyesha wazi kuwa ubatizo wa kweli ni kwa kuzamishwa ndani ya maji mengi (Yohana 3:23, Matendo 8:38). Kitendo hicho ndicho kinachoonyesha kuwa mtu amekufa, amezikwa na kufufuka pamoja na Kristo (Warumi 6:3-4). Hivyo kama kweli umeamua kumfuata Kristo na hujabatizwa katika maji mengi, ukweli umeujua. Fanya haraka ubatizwe katika maji mengi, uitimize haki yote kama Yesu alivyosema.

Vinginevyo Yesu anakushangaa kwanini unamwita Bwana lakini huyatendi aliyoagiza
Luka 6:46-49
“Kwa nini mnaniita, ‘Bwana, Bwana,’ nanyi hamfanyi ninayowaambia? Nitawaonesha jinsi alivyo mtu yule anayekuja kwangu na kusikia maneno yangu na kuyatenda. Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba, akachimba chini sana, na kuweka msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipokuja, mkondo wa maji ukaipiga ile nyumba, lakini haikutikisika, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri. Lakini yeye anayesikia maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ikaanguka mara na kubomoka kabisa.”
 
Duh, pole sana BLACKTIGER . Familia walifurahi kweli sasa wanasikitika umerudi nyuma.
Huna tofauti na mwana mpotevu katika Luka 15:11-32.
Nakuombea urudi tena kwa Baba..
Nilikuwa mfungwa na sasa nipo huru Siwezi kurudi tena gerezani..
nakushauri na wewe ujitathimini mienendo yako naamini ipo siku utatoka kwenye hilo gereza la giza kama mimi!
 
Wokovu unauona gereza kwa sababu bado unapenda maisha ya dhambi.
Hata huo ubatizo unaosema ulibatizwa, nafikiri wazazi wako walikulazimisha tu ubatizwe. Ulikuwa hujaamua kuokoka. Ulikuwa bado hujachukia tamaa ya mwili, tamaa ya macho na kiburi cha uzima.
1 Yohana 2:15-17
Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.

Cha kunifanya nirudi dhambini ni nini. Sina ninachopungukiwa kwenye wokovu. Nina amani tele. Nina furaha tele. Pesa ninazo. Mungu amenifanikisha kikazi, kibiashara. Hata mazao yangu shambani Mungu ameyabariki kwa viwango vya juu. Ndoa yangu iko imara na yenye furaha. Zaidi ya yote nautarajia uzima wa milele Yesu atakapokuja kuwachukua watakatifu. Nirudi tena kwenye matapishi? SI-DA-NGA-NYI-KIIIIIII
 
Ubatizo wa maji mengi ni ishara yenye maana sana kiroho. Mtu anapozamishwa ndani ya maji mengi, wakati wa kubatizwa, anaonyesha kuwa utu wake wa kale uliojaa dhambi, umekufa na kuzikwa pamoja na Kristo. Na anapotoka majini, ni ishara ya kufufuka pamoja na Yesu na kuanza maisha mapya ya utakatifu.

Mtume Paulo anasema katika
Warumi 6:4
"Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.”

Ubatizo wa maji mengi ni kitendo cha kuonyesha hadharani kwamba mtu ameacha maisha ya kale, amekubali Yesu Kristo awe Mwokozi wake, na sasa anaishi maisha mapya ya wokovu.
So what, pointi yako ni nini?
 
So what, pointi yako ni nini?
Mada hii inawahusu zaidi Wakristo. Hivyo, kama wewe ni Mkristo, point yangu ni hii:
Wakati huu tunaposherehekea kufa, kuzikwa na kufufuka kwa Yesu tusisahau kuwa tukio hilo linahusiana pia na ubatizo wa maji mengi. Hivyo mtu akisema anamwamini Yesu Kristo, akubali pia kuonyesha ishara ya kuzikwa na kufufuka na Yesu kwa njia ya ubatizo wa maji mengi. Kuna watu wengi wanamwamini Yesu lakini ukiwaambia wabatizwe katika maji mengi, wanakuwa wabishi. Mada hii imefafanua kwa kina umuhimu wa kubatizwa katika maji mengi.
Umenipata, mkuu?
 
Wale waliobatizwa maji machache hawajabatizwa?
 
Hata mimi nilikuwa mbishi kama wewe tungatagaga kabla sijabatizwa katika maji mengi. Ila nilipoujua ukweli, nikakubali kubatizwa kwa kuzamishwa ndani ya mto, kama Yesu alivyobatizwa.
Umefanya vema sana kuchukua hatua hiyo ya kwanza ya kuamini kwamba Yesu Kristo ni Bwana na Mwokozi wako. Hatua ya pili ni kubatizwa(kuzamishwa).

Nafikiri hujaielewa maana ya ubatizo.
Neno "ubatizo" limetokana na neno la Kigiriki "baptizo" linalomaanisha kuzamishwa kabisa. Wengine hawajui hili, hivyo wanatumia maji machache wakidhani inatosha. Lakini kama tulivyoona, Maandiko yanaonyesha wazi kuwa ubatizo wa kweli ni kwa kuzamishwa ndani ya maji mengi (Yohana 3:23, Matendo 8:38). Kitendo hicho ndicho kinachoonyesha kuwa mtu amekufa, amezikwa na kufufuka pamoja na Kristo (Warumi 6:3-4). Hivyo kama kweli umeamua kumfuata Kristo na hujabatizwa katika maji mengi, ukweli umeujua. Fanya haraka ubatizwe katika maji mengi, uitimize haki yote kama Yesu alivyosema.

Vinginevyo Yesu anakushangaa kwanini unamwita Bwana lakini huyatendi aliyoagiza
Luka 6:46-49
“Kwa nini mnaniita, ‘Bwana, Bwana,’ nanyi hamfanyi ninayowaambia? Nitawaonesha jinsi alivyo mtu yule anayekuja kwangu na kusikia maneno yangu na kuyatenda. Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba, akachimba chini sana, na kuweka msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipokuja, mkondo wa maji ukaipiga ile nyumba, lakini haikutikisika, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri. Lakini yeye anayesikia maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ikaanguka mara na kubomoka kabisa.”
Sijabisha ndugu nimesema wanaobatizwa kwa maji mengi au madogo ni vema.Kilichozaliwa kwa maji ni maji na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho.Unaweza kubatizwa kwenye ziwa lakini bado hujazaliwa Mara ya pili.Makanisa yasiyo ya kisabato hubatiza watu wakiwa bado wananyonya si vema kuwazamisha katika maji mengi kwa usalama wao.Lakini wanapoongezeka umri hupata mafunzo ya kateksim na kubarikiwa baada ya wao wenyewe kumkana shetani.Maji mengi sio kigezo cha kuingia katika ufalme wa Mungu
 
Aise nakumbuka mara ya mwisho natoka ndani ya maji baada
ya ubatizo nikafunikwa na blanket zito
tukapiga picha na ndugu na familia wakifurah kweli

Ndo ilikuwa mara yangu ya mwisho kukanyaga kanisani mpaka leo na siji kurudia tena ujinga ule!
Nimeokoka nipo huru.
Kwa hiyo kwenda kanisani kwako ni ujinga? Haya bwana na Mungu akurehemu!
 
Back
Top Bottom