Je, unajua tatizo la kuku kula mayai, kudondoana na kunyonyoka manyoya?

farmersdesk

Senior Member
May 26, 2012
164
120
TATIZO la kuku kuwa na TABIA zisizo faa/cannibalism limekua shida kubwa kwa WAFUGAJI wengi wa kuku aina zote, ilaa limekua likijitokeza sana hasa kwa KUKU wa MAYAI.

Tatizo hili pia limekua likijitokeza kwa kuku wa rika tofauti tofauti..ilaa linazidi pale kuku wanapo anza kutaga mayai

CHANZO CHA TATIZO
🐓Kuku kuwa wengi kwenye banda dogo kuzidi uwezo wa banda kuhifadhi kuku

🐓Kukosekana kwa vifaa vya kutosha vya chakula na maji pia kuku kukosa chakula cha kutosha

🐓Upungufu wa protini, na madini kama calcium kwenye chakula cha kuku

🐓Kuwa na idadi kubwa ya majogoo bandani kuzidi idadi inayotakiwa

🐓Kuku kuchoka au kuzeeka pale muda wake utakapo kua umefika mwishoni

SULUHISHO☑️
📌Kwa kuku anaekula mayai, mwongezee kiwango cha chakula chenye protein kwenye chakula kama soya meal na dagaa,,,pia mwongezee vitamins kuku wako atapunguza kula mayai pia waongezee kiwango cha mifupa au chokaa kwenye chakula chao,,kama utatumia magamba ya konokono hakikisha usalama wake maana wakati mwingine hupelekea Typhoid

📌Kwa kuku wanao donoana, weka kiwango sahihi cha vifaa vya maji na chakula, weka idadi sahihi ya kuku bandani wapate nafasi, wawekee majani muda fulani ili chakula kikiisha wawe busy kula wasipate muda wa kudonoana

📌Kwa kudonoana na kula mayai..endapo utatumia mbinu zote hapo juu na isisaidie njia ya mwisho kabisa ni kuwakata kuku midomo kwa kutumia kifaa maalumu cha kukatia midomo de-beacker...au kuchoma mdomo kwa njia za kienyeji...baada ya kuwakata midomo wape chakula kingi na vitamins kwa wingi

📌Kwa kuku wanao nyonyoka manyoya, waweke jogoo kwa uwiano na tetea,,jogooo mmoja kwa tetea 8-10, wape chakula chenye mchanganyiko wa madini ya calcium, zuia wadudu kama utitiri viroboto au kupe kwa kupulizia dawa ya Akheri powder au Paranex piaa usafi bandani uwe wakuridhisha.

📌Kikubwa cha kufahamu hapa ukifuatilia kwa makini hizi changamoto huwapata zaidi kuku ambao wafugaji hujichanganyia chakula chao, hivo ni vema ukachanganya chakula kutokana na uhitaji wa kuku na umri wa kuku na utumie formula sahihi ya mchanganyiko wa chakula.
Karibu Instagram @farmers desk tuendelee kujifunza
 
Umesahau pia tabia, kuna wengine unakuta ni genetic zao tu na hawa hawaachi kamwe labda uwachinje au uwakate midomo.

Niliona Docomentary moja Ulaya kwa sababu hawaruhusu kukata kuku midomo sasa wana develop breed ambayo haina tabia za kulana
 
Umesahau pia tabia, kuna wengine unakuta ni genetic zao tu na hawa hawaachi kamwe labda uwachinje au uwakate midomo.

Niliona Docomentary moja Ulaya kwa sababu hawaruhusu kukata kuku midomo sasa wana develop breed ambayo haina ya
Mchango mzuri
 
Ungeweka pia formula ya mchanganyo wa chakula Cha kuku ingekuwa vizuri zaid.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom