SoC01 Je, umejiandaa na mabadiliko ya mfumo wa fedha?

Stories of Change - 2021 Competition

Tyler Durden

Member
Aug 5, 2021
73
114
Katika hatua za mwanzo kabisa za Maisha ya mwanadamu hakukuwepo na kitu kinaitwa Pesa. Njia pekee ya kununua na kuuza ilikuwa ni kupitia mabadilishano. Unahitaji ngombe wangu unanipa gunia kadhaa za mahindi. Tumemalizana, kitaalamu iliitwa Barter Trade).

Mfumo huu ulikuwa na mapungufu mengi, mfano, nipo tayari kukupa ngombe lakini sihitaji mahindi, nahitaji viazi na wewe huna viazi mwisho wa siku biashara haifanyiki.. hapa ndipo zikaibuka sarafu. Kwa kuwa zilikuwa zikitengenezwa na madini yenye thamani kama dhahabu na fedha, kila mtu alizikubali kama njia ya malipo kwa sababu zilikuwa na thamani fulani. Hiki ndio ilisababisha pesa ya Uingereza iitwe pauni, kwa sababu pauni yao moja ilikuwa ni madini ya fesdha yenye uzito wa pauni moja.

Changamoto ya kusafiri na madini yenye thamani kubwa ikapelekea kuundwa benki, kwa ajili ya kuhifadhi dhahabu na fedha, kisha wanakuandikia karatasi yenye maelezo kuwa una kiasi flani cha dhahabu au fedha kisha unakwenda kufanya biashara na hiyo karatasi. Hivyo ndivyo pesa ya karatasi au noti ilivyoibuka.
1628741726018.png

Baada ya matumizi ya muda mrefu ya pesa ya karatasi (noti), teknolojia ya intaneti ikasaidia kuibuka na kuanza kwa matumizi ya pesa ya kielectroniki, Pesa isiyoshikika, unanunua na kulipia huduma kwa kutumia kadi au simu yako ya mkononi. Katika hatua hii huioni wala kuishika pesa yako. Mfumo unacheza na namba tu kuzipunguza au kuziongeza katika leja za benki kadiri unavyofanya miamala.

Mnamo mwaka 2008 miezi michache baada ya anguko la uchumi wa dunia, tuliingia katika mageuzi mengine ya mfumo wa pesa. Pesa huru ya kidijitali isiyochapwa kwenye noti wala sarafu na isiyomilikiwa na mtu au taasisi yeyote.

Chapisho maarufu lilichapwa mtandaoni na mtu aliyejiita Satoshi Nakamoto (haijulikani kama ni mtu mmoja au kikundi cha watu hakujiweka wazi) . Katika chapisho hilo Satoshi alieleza nia yake ya kuanzisha mfumo wa fedha huru ya kidijitali (cryptocurrency) itayokuwa mbadala wa pesa ya sasa. Mnamo mwezi januari mwaka 2009 satoshi alitengeneza sarafu 50 katika mfumo wa blockchain na kuzipa jina Bitcoin. Baada ya mageuzi haya ya pesa zimeundwa sarafu nyingine nyingi za kidigitali Zaidi ya 4000. Nyingi zinafuata mfumo wa satosho Nakamoto, mfano , Litecoin,Dogecoin,Cardano, na nyingine kama Ethereum(ether).
1628741288247.png


Sarafu za kidigitali (cryptocurrency) ni nini.

Cryptocurrency (Kriptokarensi) ni pesa ya kidigitali iliyo katika mfumo wa mtandao kwa asilimia mia moja, haichapwi kwenye karatasi au sarafu.

Pesa hizi huitwa cryptocurrency kwa sababu zinatumia mfumo wa kimahesabu wa cryptography (kriptografi)au cryptology katika matumizi yake.

Cryptography ni mfumo wa kulinda mawasiliano mtandaoni kutoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine. Mfumo huu huficha ujumbe unaotumwa kwa kodi za siri ili tu yule mlengwa wa mawasiliano husika aweze kuuchakata na kuusoma.

Katika matumizi ya cryptocurrency kila mtumiaji anakuwa na anuani mbili ( public key na private key). Atakazotumia katika (pochi mtandao, crypto wallet). Haya yote yanafanyika katika programu ya Blockchain.

Public key ni anuani ya wazi (kama vile barua pepe) ambayo hutumika kutumiwa pesa. Private key ni anuani au namba ya siri ambayo hutumika kuruhusu matumizi ya sarafu zako. Na kuficha na kufichua muamala uliotumwa. Katika matumizi ya cryptocurrency data zote kama vile ujumbe wa muamala, hufichwa katika mfumo wa namba na herufi ambazo mlengwa hutumia alama yake ya siri kuzitafsiri kuja katika ujumbe wa awali. Zoezi hili huitwa hashing au hash system (mfumo wa hash).
1628741331818.png


Mfumo wa Blockchain

Sarafu za kidigitali hufanya kazi chini ya mfumo wa kutuma taarifa wa Blockchain. Blockchain ni teknolojia ya kuhifadhi taarifa zinazofuatana (mnyororo wa data). Tofauti ya mfumo huu na mifumo mingine ya kuhifadhi taarifa , Block chain hukusanya taarifa kwa Pamoja katika makundi yanayoitwa blocks. Bloku moja huhifadhi miamala hadi kufikia 1609. Taarifa hizi huhifadhiwa katika seva za compyuta za watumiaji wake. Mfumo huu Hauna kituo kimoja cha kuhifadhi data kama mifumo mingine ya uhifadhi wa taarifa. Data zote huifadhiwa katika kila kompyuta ya mtumiaji wa mfumo huu. Blackchain huwezesha teknolojia ya kriptocurrency kufanya kazi kwa kuhifadhi taarifa za miamala na fedha kwa mtindo wa blocku katika leja zake.

Kila muamala unaofanyika hurekodiwa katika kila compyuta iliyojiunga na mfumo wa blochain na cryptocurrency duniani. Unapofanya muamala wa pili, taarifa ya muamala wa kwanza hurekodiwa katika bloku ya muamala wa pili na apo ndipo tunapata mnyororo wa taarifa. Mfumo huu hauwezi kudukuliwa kwa sababu itambidi mdukuzi kubadilisha taarrifa za kila bloku zenye mahusiano kwenye kila compyuta duniani ili aweze kuiba pesa.
1628741374674.png



Mfumo huu huondoa pia tatizo la double spending( kutumia zaidi ya ulichonacho). Mfumo wa kawaida ambao benki husimamia pesa, huwezi kutumia zaidi ya ulichonacho kwa sababu benki zinafuatilia taarifa zako katika vitabu vyao vya leja na kukuzuia sababu ikiwa huna salio. Katika crypto currency taarifa zako zinatakiwa kudhibitishwa na watumiaji wenzio kwenye kila compyuta duniani kuwa unakiasi fulani kinachokuwezesha kufanya miamamla na happo ndipo mfumo unakuruhusu. Katika mfumo huu wasimamizi ni nyinyi wenyewe.

Mkoba wa kidijitali (Digital wallets)

Ndani ya mfumo huu wa Blockchain pesa zako zinakuwa ndania ya kitu kinaitwa mkebe au pochi ya kidijitali (Digital wallet). Hii ni njia inayokuwezesha kuhifadhi kikamilifu taarifa za ndani. Kama vile kiasi cha pesa ulichonacho, namba yako ya siri yenye nguvu, taarifa za malipo, n.k. mkoba wa kdijitali hutumika kusaini muamala, kudhibita kiasi katika account na kutuma kwenye mfumo wa blockchain.

Mikoba ya kidigitali imegawanyika mara mbili, kuna ,Hot wallet( mkoba moto) na cold wallet (mkoba baridi).

Mkoba moto ununganishwa na intanet, utahitaji huduma ya intaneti ili kuweza kufungua mkoba wako na kuweka namba za siri tayari kwa matumizi, hii haipo salama sana hasa kwa wadukuzi.
1628741414255.png


Cold wallet au mkebe baridi, huu ni mfumo unaohifadhi pesa zako na namba ya siri kwenye kifaa maalumu kisichohitaji intaneti ili kuziona pesa zako .kifaa hichi kinakuwa nje ya kompyuta yako, kinaweza kasaidia ulinzi zaidi kwa kuweka namba ya siri ya ziada.

Unapotaka Kutumia cold wallet unaunganisha na kompyuta yako kwa kutumia program maalumu. Kifaa hichi huruhusu taarifa maalumu kuhama na kinasaini chenyewe miamala inayofanyika na kuirekodi.

Uchimbaji wa sarafu (cryptocurrency Mining)

Uchimbaji au uvunaji wa sarafu, ni njia ya kujipatia sarafu za kidijitali kwa kutumia compyuta maalumu zenye nguvu ya kukokotoa , kuthibitisha uhalali, na kusasisha taarifa za watumiaji katika mfumo wa Blockchain.

Mbali na kununua sarafu za kidijitali kutoka kwa mtu anayezimiliki, uvunaji ndiyo njia nyingine inayotumika kupata sarafu mpya katika mzunguko
1628741470189.png


Kompyuta zinazotumika kuchimba sarafu hizi hutumia mpaka dakika kumi kunyambua mabilioni ya namba ili kuhakikisha uhalali wa hash liyotumwa katika miamala inayofanika, kabla ya kuiunganisha katika bloku. Kompyuta inayofanikiwa kukisia na kukamilisha bloku moja kwa mapema Zaidi huzawadiwa sarafu na mfumo. Mfano bitcoin ilipokuwa inaanza mchimbaji alikuwa anazawadiwa sarafu 50 kwa kila bloku, Sarafu hizi hupungua kwa nusu idadi kila baada ya bloku 210000 ambazo huchukua wastani wa miaka 4 kukamilika.

Kwa sasa mfumo hutoa coin 6.3 kwa kila bloku, itafuata 3, halafu 1.5 kwa mwendo huu inakadiriwa bitcoin ya mwisho itavunwa mwaka 2140. Kutokana na idadsi ya wachimbaji kuwa wengi shughuli hii imekuwa ngumu na ili kufanikiwa inahitajika mamia ya computer maalumu zenye nguvu sana, kadi za graphics, na umeme wa kiwango cha juu sana kwani compyuta hufanya kazi kwa masaa 24.

Masoko ya sarafu za kidijitali

Ili kuweza kununua na kuuza pesa zako za kidijitali, unahitaji masoko ya matandao,ili kukutana na watu wengine, masoko haya hufanya kazi sawa na masoko ya kuuza na kununua hisa au masoko ya kubadilisha fedha

Masoko haya yanakupa uwezo wa kujisajili na kununua au kuuza pesa zako chini ya ulinzi mzuri na ada kidogo. Masoko mazuri ni Pamoja na Coinbase ambayo ni rahisi kutumiana, Cashapp, Binance Pamoja n

Hizi ni baadhi ya sababu zinazofanya pesa za kidijitali kuwa na thamani.

  • Uchache(scarcity)…Satoshi alipounda bitcoins aliweka protokali kuwepo sarafu milioni 21 pekee. Uchache wa sarafu hizi unatengeneza uhitaji zaidi, mfano jinsi madini ya almasi yalivyo kwa uchache ndivyo yalivyo na thamani zaidi, sarafu nyingine zinapanda thamani kidogo sana kutokana na wingi wake, mfano Dogecoin zipo zaidi bilioni 129 katika mzunguko na hakuna kikomo katika uchimbaji.
  • Mgawanyiko (divisibility)….bitcoin inagawanyika mpaka nukta nane za desimali, hii inamaana unaweza kumiliki bitcoin 0.00000001 na bado ikawa na thamani Fulani, mgawanyiko huu ni zaidi hata ya dola za kimarekani.
  • Matumizi (Utility)….hasa katika mfumo wake wa blockchain, ambao haujakipa chombo chochote mamlaka ya kubadili chochote. Imani pekee ni baina ya watumiaji
  • Usafirishaji (Transportability)…. Bitcoin haina mipaka, unatuma na kupoke popote, ulimwenguni, Hauhitaji western union wala benki , kumtumia mtu bitcoin. Unaweza kutuma muda wowote na kwa haraka kuliko pesa za kawaida.
  • Kudumu (Durability)….pesa za kawaida zina changamoto katika kudumu, kuchanika, kuungua, na pia kutokuwa na thamani hasa hasa noti za zamani ikiwa noti mpya zimechapwa. Bitcoin haiwezi kuharibika, inadumu milele.
  • Ubandia(counterfeitability)….kutokana na jinsi ilivyotengenezwa huwezi kuwa na Bitcoin bandia, kudukua au kutumia zaidi ya mara moja.
  • Pamoja na mazuri haya bado pesa hizi zinachangamoto nyingi kama vile kupoteza pesa zako ikiwa umepoteza namba za siri. Mfano bwana James howels,35, raia wa Uingereza alijisahau na kutupa hard drive wallet kwenye pipa la taka yenye bitcoin 7500 ndani yake.
  • Pia baadhi ya serikali zimekuwa zikipinga vikali sarafu hizi baada ya kuziona kama tishio dhidi ya mfumo uliopo.
  • Yote kwa yote ni muhimu kuendelea kujifunza katika teknolojia hii itakayotupatia uhuru na kutuondoa katika unyonyaji uliopo kwenye mfumo wa sasa ikiwamo makato makubwa.
  • Karibu kwa maoni,ziada,mjadala na maswali. Hakika yajayo yanafurahisha.
 
Kuna habari inatrend kuhusu some hacker aliyeiba $600m kwenye binancechain...lakini baadae wakarudisha....nahisi labda kutokana na kutangazwa kublock all transaction zinazofika za hizo stolen coins....we still have a lot to learn but i still believe cryptocurrency is the future money....
 
Nice topic mkuu, lakini nahisi inahitaji umakini sana, small minds kama Becky hapa sijui kama tutaweza ku keep up na pace,lol nimekupa kura though
 
Nasikia kwa tafsiri rasmi ya Japanese to English satoshi nakamoto means central Intelligence (C.IA)
kwahiyo akili kumkichwa

Us amegundua huu mfumo wake wa SWIFT uko ukingoni hivyo ameunda mfumo mbadala ambao ndio hii bitcoin

Ni suala la wakati tu lakini bitcoin inakwenda kutumiwa kama reserve currency kwa dunia nzima kitu kitakachoifanya thamani yake kuwa nene sana kama sio kubwa sana
 
Nasikia kwa tafsiri rasmi ya Japanese to English satoshi nakamoto means central Intelligence (C.IA)
kwahiyo akili kumkichwa

Us amegundua huu mfumo wake wa SWIFT uko ukingoni hivyo ameunda mfumo mbadala ambao ndio hii bitcoin

Ni suala la wakati tu lakini bitcoin inakwenda kutumiwa kama reserve currency kwa dunia nzima kitu kitakachoifanya thamani yake kuwa nene sana kama sio kubwa sana
Inawezekana ....hatuna budi kwenda Na upepo....naona kwa Tanzania watu bado watu hawafuatilii sana hii kitu..
 
Yaan mtanzania kufanya biashara ya mtandaoni . Ni vigumu Sana maana hatujaielewa kabisa .
Hivi ni kama QNET ? .maana qnet nao wanafanya biashara ya fedha mtandaoni .

Wew jamaa una akili sn kwa Uzi huu 100%
 
Yaan mtanzania kufanya biashara ya mtandaoni . Ni vigumu Sana maana hatujaielewa kabisa .
Hivi ni kama QNET ? .maana qnet nao wanafanya biashara ya fedha mtandaoni .

Wew jamaa una akili sn kwa Uzi huu 100%
Hii sio kama qnet...haihusishi bidhaa....hii Ni aina mpya ya pesa ya dunia iliyo katika mfumo wa mtandao. Inahitaji kutuliza akili uweze kuielewa Na haikwepeki
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom