Je! umaskini unasababishwa na nini?

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,891
1,190
Unategemea sisi tutafahamu chanzo cha umaskini wakati JK mkuu wa kaya yetu alishasema hajui kwa nini nchi ni maskini?
 
Natalie

Senior Member
Sep 25, 2011
165
27
Hii nchi isingekuwa masikini kama kila kitu kingeenda inavyotakiwa, angalau mambo yangefuatwa kwa makini hata kwa asilimia 80 tu, tungekuwa mbali, mfano, sheria za nchi zingefuatwa na kuheshimiwa vizuri, yaani sheria ingekuwa msumeno kiukweli, kivitendo si kimaneno, yaani no one should be above the Law, sasa inashangaza wengine wanapovunja hizi sheria wanakingwa na uheshimiwa wao wakati ni wakosefu wakubwa kuliko hata majambazi wanaokamatwa na polisi kila siku, wanatumia pesa za maendeleo ya nchi kwa matumizi yao ya nyumbani na familia zao, wanatumia ofisi za serikali kama maduka yao ya biashara, yaani wanakera, walalahoi wanalipa kodi kwa manufaa ya Taifa, wao wanachukua hizo pesa kwenda kujengea mahoteli, nyumba zao, kununua fanicha zao, kusomesha watoto wao nje ya nchi, kujirusha na mahawara zao n.k, wamewakabidhi wageni madini, wanachimba kama yao, wamewalegezea sheria za kuwabana ili waweze kuwacontrol inavyotakiwa, wanachimba madini mengi na kutoa gharama ndogo kwa nchi, na vigogo wengine nchini wanaiba hiyo pesa ya madini, nilishangaa kusikia kuwa nchi zinazoongoza kwa kusafirisha Tanzanite duniani ni kenya na afrika kusini, tabia gani hii, eti twiga wakaibiwa arusha, wameibiwa au waliwapa kwa kupewa kitu kidogo, si vichekesho, bora wangekuwa wanyama wadogo kama nyoka, ingeleta maana zaidi, na hii elimu yetu ya bora elimu, badala ya elimu bora!, wahitimu wengi, wahitimu cheti, hawana uwezo wa kufanya kazi walizosomea, kila kitu kimekuwa bora liende, hakuna walimu bora, viongozi bora wala barabara bora, wanaingia kwenye uongozi kwa faida zao na familia zao, ili wachakachue kodi za wananchi na rasilimali za nchi kwa manufaa yao binafsi bila kujali maendeleo ya kweli ya nchi, yaani inakera kweli, sijui lini watabadilika kuwa viongozi wazuri kwa kupunguza ubinafsi wao kama si kuuacha kabisa, ili angalau wananchi waishi kwa raha, waache kushabikia siasa hovyo kwa faida zao binafsi bila kujali wananchi, wawajali wananchi na taifa kwa ujumla, miaka 50 ya uhuru bado tunachechemea, embu tuige mifano kutoka kwenye baadhi ya nchi za Asia bwana!.
 
Arkad

Member
Jan 16, 2011
25
9
Nini chanzo cha mtu kuitwa maskini? afanye nini kutoka katika hali hiyo?

Umasikini unasababishwa na fikra mbaya zisizohamsha maaendeleo au kufikiri A na kutenda Z. Mtu anaitwa masikini pale anapoishi chini ya $ 1 kwa siku kwa nchi kama Tanzania .

Mtu anatakiwa kujikomboa kupitia elimu yaani sio lazima aende shule anaweza kujifundisha mwenyewe mambo kadhaa kisha kuyatumia mambo hayo kuondoka katika kundi la masikini.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,743
74,365
Inategemea na ulipo, hata kwa kuonewa huruma tu unaweza ukaitwa maskini.

Nilibahatika kufika Saudi Arabia zamani sana (waliofika watathibitisha hili), nikakuta kina mama wanaomba omba huku wamevaa dhahabu kwa kiwango chetu huku ni mtu tajiri ndio anaweza akavaa dhahabu za kiwango hicho.
 
VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,201
1,330
Inategemea na ulipo, hata kwa kuonewa huruma tu unaweza ukaitwa maskini.

Nilibahatika kufika Saudi Arabia zamani sana (waliofika watathibitisha hili), nikakuta kina mama wanaomba omba huku wamevaa dhahabu kwa kiwango chetu huku ni mtu tajiri ndio anaweza akavaa dhahabu za kiwango hicho.

Nadhani kuitwa masikini haimaanishi kwamba wewe ni maskini (wala kuwa omba omba hii ni tabia wala haimaanishi wewe ni maskini)

Sasa hao kina mama wanaleta utani kwanini wasiuze hizo dhahabu na walizipata wapi hizo dhahabu..., ikiwa mtu anapata basic needs basi huyo sio maskini

na utajiri (Wealthy) ni pale mtu ambapo Income = Expenditures + Savings...; hivyo basi kama mimi na matumizi yangu na shida zangu zote na kujirusha kwangu naweza kutumia pesa na zikabaki nikaweza kupata savings basi mimi sio maskini; ila kama napata mshahara wangu tarehe 30 lakini tarehe 5 umeshakwisha.., basi mimi ni maskini hata kama kipato changu milioni tano, tofauti na yule ambae anapata laki moja lakini anapeleka watoto wake shule anakula vizuri na kubaki na tu-savings twake
 
Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,810
3,178
Nini chanzo cha mtu kuitwa maskini? afanye nini kutoka katika hali hiyo?

1........Mahitaji muhimu matatu ya binadamu ni malazi (safe housing), mavazi (kuweza kustahimili hali ya mazingira yako) na uhakika chakula. Going without any of those three basic needs your bound to suffer and that constitutes the true meaning of poverty or absolute poverty.

2.....Dunia ya leo kuna man made definitions of poverty depending on what society you happen to live in, the measurement of this new definition is based on materials especially in societies which are rich. Since these societies can provide the three most basic needs to its people the question of poverty shifts on how comfortable people are in society and what sort of life goods are people consuming. Therefore households are expected to have certain gadgets, be able to afford certain social expenditures (such as holidays) and the type of diet one consumes. They refer to this measurement as 'relative poverty' and is purely based on income gaps (class), life chances one is born with and what politics can do to improve the situation of those at the bottom. In fact the main theme in western politics (especially home politics) is centred round these arguments.
 
AMINATA 9

JF-Expert Member
Aug 6, 2011
2,128
640
Nini chanzo cha mtu kuitwa maskini? afanye nini kutoka katika hali hiyo?
chanzo cha mtu kuitwa maskini ni mtu mwenyewe kutojitambua yy ni nani na haki zake nini?????????(haki nnikimaanisha haki ya elimu,afya bora,maisha bora na mazingira bora,kupinga maovu)na kujipigania kujikomboa)
ila akijua hayo yote anaondokana na umaskini fasta mbona
 
Roulette

JF-Expert Member
Dec 15, 2010
5,592
5,337
kama anavosema AMINATA umasikini unaanzia kichwani. Wamasikini wote wanafikiria wako masikini, na wataendelea kua hivo. Ila akianza kukataa hiyo hali na kupiganisha tayari ameanza msafara wa kujiokoa.
Kwa kujitoa lazima awe na destination, what I call a vision. Anataka kwenda wapi, ni hali gani anaona sio umasikini kwake? then apange muda wa kufikia lengo hilo, huku akiweka objectives fupi fupi kati kati:
ex: anataka kufungua duka:
objective 1. ajifunze duka linatumika vipi,
2. ajifunze anahitaji pesa ngapi na institutions gani zinaweza kumpa hizo pesa au kazi gani anaweza kufanya, kwa muda gani, kupata hizo pesa.
3. Atafute eneo nzuri (hata kabla hajapata hela) na asema ningependa duka langu liwe hapa. aulize wanakodisha au wanauzaje.
4. aanze kuandika ma barua za kutafuta kazi au za kukopa hela. etc.
Katika hatua zote hizo anaendelea kukeep final destination kwa akili na kama anatakiwa kuvuta objective moja au kuireplace na nyingine it is fine tu, muhimu ni kufika anakoenda.
Asichoke na asiwe disapointed kama hafikii lengo lake katika wakati alijipangia, anaweza kufanya extention sababu so long as anaenda mbele, anazidi kuweka distance kati yake na hali ya umasikini
 
Kwani huyu jamaa katakajua maana ya umaskini au jinsi ya kujiendeleza maana mi hata sielewei haya mambo ya maduka na mikopo yanahusiana vipi kwenye tafsiri ya umaskini anyway nauliza tu.
 
The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
44,219
91,808
umasikini wa nchi hii unasababishwa zaidi na kununua bidhaa nje badala ya kutengeneza wemyewe

nguo,mafagio,mikeka,peni,masufuria na vingine viingi vinaagizwa kutoka nje....

ni sawa wewe na familia yako muwe kila kitu mnanunua,
chakula mnanunua from restaurant,kufagia mnaita watu kutoka nje....lazima muwe malofa
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,743
74,365
Nadhani kuitwa masikini haimaanishi kwamba wewe ni maskini (wala kuwa omba omba hii ni tabia wala haimaanishi wewe ni maskini)

Sasa hao kina mama wanaleta utani kwanini wasiuze hizo dhahabu na walizipata wapi hizo dhahabu..., ikiwa mtu anapata basic needs basi huyo sio maskini

na utajiri (Wealthy) ni pale mtu ambapo Income = Expenditures + Savings...; hivyo basi kama mimi na matumizi yangu na shida zangu zote na kujirusha kwangu naweza kutumia pesa na zikabaki nikaweza kupata savings basi mimi sio maskini; ila kama napata mshahara wangu tarehe 30 lakini tarehe 5 umeshakwisha.., basi mimi ni maskini hata kama kipato changu milioni tano, tofauti na yule ambae anapata laki moja lakini anapeleka watoto wake shule anakula vizuri na kubaki na tu-savings twake

Mimi nimejibu swali la "chanzo cha mtu kuitwa maskini" na si lazima awe fukara, kumbuka umaskini na ufukara ni vitu tofauti, unaweza kuwa na mali lakini huwezi kujisaidia kwa mali yako, kwa hiyo wewe ni maskini na wakuonewa huruma. Ufukara ni kitu kingine, sasa kama mnatalka tuibadili mada haya, na ndio maana nikatowa mfano wa niliouona Saudia. Ufukara ni kitu kingine, mfano mzuri ni Tanzania, tunaitwa nchi maskini, lakini tuna mali za kutosha, kwa nini? ni wakuonewa huruma umaskini wetu, kwa ujinga wetu, lakini si wakukosa mali na rasilmali.
 
Kanyigo

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
1,028
188
race,color n,k na mwambao unako ishi..kwa mfano katika Africa nchi nyingi ni masikini sana isipokua zile zenye watu weupe ka Afrika kusini,misri n.k na kule marekani wamarekani weusi ni maskini sana wakati huohuo wamarekani weupe ni matajiri.kwahiyo black ni cursed race..
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,743
74,365
1........Mahitaji muhimu matatu ya binadamu ni malazi (safe housing), mavazi (kuweza kustahimili hali ya mazingira yako) na uhakika chakula. Going without any of those three basic needs your bound to suffer and that constitutes the true meaning of poverty or absolute poverty.

2.....Dunia ya leo kuna man made definitions of poverty depending on what society you happen to live in, the measurement of this new definition is based on materials especially in societies which are rich. Since these societies can provide the three most basic needs to its people the question of poverty shifts on how comfortable people are in society and what sort of life goods are people consuming. Therefore households are expected to have certain gadgets, be able to afford certain social expenditures (such as holidays) and the type of diet one consumes. They refer to this measurement as 'relative poverty' and is purely based on income gaps (class), life chances one is born with and what politics can do to improve the situation of those at the bottom. In fact the main theme in western politics (especially home politics) is centred round these arguments.

Nadhani swali haliulizi umaskini ni nini, swali linauliza "umaskini unasababishwa na nini".

Nnavyosema mimi ni kuwa unaweza kuwa na mali lakini bado ukawa maskini. Umaskini na kuitwa maskini inategemea ni wapi ulipo na si nini (materially) ulicho nacho au kutokuwa nacho.

Ufukara ndio kutokuwa nacho (materially) na ufukara si umaskini. Unaweza kuwa fukara lakini usiwe maskini, na unaweza kuwa maskini na ukawa fukara au una mali au tajiri, lakini huwezi kuwa fukara na ukawa tajiri au una mali.

Unaweza kuwa tajiri lakini huna macho, hapo una qualify kuwa maskini wa macho. Au huna mguu, au huna akili, au huna mume, au huna mtoto, au huna baba au huna mama.

Nadhani tumeelewana, kama tulivyo: Tanzania ni maskini lakini si kuwa hatuna mali au rasilmali, tu maskini kwa kuwa ni wajinga, na ndio maana tuna qualify (generally) kuitwa maskini. Na kati yetu wako mafukara na wako matajiri.
 
FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
73,743
74,365
race,color n,k na mwambao unako ishi..kwa mfano katika Africa nchi nyingi ni masikini sana isipokua zile zenye watu weupe ka Afrika kusini,misri n.k na kule marekani wamarekani weusi ni maskini sana wakati huohuo wamarekani weupe ni matajiri.kwahiyo black ni cursed race..

Kwa nini isiwe reversal? nijuavyo mimi tajiri ndio taabu kuingia peponi, ni mtihani mkubwa sana, nakumbuka kisa kinachosema Tajiri kuingia peponi chance yake ni sawa na Ngamia kupita kwenye tundu ya sindano, sasa hapo nani cursed?
 
Eric Cartman

JF-Expert Member
May 21, 2009
6,810
3,178
Nadhani swali haliulizi umaskini ni nini, swali linauliza "umaskini unasababishwa na nini".

Nnavyosema mimi ni kuwa unaweza kuwa na mali lakini bado ukawa maskini. Umaskini na kuitwa maskini inategemea ni wapi ulipo na si nini (materially) ulicho nacho au kutokuwa nacho.

Ufukara ndio kutokuwa nacho (materially) na ufukara si umaskini. Unaweza kuwa fukara lakini usiwe maskini, na unaweza kuwa maskini na ukawa fukara au una mali au tajiri, lakini huwezi kuwa fukara na ukawa tajiri au una mali.

Unaweza kuwa tajiri lakini huna macho, hapo una qualify kuwa maskini wa macho. Au huna mguu, au huna akili, au huna mume, au huna mtoto, au huna baba au huna mama.

Nadhani tumeelewana, kama tulivyo: Tanzania ni maskini lakini si kuwa hatuna mali au rasilmali, tu maskini kwa kuwa ni wajinga, na ndio maana tuna qualify (generally) kuitwa maskini. Na kati yetu wako mafukara na wako matajiri.

Lets just say poverty is associated with material deprivation and there are two types of poverty absolute and relative. Something tells me tukianza haya mambo yako unayotaka leta ya definition ya ufukara na umaskini tutajikuta tumetoka kwenye point muhumu wakati suala lenyewe lipo based on' want' dont you think so?

Ukitaka hayo ya tafsiri za ufukara na umaskini nadhani umsubiri kiranga huyo jamaa lugha ndio fani yake lakini si 'juma contena' havent you noticed yet.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom