VoiceOfReason
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 5,194
- 1,355
Mimi nimejibu swali la "chanzo cha mtu kuitwa maskini" na si lazima awe fukara, kumbuka umaskini na ufukara ni vitu tofauti, unaweza kuwa na mali lakini huwezi kujisaidia kwa mali yako, kwa hiyo wewe ni maskini na wakuonewa huruma. Ufukara ni kitu kingine, sasa kama mnatalka tuibadili mada haya, na ndio maana nikatowa mfano wa niliouona Saudia. Ufukara ni kitu kingine, mfano mzuri ni Tanzania, tunaitwa nchi maskini, lakini tuna mali za kutosha, kwa nini? ni wakuonewa huruma umaskini wetu, kwa ujinga wetu, lakini si wakukosa mali na rasilmali.
Twende pole pole kidogo ndugu yangu hao kina mama wanaovaa gold kwanini wanaomba hawawezi kupata chakula, kazi au hawawezi kufanya kazi...? na kwa definition ya kwamba unaweza ukawa ni maskini wa macho, mume, mtoto akili n.k. (basi tunaweza tukasema kila binadamu ni maskini sababu hakuna mtu ambae ana kila kitu..)
kwahiyo ili twende vizuri naomba kwanza tu-dadavue maana ya ufukara na umaskini.... (definition..) alafu uniambie kwanini wale mama wa Kule Saudia ni maskini..?