Mongoiwe
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 524
- 263
Takwimu zinaonyesha kuwa kina cha maji cha ziwa kilishukwa kwa kasi katika kipindi cha kati ya miaka ya 2000 na 2006 na kusababisha madhara makubwa ya kiuchumi na kimazingira kwa maeneo yaliyomo kwenye Bonde la Ziwa hilo.
Mwaka 2000 kina cha maji kilipungua kwa takribani mita 1.6- kufikisha kiwango cha mita 1,133.26 kutoka usawa wa bahari. Mwaka 2006 kiwango ambacho kinaelezwa kukikaribia sana kile cha chini zaidi kilichorekodiwa Machi mwaka 1923.
Nimesikia mara kadhaa kuwa moja kati ya sababu za kupungua kwa kina cha maji ndani ya ziwa Victoria kinatokana na serikali ya Uganda kuanzisha ufuaje wa umeme kwenye Bwawa la Owen lililopo juu ya mto Nile.
a). Je, ni kweli Uganda inatumia maji toka ziwa Victoria kwa ajili ya Umeme.
b). Kama ni kweli mbona nimesikia kuwa kuna sheria (Misri) inayolinda na kuzuia utumiaji wa maji ya ziwa Victoria?
Nawasilisha.