Je, Tungekuchagua Uwe Kiongozi Mkuu wa Nchi Ungefanya Nini Mwaka wa Kwanza?

Kama ningekuwa na bunge ambalo asilimia tisini ni wabunge wa chama changu, ningelivunja siku ya pili baada ya kuapishwa na kutaka nusu ya majimbo yote chama changu hakitasimamisha mgombea! Tunafanya uchaguzi mkuu mpya ili hatimaye tuwe na Bunge ambalo linaweza kusababisha yote yaliyopendekezwa humu kutekelezwa.

Wakati bunge linafanya mambo hayo mimi nitakaa tayari kutia sahihi miswada yote ya sheria zenye maslahi ya nchi.

Lakini la pili nitamtimua Mtanzania yeyote ambate atatumia neno "Hatuwezi" au "haiwezekani". Wale watakaotumia neno "ni vigumu" tutawatafutia kisiwa ambacho watafungwa hadi fikra zao zibadilike na kuanza kutafuta msamiati mwingine..msamiati ambao hauusiani na kushindwa au kutoweza au kuwa duni!

Wakati hawa wanahangaika nitafungua gereza jipya pembezoni ya mapango ya Amboni ambako Marais wa zamani, mawaziri na watumishi wa umma waliokutwa na hatia za ufisadi watatumikia kifungo chao. Gereza hilo kazi yake kubwa ya uzalishaji itakuwa kutoa maelezo ya kwanini wasitolewe kifungoni!

Mkuu umenichekesha sana. Ila naomba ufahamu tu kwamba, ukilivunja Bunge, Katiba inakufuta uRais hapohapo na uchaguzi mpya unaitishwa. Kwa mantiki hiyo, hautakuwa na nguvu za kufanya maamuzi hayo, maana nani atakaejua kama utashinda tena? [media]https://www.jamiiforums.com/images/icons/icon10.gif[/media]
 
Mkuu umenichekesha sana. Ila naomba ufahamu tu kwamba, ukilivunja Bunge, Katiba inakufuta uRais hapohapo na uchaguzi mpya unaitishwa. Kwa mantiki hiyo, hautakuwa na nguvu za kufanya maamuzi hayo, maana nani atakaejua kama utashinda tena? [media]https://www.jamiiforums.com/images/icons/icon10.gif[/media]

hiyo ndiyo maana; kwa sababu nitakuwa bado Mwenyekiti wa Chama ama?
 
Wachangiaji,
Katika nililoandika nilisahau jambo moja kubwa sana ambalo litasaidia kupunguza matumizi. Wabunge watatoka kila wilaya. Hamna ya wilaya kuigawa katika majimbo mawili ili kuleta ulaji na mwisho wake wabunge wanakuja kuishi Dar au Dodoma. Wabunge wote watakwenda kuishi na kufanya kazi majimboni mwao. Haya ya wabunge wanaishi Dar ni upuuzi wa hali ya juu. Pia kuondoa sijui Mkuu wa Wilaya, Rais wa wilaya, Mwenyekiti wa Wilaya, Mkurugenzi wa wilaya, ........ Mbunge, hivi hawa wote wanahitajika? Mwisho wanaanza kugombana maana haijulikani hata mipaka ya kazi ikoje.
Mawaziri wote watachaguliwa NJE YA BUNGE na hawa hawatakuwa WABUNGE.
Mishahara ya WABUNGE itapangwa na MAHAKAMA YA KATIBA ikizingatia hali halisi ya Tanzania. Makamu wa Rais kweli anatakiwa kuondolewa na wabaki PM, Spiker kama wasaidizi wa Rais. Mambo yakiwa mazuri, twaweza badili baadaye.
 
ningesimamia ilani ya uchaguzi(ELECTION MANIFESTO) ya chama changu kama kingekuwa kimeshinda kuunda serikali na kama sio ningesimamia ilani ya chama kilicho madarakani.

AM
 
The first 100 days nitaanza na maswala ambayo yanahitaji mabadiliko ya haraka kisheria..
Mambo ya ndani :-

Kwanza bila shaka huwezi kuingia Ikulu kama huna baraza la Mawaziri..
1.Hakuna waziri atakaye kuwa mbunge.. baraza zima litakuwa na watu toka nje ya ya bunge kuondokana na ule mfumo wa kijamaa.. Hivyo kuwafanya wataalam wengi watarudi ktk taaluma zao..Mbunge atabakia kuwa mwanasiasa..Nadhani kipengele hiki Recta kalielezea vizuri zaidi...
2. Wakuu wote wa Mikoa na Wilaya watakuwa watu wanaochaguliwa na wananchi kama vile Wabunge na sio kazi ya rais (Mimi).. Sharti kubwa la kujiandikisha kugombea nafasi za Mkuu wa mkoa au Wilaya ni lazima awe mkazi wa sehemu hiyo sii chini ya miaka 10 akiishi na familia yake au mzawa ambaye bila kujali kabila, chama wala rangi yake maadam kaweza kuwalidhisha wananchi kuwa ni mmoja kati yao...As a matter of fact, ningependa sana kurudisha WATEMI kuwa ndio Governor wa maendeleo ya sehemu hizo..Hii ni kutokana na kuzingatia Watu na mazingira yetu kwani kila mkoa una vipaumbele vyake..
3. Hakuna mbunge wa kuteuliwa ktk bunge la Taifa..
4. Hakuna tena mwakilishi wa chama ndani ya serikali yangu.. huwezi kuwa mwenyekiti wa UWT, Waziri, mbunge na kadhalika..kwanza nitavunja UWT toka chama tawala na kuwa chama cha Wanawake wote Tanzania..Hakuna Taasisi yoyote kusimamia kundi fulani la watu wa chama tawala na kuwaacha wananwake wengine nje. Hivyo hivyo taasisi zote zenye mifano kama hii nitazivunja..Huwezi kuwa na NGO ukasema ni non Giovernment Organisation wakati inamilikiwa na chama tawala...

Policies:-
5. Nitavunja Azimio la Zanzibar na kurudisha miiko na maadili ya Uongozi kama yalivyokuwa wakati wa Azimio la Arusha..
6. UFISADI utafikia kikomo - no more untouchables inapofikia swala la kuhujumu Uchumi...Mali zote za Umma zilizobinafsishwa chini ya Ufisadi zitarudishwa kwa wananchi na kuingia soko letu DSE...
7.. Vipaumbele vya Kiuchumi vitalenga kuongeza ajira nchini ikiwa ni pamoja na malengo ya muda mfupi na yale ya muda mrefu... Ujenzi wa Miundombinu hasa ktk Kilimo, Utalii, na Viwanda utachukua fungu kubwa la bajeti ya serikali..kwa mfano kuongeza mifereji wa kilimo cha umwagiliaji, Ushuru rahisi kwa pembejeo zote za uzalishaji ktk kilimo iwe Ukilima, Uvuvi au Ufugaji..Mashirika ya nje yataruhusiwa kuingia nchini kuwekesha ktk kilimo kwa kutoa mikopo kwa wakulima madogo wadogo kama wanavyofanya Kenya.
8. Marekebisho makubwa kuhusiana na Tax exemptions pia kuimarisha mfumo mzima wa Tax nchini ambao una loopholes kibao ikiwa ni pamoja na maswala ya Upangishaji nyumba, Iwe rent au Lease hizi ni lazima wamiliki walipe tax...
9. Kuundwa kwa serikali tatu - No question, no argument..serikali kuu itashughulika na wizara muhimu tu za jamhuri ya muungano kama vile Immigration, Usalama wa Taifa na kadhalika.

Mambo ya Nje:-

CHAVEZISM...Potelea mbali wakinifungia kama Mugabe, Lakini ikifika maji ya shingo tayari nitakuwa na mtu ambaye atakuwa ametayarishwa - Putin style.
Kutokana na Mapinduzi yangu ya Utaifishaji bandia wa miradi yetu hasa Madini, Mikataba mipya itabidi iandikwe upya baada ya mimi kuondolewa hivyo kwa sababu bado nipo ndani mikataba hii itapitiwa kwa umakini zaidi..
Policy:
We won't be allied to any group of Countries iwe ktk Politics or Economic.. .. rafiki yetu ni yule mwenye kututakia maendeleo sisi na sio kusimamisha Utumwa mamboleo au Uafrika kutupandisha mkenge...Maslahi ya Tanzania mbele ya kila policy..
 
Du, Mkuu Mkandara mbona kama hiyo itachukua 10yrs kuimplement mambo yote hayo ahahahaha
 
-Mwaka wa kwanza ningeliiba na kuhakikisha mimi, mke wangu, wanangu, ndugu zangu na marafiki zangu tunajitajirisha kwa ukucha na jino. Nisingelikuwa na lingine tena la kufanya. Sasa niulize baada ya hapo ningelifanya nini!


-Nisingelikuwa tena na urafiki au undugu na mtu kwenye kazi zangu,
-Ningelitosheka.
-Nisingekuwa mroho na mlafi wa kupindukia kama mafisadi waliofichuliwa na wasiofichuliwa.
-Ningehangaika huku na huko kutatua matatizo yote ya watu kwa ushirikiano nao.
-Nisingelikubali tatizo kuendlea kuwa tatizo kwa zaidi ya mwaka mmoja.
-Ningelikumbatia nchi za mashariki kama China, India, Japani, Korea ya Kusini, Malaysia na kupeleka vijana wetu huku wakiwezesha kwenda kuchota akili za kutengeneza hiki au kile.
-Ningelihakikisha Majeshi yetu yanakuwa kitengo cha Utafiti na Maendeleo cha nchi na kuwawezesha kutengeneza matrekta, mabasi, malori na vitu kama hivyo kama Ivory Coast walivyofanya.
-Ningelihakikisha ni Tanzania na sio Rwanda inayoingilia mambo ya Kongo Demokratiki kwa kupeleka polisi, walimu wa jeshi, walimu wa shule na vyuo, madaktari na kuwasaidia Watanzania wengi kadri iwezekanavyo kuwekeza Kongo.
-Ningelihakikisha ubora wa shule na hospitali hapa nchini unavuta wateja toka kwa majirani zetu wote.
-Ningliwashikia fimbo mameya wa miji na majiji yote wahakikishe miji yao sio tu inakuwa mizuri, safi na yenye usafiri usio na usumbufu lakini pepo hapa duniani kwa wakazi wake na watalii.
-ningelihakikisha kuna mtandao ofisini mwangu unaoniwezesha kujua waziri, katibu mkuu, mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, meya, diwani, mwenyekiti wa kijiji kwa wiki 52 kila wiki anafanya nini kuhakikisha siachi kuchaguliwa tena rais kwa kipindi changu cha pili cha Urahisi wangu!

.....na mengi mengine, ajaribu kwanza huyo atakayekuwa rais, maana mimi siutaki hata mkinipa bure!!!!!
 
Moelex23,
Hapana mkuu wangu ukitazama kwa makini moja hadi saba ni sheria tu..kazi yangu kuanguka dole..8,9 na 10 ndio mimi.. hata hao Mafisadi, Takukuru watapewa baraka zote..
Tena basi mkuu wa Takukuru atakuwa Dr. Slaa akisaidiwa na Mrema!..Usifanye mchezo.
 
Ningekuwa Rais Rev. Kishoka, ningelifanya yafuatayo mwaka wangu wa kwanza

  • Kupunguza ukubwa wa Serikali kwa 25% na kudhibiti (kupunguza) matumizi yake kwa 50%, shughuli za maendeleo kuongezewa fungu kwa 30% Lengo ni kuhakikisha Serikali inapungua kwa 50% ifikapo mwaka wa tatu wa uongozi wangu
  • Kupunguza kwa 50% utegemezi wa misaada ya nje na mikopo katika bajeti yetu na kuendesha nchi yetu
  • Kuhakikisha kuwa mahesabu yote ya Serikali, mashirika na taasisi zote yanahakikiwa na yana maelezo ya kina kwa matumizi yote
  • Kuhakikisha kuwa mapato yote ya Serikali yanakusanywa ipaswavyo na matumizi yake yanafanyika kwa usahihi na kufuatilia kanuni
  • Kuleta mchakato huru wa kuunda katiba mpya ya Jamhuri itakayokuwa huru kwa ajili ya Taifa zima na si kwa Chama kimoja au kikundi fulani
  • Kujenga na kuimarisha kwa uimara misingi ya miundombinu (barabara, reli, maji, umeme, simu, nishati), elimu, afya na usalama wa Raia/Taifa
  • Kuleta na kuhakikisha ufuatiliaji wa Sheria, Kanuni na Katiba kunafuatwa kila ngazi na kila mtu, Utawala bora na haki
  • Kufuta sheria butu ambazo zinakandamiza haki na uhuru wa watu au zinazotoa upendeleo wa makusudi kwa mtu au kikundi fulani
  • Kuchochea ufanisi wa kazi kuanzia Serikalini, Mshirikani, Sekta Binafsi, Mijini na Vijijini. Uadilifu, ubunifu na utunzaji mali utakuwa kipaumbele
  • Kulipa Bunge na Mahakama mamlaka ya muda kabla ya katiba mpya kurudia na kuhakiki mikataba yote iliyoingiwa na Serikali na kufuta au kuvunja mikataba ambayo haina manufaa kwa Taifa
  • Kupitia upya sera ya Uwekezaji kwa kuondoa upendeleo kwa Wawekezaji wa nje au mianya inayowaruhusu kuliibia na kulihujumu Taifa
  • Kutangaza vita dhidi ya dhuluma, hujuma, uzembe ubadhirifu, rushwa, ufisadi na uhalifu
  • Kuunda upya Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, vyombo vya dola vya Upelelezi na Sheria
  • Kuunda sera mpya za Afya, Elimu, Kilimo, MIfugo na Uvuvi, Viwanda, Biashara, Nishati, Madini na Utalii ili kuhakikisha kuwa Taifa linatumia nyenzo zake kikamilifu kujijnga kujitegemea na kuingia ushindani wa kimataifa
  • Kurudisha hadhi ya Tanzania kuwa Taifa huru lenye msimamo huru unaofuata sheria na haki na si kuwa msindikizaji au kuonea soni wavunja haki na utu
  • Kuanzisha kampeni ya kuhakikisha kuwa Tanzania katika miaka 5 ya utawala wangu, inajenga misingi imara ya uchumi, siasa, demokrasia na kijamii ambayo itaifanya Tanzania iwe Taifa linalotegemewa Afrika na Dunia nzima
 
1. Ningehakikisha ninabadili katiba ya OVYO ya Tanzania.
2. Kuondoa wabunge wote wanaokuja kwa dezo. Badala yake kuchagua wabunge wale tu waliobobea kwenye sheria kama akina Shivji.
3. Kuongeza Madaraka ya Waziri mkuu kwa yeye kuunda baraza lake la Mawaziri na si Rais. Hii itasaidia kunipunguzia mzigo wa majukumu na Mawaziri kuwa controlled fully na PM. Mawaziri wawe na heshima kwa PM na si kama sasa, wote wamechaguliwa na Rais (Hata Mataka wa ATCL) sasa utambabaisha nini?
4. Kuupa nguvu USALAMA WA TAIFA na kuupa majukumu zaidi.
5. Kuunda Mahakama ya KATIBA (Tribunal Constitution).
6. Kuongeza marupurupu ya Rais Mstaafu, ila hapohapo kuweka katika katiba kuwa Rais MWIZI basi ashitakiwe kwa wizi wake.
7. Watoto wote wa Mawaziri, wabunge, na vigogo wote wanaoishi kwa nguvu ya kodi za watu, NI MARUFUKU kusoma shule za binafsi ila za serikali. Tutaona kama shule za serikali zitaendelea kuwa mbaya.
8. Kutibiwa ni Rais na PM na mawaziri tu ndiyo waende nje ya nchi. Wengine hawa wanakuwa kwenye msururu unaoongozwa kwa computer.
9. Kuhakikisha Tanzania kwa miaka 40 ijayo, haitakuwa na shida ya UMEME.
10. Kurudisha NYUMBA ZOTE ZA SERIKALI na kuziuza upya kwa mnada kama itaonekana inabidi ziuzwe.
11. Kuipa nguvu Mahakama na wanasheria ili wezi wote wa mali ya UMA, bila ya kujali mwaka, basi wafike sehemu inayostahili. Kama wataweza kurudisha mali walizotuibia basi waachiwe ila milele wasishike post yoyote ya UMA. JKT zote ziwe jela ya makosa mepesi na huko, kifanyike kilimo/ufugaji wa kisasa na hawa jamaa walishe Tanzania nzima.
Wewe unaota au uko serious siku ya pili bunge linapiga kura ya kutokuwa na imani na wewe.
 
1. Ili kuondoa ubabaishaji, rushwa, etc. ningeanzisha utaratibu wa kuvunja vyama vyote vya siasa (including changu), kuanzishwa vipya (vyenye safu mpya ya viongozi na ambavyo havina connection na vya zamani) ndani ya miezi 6 na kuitisha uchanguzi mpya ndani ya miezi 12.
2. Ningeunganisha polisi, takukuru na usalama wa taifa na kuuimarisha idara mpya.
 
Wewe unaota au uko serious siku ya pili bunge linapiga kura ya kutokuwa na imani na wewe.

Hapo ndipo USALAMA WA TAIFA NA JESHI NA POLISI linaanza kazi. Hawa Wapuuzi Wabunge wanaokwenda Dodoma kutesa kwenye mahoteli na minuso hawawezi kumbabaisha Rais. Mkapa aliwapa hela nyingi ili wafumbie maovu yao wanayoyafanya. Hujui madaraka ya Rais wa Tanzania ni makubwa sana? Sasa kitakachonishinda kuwarudi hawa wabunge ni nini? Au wanataka kufanya kazi au waachie ngazi wao.
Kama wanavyopokea hela za EPA, Meremeta nk, ndivyo watakavyopokea maelekezo kutoka usalama wa Taifa kuwa wafanye nini. Atakayepinga basi kesho yuko Mahakamani kwa kuingia bungeni mwaka fulani kwa kutoa hongo au kudanganya sehemu fulani. Ukiwapekua hawa utapata wengi.
Sidhani Wabunge wote hawaitakii MEMA Tanzania yao. Hawa wachache watakaotaka KUFA na wewe itabidi ndiyo iwe ngao yako. Mwisho ni azima ujuwe kuwa haya mambo hayafanywi bila ya maandalizi maalumu. Unajipanga kwanza vyema na ndipo unapoanza kuleta mabadiliko yako. Ukineda kichwa kichwa basi wee hata hufai kuwa Rais. Watusi siku zote wanaanza vita mara wakiwa na uhakika watashinda. Ndiyo maana unaona Uganda walitesa, wakatesa Rwanda, Burundi na sasa Congo. Hii ilifanyika baada ya maandalizi ya kutosha. Njia nyingine ni DEVIDE AND RULE. Hii utawapata wengi tu.
 
U RAISi, Nyerere alijua akasema ukiona mtu anakimbilia pale ikulu basi ujue hajui anachofuata, alisema ikulu ni mahali patakatifu si pa kukimbilia. Hii ni tathmini ya mtu aliyekaa ikulu miaka 24. Hivyo, inabidi kufikiri hasa na pengine kutafuta "ushauri" angalia unaweza jipeleka kwenye mdomo wa mamba~!!!!!!!!!!!!! ukashangaa
 
Uongozi ni kama mchazo wa draft, ukiwa nje unaona makosa lakini ukiingia uwanjani kwasheshe...
 
1. gawa nchi katika kanda, kanda ya kaskazini, kusini, mashariki, magharibi na kati, unganisha mikoa katika kanda husika chini ya utawala mmoja ukiwa chini ya mkuu wa kanda. ila miji ya Dar, Arusha, Mwanza hii haitakuwa ndani ya utawala wa Kanda, hii itakuwa chini ya serikali kuu.

2. zipe kanda uhuru wa kutafuta wawekezaji kutoka nchi mbali mbali duniani katika rasilimali zilizopo katika kanda husika.

3. Anzisha mchakato ili kiongozi wa kanda awe anachaguliwa kwa kura na wananchi, hapa vyama vyote vya siasa vitakavyokidhi masharti vitashiriki uchaguzi.

4. kila kanda itakuwa na baraza lake, mfano baraza la kanda ya mgharibi, mashariki, kati ,etc

5. kisha tutaendelea kuwa na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, hili litakuwa juu ya mabaraza yote ya kikanda, ndilo litakalotoa maamuzi ya mwisho juu ya ishu "contraversial" za kisera katika kanda fulani
 
mwaka wa kwanza nitautumia kuisoma system iliyopo hala mwaka unaofuata ndo nitaanza palizi ili kupata mazao safi.
 
Back
Top Bottom