Je, Tungekuchagua Uwe Kiongozi Mkuu wa Nchi Ungefanya Nini Mwaka wa Kwanza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, Tungekuchagua Uwe Kiongozi Mkuu wa Nchi Ungefanya Nini Mwaka wa Kwanza?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Allien, Jan 13, 2009.

 1. Allien

  Allien JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2009
  Joined: Jul 6, 2008
  Messages: 5,548
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Wana JF;

  Na hasa unayesoma post hii . . . .

  Je, ingetokea ukawa Rais wa Nchi hii, ungefanya nini Mwaka wa Kwanza na kwa nini?
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  1. Ningehakikisha ninabadili katiba ya OVYO ya Tanzania.
  2. Kuondoa wabunge wote wanaokuja kwa dezo. Badala yake kuchagua wabunge wale tu waliobobea kwenye sheria kama akina Shivji.
  3. Kuongeza Madaraka ya Waziri mkuu kwa yeye kuunda baraza lake la Mawaziri na si Rais. Hii itasaidia kunipunguzia mzigo wa majukumu na Mawaziri kuwa controlled fully na PM. Mawaziri wawe na heshima kwa PM na si kama sasa, wote wamechaguliwa na Rais (Hata Mataka wa ATCL) sasa utambabaisha nini?
  4. Kuupa nguvu USALAMA WA TAIFA na kuupa majukumu zaidi.
  5. Kuunda Mahakama ya KATIBA (Tribunal Constitution).
  6. Kuongeza marupurupu ya Rais Mstaafu, ila hapohapo kuweka katika katiba kuwa Rais MWIZI basi ashitakiwe kwa wizi wake.
  7. Watoto wote wa Mawaziri, wabunge, na vigogo wote wanaoishi kwa nguvu ya kodi za watu, NI MARUFUKU kusoma shule za binafsi ila za serikali. Tutaona kama shule za serikali zitaendelea kuwa mbaya.
  8. Kutibiwa ni Rais na PM na mawaziri tu ndiyo waende nje ya nchi. Wengine hawa wanakuwa kwenye msururu unaoongozwa kwa computer.
  9. Kuhakikisha Tanzania kwa miaka 40 ijayo, haitakuwa na shida ya UMEME.
  10. Kurudisha NYUMBA ZOTE ZA SERIKALI na kuziuza upya kwa mnada kama itaonekana inabidi ziuzwe.
  11. Kuipa nguvu Mahakama na wanasheria ili wezi wote wa mali ya UMA, bila ya kujali mwaka, basi wafike sehemu inayostahili. Kama wataweza kurudisha mali walizotuibia basi waachiwe ila milele wasishike post yoyote ya UMA. JKT zote ziwe jela ya makosa mepesi na huko, kifanyike kilimo/ufugaji wa kisasa na hawa jamaa walishe Tanzania nzima.
   
 3. s

  skasuku Senior Member

  #3
  Jan 13, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sikonge: Mbona point 7 na 8 zina ji-contradict?

  Pia sioni sera za Elimu, Afya, Uchumi, Ajira, Miuondombinu... in no particular order. Lakini bila hizi you are setting yourself up for failiure, na isitoshe kupopolewa na wananchi watakao kuchoka hata kabla ya siku 100 za kwanza.
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hapa yaonesha Rais atakuwa mbaguzi wa Haki za binadamu...
   
 5. s

  skasuku Senior Member

  #5
  Jan 13, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pia haimaanishi mtu aliobobea katika fani yake ndio yupo best placed kufamya kazi. Ukiishafikia katika nyadhifa za juu katika siasa, ni vyema mtu akawa msikilizaji mzuri na mtu mwenye good leadership attributes.

  Kuna mifano mingi sana unakuta waliobobea katika fani ndio huwa wana boronga. They believe they know best, na hawasikilizi ushauri.
   
 6. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama ningepata nafasi ya kuwa Rais (sijui ni ndoto ama kitu gani), mambo yafuatayo ningeyafanya mapema iwezekanavyo.
  1. Kuanza mchakato wa kurekebisha/kuunda Katiba ya kitaifa: Kuondoa vipengele vinavyotoa mamlaka makubwa kwa Rais, kuweka misingi ya utawala bora, kuainisha kwa kina mamlaka ya Mwaziri, Wabunge na Wakuu wa mikoa.
  2. Kuhakikisha kila mwananchi anapata kitambulisho cha Uraia: Kila Mtanzania anayo haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake. Kwa kuwa na vitambulisho hivyo, Raia wa Tanzania watatakiwa kuorodheshwa na kumbukumbu zao kutumika katika mambo yote yanayowahusu (shule, afya, Bank, n.k). Kufahamika kwa shughuli na uwezo (skills) wa kila mtanzania itakuwa rahisi zaidi, ili kuweza kutumia rasilimali watu vizuri zaidi.
  3. Kuhakikisha Katiba inamruhusu Rais kuteua Mawaziri bila kujali kuwa ni wabunge au vinginevyo. Kwa kuondoa vipingamizi hivyo, uwigo mpana zaidi wa kiuteuzi utawezekana kuliko ilivyo sasa. Na hivyo kuweka nafasi sawa kwa kila Mtanzania na kuongeza tija kwa viongozi hao.
  4. Kubadilisha vipengele vyote vinavyoruhusu mtu mmoja kushika nafasi nyingi katika Taasisi za uongozi wa nchi. Mathalan; Mbunge asiwe na nafasi ya uongozi katika chama chake au taasisi yoyote ya serikali. Vivyo hivyo, kiongozi katika Chama, asiwe na madaraka katika serikali ama Bunge. Hii itasaidia kutoa nafasi ya wananchi wengi zaidi kushika nyadhfa mbalimbali na kuongeza mawazo mbadala.
  5. Kuhakikisha kunakuwa na mfumo thabiti (system) ya kiutawala na uongozi wa nchi. Kwamba taasisi zote zinategemeana. Hii itasaidia kuongeza usalama wa mali na ufanisi katika shughuli mbalimbali za wananchi.
  6. Kuondoa matumizi makubwa na yasiyo ya lazima kwa serikali. Mfano; magari ya fahari, workshop zisizo za lazima, safari zasizo na tija n.k.
  7. Kuhakikisha kila mwananchi anapata fursa sawa (kama Katiba inavyotaka) ya kupata elimu yoyote anayohitaji kwa kiwango anachokitaka. Serikali itahakikisha kuwa inatoa elimu hadi ya chuo kikuu bure. Hii itasaidia kupata wataalam wa kutosha katika sekta mbalimbali na kuweka usawa wa kupata elimu kwa watu wote bila kujali uwezo wao binafsi.
  8. Kuhakikisha kuwa Serikali inaanzisha na kuendesha viwanda Mama vinavyoweza kuzalisha mbolea, pembejeo, vipuri na zana nyinginezo ambazo sio rahisi na sahihi kutegemea wawekezaji wengine kuvianzisha
  9. Kuhakikisha kuwa kila mtu anafanya kazi na kuondoa wingi/ongezeko la wazururaji mitaani. Hii itahakikisha usalama wa raia, na ongezeko la uzalishaji.
  10. Kuhakikisha kuwa wazee na yatima wanapata mahitaji yao ya lazima kwa kutunzwa na kuendelezwa na mifuko ya serikali (itakayoundwa kwa shuguli hizo)
  11. Kuhakikisha kila mtanzania anapata masaada unaohitajika mahali popote alipo duniani.
  12. Kuhakikisha mahakama na jeshi la Polisi wanapata na kutumia nyenzo za kisasa kushughulikia uhalifu na kesi kwa haraka. ikiwa ni pamoja na motisha ya kufanya kazi kwa bidii
  13. Kuweka kipaumbele kwa Waalimu na Madaktari: Kuhakikisha wanapatikana kwa wingi na wanapata motisha ya kufanyakazi kwa bidii
  14. Kuweka mikakati ya kitaifa ya kupambana na janga la Ukimwi bila kuoneana haya: Mapambano dhidi ya Ukimwi itakuwa ni vita kali ya kitaifa ili kuokoa maisha ya watu na kuepuka na ongezeko la yatima
  15. Kuhakikisha kuwa barabara zetu zinaacha kuwa machinjio ya watu kwa kuweka alama nyingi zaidi, kuzipanua, na kutengenisha barabara ninozo kinzana.
  16. Kuhakikisha kero nyingi zaidi za wananchi zinapata usuluhisho mapema inavyowezekana kwa kuanzisha taasisi ya kuzishughulikia
  17. Kuunda Tume huru za uchaguzi ambazo haziteuliwi na Rais, na zisizo na maslahi yoyote na chama chochote cha siasa.
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  7 na 8 wala haziingiliani. Hii ya 7 ipo katika kuleta ufanisi na sifa kubwa zilizokuwepo miaka hiyooo katika shule za serikali. Ila tangu wenzetu waanze kupeleka watoto wao shule za MATAWI YA JUU, na International school, huko kumebaki kwa walala hoi. Hii kwa misingi hiyo tu. Kama Watanzania wengi watakuwa na hali nzuri kusoma shule za aina tofauti, sioni haja ya kuendeleza hilo. Juu ya namba 8, hii ipo katika kuleta ufanisi katika hospital zetu na hii ikimaanisha AFYA. Mawaziri wakiwa wanatibiwa na wao katika hospital za serikali, sidhani itafika hatua kama mkoa wa Tabora, hospital ya mkoa ina Daktari mmoja Mtanzania. Hivyo, ukiangalia utagundua kuwa hii ipo ili kupeleka sana msukumo katika elimu na afya kwani mawaziri au wao au watoto wao itabidi na wao waende huko.
  Nia ya kumpa PM nguzu zaidi na yeye kuwalinda Mawaziri wake ni katika kuongeza ufanisi. Mie kama Rais, ntahangaika na PM tu na si Mawaziri. Sasa wewe huoni kila wizara itabidi iwajibke zaidi? Leo Kikwete anakuwa Rais, PM, Baba, amiri jeshi, mlezi, Waziri wa mambo ya nje, Waziri wa michezo, mambo ya ndani nk. Anataka kila kitu afanye yeye, wengine wako wapi? Tafadhali soma na tafakali upya maelezo yangu kabla ya kuanza kujibu na kusema itakuwa mweleka. Pia kumbuka imeandikwa kuwa MWAKA WA KWANZA. Haya ndiyo ntakayosukuma yaanzishwe kama msingi wangu. Nafikiri kama haya yakisimama, basi mengine yote yatafuata. Ni kama ule msemo wa "msafara wa Mamba, na Kenge wamo".
   
 8. s

  skasuku Senior Member

  #8
  Jan 13, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sikonge: ulisema I quote "8. Kutibiwa ni Rais na PM na mawaziri tu ndiyo waende nje ya nchi. Wengine hawa wanakuwa kwenye msururu unaoongozwa kwa computer."

  Sasa kama utaweka kuzuizi cha watoto wa viongozi wa serekali kusomeshwa shule za serekali ( point 7) malengo yakiwa kuboresha sekta ya elimu na hasa shule za serekali, je haoni ni sawa kama ukaweka kizuizi cha matibabu nje ya nchi kwa kila mtu.. including you The President? Hivi utaona hayo maendeleo unayoyasema.

  Please check point 8 again.
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Jan 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Heri niwe MVUNJAJI wa HAKI ZA BINADAMU, ila Watanzania wangu wawe na Maisha mazuri. Mwenyekiti wa umoja wa akina MAMA, analetwa kuwa Mbunge, atasaidia vipi Taifa? Hiyo kazi tu mbona kubwa sana? Huu ndiyo upuuzi nisioutaka. Nimesema Wanasheria wawe wabunge/washauri wangu kwani nafikiri linapokuja swala la sheria, Tanzania tuko nyuma sana. Mie siyo mtu wa sheria ila nafikiri huko ndiko mzizi wa fitina kwa Tanzania kalala. Watu wanajivunjia sheria na wala hawaogopi kitu. Ndiyo maana nikasema NITAANZISHA Mahakama ya katiba na usalama wa Taifa uwe na kazi nyingi sana zaidi ya hizi. Kama kuna fisadi, basi tujue mapema. Kama kuna mpango fulani nchi ya jirani unafanya ambao tutaathirika kiuchumi, inabidi na sisi tujue mapema. Ona kama ATCL, kumbe lengo lilikuwa iuzwe, ife na SA air waje wachukue soko la nje na ndani. Hawa UWT walikuwa wapi kujua haya? Kunapoletwa vifaa vibovu na wannachi wanauziwa madawa, TV, Friji nk, wanakuwa wapi? Hapo napo inabidi kwa kuanzia tu pazibwe. Mikataba mibovu ambayo Waziri anaweka sahihi, lazima hawa jamaa wajue kila kitu kinachoendelea na wakiona Waziri anahujumu nchi, basi wanatoa taarifa na hatua kali zinachukuliwa kabla RICHMOND hajaanza kufanya kazi.
  Inawezekana ni mambo 11 tu ila kwangu mie naona ndiyo MSINGI.
   
 10. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nimeangalia na wala silioni tatizo.
  Kwa hali ya hospital ilivyo Tanzania, kuna mambo huwezi yafunga kwa mwaka wa kwanza. Hapo ndipo utaleta kizaa zaa. Nimesema kuwa tunaanza kwa kundi fulani. Ila malengo kwa siku za mbele itakuwa kwamba, ile hospital ya Jeshi pale Lugalo, ndiyo iwe na huduma zote muhimu na hata Rais mwenyewe awe anakwenda kutibiwa pale badala ya nje. Mwisho au lengo hasa linakuwa KUJITEGEMEA. Katika watu ambao inabidi wawe wanatibiwa nje, bila kusubiri msululu ni hao tu (yaani ikibidi kwenda kutubiwa nje badala ya Muhimbili/Lugalo).
  Juu ya elimu, sijui wewe. Ila kama mie mtoto wangu angelikuwa anasoma tuseme Tabora Boys/girls na mie ni Waziri wa Elimu, basi ningelihakikisha wizara yangu inapata pesa za kutosha na hizi pesa zinakwenda mashuleni na huko mashuleni huduma zinakuwepo. Maana kama kila waziri akiwa na mwanae shule tofauti, na huko kuna wadogo zetu, watoto za wajomba nk, na ukiongeza pressure ya PM na mie kama Rais, nafikiri mambo yatakuwa mazuri.
  Kwa ufupi, 7 na 8 ni katika kupunguza kupeleka watu nje ya nchi kwa matibabu / shule hata katika level za chini ya elimu/magonjwa.
   
 11. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #11
  Jan 13, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Sikonge,

  It's the economy, stupid. Hayo mengine yote yatakuja yenyewe. Watu wakiwa na uwezo wa kushiba bila kutegemea serikali kama ilivyo sasa kwa nchi nyingi maskini, huwezi kuwababaisha tena.
   
 12. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #12
  Jan 13, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  - Ningebadili jina, badala ya kuitwa Rais ningeitwa MTUMISHI WA WATANZANIA.
  - Ningeruhusu wakulima kuuza mazao nje, au kokote kwenye faida kwao. matokeo yake wangepata hela zaidi kuwekeza kwenye kilimo.

  - Kuunda FBI ya Tanzania au Scorpion ya South Africa, yenye nguvu za kweli.
  - Kujenga Chuo kikuu kila Mkoa.
  - Kuingiza wapinzani kwenye baraza la mawaziri.
  - Kujenga chuo kikubwa sana cha madaktari. Ni aibu ka Cuba kana madaktari 70,000, wakati Africa yote hawazidi 50,000 [ according to UN].
  - Press conference every week.
  - Kubadilisha katiba ili kuwa na federal sytem.
  - Marufuku kusafirisha madini yasiyokatwa- raw- .TANZANITE inaajiri watu 50,000 huko India.
   
 13. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #13
  Jan 13, 2009
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Binafsi ningekuwa Rais,kwa mwaka wa kwanza,ningefanya yafuatayo.
  1,Ningebadilisha kabisa mfumo wetu wa uongozi,kwa kuondoa madaraka makubwa kwa rais,kufuta cheo cha makamu wa rais,hii itasaidia uwajibikaji wa moja kwa moja wa waziri mkuu na rais,pia kupunguza gharama ambazo si za lazima.
  2.Ningebomoa kabisa mfumo wa uwakilishi na kurugenzi zote,,uwakilishi wetu uwe wa makundi ya kijamii,madhalani wabunge wawakilishwe na makundi ya jamii na si wanasiasa tu,na hili ningeliweka kwa asilimia,madhalani 40% ya wabunge watoke majimboni,15% kwenye taasisi za elimu ya juu,15% wasomi na wazee wastaafuu,20% vijana,5%walemavu,15%wataalamu wa fani zote.Hii itasaidia sana katika kufikia maamuzi yenye tija kwa nchi,na kila mmoja atoe mchango wake kwa mustakabali wa Taifa.
  3.Kuweka maadili ya taifa,tena maadili ya kudumu,ambayo pia yatakuwa ndio maslahi ya taifa,ili ifike mahali kiongozi aseme "ningefanya hivi,lakini si maslahi ya taifa"
  4.Ningeitisha mkutano mkuu wa taifa ili kujadili aina ya taifa tunalotaka,katika mkutano huu pia tutajadili aina ya katiba tunayotaka,na ni mkutano wa taifa,na kila raia anayeweza ahudhurie,
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Jan 13, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  ..oops!!

  ..aisee sikuwa nimesoma heading vizuri.

  ..posting yangu haikuzingatia kwamba ni kwa mwaka wa kwanza wa Uraisi.
   
  Last edited: Jan 13, 2009
 15. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #15
  Jan 13, 2009
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mtanzania nakubaliana na wewe mojakwamoja, ITS THE ECONOMY U ............

  Asiliamia 90% ya Budget kupelekwa kwenye wizara 3 zifuatazo mwaka wa kwanza wa uongozi.

  40% Kilimo
  25% ELIMU
  25 AFYA

  Usimamizi wa moja kwa moja kuhakikisha kuwa KILIMO kinamkomboa mwananchi mikoani na pesa zote zinawafikia walengwa kwa kuwapatia mbolea, matractor ya mikopo, mbegu bora na wataalamu wa kutosha.

  Trust me, najua hapa nimesimplify sana lakini bila hila tunapiga danadana tu na hamna kipya.
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Jan 13, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  moelex23,

  ..niko interested na point yako 40% ya budget kupelekwa kwenye kilimo. naomba u-expand kidogo kwa kuelekeza nini kifanyike kufufua kilimo.

  ..actually, nimesikia kwamba ule mpango wa "the big 5" yaani mikoa inayoongoza ktk kuzalisha chakula unaweza kurudisha.

  ..mara nyingine kunakuwa na artificial shortage ya chakula Tanzania. yaani tunashindwa kusafirisha chakula toka maeneo yenye surplus kupeleka maeneo yenye shortage.
   
 17. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #17
  Jan 13, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Could not agree more.
  Screw putative humanitarian ideologies if people have to keep dying in the wait of a better tomorrow kwa kila mtanzania.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jan 13, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kama ningekuwa na bunge ambalo asilimia tisini ni wabunge wa chama changu, ningelivunja siku ya pili baada ya kuapishwa na kutaka nusu ya majimbo yote chama changu hakitasimamisha mgombea! Tunafanya uchaguzi mkuu mpya ili hatimaye tuwe na Bunge ambalo linaweza kusababisha yote yaliyopendekezwa humu kutekelezwa.

  Wakati bunge linafanya mambo hayo mimi nitakaa tayari kutia sahihi miswada yote ya sheria zenye maslahi ya nchi.

  Lakini la pili nitamtimua Mtanzania yeyote ambate atatumia neno "Hatuwezi" au "haiwezekani". Wale watakaotumia neno "ni vigumu" tutawatafutia kisiwa ambacho watafungwa hadi fikra zao zibadilike na kuanza kutafuta msamiati mwingine..msamiati ambao hauusiani na kushindwa au kutoweza au kuwa duni!

  Wakati hawa wanahangaika nitafungua gereza jipya pembezoni ya mapango ya Amboni ambako Marais wa zamani, mawaziri na watumishi wa umma waliokutwa na hatia za ufisadi watatumikia kifungo chao. Gereza hilo kazi yake kubwa ya uzalishaji itakuwa kutoa maelezo ya kwanini wasitolewe kifungoni!
   
 19. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #19
  Jan 13, 2009
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jokakuu, samahani ndugu yangu mimi sio mtaalamu wa kilimo, nimetumia kigezo kikuu kimoja kuwa asilimia 80% ya watanzania wako mikoani (especially vijijini) na wanategemea kilimo, so its only right kuweka asilimia kubwa ya budget kufikia asilimia kubwa ya wananchi.

  Of course ni benefit kubwa kwa nchi kujitosheleza kwa chakula na vile vile kuweza kuuza mazao mengine nje kuondoa ile poverty ya ajabu ambayo asilimia kubwa ya wananchi wetu inatukumba.

  Watu wa vijijini wakiinuka kiuchumi, benefit zake zitakuwa kubwa mno kwani makampuni na mashirika mengi yataongeza kipato na hii domino effect itafanya uchumi mzima wa nchi kuwa na multiplier effect kubwa mno.
   
 20. s

  skasuku Senior Member

  #20
  Jan 13, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Haya ngoja na mimi nitose fikra mbili tatu hapa:

  Kwanza kabisa nitaanzisha kampeni ya "Going Back to Basics", kwa maana hii nitahakikisha kwanza masuala yote ya msingi wa maendeleo tunatekeleza: kwa mfano:

  - Uwajibikaji katika kila ngazi ya serekali.
  - Kila idara ya serekali kuwepo na vipimo vya maendeleo (Key Performance Indicators). Na hii kuwepo hadi kila mfanyakazi wa serekali.Dhumuni lake iwe kipimo cha kama mtu anaweza kazi au hawezi. Katika mwisho wa mwaka wa kwanza, 10% of under performers kufukuzwa kazi. Hili litaleta ufanisi ambao umekosekana katika idara za serekali. Malengo yote kuwekwa mwanzo wa mwaka.
  - Kuwepo na clear reporting structure. Malengo yote kupangwa na utekelezwaji wake kuwa jukumu la kiongozi wa wizara, idara, timu n.k.
  - Kuhakikisha sera za Elimu, Afya, Uchumi, Usalama wa nchi, Sheria, Kazi na Ajira, biashara zinapewa kipaumbele na zinakwenda na wakati.
  - Kuwapa wanahabari "Freedom to Report responsibly" kwani hawa ndio macho na masikio yangu yasio na bias.
  - Kuhakikisha External Auditing zinafanyika kila mwaka na kampuni huru katika kila wizara na idara ya serekali.
  - Kuintroduce sera za ujenzi wa taifa kwakushirikiana na Private sector.
  - Rudisha JKT, na mandatory kwa kila raia. As the good old days.

  Nadhani haya kwa sasa yatatosha kuweza kurudisha some sort of utaifa katika hii nchi yetu.
   
Loading...