Leonard Robert
JF-Expert Member
- Apr 22, 2011
- 11,143
- 7,403
Kumbuka vitambaa havitolewi bure vitakuwa vinauzwa,kwahiyo ni hela yako tu,sasa kama watanzania wote tupo vizuri tutanunua quality ya juu,vinginevyo ni sawa tu viwepo vya style zote.
wananchi wakipendekeza na viatu viwemo kwenye vazi la taifa,itakua.lakini inashangaza msisitizo kuwa kitambaa.
Vazi la Taifa halitafutwi na halijawahi tafutwa! Wamasai walitafutiwa na nani Rubega? Au hao waGhana na waNigeria walitafutiwa na nani vazi lao? Am worried that we'll spend a lot of money ktk kitu kisicho na tija kwa maana at the end the mapokeo na "ownership" ya vazi kwa watanzania walio wengi isiwepo...........
If we've survived 50 years without it, why should we have it?
Nimekua nikishangazwa na mwenendo mzima wa kupata VAZI LA TAIFA..
Wahusika wakuu wa mchakato huu, kwa nyakati tofauti nimewasikia wakiongea..mara kitambaa kiwe hivi,kiwe cha rangi gani,kiwe kitambaa cha suti n.k
kibaya zaidi nimewasikia wakisema eti..kitambaa hicho kitakuwa na ubora tofauti kulingana na hadhi ya mvaaji..wakitolea mfano wabunge, eti kitambaa chao kitakua na quality tofauti pia wao wanaweza kuchagua suti waipendayo kutokana na kitambaa hicho..
Kwa ujumla mawazo yao yanajikita kwenye kitambaa na ubora wa kitambaa hicho.
Sasa wadau magreat-thinker wa jf..naomba tujadili swala hili kwa pamoja "tunataka vazi la taifa au kitambaa cha taifa" nawasilisha.
Ningefurahi sana kama waziri mwenye dhamana ya michezo angeteua kamati ya kitaifa ya kuratibu na kufufua michezo kataka taifa letu, kwanza kwa kuendeleza michezo vijana wengi sana wangepata ajira kupitia michezo mfano wenzetu wa kenya kama unafahamu kukimia tu ni tiketi ya kupata maisha bora,sasa hilo vazi la taifa litamsidiaje kijana wa leo wa kitanzania kuondokana na tatizo la ajira.
Vazi linajumuishwa na viatu au? Mi napendekeza viatu viwe raiyoo/katambuga
Vazi la Taifa ni kanzu na kofia kwa wanaume, wanaotaka kulibadili hili wana agenda za siri na kwa kina mama Khanga mbili nje ndani chochote.
Vazi la Taifa ni kanzu na kofia kwa wanaume, wanaotaka kulibadili hili wana agenda za siri na kwa kina mama Khanga mbili nje ndani chochote.
Hapa swala si aina wala ubora wa kitambaa vazi la taifa linahusisha zaidi mshono wa vazi lenyewe.Rangi,ubora ni suala la maamuzi baada ya kupata mtindo wa vazi husika.Huu ujinga wa vazi kuendana na hadhi ni upuuzi ambao wenye akili timamu hawawezi kuufikiria.
Ina maana tuweke sheria kuwa hiki kitambaa,ubora wake na mshono ni cha waziri/mbunge/Rais/Mwl au mlalahoi kama mimi,........ n.k kwamba mwingine akivaa ni kosa kisheria au?
Mbeba mkaa,kuri,mbeba zege,mkulima,mfanyabiashara ........nk sidhani kama wanataka au kusikia ubaguzi wa hiyo kamati ya kiwizi wizi.Cha msingi utoke mtindo wa ushonaji kila mtu atajua ubora wa kitambaa au rangi.
Ina maana ni miradi ya kula siyo?Utakimbizwa Apollo India haraka wewe kwa kufuatilia mishemishe za watu!