James Martin
JF-Expert Member
- Apr 2, 2016
- 1,206
- 1,509
Siku chache zilizopita mkuu wa majeshi amewafukuza vijana wapatao 854 waliofuzu mafunzo ya kijeshi kwa kushinikiza waajiriwe na jeshi kupitia mgomo wa kufanya kazi na maandamano.
Mimi binafsi siamini wanajeshi watumiwe kwenye miradi yeyote ya kujenga uchumi na kazi zozote za kiraia na polisi kama ujenzi wa ikulu, kulinda madini kule Mererani, operesheni ya kufungia ma bureau de change na ukusanyaji wa korosho kule mikoa ya kusini.
Sababu ya kwanza kwa nini napinga wanajeshi watumiwe kwenye kazi hizi ni kwamba inaweza kuwavunja morali wanajeshi hao wanaotumika. Kama hao vijana waliofuzu, wanaweza kuwa wanafanya kazi zisizokuwa na hazi ya uanajeshi. Kila mtu anajua kazi kuu ya jeshi ni kulinda mipaka ya nchi kutoka kwa adui wa nje.
Najua nchi mbalimbali hutumia wanajeshi kusaidia wananchi kwenye mambo ya majanga kama mafuriko au matetemeko ya ardhi. Hilo mimi wala silipingi kwasababu hizo ni kazi rafiki zinazosaidia kujenga uhusiano mzuri kati ya wananchi na jeshi lao. Lakini kuwatumia wanajeshi kama kwenye zile operesheni za kuzifungia bureau de change ni kuiharibu taswira ya jeshi kwa wananchi kama kitu kikienda mrama.
Pili, Serikali hutumia pesa nyingi kutoa mafunzo ya kijeshi ili kuwafanya wawe shupavu lakini pia kuwafanya wawe watiifu. Kuwaweka wanajeshi kwenye kazi za kiraia hususani zenye mianya ya kufanya ufisadi ni kuwatia hawa mashujaa kwenye majaribu. Yaani mfano wake ni kama una mtoto mtiifu hafafu unaweka bakuli lililojaa pipi sebuleni, unamwambia mtoto mimi natoka lakini usichukue pipi!
Anaweza asichukue hata moja, lakini pia kuna uwezekano akachukua! Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba tuwaache wanajeshi wajikite kwenye majukumu yao ya kuilinda mipaka yetu na tusiwatie majaribuni kwenye kazi za kiraia.