Je, tumejifunza somo gani kwa Wanajeshi kugoma kufanya kazi na kuandamana?

James Martin

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
1,206
1,509
Siku chache zilizopita mkuu wa majeshi amewafukuza vijana wapatao 854 waliofuzu mafunzo ya kijeshi kwa kushinikiza waajiriwe na jeshi kupitia mgomo wa kufanya kazi na maandamano.

Mimi binafsi siamini wanajeshi watumiwe kwenye miradi yeyote ya kujenga uchumi na kazi zozote za kiraia na polisi kama ujenzi wa ikulu, kulinda madini kule Mererani, operesheni ya kufungia ma bureau de change na ukusanyaji wa korosho kule mikoa ya kusini.

Sababu ya kwanza kwa nini napinga wanajeshi watumiwe kwenye kazi hizi ni kwamba inaweza kuwavunja morali wanajeshi hao wanaotumika. Kama hao vijana waliofuzu, wanaweza kuwa wanafanya kazi zisizokuwa na hazi ya uanajeshi. Kila mtu anajua kazi kuu ya jeshi ni kulinda mipaka ya nchi kutoka kwa adui wa nje.

Najua nchi mbalimbali hutumia wanajeshi kusaidia wananchi kwenye mambo ya majanga kama mafuriko au matetemeko ya ardhi. Hilo mimi wala silipingi kwasababu hizo ni kazi rafiki zinazosaidia kujenga uhusiano mzuri kati ya wananchi na jeshi lao. Lakini kuwatumia wanajeshi kama kwenye zile operesheni za kuzifungia bureau de change ni kuiharibu taswira ya jeshi kwa wananchi kama kitu kikienda mrama.

Pili, Serikali hutumia pesa nyingi kutoa mafunzo ya kijeshi ili kuwafanya wawe shupavu lakini pia kuwafanya wawe watiifu. Kuwaweka wanajeshi kwenye kazi za kiraia hususani zenye mianya ya kufanya ufisadi ni kuwatia hawa mashujaa kwenye majaribu. Yaani mfano wake ni kama una mtoto mtiifu hafafu unaweka bakuli lililojaa pipi sebuleni, unamwambia mtoto mimi natoka lakini usichukue pipi!

Anaweza asichukue hata moja, lakini pia kuna uwezekano akachukua! Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba tuwaache wanajeshi wajikite kwenye majukumu yao ya kuilinda mipaka yetu na tusiwatie majaribuni kwenye kazi za kiraia.
 
Kasome katiba kwanza ndipo uje.

Kwa ufupi:

Wajibu wa mwanajeshi wa jeshi la wananchi wa tanzanaia(jwtz)
1. Kulinda mipaka.
2. Kulinda katiba.
3. Kushiriki uokoaji wakati wa majanga.

4. Kusaidiana na taasisi za kiraia katika kazi mbali mbali.

Hiyo namba nne ndio wanasimama hapo,japo hawakuwa wanajeshi tayari.
 
Vijana hata hawajaandikishwa jeshini tayari mnawaita wanajeshi, wale ni vijana wa kujitolea.

We umesikia wapi wanajeshi wamegoma?

Mnalipakaza matope jeshi kwa kushindwa kutofautisha kwenu vijana wa kujitolea na wanajeshi rasmi.
Daaah afadhali umesaidia kwa kiasi kikubwa watu wengi wanaongea wasichokijua na zaidi wanafikia mpaka kusema eti uhalifu utazidi, kwanza hao sio wa kwanza kurudi na hali shwari kabisa muhimu kuzingatia Jkt haiajiri tatu hawana mafunzo kama watu wanavyotaka kuaminisha hapa asilimia kubwa ni uzalishaji mali kama kulima,kujenga,sanaa nk
 
Siku chache zilizopita mkuu wa majeshi amewafukuza vijana wapatao 854 waliofuzu mafunzo ya kijeshi kwa kushinikiza waajiriwe na jeshi kupitia mgomo wa kufanya kazi na maandamano.

Mimi binafsi siamini wanajeshi watumiwe kwenye miradi yeyote ya kujenga uchumi na kazi zozote za kiraia na polisi kama ujenzi wa ikulu, kulinda madini kule Mererani, operesheni ya kufungia ma bureau de change na ukusanyaji wa korosho kule mikoa ya kusini.

Sababu ya kwanza kwa nini napinga wanajeshi watumiwe kwenye kazi hizi ni kwamba inaweza kuwavunja morali wanajeshi hao wanaotumika. Kama hao vijana waliofuzu, wanaweza kuwa wanafanya kazi zisizokuwa na hazi ya uanajeshi. Kila mtu anajua kazi kuu ya jeshi ni kulinda mipaka ya nchi kutoka kwa adui wa nje.

Najua nchi mbalimbali hutumia wanajeshi kusaidia wananchi kwenye mambo ya majanga kama mafuriko au matetemeko ya ardhi. Hilo mimi wala silipingi kwasababu hizo ni kazi rafiki zinazosaidia kujenga uhusiano mzuri kati ya wananchi na jeshi lao. Lakini kuwatumia wanajeshi kama kwenye zile operesheni za kuzifungia bureau de change ni kuiharibu taswira ya jeshi kwa wananchi kama kitu kikienda mrama.

Pili, Serikali hutumia pesa nyingi kutoa mafunzo ya kijeshi ili kuwafanya wawe shupavu lakini pia kuwafanya wawe watiifu. Kuwaweka wanajeshi kwenye kazi za kiraia hususani zenye mianya ya kufanya ufisadi ni kuwatia hawa mashujaa kwenye majaribu. Yaani mfano wake ni kama una mtoto mtiifu hafafu unaweka bakuli lililojaa pipi sebuleni, unamwambia mtoto mimi natoka lakini usichukue pipi!

Anaweza asichukue hata moja, lakini pia kuna uwezekano akachukua! Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba tuwaache wanajeshi wajikite kwenye majukumu yao ya kuilinda mipaka yetu na tusiwatie majaribuni kwenye kazi za kiraia.
Wale hawanatofauti na mgambo, wanajeshi hawagomi kwa kuandamana.
 
Ili uitwe mwanajeshi ni vigezo vipi muhusika hutakiwa kutimiza?

Hata hatua walizochukuliwa si za kijeshi. Ni makosa kuwaita hawa vijana ni wanajeshi. Hawa ni rais wenye sehemu ya mafunzo na mbinu za kijeshi. Je wangeajiriwa moja kwa moja kuwa wanajeshi bila ya kwenda kwenye kozi stahiki za ajira hiyo na kufuzu?
 
..viongozi waache kutoa ahadi za UONGO.

..hao vijana wasingekuwa wameahidiwa ajira wasingeleta mzozo kwa makamanda wao.
 
Vijana hata hawajaandikishwa jeshini tayari mnawaita wanajeshi, wale ni vijana wa kujitolea.

We umesikia wapi wanajeshi wamegoma?

Mnalipakaza matope jeshi kwa kushindwa kutofautisha kwenu vijana wa kujitolea na wanajeshi rasmi.
Yaan hao kabla hamjatangaziwa chamoto wamekiona.
 
Ili uitwe mwanajeshi ni vigezo vipi muhusika hutakiwa kutimiza?

Hata hatua walizochukuliwa si za kijeshi. Ni makosa kuwaita hawa vijana ni wanajeshi. Hawa ni rais wenye sehemu ya mafunzo na mbinu za kijeshi. Je wangeajiriwa moja kwa moja kuwa wanajeshi bila ya kwenda kwenye kozi stahiki za ajira hiyo na kufuzu?
Kiufupi ni wazalendo
 
Back
Top Bottom