Je, tulihitaji treni ya umeme zaidi ya mengine?

Nakubaliana na wewe, lakini ukiwa sio insider kuna vitu vingine ambavyo wenzetu wameviangalia na wewe au sisi hatujaviangalia.
Mosi nimesema kumekuwepo na shida ya kupata vipuri kwa kuwa mass production setting ipo on sgr mode.
Na sisi uhitaji wetu kutokana na shida zetu ni mdogo, labda hizo spares tuchonge wenyewe, huku mlogolo-mrogoro.
Speed or time taken to deliver hizo goods and services , e.g. vegetables, maua, utalii and other businesses
mkuu kujenga kiwanda chetu cha treni hata 40b haiishi kwa sababu hio n kujenga assembly plant ya average mashine ie tren n mashine kisha vipuri kina sisi wananchi na kina lowasa tutaona fursa ya viwanda vidogo dogo vya vipuri na kadhalika
pia ukiwekeza tu kwenye engineer vizury with in a year io mgr tutaishape vizury ifike walau 120km/h na hizo usd 3bn haziishi ilia uta accomplish vitu vingi bila kusahau utakuwa umeongeza chain ya ajira na ubunifu na ushindani na hio pesa ya sgr dar to makutopora ukiiwekeza kiujanja hususani education mbona 5year tuko misri tunapokea tender

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtoa mada umeona kuna umuhimu wa kua na reli na umesema bora tungefufua iliyopo, kama umuhimu wa reli upo basi hiyo ya SGR ndio inayotakiwa kwa wakati tulio na, kuifufua hiyo iliyopo inaweza kua na gharama ndogo lakini gharama za uendeshaji zikawa ni kubwa, hatutengezi mabehewa ,injini na hata reli zenyewe na huko zinakotoka hawatengenezi za kizamani labda kwa order maalum

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwann tusitatue ya Leo kwanza hio 40yrs wawezakuta technology imekuwa na kwao isiwe msaada
Ya leo yanatatuliwa kila kukicha na ni mengi sana. Wazungu waliotutawala waliijua afrika kuliko mababu zetu, na sababu ni ile hali ya kutazama mbali.

Leo inakwisha lakini ipo Tanzania itakayofaidi matunda ya uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye miundo mbinu, ubinafsi wetu ni umaskini wetu.
 
Habari wakuu....,
Mawazo haya naamini ni ya mchana sio ya jioni.

Hapa lengo langu ni kuangalia umuhimu WA treni ya umeme kama ni sahihi kwa mazingira yetu ya sasa.

Tangu ajali ya mwaka 2001 serikali ilipunguza Nguvu ya shirika LA TRC ni kwa zaidi ya miaka 15. Migogoro na ukata ndani ya shirika vililitesa sana, wananchi na wabunge walipiga kelele lkn sauti ilianza kusikika wakati mwakyembe akiwa wazari ya usafirishaji. Mabadiliko yalitokea bajeti ya shirika ikaanza kuongezwa.
Kiukweli shirika likaanza angalu maisha mapya ya kendelea.

Mh. Magufuli na Masanja wamekuja na dhamira ya kulifufua shirika zaidi lkn standard gage tumekosea kwa sasa.

Hatuwezi kutumia t.7 kujenga kitu ambacho mbadala wake upo na wananchi bado wako kwenye mkwamo WA kiuchumi .

Reli yetu hii ya mjerumani IPO kwa nn tusiifufue completely na tukawekeza treni na mabehewa mazuri na ya kisasa ili kuendelea kuhudumia watu.

Wengi tulipanda treni nyuma ya 2001 na ulikuwa usafiri WA shida hata 2005 ulikuwepo kwa shida bado tulisafirisha msiba WA mjomba wangu.

Leo kuna treni za kisasa za reli ya zamani kwa nini tusingebaki pale kwanza?

Tumeona mabehehewa ya mwakyembe yakipata sifa kubwa lkn bado si ya kisasa na luxury.

Tungewekeza hapo kwa kuongeza treni nyingi ambapo watu wengi wangesafiri kupitia huko kwa gharama nafuu na usafiri ukawa reliable.

Mpaka leo TRC hawajajiandaa hata kuendesha shirika kisasa bado wanataka tujazane station gerezani na kwingineko, bado hawataki kuamini hata wasafi festival na fiesta tunalipa kwa simu.

Hawataki kuamin kwa haraka tunaweza toka huko kwa haraka.

Sijui kama magu atakuwa ofisini kama ndivyo anaweza kuunda shirika jipya kuhudumia standard gage kwa kuwa TRC hawajiandaa.

Naeleza haya nikijua ni mchana.

T.3 za juzi tulizokopa tungeamua kuimarisha kilimo cha kisasa kama Israel isingenufaisha watu WA nchi hii?

T.3 zilizotumika zingekopeshwa wakulima walioko kwenye vyama vya ushirika kuimarisha ukulima wao kwa mbegu, viuatilifu, mbolea na wataalamu kwa kuwaajiri tusingelikomboa hill taifa?

Tungewakopesha wafanyabiasha WA kati kufungua viwanda vya vidogo vya m.15 - 50 je tusingekuwa China WA Africa?

Basis tungezikopesha timu za ligi kuu kujenga viwanja ili tupate mapato

Basi tungegharamia elimu na afya yetu kwa miaka 3 tuone Ustawi WA watu baada ya hapo je, tusingekuwa na elimu bora pia health facilities nzuri katika nchi za maziwa makuu, pia better public health care

Je, tungezitumia kuongeza ajira za umma kwa usawa WA client na service provider, mishahara mizuri tusingeimarisha uwezo wetu WA uchumi WA nchi, kipato cha MTU mmoja kisingeongezeka? Benki zisingekuwa imara.

Basi tungetumia kutengeneza tasnia ya madini na utalii, tungetengeza vinu vya kuchenjua makinikia, tungetangaza vivutio vyetu nje na matangazo kwa mwaka mzima watalii wasingeongezeka? Matangazo discovery channel, kwenye ndege, EPL, na NBA hata mashirika ya habari na magazeti tusingeongeza utalii Mara tano kama sasa kwa miaka zaidi ya 10 mfululizo?

Sijui treni ya umeme tunawahi wap?
Kazini, likizo, mikutano, biashara, au mizigo?

Ulaya ilitumia standard gage kwakuwa imeungana na wanamiliki mapato.
Uwezo wao wa uchumi n mkubwa kuliko sisi.

Ahaa Kenya, purchasing power in kubwa kuliko tz lkn pia haikutakiwa kwa sasa.

Shida ya nchi zinazoendelea nikuhitaji yaliyo dunia ya kwanza bila kujali tunatumia pesa nyingi kwenye miundombinu isiyonatija kwa watu wengi kwenye uchumi wa taifa husika.
Tunatatizo na wanaofikir kwa niaba ya taifa

Tuna shida na system ya nchi
Tuna shida na bunge ambao wanapaswa kufikir juu ya ustawi wa watu

MTU aniambie kati ya standard gage na hayo yapi yanatija kwa watu robo tatu ya watanzania?
Mkuu kabla ya kuririka haya yote,umefanya karesearch hata kadogo kwa maana ya kusoma papers au kufuatilia mradi huu kwa kina na kwa ukaribu?!Nilitegemea unge'dig kujua kwanza kbs malengo makuu ya kuanzishwa na kutekelezwa kwa mradi huu mkubwa kutoka kwa wahusika wenyewe,kama umefanya hivyo tuongezee kwny bandiko lako,tuweze kupata msingi wa kujadili kwa mapana zaidi, na pili hayo uliyoyaorodhesha yote kwny sekta nyingine hayafanyiki?!!,Ulivyoongea utafikiri mambo mengine yote yamesimama kbs. Ni vyema kufanya research kwa pande hizo zingine pia kuona kama kuna progress na kuja na hoja iliyoshiba yenye mifano halisi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ungekuta ni mnaona mbele mngezalishwa ma engneer wa kueleweka ndani ya 3 years hao wangejenga sgr ya 400km/h ambayo ingekuwa ni sehemu ndogo tu ya technology tutakayokuwa sasa hii ya sgr ya 160km/h ambayo izo nchi zilizoendelea kwao tokea 1900+ walishatumia sa hv wanafanya 300+km/h kama peace of cake hii yetu ya 160km/h inatutoa jasho na itatutoa ndani ya more than 7 years kumaliza kwa msaada wa wageni kwenye ujuzi ila tungewekeza kwenye elimu with in 3 years reli 1000km kwa speed ya 400km/h ingekuwa ni sehemu ya mafunzo ATC

Sent using Jamii Forums mobile app

skia dogo! hakunaga perfect investment, everything is trial and learning! unaweza jenga SGR na ukakutana na opportunities mpya kabisa thats how life is, and it might as well fail, failing isnot a sin, sasa nyie mnataka kila kitu yaani kikiwekezwa apo apo ela zije, things dont work that way, hata barabara hazijengwi zote kwa sku moja, unaanza unajenga kuanzia point flan mpaka flan serikali ingine inafuata na vipande vingine! mwishowe mnakua mmemaliza barabara nchi nzima
 
Asante sana kwa kunitag mkuu.

Nilichomuelewa jamaa anasema miradi mingi ya serikali si lazima ipate faida kubwa. Miradi mingi ya serikali inakuwa ni MTAMBUKA ambayo inasababisha sekta nyingine kukua kupitia MRADI fulani.

Kwani huoni hata kama atutopata FAIDA kwa muda mfupi lakini SGR au ununuzi wa NDEGE ni miradi ya MTAMBUKA mkuu?

..ndege tutapata hasara tusilete ubishi.

..sgr tukijipanga na kujiandaa vizuri tunaweza kutoboa.

..kinachoniogopesha mimi ni kwamba hatutaki kujiuliza maswali magumu, na yeyote anayefanya hivyo anaonekana msaliti.
 
Ya tazara tatizo ni mkataba wa uendeshaji wake una ipa Zambia priority , na nina kumbuka Mwakyembe alitaka itumike kwa shughuli zetu internally akakumbana na vikwanzo.
Mpaka hayo yatatuliwe ndio tazaraitakuwa more effective or more efficient.

..hiyo ni moja ya sababu.

..lakini sababu kubwa zaidi ni za kiuchumi.

..na sababu hizohizo zinaweza kuathiri sgr.
 
..usiseme uduma, sema huduma.

..reli inatakiwa ijiendesha kibiashara, kwa maana irudishe fedha zilizotumika ktk uwekezaji.
Asante kwa marekebisho hayo. Na vipi kuhusu hospitali na vituo vya afya, hatuhitaji pesa zirudi au hospitali hazihitaji kujiendesha kibiashara?! Na vipi barabara zinazojengwa zenyewe hazihitaji kujiendesha kibiashara turudishe pesa zilizotumika kuzijenga?!
Serikali imeweka huduma kwa wananchi wake, hivyo sio kila kitu tunahitaji kurudisha pesa.
Hata wewe unapokula na kunywa ni huduma unajipa, uhitaji kujilipa.
Hili nadhani serikali imeweka kama semi service na semi business, return haitakuwa kwa muda mfupi.
 
..ndege tutapata hasara tusilete ubishi.

..sgr tukijipanga na kujiandaa vizuri tunaweza kutoboa.

..kinachoniogopesha mimi ni kwamba hatutaki kujiuliza maswali magumu, na yeyote anayefanya hivyo anaonekana msaliti.
Zamani ulikuwa uni let down kabisa ila sasa naona unakitumikia chama chako🤣

Btw naomba uje na andiko la suluhisho kitu gani kifanyike ili SGR iwe viable na kwanini ndege HASARA na maswali magumu gani ya kujiuliza kama taifa ila usiwe biased tu.

Natumaini utaleta UZI ASAP mkuu.
 
Asante kwa marekebisho hayo. Na vipi kuhusu hospitali na vituo vya afya, hatuhitaji pesa zirudi au hospitali hazihitaji kujiendesha kibiashara?! Na vipi barabara zinazojengwa zenyewe hazihitaji kujiendesha kibiashara turudishe pesa zilizotumika kuzijenga?!
Serikali imeweka huduma kwa wananchi wake, hivyo sio kila kitu tunahitaji kurudisha pesa.
Hata wewe unapokula na kunywa ni huduma unajipa, uhitaji kujilipa.
Hili nadhani serikali imeweka kama semi service na semi business, return haitakuwa kwa muda mfupi.

..kwa kawaida mashirika ya reli na ndege yanatakiwa yaendeshwe kibiashara kwa faida.

..pia lazima ujiulize kama uchumi wetu unaruhusu kubeba mzigo wa shirika la reli lisilojiendesha kibiashara bila kuathiri kwa kiasi kikubwa sekta muhimu kama elimu, afya, ulinzi, etc etc.
 
Zamani ulikuwa uni let down kabisa ila sasa naona unakitumikia chama chako🤣

Btw naomba uje na andiko la suluhisho kitu gani kifanyike ili SGR iwe viable na kwanini ndege HASARA na maswali magumu gani ya kujiuliza kama taifa ila usiwe biased tu.

Natumaini utaleta UZI ASAP mkuu.

..suala la manunuzi ya ndege limeelezewa kwa kirefu humu ndani.

..Na majuzi Prof.Nguyuru Ibrahim Lipumba ktk mahojiano na wahariri wa gazeti la mwananchi ameeleza kwa lugha rahisi sana kwanini ununuzi wa ndege ni biashara kichaa.
 
Mkuu kabla ya kuririka haya yote,umefanya karesearch hata kadogo kwa maana ya kusoma papers au kufuatilia mradi huu kwa kina na kwa ukaribu?!Nilitegemea unge'dig kujua kwanza kbs malengo makuu ya kuanzishwa na kutekelezwa kwa mradi huu mkubwa kutoka kwa wahusika wenyewe,kama umefanya hivyo tuongezee kwny bandiko lako,tuweze kupata msingi wa kujadili kwa mapana zaidi, na pili hayo uliyoyaorodhesha yote kwny sekta nyingine hayafanyiki?!!,Ulivyoongea utafikiri mambo mengine yote yamesimama kbs. Ni vyema kufanya research kwa pande hizo zingine pia kuona kama kuna progress na kuja na hoja iliyoshiba yenye mifano halisi.
Bandiko langu halipingi uwepo na umuhimu WA treni ya umeme lkn je, hilo ni muhimu kuliko mengine?

Tathimini binafsi Halafu tuambie kiasi gani cha fedha kimetumika katika tasnia ya usafirishaji na uchukuzi kuanzia mwaka 2016 hadi Leo?
Linganisha hicho kiasi dhidi ya sekta ya kilimo au viwanda, biashara na ujasriamali au elimu kama vinalingana kwa miaka yote hiyo kwa mojamoja au kwa kuziunganisha, unaweza kuunganisha hizo sekta hapo juu ukakuta serikali imetumia kwenye usafirishaji zaidi ya hizo nyingine na hapo unagundua nchi hii inataka nn kwa watu wake?

Wewe tuambie je ni kweli usafirishaji ni muhimu kuchukua pesa nyingi kiasi hicho? Tena zingine ni mikopo? Kwa kitu kisicho na tija kwa maisha ya Leo kama hizo sekta zingine nilizozitaka serikali izipe kipaumbele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu....,
Mawazo haya naamini ni ya mchana sio ya jioni.

Hapa lengo langu ni kuangalia umuhimu WA treni ya umeme kama ni sahihi kwa mazingira yetu ya sasa.

Tangu ajali ya mwaka 2001 serikali ilipunguza Nguvu ya shirika LA TRC ni kwa zaidi ya miaka 15. Migogoro na ukata ndani ya shirika vililitesa sana, wananchi na wabunge walipiga kelele lkn sauti ilianza kusikika wakati mwakyembe akiwa wazari ya usafirishaji. Mabadiliko yalitokea bajeti ya shirika ikaanza kuongezwa.
Kiukweli shirika likaanza angalu maisha mapya ya kendelea.

Mh. Magufuli na Masanja wamekuja na dhamira ya kulifufua shirika zaidi lkn standard gage tumekosea kwa sasa.

Hatuwezi kutumia t.7 kujenga kitu ambacho mbadala wake upo na wananchi bado wako kwenye mkwamo WA kiuchumi .

Reli yetu hii ya mjerumani IPO kwa nn tusiifufue completely na tukawekeza treni na mabehewa mazuri na ya kisasa ili kuendelea kuhudumia watu.

Wengi tulipanda treni nyuma ya 2001 na ulikuwa usafiri WA shida hata 2005 ulikuwepo kwa shida bado tulisafirisha msiba WA mjomba wangu.

Leo kuna treni za kisasa za reli ya zamani kwa nini tusingebaki pale kwanza?

Tumeona mabehehewa ya mwakyembe yakipata sifa kubwa lkn bado si ya kisasa na luxury.

Tungewekeza hapo kwa kuongeza treni nyingi ambapo watu wengi wangesafiri kupitia huko kwa gharama nafuu na usafiri ukawa reliable.

Mpaka leo TRC hawajajiandaa hata kuendesha shirika kisasa bado wanataka tujazane station gerezani na kwingineko, bado hawataki kuamini hata wasafi festival na fiesta tunalipa kwa simu.

Hawataki kuamin kwa haraka tunaweza toka huko kwa haraka.

Sijui kama magu atakuwa ofisini kama ndivyo anaweza kuunda shirika jipya kuhudumia standard gage kwa kuwa TRC hawajiandaa.

Naeleza haya nikijua ni mchana.

T.3 za juzi tulizokopa tungeamua kuimarisha kilimo cha kisasa kama Israel isingenufaisha watu WA nchi hii?

T.3 zilizotumika zingekopeshwa wakulima walioko kwenye vyama vya ushirika kuimarisha ukulima wao kwa mbegu, viuatilifu, mbolea na wataalamu kwa kuwaajiri tusingelikomboa hill taifa?

Tungewakopesha wafanyabiasha WA kati kufungua viwanda vya vidogo vya m.15 - 50 je tusingekuwa China WA Africa?

Basis tungezikopesha timu za ligi kuu kujenga viwanja ili tupate mapato

Basi tungegharamia elimu na afya yetu kwa miaka 3 tuone Ustawi WA watu baada ya hapo je, tusingekuwa na elimu bora pia health facilities nzuri katika nchi za maziwa makuu, pia better public health care

Je, tungezitumia kuongeza ajira za umma kwa usawa WA client na service provider, mishahara mizuri tusingeimarisha uwezo wetu WA uchumi WA nchi, kipato cha MTU mmoja kisingeongezeka? Benki zisingekuwa imara.

Basi tungetumia kutengeneza tasnia ya madini na utalii, tungetengeza vinu vya kuchenjua makinikia, tungetangaza vivutio vyetu nje na matangazo kwa mwaka mzima watalii wasingeongezeka? Matangazo discovery channel, kwenye ndege, EPL, na NBA hata mashirika ya habari na magazeti tusingeongeza utalii Mara tano kama sasa kwa miaka zaidi ya 10 mfululizo?

Sijui treni ya umeme tunawahi wap?
Kazini, likizo, mikutano, biashara, au mizigo?

Ulaya ilitumia standard gage kwakuwa imeungana na wanamiliki mapato.
Uwezo wao wa uchumi n mkubwa kuliko sisi.

Ahaa Kenya, purchasing power in kubwa kuliko tz lkn pia haikutakiwa kwa sasa.

Shida ya nchi zinazoendelea nikuhitaji yaliyo dunia ya kwanza bila kujali tunatumia pesa nyingi kwenye miundombinu isiyonatija kwa watu wengi kwenye uchumi wa taifa husika.
Tunatatizo na wanaofikir kwa niaba ya taifa

Tuna shida na system ya nchi
Tuna shida na bunge ambao wanapaswa kufikir juu ya ustawi wa watu

MTU aniambie kati ya standard gage na hayo yapi yanatija kwa watu robo tatu ya watanzania?
Au tungeamua hizo hela tukawa tuna walisha watanzania balanced diet milo mitatu kila siku mpaka zikaisha! Hii ingepunguza magonjwa na matumizi hospitalini yange pungua, watu wangekuwa na afya njema, nguvu na kuchapa kazi. Pia watoto wangekuwa na akili nyingi hadi kurushwa madarasa.
Hivyo hivyo, tungeendelea kununua chakula bora kila taifa linapopata hela ya kodi.
Ndege, treni, barabara nk. Havina maana yoyote. Tule tu!
 
Hoja yako ni nzuri hasa kwa sababu inaonyesha kuwa tatizo ulilonalo ni ujinga ambao unahitaji tu kuelimishwa!

Kumbuka ujinga sio tusi kwa sababu mjinga akielimishwa huelimika lakini mpumbavu hawezi kuelimishwa!

Umeandika, ''Hapa lengo langu ni kuangalia umuhimu WA treni ya umeme kama ni sahihi kwa mazingira yetu ya sasa''!

Hutujengi reli ya treni ya umeme kwa mazingira ya sasa pekee bali pia mazingira ya miaka mingi ijayo. Unaweza kuona haina manufaa kwa sasa kwa sababu faida yake kama reli haiwezi kupatikana kwa sasa lakini uwepo wake unajenga mazingira ya uwekezaji kwa ujumla katika nyanja zingine uwe wa kuvutia.

Kumbuka reli ya kati ambayo unaisifia ilijengwa mwaka 1905 na ninaamini watu kama wewe wa wakati huo walisema hivi hivi kama unavyosema wewe eti ''haifai kwa mazingira ya sasa''

Mwaka 1905 hata Dar hii unayoiona kwa sasa sehemu kubwa ilikuwa pori achilia mbali maeneo mengine katika mikoa ambayo reli ya kati inapita!

James Freeman Clarke aliwahi kusema, ''The difference between a politician and a statesman is that a politician thinks about the next election while the statesman think about the next generation''
Nchi inakwama sababu ya mapoyoyo kama nyie.utakua ccm wewe
 
Mjerumani hakujenga reli kwa mazingira yajayo Bali ya wakati huo, alihitaji kusafirisha mazao kuja dar kwa gharama nafuu na kwa urahisi.

Hawakulenga kusafirisha watanzania ila ni nini sisi watz ndio tulioamua iwe ilivyo Leo na kwakuwa maeneno mengine haikuwa na umuhimu nyerere aling'oa reli ya mtwara- mbamba bay
Nashukuru kwa ujinga na upumbavu wangu unaniwezesha kuona haya Leo, nakuomba nieleze je hayo niliyosema hayana tija Leo na kesho kwa robotatu ya watz?

Mi nadhani unashida ya kung'amua uzuri na ubaya WA jambo kwa Leo na kesho

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unawaza kisiasa zaidi na kikanda.

Mwenzio anawaza kitaifa na kibinadamu.

Wewe ni ripota wa mbowe na mwenzio ni ripota wa wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bandiko langu halipingi uwepo na umuhimu WA treni ya umeme lkn je, hilo ni muhimu kuliko mengine?

Tathimini binafsi Halafu tuambie kiasi gani cha fedha kimetumika katika tasnia ya usafirishaji na uchukuzi kuanzia mwaka 2016 hadi Leo?
Linganisha hicho kiasi dhidi ya sekta ya kilimo au viwanda, biashara na ujasriamali au elimu kama vinalingana kwa miaka yote hiyo kwa mojamoja au kwa kuziunganisha, unaweza kuunganisha hizo sekta hapo juu ukakuta serikali imetumia kwenye usafirishaji zaidi ya hizo nyingine na hapo unagundua nchi hii inataka nn kwa watu wake?

Wewe tuambie je ni kweli usafirishaji ni muhimu kuchukua pesa nyingi kiasi hicho? Tena zingine ni mikopo? Kwa kitu kisicho na tija kwa maisha ya Leo kama hizo sekta zingine nilizozitaka serikali izipe kipaumbele.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mie naona ni sawa tu kwa sababu ya umuhimu wake katika kujenga misingi imara na ya uhakika katika kukuza uchumi wetu leo na hapo baadae,yawezekana kbs kuwekeza kwny miundo mbinu ya uhakika kutasaidia kukuza sekta hizo zingine kwa kasi zaidi kuliko ungeanza kuwekeza kwny hizo sekta ulizozitaja,chukua mfano wa kilimo kwanza tu kama study. Swala la nishati miundo mbinu ya uhakika ni la msingi sana,hebu tuizungumzie kdg reli hii ya mgr unayotaka iboreshwe reli hii ni ya mwaka gani tunazungumzia teknologia ya miaka gani?!!!, Ili kuiupgrade iendane at least na ulimwengu wa leo itagharimu kiasi gani, span ya maisha yake itakuwa ni ya miaka mingapi baada ya kuwaupraded,chukua cost ya reli mpya minus ya zamani ikiwa upgraded, tazama tofauti, chukua faida na hasara ya pande zote mbili kwa upana wake tengeneza picha kubwa ukihusisha pia na dots halafu ujijibu.
 
Mbona hauwazi sawa sawa na bandiko langu LA kwanza, inawezekana unafahamu kilicho ndani ya kapeti kuliko sisi lkn kwa mnaendelea kuiboresha, kuifufua na kununua mabehewa ya kisasa?
Hatutaki upgrade hiyo reli kwa kuwa tunatuitumia sasa ikiwa hivyo, na kama wanawaza kama wewe kwa nini hawakutegeneza sgr badala ya mgr kule tanga na arusha?
Kwa nini watz wanafurahia uwepo WA hiyo treni ?
Sgr inalenga watu WA kipato cha juu na first grade WA kipato cha kati.
Mimi nakwenda mwanza kwa 24000 lkn hiyo sgr nitaenda kwa shngapi hadi huko?
Sgr ni mbadala WA mabasi hivyo mnawaza kama basi ni 8000-10000 morogoro basi treni ya umeme I we 5500 au 6500 nje ingekuwa treni yetu hii ya mafuta ambayo zamani ilikuwa ya kuni na makaa yaani garimoshi, dereva anachoka kama analima ingekuwa labda 3000 je, Morogoro tusingeenda kwa mgr badala mabasi kwa kuunganisha maelezo ya bandiko langu LA kwanza kukujibu.

Mtafakari nje ya box Linaloitwa serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unawaza kisiasa zaidi na kikanda.

Mwenzio anawaza kitaifa na kibinadamu.

Wewe ni ripota wa mbowe na mwenzio ni ripota wa wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Una uwezo kureason kweli hoja za watu na uhalisia WA maisha unayoishi na jamaa zako wote?

Ninayemzungumzia hapa ni timu mbowe au timu wananchi.

Hivi kupuuza cha wengi na kubariki cha wachache kwa hoja nyepesi unaona kwako ndiyo ubibadamu?
Pole

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bila cargo ya kutosha, kwa abiria wengi watumiaji njia hiyo treni ya umeme sio priority.
 
Back
Top Bottom