Je, tulihitaji treni ya umeme zaidi ya mengine?

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,989
1,441
Habari wakuu....,
Mawazo haya naamini ni ya mchana sio ya jioni.

Hapa lengo langu ni kuangalia umuhimu WA treni ya umeme kama ni sahihi kwa mazingira yetu ya sasa.

Tangu ajali ya mwaka 2001 serikali ilipunguza Nguvu ya shirika LA TRC ni kwa zaidi ya miaka 15. Migogoro na ukata ndani ya shirika vililitesa sana, wananchi na wabunge walipiga kelele lkn sauti ilianza kusikika wakati mwakyembe akiwa wazari ya usafirishaji. Mabadiliko yalitokea bajeti ya shirika ikaanza kuongezwa.
Kiukweli shirika likaanza angalu maisha mapya ya kendelea.

Mh. Magufuli na Masanja wamekuja na dhamira ya kulifufua shirika zaidi lkn standard gage tumekosea kwa sasa.

Hatuwezi kutumia t.7 kujenga kitu ambacho mbadala wake upo na wananchi bado wako kwenye mkwamo WA kiuchumi .

Reli yetu hii ya mjerumani IPO kwa nn tusiifufue completely na tukawekeza treni na mabehewa mazuri na ya kisasa ili kuendelea kuhudumia watu.

Wengi tulipanda treni nyuma ya 2001 na ulikuwa usafiri WA shida hata 2005 ulikuwepo kwa shida bado tulisafirisha msiba WA mjomba wangu.

Leo kuna treni za kisasa za reli ya zamani kwa nini tusingebaki pale kwanza?

Tumeona mabehehewa ya mwakyembe yakipata sifa kubwa lkn bado si ya kisasa na luxury.

Tungewekeza hapo kwa kuongeza treni nyingi ambapo watu wengi wangesafiri kupitia huko kwa gharama nafuu na usafiri ukawa reliable.

Mpaka leo TRC hawajajiandaa hata kuendesha shirika kisasa bado wanataka tujazane station gerezani na kwingineko, bado hawataki kuamini hata wasafi festival na fiesta tunalipa kwa simu.

Hawataki kuamin kwa haraka tunaweza toka huko kwa haraka.

Sijui kama magu atakuwa ofisini kama ndivyo anaweza kuunda shirika jipya kuhudumia standard gage kwa kuwa TRC hawajiandaa.

Naeleza haya nikijua ni mchana.

T.3 za juzi tulizokopa tungeamua kuimarisha kilimo cha kisasa kama Israel isingenufaisha watu WA nchi hii?

T.3 zilizotumika zingekopeshwa wakulima walioko kwenye vyama vya ushirika kuimarisha ukulima wao kwa mbegu, viuatilifu, mbolea na wataalamu kwa kuwaajiri tusingelikomboa hill taifa?

Tungewakopesha wafanyabiasha WA kati kufungua viwanda vya vidogo vya m.15 - 50 je tusingekuwa China WA Africa?

Basis tungezikopesha timu za ligi kuu kujenga viwanja ili tupate mapato

Basi tungegharamia elimu na afya yetu kwa miaka 3 tuone Ustawi WA watu baada ya hapo je, tusingekuwa na elimu bora pia health facilities nzuri katika nchi za maziwa makuu, pia better public health care

Je, tungezitumia kuongeza ajira za umma kwa usawa WA client na service provider, mishahara mizuri tusingeimarisha uwezo wetu WA uchumi WA nchi, kipato cha MTU mmoja kisingeongezeka? Benki zisingekuwa imara.

Basi tungetumia kutengeneza tasnia ya madini na utalii, tungetengeza vinu vya kuchenjua makinikia, tungetangaza vivutio vyetu nje na matangazo kwa mwaka mzima watalii wasingeongezeka? Matangazo discovery channel, kwenye ndege, EPL, na NBA hata mashirika ya habari na magazeti tusingeongeza utalii Mara tano kama sasa kwa miaka zaidi ya 10 mfululizo?

Sijui treni ya umeme tunawahi wap?
Kazini, likizo, mikutano, biashara, au mizigo?

Ulaya ilitumia standard gage kwakuwa imeungana na wanamiliki mapato.
Uwezo wao wa uchumi n mkubwa kuliko sisi.

Ahaa Kenya, purchasing power in kubwa kuliko tz lkn pia haikutakiwa kwa sasa.

Shida ya nchi zinazoendelea nikuhitaji yaliyo dunia ya kwanza bila kujali tunatumia pesa nyingi kwenye miundombinu isiyonatija kwa watu wengi kwenye uchumi wa taifa husika.
Tunatatizo na wanaofikir kwa niaba ya taifa

Tuna shida na system ya nchi
Tuna shida na bunge ambao wanapaswa kufikir juu ya ustawi wa watu

MTU aniambie kati ya standard gage na hayo yapi yanatija kwa watu robo tatu ya watanzania?
 
Hoja yako ni nzuri hasa kwa sababu inaonyesha kuwa tatizo ulilonalo ni ujinga ambao unahitaji tu kuelimishwa!

Kumbuka ujinga sio tusi kwa sababu mjinga akielimishwa huelimika lakini mpumbavu hawezi kuelimishwa!

Umeandika, ''Hapa lengo langu ni kuangalia umuhimu WA treni ya umeme kama ni sahihi kwa mazingira yetu ya sasa''!

Hutujengi reli ya treni ya umeme kwa mazingira ya sasa pekee bali pia mazingira ya miaka mingi ijayo. Unaweza kuona haina manufaa kwa sasa kwa sababu faida yake kama reli haiwezi kupatikana kwa sasa lakini uwepo wake unajenga mazingira ya uwekezaji kwa ujumla katika nyanja zingine uwe wa kuvutia.

Kumbuka reli ya kati ambayo unaisifia ilijengwa mwaka 1905 na ninaamini watu kama wewe wa wakati huo walisema hivi hivi kama unavyosema wewe eti ''haifai kwa mazingira ya sasa''

Mwaka 1905 hata Dar hii unayoiona kwa sasa sehemu kubwa ilikuwa pori achilia mbali maeneo mengine katika mikoa ambayo reli ya kati inapita!

James Freeman Clarke aliwahi kusema, ''The difference between a politician and a statesman is that a politician thinks about the next election while the statesman think about the next generation''
 
Mjerumani hakujenga reli kwa mazingira yajayo Bali ya wakati huo, alihitaji kusafirisha mazao kuja dar kwa gharama nafuu na kwa urahisi.

Hawakulenga kusafirisha watanzania ila ni nini sisi watz ndio tulioamua iwe ilivyo Leo na kwakuwa maeneno mengine haikuwa na umuhimu nyerere aling'oa reli ya mtwara- mbamba bay
Nashukuru kwa ujinga na upumbavu wangu unaniwezesha kuona haya Leo, nakuomba nieleze je hayo niliyosema hayana tija Leo na kesho kwa robotatu ya watz?

Mi nadhani unashida ya kung'amua uzuri na ubaya WA jambo kwa Leo na kesho
Hoja yako ni nzuri hasa kwa sababu inaonyesha kuwa tatizo ulilonalo ni ujinga ambao unahitaji tu kuelimishwa!

Kumbuka ujinga sio tusi kwa sababu mjinga akielimishwa huelimika lakini mpumbavu hawezi kuelimishwa!

Umeandika, ''Hapa lengo langu ni kuangalia umuhimu WA treni ya umeme kama ni sahihi kwa mazingira yetu ya sasa''!

Hutujengi reli ya treni ya umeme kwa mazingira ya sasa bali mazingira ya miaka mingi ijayo.

Kumbuka reli ya kati ambayo unaisifia ilijengwa mwaka 1905 na ninaamini watu kama wewe wa wakati huo walisema hivi hivi kama unavyosema wewe eti ''haifai kwa mazingira ya sasa''

Mwaka 1905 hata Dar hii unayoiona kwa sasa sehemu kubwa ilikuwa pori achilia mbali maeneo mengine katika mikoa ambayo reli ya kati inapita!

James Freeman Clarke aliwahi kusema, ''The difference between a politician and a statesman is that a politician thinks about the next election while the statesman think about the next generation''

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipaumbele vinawekwa na rais KISHA kujadiliwa na bunge hivyo ni ngumu bunge kuweka vipaumbele vya taifa.

Hatukupaswa kuwa mawaziri bungeni isipokuwa waziri Mkuu ili hoja ziwe chache za serikali zinazoingia bungeni kuliko zinazotoka bungeni kwenda serikalini.

Bunge LA marekani linaweza kutunga sheria yeyote bila mswada kuletwa na serikali
Tuimarishe bunge tuijenge nchi

Leo bunge limekuwa kimbilio kwa kuwa n sehemu ya soga na upigaji kwani si kwa maslahi ya taifa
Hatuna vipaumbele kama taifa, tunaenenda kwa matakwa ya mtu mmoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siamini juu ya standard gage kwa kuwa mbadala upo angalau ndege naweza kuamini kuwa tulihitaji kufufua shirika, wingi WA ndege zisizo na faida ni jambo lingine japo napo hatupaswa lazima kuwa na shirika LA ndege LA taifa kwa kuwa za serikali zipo, mashirika binafsi yangetosha.

Fedha zilizotumika kwenye reli zinaniuma sana, tena hasa tulizokopa juz

Rufiji nako tunaenda kukopa t.4-5 watanzania sisi tunashida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipaumbele vya wanasiasa huwa si vipaumbele vya wananchi wanasiasa wanajali vipaumbele vinavyowapa sifa wanasiasa hawajali kuhusu riba bali sifa maana riba italipwa na walipa kodi wao haiwahusu.Kama taifa hatuna vipaumbele vyetu bali kila mtawala uja na vyake kwa kuviponda vya mtangulizi wake nae uja na vipya navyo haivimalizi.

Nchi inakuwa masikini sababu ya ubinafsi wa wanasiasa kisha lawama wanabebeshwa mabeberu mara sijui ukoloni mambo Leo wakati kupitia mabeberu na ukoloni mambo Leo nchi za Asia wao wanaendelea sababu wana vipaumbele kama taifa.
 
Hakuna mwanachi yeyeto labda maisha yake yameathirika sababu hakuna SGR hakuna mzigo wowote uliokwama dar ukisubiria SGR ili usafirishwe.Hitaji la kwanza la wananchi ni elimu,afya na shibe.

Gharama za kujenga SGR zinatosha kujenga vyuo vya ufundi na vya maendeleo tena vya kisasa kila kata nchini na vijana wote nchi nzima zaidi ya milioni 15 wakapata elimu bure yaani kila mmoja akasoma kozi aitakayo ili awe na tija aweze kuzalisha na kuchochea ukuaji wa uchumi na kuondoa tatizo la ajira nchini.

Tofauti na sasa vijana wametelekezwa kama kuku wasio na baba wanajiendea tu hakuna program iwafahayo,wamegeukia kwenye udalali wa viwanda vya wachina ( kuendesha bodaboda na kuwa machinga) hakuna future hapa.

Vijana ni masikini kwa sababu hawana maarifa ya kutosha kuzitumia raslimali zilizopo.
 
..nataka kujua kama SGR itaendeshwa kibiashara, itatuletea faida, na itarudisha fedha tulizowekeza.
Tumeshindwa mwendokasi wapewa kila kitu kuanzia njia,abiria,mabus,nk lkn tumeshindwa management sasa sijui kuhusu SGR.
Vipaumbele vinawekwa na rais KISHA kujadiliwa na bunge hivyo ni ngumu bunge kuweka vipaumbele vya taifa.

Hatukupaswa kuwa mawaziri bungeni isipokuwa waziri Mkuu ili hoja ziwe chache za serikali zinazoingia bungeni kuliko zinazotoka bungeni kwenda serikalini.

Bunge LA marekani linaweza kutunga sheria yeyote bila mswada kuletwa na serikali
Tuimarishe bunge tuijenge nchi

Leo bunge limekuwa kimbilio kwa kuwa n sehemu ya soga na upigaji kwani si kwa maslahi ya taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
Miradi yote mikubwa haikupita bungeni bali ni vipaumbele vya rais kwa maana kawapumbelia wananchi wawe wanataka au hawavitaki na sio vipaumbele vya wananchi.Miradi mingi huwa inakwama mbali na 10% lkn huwa watumiaji huwa awashirikishwi wao wanalazimishwa kuitumia,mfano mradi wa machinga complex umebuma sababu hakuna machinga aliyeshirikishwa
 
Naunga mkono hoja, tukubali tukatae sisi Tanzania tuna tatizo katika kupanga vipaumbele vyetu kwasababu ya ama kutaka kushindana ama ubishoo kama wa ndege!.
P
Nyie wasukuma si ndio zenu hata mkishavuna pamba huwa mnarundika vitu vingi kuwakoga wengine ili mpate sifa za leo na sio kujali kesho ya watoto wenu.Haya tumeyaona sana shinyanga na mwanza radio kubwa,baiskeli mpya,asili ya mtu uathiri maisha yake
 
Litaendelea kama ataendelea kuwa hapo alipo. Akitoka inapotea

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama lilivopita la uchumi wa gesi,kilimo kwanza, nk.Ataingia mwingine utaisikia atauza ndege,ataitelekeza chato,Dodoma na ikulu ya Dodoma itakuwa ya kufugia popo,furusha wahamiaji haramu wote waliofata asali ccm haya yote ufanyika Africa angalau Africa kaskazini ile ya waarabu yaani Algeria, Tunisia,Misri wao wana akili sie maendeleo ni ndoto
 
Tumeshindwa mwendokasi wapewa kila kitu kuanzia njia,abiria,mabus,nk lkn tumeshindwa management sasa sijui kuhusu SGR.
Miradi yote mikubwa haikupita bungeni bali ni vipaumbele vya rais kwa maana kawapumbelia wananchi wawe wanataka au hawavitaki na sio vipaumbele vya wananchi.Miradi mingi huwa inakwama mbali na 10% lkn huwa watumiaji huwa awashirikishwi wao wanalazimishwa kuitumia,mfano mradi wa machinga complex umebuma sababu hakuna machinga aliyeshirikishwa

..mradi hata ungepita bungeni sidhani kama tungepata matokeo au maamuzi tofauti.
 
Kama lilivopita la uchumi wa gesi,kilimo kwanza, nk.Ataingia mwingine utaisikia atauza ndege,ataitelekeza chato,Dodoma na ikulu ya Dodoma itakuwa ya kufugia popo,furusha wahamiaji haramu wote waliofata asali ccm haya yote ufanyika Africa angalau Africa kaskazini ile ya waarabu yaani Algeria, Tunisia,Misri wao wana akili sie maendeleo ni ndoto
Ukwel mchungu

Sent from my TECNO LB6 using Tapatalk
 
Hoja yako ni nzuri hasa kwa sababu inaonyesha kuwa tatizo ulilonalo ni ujinga ambao unahitaji tu kuelimishwa!

Kumbuka ujinga sio tusi kwa sababu mjinga akielimishwa huelimika lakini mpumbavu hawezi kuelimishwa!

Umeandika, ''Hapa lengo langu ni kuangalia umuhimu WA treni ya umeme kama ni sahihi kwa mazingira yetu ya sasa''!

Hutujengi reli ya treni ya umeme kwa mazingira ya sasa bali mazingira ya miaka mingi ijayo.

Kumbuka reli ya kati ambayo unaisifia ilijengwa mwaka 1905 na ninaamini watu kama wewe wa wakati huo walisema hivi hivi kama unavyosema wewe eti ''haifai kwa mazingira ya sasa''

Mwaka 1905 hata Dar hii unayoiona kwa sasa sehemu kubwa ilikuwa pori achilia mbali maeneo mengine katika mikoa ambayo reli ya kati inapita!

James Freeman Clarke aliwahi kusema, ''The difference between a politician and a statesman is that a politician thinks about the next election while the statesman think about the next generation''
Nashangaa mpaka sasa una like 2! Hii inamasnisha nijinsi gani tuna maboya humu yanayo jidai kuwa ni ma great thinkers.

Niunge hoja yako mkono; mleta uzi ni mjinga kama hajakuelewa basi ni mpumba**

Hivi wewe mleta uzi, unaweza kuendeleza kilimo bila miundo mbinu? Hivi Unajua kwanini Kenya wanatushinda kusafirisha bidhaa nje?

Swali lingine hivi train inayotumia masaa kadhaa kufika pahala fulani na inayotumia siku kadhaa ni ipi ina unafuu.

Hivi ninani amekuambia kwamba nauli ya treni ya umeme itakuwa ghali kushinda ya kati?

Nimetamani sana nikutukane lakini roho mtakatifu akanikataza.

NB: hayao malori yenu mtatafuta pa kuyapeleka Ramark

God save us
 
Naunga mkono hoja, tukubali tukatae sisi Tanzania tuna tatizo katika kupanga vipaumbele vyetu kwasababu ya ama kutaka kushindana ama ubishoo kama wa ndege!.
P
Wewe nilikuwa naona watu wanakushambulia humu nikadhani wanakuonea kumbe walikuwa sahihi. Nimekudharau sana.

Njaa ni mbaya sana. Hivi elimu yako ni kiwango gani P?

God save us
 
Back
Top Bottom