Je, tulihitaji treni ya umeme zaidi ya mengine?

Je, tulihitaji treni ya umeme zaidi ya mengine?

Hii nchi ina laana ya asili kwahiyo tuache mzee magu aendelee kukopa na kuwekeza kwenye kitu amabacho mpaka kinakamilika itakuwa imekuja teknolojia nzuri zaidi
 
Naunga mkono hoja, tukubali tukatae sisi Tanzania tuna tatizo katika kupanga vipaumbele vyetu kwasababu ya ama kutaka kushindana ama ubishoo kama wa ndege!.
P
Mkuu sababu ni kuangalia jirani amefanya nini? Lakini tungekuwa tunavipaumbele vyetu kama Taifa tungefanya yetu tu. Sasa tungalizia kwa majirani hii ni tatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JokaKuu nina uhakika unajua kabisa umuhimu wa usafiri katika nchi yoyote na faida zake unazijua. Usafiri ni nyenzo muhimu sana nchi yoyote na faida yake haipimiki. Na usafiri uliyo rahisi na wa uhakika ni reli. Unataka kunimbia hujui faida ya watu kusafiri, kusafirisha mazao na bidhaa nyingine? Ukitaka kufanya mapinduzi ya kilimo unaanza na usafiri wa rahisi na uhakika.
Mbona hamkuanza kuajiri madaktari na manesi kabla ya kujenga hospitality, vituo vya afya na zahanati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Daraja ka kiyegeya linasumbua nchi kwa sasa ba wakati reli ya kati bw. Masanja alishughulikia ndani ya wiki moja kwa kuhamisha njia na ukarabati mkubwa baadae.

Kwanini mnabaki kwenye Barbara na wakati mizigo ingetumia treni ya kawaida tusingekuwa hapo kwenye gharama kubwa ya kurepair daraja ambalo kesho linaharibika tena, mizigo inaharibu barabara na watu walishazungumza humu lkn hatusikii
Mizigo ya watu ingekuwa inafika kwa wakati na labda tungeongeza njia za reli zikawa mbili kwa uhakika ili kuepusha ajali kama ile ya Dodoma hivyo mwanza tren mbili, arusha mbili na kigoma mbili na railways zikawa hivyo hivyo naamin mapato yangekuwa makubwa na watu mabasi tungeyasikia kwa wachache kama miaka ya ya tisin na mwanzon mwa 2000. Naamin mizigo ingekuwa na uhakika hivyohivyo kwa kuwa treni za mizigo za kutosha kukidhi mahitaji yaani ikiwezekana kila siku treni ya mizigo inaondoka kwenda kigoma na mwanza naamin sisi WAkaskazin tusingeagiza kupitia Mombasa maana tungekuwa na uhakika WA bandari ya Dar na mizigo naamin ingefika mapema zaidi ya roli.

Ni hayo tu

Lkn kwa kutokuata katiba kwa serikali yangu ibara 8:-1 (b) ......Ustawi WA wananchi.
Hata Corona si kipaumbele kama utalii na uwekezaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya maamuzi Bora yaliyowahi kufanywa na CCM au Mh Maghufuli ni ujenzi huu wa STD GAUGE.

Ni miongoni mwa zidumu fikra sahihi za aliyebuni na kusimamia ujenzi. Huuu.

Kilichobaki ni kuulinda na kuuenzi. Usafiri huu wa masaa toka Mwanza mpaka Dar .Tena safari zaidi ya 1 kwa siku.

MWENYEZI MUNGU atupe nn? Jamani tuwe watu wa shukrani uwe unakaa linakopita au lisikopita .Hilo linaenda sambamba na ule mraadi mkubwa wa umeme.

Mungu walinde na wajaalie waliofikiria hayo.
 
Nani alikwambia ni treni ya Umeme? Ujinga hasara
 
..nataka kujua kama SGR itaendeshwa kibiashara, itatuletea faida, na itarudisha fedha tulizowekeza.
Mimi sidhani kama kwenye treni tumewekeza kama kitega uchumi. Hii imejengwa kama huduma kwa wananchi, SIYO UWEKEZAJI, ni kama kujenga Hospitali ya wilaya ya Mkuranga.

Uwekezaji huwa unalenga kupata faida, lakini lengo la serikali halikuwa hilo, ilikuwa ni kupata treni itakayokimbia faster ili kuwezesha uwekezaji mwingine huko peripheral(mikoani) wafanyabiashara wawe wanawahi kuchukua mizigo na kuikimbiza huko bara kwa haraka.
 
..kwa hiyo SGR tumelenga kupata HASARA

..na DREAMLINER vilevile lengo letu ni kupata HASARA.

cc misasa
 
Hoja yako ni nzuri hasa kwa sababu inaonyesha kuwa tatizo ulilonalo ni ujinga ambao unahitaji tu kuelimishwa!

Kumbuka ujinga sio tusi kwa sababu mjinga akielimishwa huelimika lakini mpumbavu hawezi kuelimishwa!

Umeandika, ''Hapa lengo langu ni kuangalia umuhimu WA treni ya umeme kama ni sahihi kwa mazingira yetu ya sasa''!

Hutujengi reli ya treni ya umeme kwa mazingira ya sasa pekee bali pia mazingira ya miaka mingi ijayo. Unaweza kuona haina manufaa kwa sasa kwa sababu faida yake kama reli haiwezi kupatikana kwa sasa lakini uwepo wake unajenga mazingira ya uwekezaji kwa ujumla katika nyanja zingine uwe wa kuvutia.

Kumbuka reli ya kati ambayo unaisifia ilijengwa mwaka 1905 na ninaamini watu kama wewe wa wakati huo walisema hivi hivi kama unavyosema wewe eti ''haifai kwa mazingira ya sasa''

Mwaka 1905 hata Dar hii unayoiona kwa sasa sehemu kubwa ilikuwa pori achilia mbali maeneo mengine katika mikoa ambayo reli ya kati inapita!

James Freeman Clarke aliwahi kusema, ''The difference between a politician and a statesman is that a politician thinks about the next election while the statesman think about the next generation''

Umeiweka vizuri sana asante.
 
..kwa hiyo SGR tumelenga kupata HASARA

..na DREAMLINER vilevile lengo letu ni kupata HASARA.

cc misasa
Hapana, hatupati hasara kwa kupata uduma. HASARA gani? Zimejengwa kwa ajili yetu kupata uduma. Faida yetu ni sisi wananchi kutumia.
 
Reli binafsi naiunga mkono maana itasafirisha mamizigo na watu kwa gharama nafuu actually itakomboa wakulima,wafanyabiashara na wafanyakazi kusafiri chapu na bei nzuri. Pia ni uhakika itadumu miaka mingi na itasaidia barabara kuelemewa malori ya mizigo.
Nisahihi kujengwa sasa maana inakomboa makundi mengi tena yachini hakuna uwekezaji sustainable uliofanywa awamu hii kama SGR achana na ndege zisizobeba mizigo bali mabishoo wachache,achana na JNHPP inayosemekana haitodumu nk. SGR ni mkombozi na stimulant wa uchumi.
 
kwa mawazo ya maslahi ya Mtu anayemilikiwa na Jamhuri uko sahihi, Ila kwa Jamhuri inayokumiliki ni Kwamba Reli ikusaidie wewe Mali yake Jamhuri ufanye Mambo yako ya kiuchumu chap chap (accelerate)bila mkwamo ili ustawi wewe, Jamhuri ikusanye Kodi kubwa kwenye kipato chako kilichowezeshwa kuwa kikubwa, faida zitokanazo na nauli sio mchango pekee wa Rail.
..usiseme uduma, sema huduma.

..reli inatakiwa ijiendesha kibiashara, kwa maana irudishe fedha zilizotumika ktk uwekezaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Reli binafsi naiunga mkono maana itasafirisha mamizigo na watu kwa gharama nafuu actually itakomboa wakulima,wafanyabiashara na wafanyakazi kusafiri chapu na bei nzuri. Pia ni uhakika itadumu miaka mingi na itasaidia barabara kuelemewa malori ya mizigo.
Nisahihi kujengwa sasa maana inakomboa makundi mengi tena yachini hakuna uwekezaji sustainable uliofanywa awamu hii kama SGR achana na ndege zisizobeba mizigo bali mabishoo wachache,achana na JNHPP inayosemekana haitodumu nk. SGR ni mkombozi na stimulant wa uchumi.

..Tazara ime-stimulate uchumi kiasi gani?
 
kwa mawazo ya maslahi ya Mtu anayemilikiwa na Jamhuri uko sahihi, Ila kwa Jamhuri inayokumiliki ni Kwamba Reli ikusaidie wewe Mali yake Jamhuri ufanye Mambo yako ya kiuchumu chap chap (accelerate)bila mkwamo ili ustawi wewe, Jamhuri ikusanye Kodi kubwa kwenye kipato chako kilichowezeshwa kuwa kikubwa, faida zitokanazo na nauli sio mchango pekee wa Rail.

Sent using Jamii Forums mobile app

..kodi tunayolipa inaweza isitoshe kuendesha reli na kulipa deni la mkopo wa ujenzi.

..tunaweza kuwa kama mfanyakazi wa mshahara kima cha chini halafu amekwenda kukopa gari la bei mbaya. sasa mfanyakazi huyo mapato yake yote yanaweza kuishia kuhudumia gari tu, na asiweze kuwa na fedha za ziada kufanya mambo mengine ya msingi.

..hoja yangu ni kwamba tuanze kujipanga kuhakikisha reli hii inaendeshwa kwa kibiashara, ili isiwe mzigo kwa walipa kodi.
 
Vitu vya share ni matatizo. Hakuna usafiri bora wa mizigo duniani kama na treni pasipo na meli that's it!!

..sgr tuta-share na rwanda na burundi.

..lakini siyo kila mzigo una faida kusafirishwa kwa reli.

..kuna mizigo inayotoka shambani inapaswa kwenda moja kwa moja kiwandani.

..na kuna mizigo inatoka kiwandani inatakiwa iende moja kwa moja dukani au sokoni.

..swali ni je, tunayo mizigo ya kutosha inayohitaji usafiri wa reli, tena reli iliyojengwa kwa bei mbaya?
 
Back
Top Bottom