Je, teknolojia ya roboti wanaoongea ilikuwepo wakati wa Musa na Haruni kama Kurani?

SANCTUS ANACLETUS

JF-Expert Member
Mar 5, 2016
3,337
4,664
Wanabodi:

Baadhi ya Wanazuoni wa Kiislamu hawataki kukubali kwamba Kurani ina maelezo au masimulizi ya visa ambavyo ama havikuwahi kutokea katika historia ya maisha ya mwanadamu au kwamba visa hivyo haviko kama vinavyoelezwa na Kurani yenyewe.

Leo,ninacho kisa kingine kinachomuhusu Musa na Kaka yake, Haruni, wakiwa na wanaisrael.Kisa hicho, tunakikuta katika Biblia,Agano la Kale,Kutoka Kitabu cha Kutoka 32:1-10:

“1Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.2 Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee.3 Watu wote wakazivunja pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, wakamletea Haruni.4 Akaipokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha; nao wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.5 Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema, Kesho itakuwa sikukuu kwa Bwana.6 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaondoka wacheze.7 Bwana akamwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao,8 wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.9 Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu10 basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize, nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.”

Kurani na yenyewe katika Sura Ta Ha 20: 85-96,inasimulizi lile lile, ila ambalo inaonekana limefanyiwa editing kidogo.Tofauti na inavyoelezwa katika Biblia,katika Kurani Muhammad, anasema aliyewatengenezea Waisrael sanamu ya Ndama huyo ni Msamaria mmoja,ambaye hamtaji jina.Kitu kingine ambacho Muhammad anakisema kuhusiana na kisa hicho, ni kwamba sanamu hiyo ya Ndama ilikuwa na uwezo wa kuongea!Jambo la tatu, ni kwamba eti Mungu ndiye aliyewatega waisrael kuona kama ni wavumilivu,hasa baada ya Musa kuwa amewaacha Waisraeli na kaka yake Haruni,kwa muda mrefu bila kurudi.

SASA, Wasamaria ni akina nani?

Wasamaria wanatajwa kuwepo baada ya utawala wa Israeli kwa upande wa Kaskazini katika Palestina kuangukia mikononi mwa dola ya Assyria mnamo mwaka 722KK na hiyo ni kama karne saba baada ya Musa kuondoka duniani.

Wasamaria ilikuwa ni jamii ya watu waliokuwa wakiishi katika Dola ya Kaskazini mwa Israeli(Northern Kingdom of Israel).Samaria ni jina la mji uliokuwa makao makuu ya Dola hiyo (Ufalme huo) na hivi watu walioshi katika dola hiyo ya Samaria waliitwa Wasamaria.Mji wa Samaria, ulikuwa katikati ya mji wa Galilaya (kwa upande wa kaskazini) na mji wa Yudea(kwa upande wa Kusini).Wasamaria kwa rangi walikuwa mchanganyiko wa Wayahudi na uzao wa wapagani(racially mixed society with Jewish and pagan ancestry).

Kiimani pamoja na kwamba,wasamaria walikuwa wakimuabudu YAHWEH(Mungu, kama Wayahudi walivyokuwa wakimuita), sawa na wayahudi walivyofanya,dini yao haikuwa dini kuu ya Kiyahudi(mainstream Judaism).Wasamaria walikuwa wakivikubali vitabu vitano tu kati ya orodha ya vitabu viliyokuwa vikikubaliwa, na Hekalu lao lilikuwapo katika Mlima Gerazimu(Gerazim) badala ya lile Hekalu la Kiyahudi lililokuwa katika Mlima Sioni,kule Yerusalemu kama tusomavyo katika Injili ya Yohana 4:9,20-21:

“9Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.20 Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. 21Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu.”

Wasamaria wa nyakati za Yesu walikuwa wakiamini kwa dhati juu ya Mungu mmoja kuliko hata Wayahudi wenyewe na namna fulani walikuwa wameshika sana sheria za Musa kuliko hata Wayahudi,kwa namna ya pekee,suala la Sheria za Sabato.Tofauti ya Wayahudi na Wasamaria ilikuwa ni kwamba wayahudi hawakuruhusiwa kutamka jina takatifu la Mungu “YAHWEH” katika viapo, isipokuwa aliyeruhusiwa kufanya hivyo alikuwa Kuhani Mkuu tu,tena akiwa huko patakatifu pa patakatifu,tena mara moja kwa mwaka na hiyo ilikuwa katika siku ile ya toba ya taifa (ndiyo,Yom Kippur). Wasamaria wao kutamka jina takatifu “YHWH” (soma “YAHWEH” ) kwa sauti au kimya kimya halikuwa tatizo hata kidogo.`

Kwa hiyo, Wayahudi wote wa kawaida hawakuwa na ruhusa na hata leo bado hawaruhusiwi kusoma, si kwa sauti tu wala kimya kimya,herufi za jina takatifu la Mungu, YHWH, kwa sababu ya utakatifu wa jina la Mungu wao. Kwa nini? Kwa sababu kuzisoma bure bure kungelingana na utovu wa heshima kwa Mungu mkuu na kuivunja amri ya Mungu ya kutolitaja bure jina lake, DECALOGUE. Ndiposa, ilikuwa marufuku na bado ni marufuku kabisa Myahudi wa kawaida kuzisoma na kuzitamka herufi hizo.

Kwa hiyo,kutokana na wasamaria kuonekana hawashiki sawa sawa dini ya Kiyahudi na kwamba walikuwa na vinasaba vya damu ya kipagani,basi walikuwa wakidhauriwa na kutengwa na wayahudi wa Kawaida.Na ndiyo maana utashangaa kwa nini wayahudi walipokuwa wakisafiri kutoka Yudea kwenda Galilaya au Galilaya kwenda Yudea,walilazimika kuvuka mto Jodani kisha kuambaaambaa ng’ambo ya Jodani na kisha kuvuka tena mto Jodani walipokaribia kufika Galilaya au Judea ili kukwepa kupitia ardhi ya Samaria kwa kukwepa wasije wakanajisika. Kwa hali hiyo,wayahudi hawakuchangamana na wasamaria na walijengeana chuki au uhasama dhidi ya Wayahudi wa kawaida. Ni kutokana wasamaria na ni kwa mazingira haya,ndiyo kisa hata Yesu alinyimwa sehemu ya kulala katika Kijiji kimoja walipokuwa wakiishi Wasamaria, kwa sababu tu ya Uyahudi wake na wala si kwa sababu hakuwa na uwezo wa kulipia sehemu hiyo.Soma Luka 9:51-56:

“51 Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu;52 akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.53 Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.54 Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?55 Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]56 Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa.Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.”


Maswali ya Kujiuliza:

  • Je,Muhammad anaposema kuwa Msamaria alimshika Unyayo,anataka kuieleza na kuiaminisha jamii ya Kiislamu kwamba wakati sanamu ya ndama huyo inatengenezwa yeye alikwisha kuzaliwa, hata iwezekane kwa huyo msamaria kumshika unyayo kabla ya kumuunda ndama huyo?

  • Kwa namna inavyosimuliwa katika aya hiyo nukuliwa ya Kurani,mbona inatoa tafsiri kuwa yeye Muhammad alikuwa sehemu ya mchakato wa kuwezesha kuundwa kwa sanamu hiyo baada ya kuwa ameguswa unyayo wake? Na kama ndivyo,je,Muhammad haoni kama na yeye alikuwa ni sehemu ya kumkufuru Mungu sawa na yule msamaria?

  • Je,ikiwa Muhammad ni mtume wa mwenyezimungu (na msamaria aliwaundia waisrael sanamu iliyochukua nafasi ya Mungu, jambo ambalo ni kufuru),iliwezekanaje kwa Muhammad kukubali kushikwa unyayo na msamaria ambaye alikuwa na nia ovu ya kuwapotosha waisrael kwa kuwaundia kikaragosi cha Mungu?

  • Je, simulizi la Kisa hiki nalo limetumia lugha ya picha kama ilivyo katika kisa cha ndege na mchwa kutumika kama wanamgambo, kama tulivyoelezwa na wanazuoni wa Kiislamu katika mjadala uliopita, wa Ndege kutumika kama maaskari katika vita?

  • Je,kwa kuchukulia kweli kwamba msamaria ndiye aliyeunda roboti ya ndama iliyokuwa inaongea,msamaria huyo alikuwa na nguvu za kutenda miujiza? Na kama msamaria hakuwa na uwezo huo wa kimiujiza,je, alitumia tekinolojia gani wakati huo kuweza kuunda sanamu iliyokuwa inaoongea?

  • Historia inaonyesha Muhammad alizaliwa mwaka 570BK na kufariki dunia mwaka mnamo tarehe 8 Juni 632BK. Na Musa na Haruni(pamoja na huyo msamaria aliyetengeneza roboti la Ndama), waliishi miaka mingi sana kabla ya Yesu. Je,iliwezekanaje kwa huyo msamaria kuweza kumshika mtume unyayo katika mchakato wa kuliunda lile roboti wakati Mtume(Muhammad) hakuwa amezaliwa bado?

  • Je,kwa kadri ya historia ya uhasama kati ya Waisraeli na Wasamaria,na iwapo tukizingatia maelezo ya Muhammad, iliwezekanaje kwa Waisraeli kuweza kuchangamana na huyo msamaria, hata waweze kukubali kutengenezewa sanamu(roboti) na adui yao?

  • Kwa kuwa Kurani ni maneno ya Mungu yaliyoshushwa moja kwa moja kwa Muhammad(bila editing yoyote) toka kwa Mungu,je, kwa kisa hiki ambacho imeonekana ni uongo wa kihistoria,ni nani muongo?Ni Mungu anayedaiwa kumpelekea Muhammad Kurani au ni Muhammad tu ndiye alijisingizia kuwa Kurani ni maneno ya moja kwa moja,ambayo hayahaririwa,toka kwa Mungu?
Kwa maswali haya pamoja na mengineyo munayoweza kuongezea,nawakaribisheni,sasa kwa mjadala.
 
Kurani imeandikwa na mtu baada ya kusoma biblia....

Alibadili visa kadhaa na kuja mbadala wa kitu Fulani!

Wanazuoni wa kiislamu wanadai iliandikwa na Mungu na kisha akampatia malaika Jibrili(Gabrieli?) bila kufanya editing yoyote ile akampasia Muhammad na Muhammad akiisha kuipokea, hakuwahi kuichezea na hata leo waislamu hawajaichezea aslani.
 
Wanazuoni wa kiislamu wanadai iliandikwa na Mungu na kisha akampatia malaika Jibrili(Gabrieli?) bila kufanya editing yoyote ile akampatia Muhammad na Muhammad akiisha kuipokea, hakuwahi kuichezea na hata leo waislamu hawajaichezea aslani.
Huo ni urongo wa mchanamchana,kurani ni mwandiko wa mtu aliyeihariri biblia na kuleta kitabu chake.
 
Nitatoaje hitimisho, mkuu,wakati maswali niliyouliza hayajajibiwa?
Biblia haiwezi kuwa reference ya Quran. Wapo walioanza kupinga Quran a thousand years ago....wewe sio wa mwanzo. Waachie wenyewe dini yao. Unatumia zaidi ubongo wako kutafsiri maandiko huku ukiwa tayari na majibu yako. Namna hii hautafanikiwa.

Dini ni matokeo ya kuzaliwa tu na wazazi wa dini fulani. Tuthibitishie hapa wewe kama ulipewa fursa ya kuchagua dini utakayo na walio kulea. Upunguani ulioje kuwakejeli wenzio kwa dini ambazo mmepangiwa tu?

Jiangalie Kubwa Jinga weye.

Sent using my NOKIA torch
 
Biblia haiwezi kuwa reference ya Quran. Wapo walioanza kupinga Quran a thousand years ago....wewe sio wa mwanzo. Waachie wenyewe dini yao. Unatumia zaidi ubongo wako kutafsiri maandiko huku ukiwa tayari na majibu yako. Namna hii hautafanikiwa.

Dini ni matokeo ya kuzaliwa tu na wazazi wa dini fulani. Tuthibitishie hapa wewe kama ulipewa fursa ya kuchagua dini utakayo na walio kulea. Upunguani ulioje kuwakejeli wenzio kwa dini ambazo mmepangiwa tu?

Jiangalie Kubwa Jinga weye.

Sent using my NOKIA torch

Mkuu,Sijakuelewa kabisa.Mbona umeingia katika Fallacy of Irrelevance? Ndio kusema umeacha hoja ya msingi na wewe umejenga hoja nyingine mpya.Sawa,Biblia siyo reference ya Kurani, lakini mbona munasema Biblia ilitabiri kuja kwa Mtume Muhammad katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 18:18-19:

"“18 Nitawateulia miongoni mwa ndugu zao wenyewe nabii kama wewe; nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.19 Yeyote ambaye hatasikia maneno atakayosema nabii huyo kwa jina langu, mimi mwenyewe nitamwadhibu.”

Na tena mwasema Yesu Kristu aliposema katika Agano Jipya kuwa "nitawaleteeni msaidizi baada yangu..." eti alikuwa akimtabiria Muhammad?

Je,kama Biblia haina mafungamano na Kurani, ni kwa nini mnaitumia katika kumthibitishia Muhammad utme wake?
 
mkuu nondo zako huwa hazijibiki kwa hoja, znajibika kwa vitisho na matusi tu

Na ndio maana tunaendelea kuleta hoja zingine zaidi.

Tumewakusudia wanazuoni wa kiislamu wathibitishe kweli kwamba Mungu ndiye chimbuko la Uislamu na kama ndiye ni kweli yeye anaweza akawa amewafunulia waislamu njia ya matusi badala ya hoja na busara katika kuwajibu wale walio na mashaka na ujumbe fulani katika Kurani yake?

Ikiwa wanazuoni, wanaanza na kuishia kuporomosha matusi badala ya kujibu hoja,wanakusudia kutufundisha kwamba huo msingi wa matusi umo katika Kurani?
 
Mkuu,Sijakuelewa kabisa.Mbona umeingia katika Fallacy of Irrelevance? Ndio kusema umeacha hoja ya msingi na wewe umejenga hoja nyingine mpya.Sawa,Biblia siyo,reference ya Kurani, lakini mbona munasema Biblia ilitabiri kuja kwa Mtume Muhammad katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati 18:15-18:

"“18 Nitawateulia miongoni mwa ndugu zao wenyewe nabii kama wewe; nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.19 Yeyote ambaye hatasikia maneno atakayosema nabii huyo kwa jina langu, mimi mwenyewe nitamwadhibu.”

Na tena mwasema Yesu Kristu aliposema katika Agano Jipya kuwa "nitawaleteeni msaidizi baada yangu..." eti alikuwa akimtabiria Muhammad?

Je,kama Biblia haina mafungamanon na Kurani, ni kwa nini mnaitumia katika kumthibitishia Muhammad utme wake?
Wapi mimi nimekwambia ni Muislamu? Hizo dini zenu za kuletewa ni upuuzi kubishana hapa. Huo muda unaotumia kuandika thread ndefu ungesoma kitu fulani ukaongeza maarifa. Waachie dini yao.

Wewe una Mungu wako na wao wana Mungu wao. Hawaatabudu unachoakiabudu na wewe hutaabudu wanachokiabudu.

Lengo la hizi nyuzi zako nini haswa?

Sent using my NOKIA torch
 
Sawa mkuu.

Hebu tusaidie, Kwa maoni yako,kwa uweledi wako, tekinolojia hiyo ya kuunda roboti zinazoongea (kama ambavyo tumeshuhudia hivi karibuni,wachina wakiunda roboti zinazoweza kusalimia au kukaribisha wateja dukani), ilikwisha kuwepo duniani wakati wa Haruni na Musa?
hakuna kitu kama hicho labda kama ilitumika magic fulani
 
Hebu subiria,wanazuoni wa Kiislamu waje watupatie ukweli wa mambo kupitia kisa hiki.Nina imani mada hii leo itatupatia mwanga na pengine kukata mzizi wa ubishi.
Tatizo lako hoja zako ni za upande mmoja, na ule mwingine unaishia kutaja madhaifu kwa namna akili yako inavokutuma...
Kwa mtu yoyote ambaye haujui uislamu, ukristo wala dini nyingine yoyote akisoma bandiko lako ataishia kuutuka tu uislamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe mpumbavu tu unayetafuta maarufu. Kuna mwenzio mgen mpaka leo hajafanikiwa lolote seuze wewe? Acheni upuuzi wenu.

Sent using my NOKIA torch
 
Back
Top Bottom