Uchaguzi 2020 Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli...

Wanabodi,

Kipenga cha kuanza kwa kampeni za Uchanguzi Mkuu ujao kimepulizwa leo na fungua dimba amekuwa Chadema.
Nimeangalia kidogo kupitia live ya TBC, kiukweli nilichoshuhudia, ndicho kimenipelekea mimi kuanzisha huu uzi ambao ni swali.

Je, Tanzania tuna upinzani wa kweli, upinzani makini, wenye the ability, the capacity and the capabilities za kuleta upinzani wa kweli wenye uwezo wa kuing'oa CCM madarakani?, au upinzani wetu hapa Tanzania ni bado sana?.

Nimeuliza hivi kufuatia nilichokishuhudia leo, kwenye uzinduzi kampeni za Chadema, pale uwanja wa Mbagala Zakhem, kiukweli ...
kwa vile na mimi siku hizi ni kada, kuna vitu naomba nisiviseme nikaonekana ni kupiga siasa!.

Kwanza natoa hongera kwa Television ya Taifa, TBC kutangaza live uzinduzi huo wa kampeni za Chadema!. Japo matangazo yenyewe ni kwa kukata kata, lakini something is better than nothing!.

Je, kitendo alichofanya M/Kiti Mbowe, kuwafukuza live TBC, huku wakiwa live ni sawa?!.

Nimetoa pongezi na hongera kwa TBC kutangaza live matangazo ya uzinduzi kampeni za Chadema!, ile tuu TBC kukubali kutangaza live uzinduzi wa Chadema huku unajua kabisa watu wa type yao ni wasemji wa namna gani!, huku Mbowe, huku Lissu, huku Lema, na bado TBC ikakubali kuwapa live, hatua hii pekee, inastahili pongezi.

Lakini Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Mbowe aliposimama kuzungumza, aliwafukuza live TBC huku wakiwa live hewani!. Kitendo alichofanya Mwenyekiti Mbowe, cha kuwafukuza TBC, sio sawa, it is not right, hajaitendea haki TBC, hajaitendea haki media, hajaitendea haki Chadema, hajawatendea haki Watanzania kukosa kusikia sera za Chadema.

Hasira za Mkizi kwenye siasa, kiukweli kabisa hazisaidii kitu!.

Wakati Mhe Mbowe anasema TBC wamekata matangazo, TBC ilikuwa iko live wakati Mhe. Mbowe akitangaza kuwafukuza na kuwasingizia kuwa TBC wamekata matangazo, ilikuwa sii kweli kwasababu TBC walikuwa live kabisa na hawajakata matangazo!, kitendo cha Mwenyekiti Mbowe kuwafukuza TBC na kuwaambia TBC waondoke, sio kitendo cha kistaarabu, hakikubaliki, vyama vya habari tusilinyamazie hili, Mhe. Mbowe akemewe, Chadema ikemewe, na TBC ipongezwe kwa kujaribu.

Kitu ambacho ni kweli nilikiona ni TBC kuwa na kibarua kigumu cha kufanya censorship matamshi yoyote hatarishi na ya kichochezi. Sii wengi wanajua kuwa kwenye matangazo ya live, mtu ambaye yuko responsible na kinachorushwa hewani, sio yule msemaji, bali ni mrusha matangazo, yaani TBC, hivyo mwanasiasa anapoibuka na kutoa kauli za kiajabu ajabu, ambazo ni za uchochezi au kuhatarisha amani, utulivu na mshikamano wetu, then TBC wanakuwa hawana jinsi zaidi ya kufanya censorship, ndio maana matangazo yalikuwa yanakatwa katwa na kurudishwa studio.

NB. Ikitokea Chadema ikashindwa kwenye uchaguzi, isilalamike kuwa CCM imebebwa na TBC ndio maana ikashinda, Chadema wamepewa fursa ya kuitumia TBC, Chadema wenyewe ndio wamekataa na kuwafukuza TBC, hivyo sasa wanategemea nini?.

Hizi ni Hasira za Mkizi!

Hata hivyo, TBC tunapoelekea kwenye uchaguzi wa vyama vingi, TBC inatakiwa iji redifine its role kwenye uchaguzi, wengi wanaidhania TBC kuwa ni TV ya serikali!, kiukweli, TBC japo inagharimiwa na serikali sio kama TV yake, TBC sio TV ya serikali, TBC na RTD ni Public Broadcasting Stations, ambayo ni TV ya umma na Redio ya umma ambayo is paid by taxpayers money kutoka serikalini lakini inatakiwa kuwatumikia Watanzania wote , wa vyama vyote kwa haki sawa na kwa usawa bila upendeleo unaoonekana kwa CCM kupendelewa zaidi!.

TBC inabidi iwatumikie watu wote ikiwemo serikali na sio kuitumikia serikali as if kwasababu ni malí yake, TBC sio mali ya serikali ni mali ya umma kwa udhamini wa serikali kama ilivyo BBC!. Vyombo vya habari vya serikali ni gazeti la Daily News, Habari Leo, Idara ya Habari Maelezo, na The Government Gazzette.

Kwa hali ya siasa ilivyo sasa, TBC is as if inaipendelea sana serikali na CCM kwa kurusha matukio ya serikali au ya CCM bila any censorship lakini kwenye mikutano ya upinzani kwa kufanya censorship ya kiana kwa kurejea studio.

Viongozi wa TBC na viongozi serikali wanapaswa kuiwezesha TBC kwa rasilimali watu na rasilimali fedha kuweza kuwatumikia wananchi wote Watanzania kikamilifu na hata kuisaidia serikali kwa kuweka vipindi critical kwa serikali ambavyo vitafanya a constructive criticism kwa lengo la kujenga na sio kubomoa na huko ndiko kuisaidia serikali kiukweli.

Na nyinyi CCM na waserikali, msiitumie TBC as if ni TV yenu tuu au ni mali yenu. TBC ni TV yetu sisi sote Watanzania, tuna wajibu wa kuhakikisha Watanzania wote, tunapata excess ya kuitumia TBC kwa manufaa ya taifa na sio kama ilivyo sasa, kutumika zaidi kwa manufaa ya serikali mpaka wengi wakiidhania TBC ni TV ya Serikali, kitu ambacho sio cha kweli!. TBC ifungue zaidi milango yake ya vipindi kwa kuruhusu vipindi kutoka outside kwa independent producers na production houses ili kupata diversity na good mix from the society.

Wito kwa wapinzani, mnapapata fursa za kuwa coved live, mna wajibu wa kuwa wastaarabu kwa kutangaza sera, na kutumia lugha za staha na sio lugha za kuudhi.

Ndio maana nimeuliza, kama upinzani wenyewe ndio huu tuliouona kwa Chadema, halafu hawa ndio watu wanaotaka Watanzania tuwape Ikulu yetu watutawale, kama hata kujitawala wenyewe tuu ni issue, hili la kuwapa nchi, itakuwaje?

Namalizia kwa lile swali la msingi la bandiko hili, jee Tanzania tuna upinzani wa kweli, upinzani makini, wenye the ability, the capacity and the capabilities za kuleta upinzani wa kweli wenye uwezo wa kuing'oa CCM madarakani na wenyewe kutawala nchi yetu?, au upinzani wetu hapa Tanzania kiukweli kabisa ni bado sana?

Paskali
Kweli umejitoa ufahamu, Siku zote nasema kuitetea ccm inakupasa uwe na akili mwendawazimu
 
Mie naona Sawa tu mkutano Ni wa chadema wanao Uhuru wa kusema wewe ondoka wewe Baki, hata angeenda makonda wangemwambia toka na akatii, chamsingi wasije lalamika kuwa TBC hawarushi taarifa zao
 
Na nyinyi CCM na waserikali, msiitumie TBC as if ni TV yenu
Sisi ccm tuna channel ten na redio Uhuru,usituingize huko
Vyombe vya habari vinapaswa vigomee mikutano yote ya chadema kuonesha mshikamano,ingekua suala hili limefanywa na ccm kwa chombo binafsi tungesikia kelele nyingi sana
 
Huyu nae ni mwandishi wa habari...Yani nimekuwa nikikufatilia sn kwa muda kwa sbb nilikuwa bado kuna vitu na-kuasses...leo nimejiridhisha njaa haina baunsa na TANZANIA inaweza kuwa nchi ya Kwanza duniani yenye watu wanafiki...MAYALLA wewe ni mwandishi wa habari kweli!

Au njaa na unafiki...Hivi yote yanayowatokea wapinzani mpaka Sasa hujaona mahala pa wewe km mwandishi kuandika Jambo...ila umekereka jinsi TBC walivyokumbushwa unafiki wao...najua kuna Sheria ya maudhui ambayo pia ni hovyo (ndo mana clouds wamefungiwa lkn gazeti la uhuru halijafungiwa kwa kuripoti kitu kilekile na siku hiyohiyo.)..UNAFIKI...nimefatilia namna tbc walivyokumbushwa wakirusha matangazo ...hata mm nilikuwa natamani kuingia ndani ya tv niwachape...

Hivi kurusha kitu LIVE maana yake nn?...mbowe anaongea wao wanaendelea na uchambuzi...kisa maudhui....NGOJA TUONE KESHO,, MATANGAZO YATARUSHWA LIVE KUANZIA KUFAGIA UWANJA, KUPAKI MAGARI, KUKATA VIUNO MPAKA GIZA NA HAKUTAKUA NA INTERAPTION.. kwa mantiki hii Leo nahitimisha utafiti wangu kuwa Paskalia ni UTOPOLO

Kwa kweli watu wa jinsi ya Mayalla wanakera sana!
 
Nilidhani kuwa huu ndio mtazamo wako.
'You are not supposed to be so blind with patriotism that you can't face reality. Wrong is wrong no matter who says it'. Malcom X
Hivi hii 'quote' inaendanaje na uliyobwabwaja juu?

Tena sana

Umetumia neno bwabwaja

Ni kuwa hauko comfortable kabisa na moyo wako, kuna kitu kinakusuta, ila hauwezi kuongea

Rudi nyuma naongea lolote lenye ukweli wowote ule
 
Suppose ni kweli Watanzania wakiamua kuipumzisha CCM, kwa maoni yako, ni chama gani kinaweza kukabidhiwa Ikulu yetu kikaendesha nchi?.
P
Chama cha Mboe.
Nadhani siasa ya vyama vingi itaanza rasmi baada ya chama kimojawapo cha upinzani kushinda.Tutapata NEC mpya na katiba mpya na maendeleo ya haraka zaidi.
 
Suppose ni kweli Watanzania wakiamua kuipumzisha CCM, kwa maoni yako, ni chama gani kinaweza kukabidhiwa Ikulu yetu kikaendesha nchi?.
P
Vyama vyote vina mechanisms vinaweza kuongoza nchi, wanasiasa ni wachache kuliko Raia wa ujumla, wataalam wapo wa kila sekta sio lazima wawe ktk vyama, kikubwa ni kutengeneza sera zinazoeleweka, kutekelezeka na kuzisimamia
 
Chama gani hicho chenye hizo sera zinazoeleweka, kutekelezeka na kuzisimamia ?
P
 
Wanabodi,

Kipenga cha kuanza kwa kampeni za Uchanguzi Mkuu ujao kimepulizwa leo na fungua dimba amekuwa Chadema.
Nimeangalia kidogo kupitia live ya TBC, kiukweli nilichoshuhudia, ndicho kimenipelekea mimi kuanzisha huu uzi ambao ni swali.

Je, Tanzania tuna upinzani wa kweli, upinzani makini, wenye the ability, the capacity and the capabilities za kuleta upinzani wa kweli wenye uwezo wa kuing'oa CCM madarakani?, au upinzani wetu hapa Tanzania ni bado sana?.

Nimeuliza hivi kufuatia nilichokishuhudia leo, kwenye uzinduzi kampeni za Chadema, pale uwanja wa Mbagala Zakhem, kiukweli ...
kwa vile na mimi siku hizi ni kada, kuna vitu naomba nisiviseme nikaonekana ni kupiga siasa!.

Kwanza natoa hongera kwa Television ya Taifa, TBC kutangaza live uzinduzi huo wa kampeni za Chadema!. Japo matangazo yenyewe ni kwa kukata kata, lakini something is better than nothing!.

Je, kitendo alichofanya M/Kiti Mbowe, kuwafukuza live TBC, huku wakiwa live ni sawa?!.

Nimetoa pongezi na hongera kwa TBC kutangaza live matangazo ya uzinduzi kampeni za Chadema!, ile tuu TBC kukubali kutangaza live uzinduzi wa Chadema huku unajua kabisa watu wa type yao ni wasemji wa namna gani!, huku Mbowe, huku Lissu, huku Lema, na bado TBC ikakubali kuwapa live, hatua hii pekee, inastahili pongezi.

Lakini Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Mbowe aliposimama kuzungumza, aliwafukuza live TBC huku wakiwa live hewani!. Kitendo alichofanya Mwenyekiti Mbowe, cha kuwafukuza TBC, sio sawa, it is not right, hajaitendea haki TBC, hajaitendea haki media, hajaitendea haki Chadema, hajawatendea haki Watanzania kukosa kusikia sera za Chadema.

Hasira za Mkizi kwenye siasa, kiukweli kabisa hazisaidii kitu!.

Wakati Mhe Mbowe anasema TBC wamekata matangazo, TBC ilikuwa iko live wakati Mhe. Mbowe akitangaza kuwafukuza na kuwasingizia kuwa TBC wamekata matangazo, ilikuwa sii kweli kwasababu TBC walikuwa live kabisa na hawajakata matangazo!, kitendo cha Mwenyekiti Mbowe kuwafukuza TBC na kuwaambia TBC waondoke, sio kitendo cha kistaarabu, hakikubaliki, vyama vya habari tusilinyamazie hili, na mkinyamaza nitawashangaa!, maana kwa wafuasi wa Chadema ninaowafahamu mimi, kitendo cha TBC kutoka salama mahali pale baada ya amri batili ya Mhe. Mbowe ni cha kushukuru Mungu, maana wangeweza kufanya chochote. Media ni kama Red Cross vitani, hawapasi kufukuzwa kivile!. Mhe. Mbowe akemewe, aombe radhi, Chadema ikemewe, ifunzwe kauli za kutoa kwenye live Broadcasting, na TBC ipongezwe kwa kujaribu, ila pia TBC ifunzwe political tolerance, na managing political diversity na kuepuka double standards kwa kuipendelea CCM!, kesho shuhudieni ufunguzi wa kampeni za CCM, muone kama matangazo ya CCM yatakatwa katwa kama ya Chadema, wakati kiukweli kuna wakati hata viongozi wa CCM wanasema vitu ambayo sio!.

Hili la viongozi kusema sema, niliwahi kushauri
Je, aachwe aseme tu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?!.

Kitu ambacho ni kweli nilikiona ni TBC kuwa na kibarua kigumu cha kufanya censorship matamshi yoyote hatarishi na ya kichochezi. Sii wengi wanajua kuwa kwenye matangazo ya live, mtu ambaye yuko responsible na kinachorushwa hewani, sio yule msemaji, bali ni mrusha matangazo, yaani TBC, hivyo mwanasiasa anapoibuka na kutoa kauli za kiajabu ajabu, ambazo ni za uchochezi au kuhatarisha amani, utulivu na mshikamano wetu, then TBC wanakuwa hawana jinsi zaidi ya kufanya censorship, ndio maana matangazo yalikuwa yanakatwa katwa na kurudishwa studio.

NB. Ikitokea Chadema ikashindwa kwenye uchaguzi, isilalamike kuwa CCM imebebwa na TBC ndio maana ikashinda, Chadema wamepewa fursa ya kuitumia TBC, Chadema wenyewe ndio wamekataa na kuwafukuza TBC, hivyo sasa wanategemea nini?.

Hizi ni Hasira za Mkizi!

Hata hivyo, TBC tunapoelekea kwenye uchaguzi wa vyama vingi, TBC inatakiwa iji redifine its role kwenye uchaguzi, wengi wanaidhania TBC kuwa ni TV ya serikali!, kiukweli, TBC japo inagharimiwa na serikali sio kama TV yake, TBC sio TV ya serikali, TBC na RTD ni Public Broadcasting Stations, ambayo ni TV ya umma na Redio ya umma ambayo is paid by taxpayers money kutoka serikalini lakini inatakiwa kuwatumikia Watanzania wote , wa vyama vyote kwa haki sawa na kwa usawa bila upendeleo unaoonekana kwa CCM kupendelewa zaidi!.

TBC inabidi iwatumikie watu wote ikiwemo serikali na sio kuitumikia serikali as if kwasababu ni malí yake, TBC sio mali ya serikali ni mali ya umma kwa udhamini wa serikali kama ilivyo BBC!. Vyombo vya habari vya serikali ni gazeti la Daily News, Habari Leo, Idara ya Habari Maelezo, na The Government Gazzette.

Kwa hali ya siasa ilivyo sasa, TBC is as if inaipendelea sana serikali na CCM kwa kurusha matukio ya serikali au ya CCM bila any censorship lakini kwenye mikutano ya upinzani kwa kufanya censorship ya kiana kwa kurejea studio.

Viongozi wa TBC na viongozi serikali wanapaswa kuiwezesha TBC kwa rasilimali watu na rasilimali fedha kuweza kuwatumikia wananchi wote Watanzania kikamilifu na hata kuisaidia serikali kwa kuweka vipindi critical kwa serikali ambavyo vitafanya a constructive criticism kwa lengo la kujenga na sio kubomoa na huko ndiko kuisaidia serikali kiukweli.

Na nyinyi CCM na waserikali, msiitumie TBC as if ni TV yenu tuu au ni mali yenu. TBC ni TV yetu sisi sote Watanzania, tuna wajibu wa kuhakikisha Watanzania wote, tunapata excess ya kuitumia TBC kwa manufaa ya taifa na sio kama ilivyo sasa, kutumika zaidi kwa manufaa ya serikali mpaka wengi wakiidhania TBC ni TV ya Serikali, kitu ambacho sio cha kweli!. TBC ifungue zaidi milango yake ya vipindi kwa kuruhusu vipindi kutoka outside kwa independent producers na production houses ili kupata diversity na good mix from the society.

Wito kwa wapinzani, mnapapata fursa za kuwa coved live, mna wajibu wa kuwa wastaarabu kwa kutangaza sera, na kutumia lugha za staha na sio lugha za kuudhi.

Ndio maana nimeuliza, kama upinzani wenyewe ndio huu tuliouona kwa Chadema, halafu hawa ndio watu wanaotaka Watanzania tuwape Ikulu yetu watutawale, kama hata kujitawala wenyewe tuu ni issue, hili la kuwapa nchi, itakuwaje?

Namalizia kwa lile swali la msingi la bandiko hili, jee Tanzania tuna upinzani wa kweli, upinzani makini, wenye the ability, the capacity and the capabilities za kuleta upinzani wa kweli wenye uwezo wa kuing'oa CCM madarakani na wenyewe kutawala nchi yetu?, au upinzani wetu hapa Tanzania kiukweli kabisa ni bado sana?

Paskali
Mgombea wetu wa CCM akiwa Zanzibar anawaeleza Wazanzibar kuwa wasiondoke uwanjani hapo maana akimaliza hotuba bado Kuna show kabambe kutoka kwa wasanii na watamuona nae akicheza.... Wazenji nao viburi wakaondoka wakati anazungumza. Aisee!
 
Back
Top Bottom