Je, taarifa binafsi (Mitihani na CV's) zinazotumiwa kama vifungashio na wafanyabiashara zinatoka wapi?

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,563
Taarifa Binafsi ni maelezo fulani ambayo yanamtambulisha mtu, au kueleza jambo fulani kuhusu maisha yake.

Taarifa Binafsi huweza kuwa majina ya mtu, namba ya simu, mwaka na tarehe ya kuzaliwa, dini, kabila, mahali anapoishi na mengineyo yanayombainisha mtu fulani.

Aidha, vifungashio navyovizungumzia hapa ni jumla ya vifaa vyote ambavyo wanavitumia wafanyabiashara kwa ajili ya kuwafungia bidhaa mbalimbali wateja wao kama vile karatasi au bahasha.

Nikirudi kwenye mada yangu ni kwamba nimeshuhudi kuwapo kwa wimbi kubwa la wafanyabiashara kuwafungia wateja bidhaa mbalimbali kwa kutumia vifungashio mbalimbali vyenye taarifa binafsi za watu.

Wafanyabiashara wengi mitaani kwetu unaponunua ukinunua bidhaa kama maadazi au chips muuzaji kuna wakati wanakufungia kwa kutumia makaratasi au bahasha zenye taarifa Binafsi za watu fulani. Mfano, mitihani au nakala za kazi za watu fulani (barua za kikazi na CV's) karatasi za benki nk.

Je, Kuna ubaya wowote wa taarifa hizi kutumika katika vifungashio wazi?
Jibu ni ndio kuna unaya mkubwa sana. Jambo hili huenda lisionekane zito au baya kwako endapo tu halijakupata. Nitajatibu kukupitisha kwenye mifano hii mitatu ili uhisi ubaya wa jambo hili ukoje:

1. Chukulia Mfano unakutana na mtihani wako uliofanya ukiwa shuleni na ukawa ulipata maksi mbaya sana labda 0/100 umetumika kumfungia maandazi jirani yako mtaani anayekujua utajisikiaje?

2. Chukulia Mfano barua ya kazi na CV yako uliyoituma sehemu ukaikuta imefungiwa chips kwenye kibanda fulani mtaani kwako kwa watu wanaokujua utajisikiaje?

3. Chukulia Mfano tapeli wa mtandaoni, au tapeli anayetumia taarifa za watu kujinufaisha anafungiwa bidhaa kwa karatasi yenye namba zako za simu, majina yako kamili na pengine mtaa unaokaa itakuaje?

Mifano ipo mingi lakini natumai kwa hii michache inatosha kwako kuhisi ubaya wa kuanikwa kwa taarifa zako Binafsi hasa hizi zilizo kwenye vifungashio.

Kwa ufupi, Uanikaji wa taarifa Binafsi za watu kwa namna yoyote ni mbaya na hatari sana kwa usalama wa mtu husika na pia ni uvunjifu wa haki ya falagha ya mtu husika. Kila mtu ana taarifa zake Binafsi ambazo hapendi au hayupo tayari kabisa watu wengine wazijue. Mathalani, sio kila mtu anapenda namba zake simu, majina yake kamili, umri wake na elimu yake itambuliwe na kila mtu.

Hivyo, kupitia andiko hili natoa wito kila mtu kwa nafasi yake akemee matumizi ya vifungashio hivi vyenye taarifa za watu.

Sambamba na hilo, natoa wito kwa taasisi mbalimbali zikwamo Vyuo, Shule na Ofisi kuziteketeza taarifa Binafsi za watu baada ya kumaliza kuzitumia kuliko kuzigawa kwa wafanyabiashara.

Ulinzi wa data Binafsi ni jukumu langu na lako, tuungane kuelimisha na kupambana na tabia zote zinazopelekea kuanika taarifa za watu.

Alamsiki
 
Lakini siku hizi mambo mengi si yanakua online ndugu? Maana wengi wanasema utume taarifa zako kwa email hasahasa cv na cover letter af incase wakikuita kwenye intavyuu unaenda na vyeti vyako kuthibitishwa
 
Kwan online, hawa print CV na Barua za kazi??
 
Lakini siku hizi mambo mengi si yanakua online ndugu? Maana wengi wanasema utume taarifa zako kwa email hasahasa cv na cover letter af incase wakikuita kwenye intavyuu unaenda na vyeti vyako kuthibitishwa
Sio kampuni zote zinapokea taarifa kwa njia ya dijitali
 
Taarifa Binafsi ni maelezo fulani ambayo yanamtambulisha mtu, au kueleza jambo fulani kuhusu maisha yake.
Taarifa Binafsi huweza kuwa majina ya mtu, namba ya simu, mwaka na tarehe ya kuzaliwa, dini, kabila, mahali anapoishi na mengineyo yanayombainisha mtu fulani.

Alamsiki
Haya twende sawa.

Nafasi ya kazi inatangazwa moja, wanafanya maombi watu mia 5 kupitia posta.

Kule zinakoenda jalia zinafika barua mia 4(kwenye bahasha kuna nyaraka zaidi ya 7). Hapo zipo bahasha mia 4(fanya jumla ya makabrasha mwenyewe)

Baada ya usahili na kumpata muhusika, zinabaki kuwa uchafu. Je zitupwe/zichomwe moto? La hasha, kuna watengeneza vifungashio. Zinageuka kuwa fursa, HR anapata hela ya mboga.

Kuhusu usiri wa data, zikifika kwake zinakuwa mali yake. Huwezi kumpangia tena matumizi
 
Back
Top Bottom