Aina ya wawekezaji nayo inaathiri bei za hisa. asilimia kubwa ya wawekezaji sio wale wa kuuza na kununua. wengi ni wale wa kuhold kwa ajili ya baadaye. Hii inafanya bei ya hisa kuwa stable hata kwa dhoruba zinazotokea. Kwa kifupi wanunuaji wengi wa hisa hatuna elimu kamili ya hisa.
Masoko ya nje yapo busy. Ila ukiangalia masoko yetu karibu kila siku demand ni kubwa kuliko supply hii ina maana watu hawataki kuuza hisa zao. Kuna kipindi hisa za CRDB zilifika 1600 ila watu wakagoma kuuza na sasa ni 1160 unashangaa are we insane? Umenunu hisa kwa 500 inafika 1600 bado umehold? why not selling it and repurchase when the price drop again even for 50 Tshs....
Umenena vyema kabisa, ila bado haya maelezo yako hapa yana mkanganyiko kidogo kiasi cha kuacha maswali..
Ndio ni kweli kwa mujibu wa financial markets principles wauzaji wakiwa wachache kuliko wanunuzi price inapanda, lakini pia kumbuka soko la hisa ali operate kwa kufuata demand and supply zinasema nini....
...how the whole market operate involves a lot of factors at interplay like business perfomance,economic state at macro levels,company image au outlook etc..!!
...Hivyo mpaka tunaona share price kwenye chart ni balance ya combinations ya hizo factors.
Sasa kampuni haiwezi kuwa na perfomance mbaya kwa zaidi ya miezi miwili kiasi cha kufanya mpaka baadhi ya investors kukimbia halafu share value isishuke, eti kisa tu watu wengi hawako tayari kuuza hisa zao.
Walichopitia bank ya CRDB miezi miwili iliyopita kilitengeneza negative outlook to the company na kusababisha negative market sentiment to the public..
..na kawaida kampuni ikiwa na negative market sentiment huwa inapelekea watu wasite kujuhisisha nayo kwa namna yoyote ile, hivyo nyie investors ambao mnamiliki hisa zenu hapo mnaweza mkawa hamtaki kuuza lakin pia vile vile watu walioko huku nje hawataki kuzinunua, maana wana wasi wasi.
Na ndio maana mimi narudi pale pale kuna mchezo wa kihuni ulifanyika hili kulinda hizo share za crdb....
...Kwanza nilivyoona tu governor wa BOT eti anampongeza GD wa crdb sijui kwa kazi nzuri aliyoifanya, nikajua tu hakuna kitu hapa, hawa wapuuzi wanapongezana baada zoezi lao la kihuni kufanikiwa.