Je, soko la HISA ni utapeli?

Je, soko la HISA ni utapeli?

Ndio nimeelewa mkuu hio hio CCMRDB ndio nimesema akaunti ya bank sio yako ni ya bank kwa hio siku nyingine usije ukafungua akaunti bank ukaanza kujisifu nina akaunti yangu bank sio akaunti yako ni akaunti ya bank

Naongelea CRDB si CCMRDB.

Straight to ignore list.

Kuanzia hapa sitaona unachoandika.
 
Niliacha kuifuatilia DSE na makampuni yaliyosajiriwa humo baada ya channels na page rasmi za DSE kuifanyia promo ile kampuni ya kilimo ya kitapeli JATU PLC iliyokuwa inauza hisa moja shilingi 5,000.

Kampuni hiyo ilikuwa inalipa wasanii mmojawapo kama sikosei alikuwa Mrisho Mpoto, walikuwa wanapanda kwenye Canter na wanenguaji wakitangaza kushawishi watu wanunue hisa. Nikajua hamna kitu pale, wewe tangu lini mwekezaji akashawishika kwa kutumia wanenguaji. Sasa DSE ndio ilikuwa inapigia promo JATU iliyokuwa sijui ndio inatoa I.P.O muda ule.

Tangu lini TFF regulator wa kandanda ikahamisha Watanzania washabikie Namungo kwenye ligi kuu.
Hivi DSE walishatoa tamko au maelezo kuhusu JATU?!
 
Soko la hisa huendeshwa na mwenendo wa kampuni husika.

Iweje hisa za CRDB zisiyumbe baada ya CRDB kukosekana hewani na kuleta shida kwa watumiaji wa huduma zake?

Iweje Vodacom imepata faida ya 90bil ila hisa zake imebaki 580 ile ile?

Tumezoea kuona masoko ya nje kama nasdaq, nyse, lse, hangseng zote hizo ikitokea kampuni imefanya vibaya au vizuri basi athari zinaonekana moja kwa moja (hasi na chanya).

Je DSE wanacheza kwa kuongeza thamani na kushusha wajisikiavyo?

Juzi ORACLE imeongezeka thamani kwa 41% baada ya faida kubwa kuliko matarajio, iweje voda thamani yake ibaki vile vile?
Nawashangaa sana watu wanaowekeza hela sehem ambapo siasa ndio inaamua uchumi badala ya uchumi uamue siasa. Ukuaji wako utategemea kauli ya mwanasiasa. Bora ununue hisa hapo kenya angalau soko ndio linaamua uchumi sio wanasiasa.
 
Ni Uswahili wa hali ya juu walifanya hata nikaacha follow pages zao na app yao nikatoa kwa simu. Nikawa na wasiwasi nao kuna siku watapoteza watu, wewe msomi gani wa uchumi anaruhusu JATU kuwa listed kwenye stock exchange. Model yenyewe tu ilionekana ponzi. Haikuchukua hata 2 yrs, sasa hapo kuna regulator serious kweli au wala mishahara tu.
Hiyo ni crime kabisa.
Walitakiwa wafungwe watu hapo DSE.
 
Ni Uswahili wa hali ya juu walifanya hata nikaacha follow pages zao na app yao nikatoa kwa simu. Nikawa na wasiwasi nao kuna siku watapoteza watu, wewe msomi gani wa uchumi anaruhusu JATU kuwa listed kwenye stock exchange. Model yenyewe tu ilionekana ponzi. Haikuchukua hata 2 yrs, sasa hapo kuna regulator serious kweli au wala mishahara tu.
Ila kwa kweli hapo kwa JATU naunga mkono hoja,sasa sisi wenye vipato vidogo tukaweke wapi hela zetu🙆🏾‍♀️🙆🏾‍♀️huko UTT ndio sikuamini nafsi yangu imegoma japo napewa elimu sana.
 
Mifumo yao ya uendeshaji wa masoko ya Hisa ni tofauti. Huko Duniani unaweza kununua na kuuza hisa instantly over the counter, taarifa yoyote itakayotokea huwa inaathiri maamuzi ya wawekezaji na wana uwezo wa kuuza ama kununua hisa kulingana na uelekeo wa upepo hata kwa ndani ya dakika 5. Tofauti na huku kwetu, ukinunua tena kwa kusainishana ndiyo imetoka hiyo.
 

Attachments

  • IMG_20250917_131011.jpg
    IMG_20250917_131011.jpg
    33.5 KB · Views: 40
Kabisa mtu na akili zake anaenda kuwekeza kwenye stock market ya bongo in a long run?

Bongo hii ambayo imejazaa uhuni na siasa kila kona mtu anaweka mamilioni yako eti unasubiri faida baada ya miaka kadhaa na wakati mkipata mwanasiasa mwehu tu hela zako zote zinayeyuka kama ilivyokuwa kwa precision air shares kipindi cha magufuli?

Ni heri nijichange change nikanunue zangu shares za apple huko kwenye masoko yanayoeleweka.
Umeongea vizuri sana. Bora Ujichange ukimbulie nje ukawekeze maana Wenzetu wana regulations nzuri sana

Hata Rostam alishasema Hakuna Mwekezaji atakayekuja Kuwekeza kwenye nchi ambayo Wanasiasa wana nguvu kuliko sheria za Kibiashara
 
Umeongea vizuri sana. Bora Ujichange ukimbulie nje ukawekeze maana Wenzetu wana regulations nzuri sana

Hata Rostam alishasema Hakuna Mwekezaji atakayekuja Kuwekeza kwenye nchi ambayo Wanasiasa wana nguvu kuliko sheria za Kibiashara
Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu kipindi kile Elon Musk anawavuruga sana wamarekani na wizara yake mpya ya DOGE.

Wamarekani wengi waliisusia kampuni yake ya TESLA wakaanza kurudisha magari kwenye dealership, mauzo yakapungua kwa zaidi ya 30% hali hiyo ilipekea hata bei ya hisa za TSL kushuka kutoka $320 mpaka $197 ndani ya miezi minne tu...

Haya njoo kwetu sasa hapa wiki mbili zilizopita kila mtu anajua mauza uza yaliyotokea kwenye benki ya CRDB hali ambayo imelekea watu kuhamisha pesa zao kwa fujo sana, na hata baadhi ya investors kukimbiza pesa zao.... ila sasa cha kustahajabisha bei ya hisa za CRDB ziko almost pale pale licha ya hili dhaama lililoikuta benki hiyo... kama sio uhuni wa ku inflate share price artificially ni nini hapo???

Yaan tukienda na marketing principles za financial market ilipaswa sasa hivi share za CRDB bei yake iwe kwenye 200/= hapo na sio eti 1000+/= huko.

Kwa serious investor ameshaona kuna walikini mkubwa sana kwenye hiyo kampuni ya CRDB.

Alichokisema Rostam ni kweli nchi za dunia ya tatu hizi mfanyabiashara mkubwa hawezi kuja kutupa hela zake, maana wanasiasa wana nguvu kuliko hata market forces.
 
Back
Top Bottom