Warumi 14:2,14,20
2 Mtu mmoja anayo imani, anakula
vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula
mboga.
14 Najua, tena nimehakikishwa
sana katika Bwana Yesu, ya kuwa
hakuna kitu kilicho najisi kwa asili
yake, lakini kwake yeye akionaye
kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu
kile ni najisi.
20 Kwa ajili ya chakula usiiharibu
kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi;
bali ni vibaya kwa mtu alaye na
kujikwaza.
Marko 7:18-19
18 Akawaambia, Hivi hata ninyi
hamna akili? Hamfahamu ya
kwamba kila kitu kilicho nje ya
mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia
unajisi;
19 kwa sababu hakimwingii
moyoni, ila tumboni tu; kisha
chatoka kwenda chooni? Kwa
kusema hivi alivitakasa vyakula
vyote.
Wakolosai 2:16
16 Basi, mtu asiwahukumu ninyi
katika vyakula au vinywaji, au kwa
sababu ya sikukuu au mwandamo
wa mwezi, au sabato;
Waebrania 13:9
9 Msipeperushwe huku na huku
kwa mafundisho tofauti ya kigeni.
Neema ya Mungu ndiyo
inayoimarisha roho zetu na wala si
masharti juu ya chakula; Masharti
hayo kamwe hayakumsaidia mtu
yeyote aliyeyafuata.