Je, Sabaya kuwa mmoja wa mashahidi kwenye kesi ya Mbowe?

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,976
Kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe inavyoenda, kuna uwezekano wa aliyekuwa Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kuwa ni mmoja wa mashahidi kwa upande wa serikali.

Inavyodaiwa kwenye hati ya mashitaka ya Mbowe, wakati njama za kutenda makosa zinapangwa katika wilaya ya Hai, Sabaya ndiye alikuwa Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Ieleweke kuwa moja ya majukumu ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ni kuandaa ripoti za tathmini za hali ya ulinzi na usalama katika wilaya na kuziwasilisha kwa Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Ulinzi na Usalama wa Taifa ya Mwaka 2010 (NSC Act).

Kwa sababu kesi ya Mbowe inaangukia katika makosa ya kigaidi, kuna uwezekano Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wake kwa wakati makosa haya yanatendekea ikawajibika kama shahidi katika kesi hii.

Kuna baadhi ya watu watasema, Sabaya hawezi kuwa shahidi kwa sababu kwa sasa ni mshitakiwa wa makosa ya jinai katika kesi inayoendelea mahakamani.

Kwa sheria zetu za jinai ambazo tumechukua kutoka Uingereza na India, huwezi kuhitimisha kwa sasa kuwa Sabaya ana makosa ya jinai mpaka pale mahakama itakapotoa hukumu(the right to be presumed innocent until proven guilty). Hii ina maana kuwa, kisheria Sabaya bado ni mwananchi ambaye hana kosa/makosa yoyote na kwa sababu hiyo hawezi kuhesabiwa kama ni shahidi asiyeaminika (unreliable witness).

Ukichunguza utagundua kuwa, kesi ya Mbowe imeifanya CHADEMA kupigwa na ''ganzi''. Viongozi wa CHADEMA wa juu kitaifa hawajui wafanye nini katika kukabiliana na mashitaka ya Mbowe. Ndio maana imewachukua zaidi ya siku sita kutoa tamko ambalo ukilichunguza kwa undani halina hata mwelekeo wowote!

Kukamatwa kwa mbowe kumeiathiri sana CHADEMA kisaikologia. Viongozi waliobaki hawajui wafanye nini kwa sasa kwa sababu Mbowe alikuwa kila kitu ndani ya CHADEMA. Kutokujua wafanye nini kunasababisha marumbano kati yao kwenye mitandao ya jamii.

Je, Sabaya atamkaanga Mbowe mahakamani au atakuwa kama jiwe walilolikataa wanaCHADEMA linakuwa jiwe kuu la pembeni?

Siasa za Tanzania zinaenda kwa kasi sana!

UPDATE:
View attachment 1904746
 
Inasemekana atakuwa upande wa Mbowe kumtetea na kuthibitisha hana kosa.

Akimaliza arudi kisongo

Ikiwa ndivyo atawaoa Chadema wote. Hadi Twitter Republic
 
Hivi nyie think tank wa CCM hamuoni aibu?

Jambazi kama hili linaanzaje kutoa ushahidi mbele ya kesi ya kubumba?

Sabaya aliyekua na vigezo vyote vya kuswekwa lupango hata bila kupepesa macho leo hii akawe shahidi kwa mtu aliyemvamia?

Mbowe hana hata kikundi cha wanamgambo alioonekana nao wakiwa hata na upinde na mishale.

Sabaya alikua akipewa backup na jiwe Sabaya alikua na hadi silaha za moto anatumia licha ya kuwa na walinzi wasio rasmi.

It's high time for you guys to stop taking us for a ride.
 
Sabaya anaweza kumuokoa Mbowe!

Umdhaniaye siye ndiye!
Labda kwa miujiza,na iwe,kesi zinazomkabili zinaendeshwa kwa uhalisia kama ilivyo na aone no way jela Maisha,aamue mwenyewe kuwa fair.Kwani binafsi namfungamanisha na kundi mbambikizi linaloogopa dai pendwa la watanzania la Katiba mpya.
 
Mbowe /CHADEMA wamefungua shauri Mahakama kuu washtakiwa ni IGP, AG & DPP sasa hiyo ganzi ni ipi au unafikiri kuna watu wajinga kama wewe.
 
Unajua kuna msiba wa kitaifa lakini? Au sikuhizi waziri akifa mnawaza kuchukua nafasi yake tu
Nadhani hujui hata maana ya msiba wa kitaifa katika sheria na kanuni zinazohusu viongozi wa kitaifa nchini na misiba yao!
 
Inasemekana atakuwa upande wa Mbowe kumtetea na kuthibitisha hana kosa.
Akimaliza arudi kisongo

Ikiwa ndivyo atawaoa cdm wote. Hadi twiter Republic
Kama nilivyoandika pale juu, umdhaniaye siye ndiye!
 
Nadhani hujui hata maana ya msiba wa kitaifa katika sheria na kanuni zinazohusu viongozi wa kitaifa nchini na misiba yao!
Hebu nieleweshe msiba wa kitaifa ni upi na usio wa kitaifa ni upi. Maana taifa limepotelewa na kiongozi mkubwa sasa huo sijui ni msiba wa kinzengo
 
Kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe inavyoenda, kuna uwezekano wa aliyekuwa Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kuwa ni mmoja wa mashahidi kwa upande wa serikali.

Inavyodaiwa kwenye hati ya mashitaka ya Mbowe, wakati njama za kutenda makosa zinapangwa katika wilaya ya Hai, Sabaya ndiye alikuwa Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Ieleweke kuwa moja ya majukumu ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ni kuandaa ripoti za tathmini za hali ya ulinzi na usalama katika wilaya na kuziwasilisha kwa Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Ulinzi na Usalama wa Taifa ya Mwaka 2010 (NSC Act).

Kwa sababu kesi ya Mbowe inaangukia katika makosa ya kigaidi, kuna uwezekano Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ikiongozwa na Mwenyekiti wake kwa wakati makosa haya yanatendekea ikawajibika kama shahidi katika kesi hii.

Kuna baadhi ya watu watasema, Sabaya hawezi kuwa shahidi kwa sababu kwa sasa ni mshitakiwa wa makosa ya jinai katika kesi inayoendelea mahakamani.

Kwa sheria zetu za jinai ambazo tumechukua kutoka Uingereza na India, huwezi kuhitimisha kwa sasa kuwa Sabaya ana makosa ya jinai mpaka pale mahakama itakapotoa hukumu(the right to be presumed innocent until proven guilty). Hii ina maana kuwa, kisheria Sabaya bado ni mwananchi ambaye hana kosa/makosa yoyote na kwa sababu hiyo hawezi kuhesabiwa kama ni shahidi asiyeaminika (unreliable witness).

Ukichunguza utagundua kuwa, kesi ya Mbowe imeifanya CHADEMA kupigwa na ''ganzi''. Viongozi wa CHADEMA wa juu kitaifa hawajui wafanye nini katika kukabiliana na mashitaka ya Mbowe. Ndio maana imewachukua zaidi ya siku sita kutoa tamko ambalo ukilichunguza kwa undani halina hata mwelekeo wowote!

Kukamatwa kwa mbowe kumeiathiri sana CHADEMA kisaikologia. Viongozi waliobaki hawajui wafanye nini kwa sasa kwa sababu Mbowe alikuwa kila kitu ndani ya CHADEMA. Kutokujua wafanye nini kunasababisha marumbano kati yao kwenye mitandao ya jamii.

Je, Sabaya atamkaanga Mbowe mahakamani au atakuwa kama jiwe walilolikataa wanaCHADEMA linakuwa jiwe kuu la pembeni?

Siasa za Tanzania zinaenda kwa kasi sana!
Tuongee ujinga wetu wote ila tukumbuke ya rwakatare na maneno ya mwigulu pale bungeni
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom