Idugunde
JF-Expert Member
- May 21, 2020
- 6,273
- 6,637
Rais wangu kipenzi cha watanzania,najua kuwa unakwenda kushinda urais kwa kishindo kizito. Hii ni dalili kuwa watu wana imani kwako.
Natolea mfano tu leo umezindua reli ya Arusha Dar ambayo ilikuwa imekufa kwa zaidi ya miaka 30. Kwa hiyo wewe kwa watu wa Arusha ni shujaa na jembe lao,maana sasa watasafiri kwa 16000 tu mpaka Arusha toka Dar. Kwa ufupi umeyatumia mapato ya taifa hili vizuri kwa manufaa ya watanzania. Maana usafiri wa reli ni nafuu na una manufaa kwa wananchi.
Lakini rais wangu idara ya mahakama na jeshi la polisi limekushinda. Hii sio siri maana malalamiko ni mengi sana,kama wawakilishi wako kama wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa wangekuwa wanafanya kazi ipasavyo tusinge pata hii aibu kwa taifa hili.
Hapa tulipo bado tuna siku mbili tu tufanye uchaguzi lakini kila unapopita ni malalamiko juu ya polisi na mahakama juu ya watu kunyimwa haki zao. Umeyashuhudia haya kila mkoa uliokuwa unakwenda na baadhi ya watu waliodhurumiwa haki zao walikuwa wanazuiwa wasikuone au kuonyesha mabango yao.
Kama rais wetu JPM umeweza kufanya makubwa sekta ya afya,elimu na miundo mbinu kama ulivyofufua reli leo je mahakama na polisi umeshindwa kuwadhibiti?
Wananchi wanaumia moyoni kwa kukosa haki zao za msingi, awwmu hii ya pili fanya mabadiliko makubwa mahakama na polisi ili haki za wananchi zipatikane. Maendeleo ni pamoja na kupata haki za msingi ambazo katiba ya JMT imeziweka wazi.