Je, Rais anahujumiwa Shirika la Reli?

Je, Rais anahujumiwa Shirika la Reli?

Anatajwa rais sababu ndiye mwenye maamuzi ya mwisho.sio kwa sababu train ni ya kwake.

Wewe kama mhujumiwa unatakiwa uchukue hatua kama za mleta mada,sio kujisifu kwa kodi unayolipa ambayo kwa maelezo ya mleta mada kama inatolewa kwa mfumo huo,inapotea bure.
Wewe pia ni muimba pambio za kusifu na kuabudu Jiwe?
 
Raisi anahujumiwa vipi !?
Kwani hiyo treni ni mali ya raisi !?
Umeandika vya maana, vyema uweke title inayoeleweka. Wanaohujumiwa ni mm na wewe. Bila mimi na wewe kulipa kodi hata hiyo treni ingekuwa hadithi.
Kila kitu raisi, raisi, miaka yote hakukuwa na maraisi hadi sasa hv !? Au huyu wa sasa hivi ni muwekezaji na sisi ni assets zake !?
Umeandika mtazamo wako. Hujui majukumu ya rais na mwelekeo wa nchi, sina cha kuongeza.
 
Ndo maana katika usafiri wa ndege kuna low season na high season kwa hiyo hata katika usafiri wa mabasi na train sio siku zote abiria watakuwa wanasafiri kwa wingi e.g. Wakati wa xmass mabasi yote yanakuwa yanajaa pamoja na train therefore don't exaggerate things for your own and your bosses for mileage
Nimeongea jambo nililokutana nalo, sasa wewe unayetetea usichokijua unakosea sana. Watu wanalalamika treni imejaa wakati mabehewa yanakwenda tupu!! You are missing the point.
 
Anatajwa rais sababu ndiye mwenye maamuzi ya mwisho.sio kwa sababu train ni ya kwake.

Wewe kama mhujumiwa unatakiwa uchukue hatua kama za mleta mada,sio kujisifu kwa kodi unayolipa ambayo kwa maelezo ya mleta mada kama inatolewa kwa mfumo huo,inapotea bure.
Mwenye maamuzi ya mwisho ?
Hivi mgawanyiko wa madaraka na utendaji hauonekani ?
Hakuna waziri? Hakuna wizara ambazo ndio zinahusika ?
Tuongee uhalisia, mambo ya ushabiki weka pembeni. Tatizo linapoonekana kuna wahusika wa moja kwa moja ambao ndio wa kuwasilishiwa taarifa. Sio kila kitu anahujumiwa raisi. Kodi za wananchi, anayehujumiwa ni raisi !?
Huu ni ukondoo
 
Haya mashirika yalishatushinda tangu enzi za mwalimu, hata hilo la Ndege nalo ni suala la muda tu!!
 
Rais haujumiwi, hiyo reli inajengwa kwa hela tunazolipa sisi kama kodi sio hela za rais, so kama kuna mtu anaibiwa ni watanzania. Grow up people, tumieni ubongo sio kutumia oxygen bure tu
 
Raisi anahujumiwa vipi !?
Kwani hiyo treni ni mali ya raisi !?
Umeandika vya maana, vyema uweke title inayoeleweka. Wanaohujumiwa ni mm na wewe. Bila mimi na wewe kulipa kodi hata hiyo treni ingekuwa hadithi.
Kila kitu raisi, raisi, miaka yote hakukuwa na maraisi hadi sasa hv !? Au huyu wa sasa hivi ni muwekezaji na sisi ni assets zake !?
Hili tatizo la kila kitu rais ni moja ya sababu kubwa ya umasikini wetu.
 
Umeandika mtazamo wako. Hujui majukumu ya rais na mwelekeo wa nchi, sina cha kuongeza.
Acha ushabiki usio na tija.
Majukumu ya raisi wanasoma wanafunzi wa primary na kidato cha pili(civics).

Wewe Unafahamu mahali hii nchi inaelekea !?

Serikali isiyo na mihimili inayojitegemea ni serikali gani ? Monarchy? Dictatorship?
 
Hivi mkuu first class ikoje na ni kiasi gani?
 
Raisi anahujumiwa vipi !?
Kwani hiyo treni ni mali ya raisi !?
Umeandika vya maana, vyema uweke title inayoeleweka. Wanaohujumiwa ni mm na wewe. Bila mimi na wewe kulipa kodi hata hiyo treni ingekuwa hadithi.
Kila kitu raisi, raisi, miaka yote hakukuwa na maraisi hadi sasa hv !? Au huyu wa sasa hivi ni muwekezaji na sisi ni assets zake !?
Heri umenena wewe maana tumechoka na kila kitu kumtanguliza Magufuri as if before him no one did anything. Urais ni taasisi siyo mali ya mtu na yeye alichaguliwa humohumo. Nyimbo vulizoimba kuhusu Nyerere zinatosha sasa basi.
 
Ndo maana katika usafiri wa ndege kuna low season na high season kwa hiyo hata katika usafiri wa mabasi na train sio siku zote abiria watakuwa wanasafiri kwa wingi e.g. Wakati wa xmass mabasi yote yanakuwa yanajaa pamoja na train therefore don't exaggerate things for your own and your bosses for mileage
HIvi mleta hoja umemuelewa lakini?
 
Wakuu, wiki hii nilifanya safari kwenda Tabora kwa kutumia usafiri wa treni (delux ama wengine huiita express). Nilishangaa kuona mabehewa karibu yote ya daraja la pili yakiwa matupu na baadhi tu yakiwa na abiria wachache mno!! Nikajua labda ni tofauti ya bei, kwani daraja la tatu mpaka Tbr kwa mfano ni tshs 20,000 wakati daraja la pili kukaa ni tshs 25,000. Tofauti ya tshs 5,000 ni kubwa sana kwa maisha ya sasa.

Nikiwa naendelea na safari niliamua kuhamia kwenye mojawapo ya behewa lililokiwa tupu kabisa, nikakaa humo, kufika dodoma waliingia watu kama wanne hivi tukajumuika. Basi alipokuja TT akikagua tiketi, kumbe wale watu waliukwa na tiketi za daraja la tatu, wakatakiwa kuongeza pesa ili wakae humo kihalali. Watu wale walilalama sana kwa sababu kumbe tangu awali walitaka kukata tiketi za daraja la pili lakini waliambiwa treni imejaa, hivyo wakate daraja la tatu kusimama bila siti. Walichukizwa kukuta mabehewa yakiwa tupu huku abiria wengi wakiwa wameahirisha safari kwa kukosa siti. Inasemekana huu ni mchezo wa kila mara.

Tulisafiri mpaka Tabora niliposhuka wala asiongezeke abiria hata mmoja. Nakumbuka Dar kuna behewa liliachwa kwamba ni la abiria wa Dodoma, hivyo tiketi kuwa ngumu kupata, lakini hakukuwa na abiria wowote kwa mabehewa yote manne.

Naomba TRL wawe wazalendo, kwani usafiri huu ni msaada mkubwa kwa watu wenye kipato cha chini na kwa wasafiri wengine wanaopenda kusafiri kwa starehe.View attachment 1242747
Kufika tabora unatumia muda gani?
 
Acha ushabiki usio na tija.
Majukumu ya raisi wanasoma wanafunzi wa primary na kidato cha pili(civics).

Wewe Unafahamu mahali hii nchi inaelekea !?

Serikali isiyo na mihimili inayojitegemea ni serikali gani ? Monarchy? Dictatorship?
Mtazamo wwko, m oppose everything. Wenye ufahamu wameelewa, by the way halikuwa lengo langu kubishana bali kufikisha ujumbe. Unaweza kujadili contents ama kushikilia kubisha kuhusu title, ndio ufahamu wetu ulipoishia.
 
Niliondoka saa mbili asubuhi, nikafika saa moja asubuhi kesho yake.
Asante kumbe sio mbaya
Njiani hakuna wizi katika vituo vyao ?
Nilishawahi kusikia kuwa katika treni kuna kunguni ni kweli?
 
Raisi anahujumiwa vipi !?
Kwani hiyo treni ni mali ya raisi !?
Umeandika vya maana, vyema uweke title inayoeleweka. Wanaohujumiwa ni mm na wewe. Bila mimi na wewe kulipa kodi hata hiyo treni ingekuwa hadithi.
Kila kitu raisi, raisi, miaka yote hakukuwa na maraisi hadi sasa hv !? Au huyu wa sasa hivi ni muwekezaji na sisi ni assets zake !?
Safi sana.

Tanzania ya sasa ujinga mtupu.

Rais amegeuka Mungu au Yesu Kristo.

Pambaf kabisa.
 
Mwenye maamuzi ya mwisho ?
Hivi mgawanyiko wa madaraka na utendaji hauonekani ?
Hakuna waziri? Hakuna wizara ambazo ndio zinahusika ?
Tuongee uhalisia, mambo ya ushabiki weka pembeni. Tatizo linapoonekana kuna wahusika wa moja kwa moja ambao ndio wa kuwasilishiwa taarifa. Sio kila kitu anahujumiwa raisi. Kodi za wananchi, anayehujumiwa ni raisi !?
Huu ni ukondoo
Unasukumwa na mihemko bro.
 
Nimeongea jambo nililokutana nalo, sasa wewe unayetetea usichokijua unakosea sana. Watu wanalalamika treni imejaa wakati mabehewa yanakwenda tupu!! You are missing the point.
Vipi mkuu wakati wa kukata tiketi hawakukuomba kitambulisho pamoja na barua kutoka serikali ya mtaa?
Kuna ujinga mwingi sana unaofanywa kwenye hii treni ya delux,
Hujuma nyingine kwenye treni hii ni kuondoa route ya Dar - Mwanza kwa madai kua hamna abiria wa kutosha.
Management nzima ya TRL inapaswa iwajibishe na ikiwezekana wafungulie kesi ya uhujumu uchumi kwa mambo wanayoyafanya.
 
Back
Top Bottom