Je, Rais anahujumiwa Shirika la Reli?

Je, Rais anahujumiwa Shirika la Reli?

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,843
Reaction score
10,765
Wakuu, wiki hii nilifanya safari kwenda Tabora kwa kutumia usafiri wa treni (delux ama wengine huiita express). Nilishangaa kuona mabehewa karibu yote ya daraja la pili yakiwa matupu na baadhi tu yakiwa na abiria wachache mno!! Nikajua labda ni tofauti ya bei, kwani daraja la tatu mpaka Tbr kwa mfano ni tshs 20,000 wakati daraja la pili kukaa ni tshs 25,000. Tofauti ya tshs 5,000 ni kubwa sana kwa maisha ya sasa.

Nikiwa naendelea na safari niliamua kuhamia kwenye mojawapo ya behewa lililokiwa tupu kabisa, nikakaa humo, kufika dodoma waliingia watu kama wanne hivi tukajumuika. Basi alipokuja TT akikagua tiketi, kumbe wale watu waliukwa na tiketi za daraja la tatu, wakatakiwa kuongeza pesa ili wakae humo kihalali. Watu wale walilalama sana kwa sababu kumbe tangu awali walitaka kukata tiketi za daraja la pili lakini waliambiwa treni imejaa, hivyo wakate daraja la tatu kusimama bila siti. Walichukizwa kukuta mabehewa yakiwa tupu huku abiria wengi wakiwa wameahirisha safari kwa kukosa siti. Inasemekana huu ni mchezo wa kila mara.

Tulisafiri mpaka Tabora niliposhuka wala asiongezeke abiria hata mmoja. Nakumbuka Dar kuna behewa liliachwa kwamba ni la abiria wa Dodoma, hivyo tiketi kuwa ngumu kupata, lakini hakukuwa na abiria wowote kwa mabehewa yote manne.

Naomba TRL wawe wazalendo, kwani usafiri huu ni msaada mkubwa kwa watu wenye kipato cha chini na kwa wasafiri wengine wanaopenda kusafiri kwa starehe.
20191024_093734.jpg
 
Raisi anahujumiwa vipi !?
Kwani hiyo treni ni mali ya raisi !?
Umeandika vya maana, vyema uweke title inayoeleweka. Wanaohujumiwa ni mm na wewe. Bila mimi na wewe kulipa kodi hata hiyo treni ingekuwa hadithi.
Kila kitu raisi, raisi, miaka yote hakukuwa na maraisi hadi sasa hv !? Au huyu wa sasa hivi ni muwekezaji na sisi ni assets zake !?
 
Watu wale walilalama sana kwa sababu kumbe tangu awali walitaka kukata tiketi za daraja la pili lakini waliambiwa treni imejaa, hivyo wakate daraja la tatu kusimama bila siti. Walichukizwa kukuta mabehewa yakiwa tupu huku abiria wengi wakiwa wameahirisha safari kwa kukosa siti. Inasemekana huu ni mchezo wa kila mara.

Dawa yake ni kuweka e ticketing system, mtu anunue ticket kwa mtandao ili wakatisha ticket wakapangiwe kazi nyingine
 
Ndo maana katika usafiri wa ndege kuna low season na high season kwa hiyo hata katika usafiri wa mabasi na train sio siku zote abiria watakuwa wanasafiri kwa wingi e.g. Wakati wa xmass mabasi yote yanakuwa yanajaa pamoja na train therefore don't exaggerate things for your own and your bosses for mileage
 
Raisi anahujumiwa vipi !?
Kwani hiyo treni ni mali ya raisi !?
Umeandika vya maana, vyema uweke title inayoeleweka. Wanaohujumiwa ni mm na wewe. Bila mimi na wewe kulipa kodi hata hiyo treni ingekuwa hadithi.
Kila kitu raisi, raisi, miaka yote hakukuwa na maraisi hadi sasa hv !? Au huyu wa sasa hivi ni muwekezaji na sisi ni assets zake !?
Bila shaka unawaambia wasio na macho
 
Mnyama SGR amalizike mapema watu wasafiri....

Tatizo litakuwa usimamizi
Wala haiwezi kuwa suluhisho hiyo, kwa jamii ambayo ni masikini wao muda mrefu wa safari sio inshu sana!! Hata hiyo express , utofauti wa nauli kati ya second, na third ni mdogo sana lakini kwa masikini hiyo tofauti ni kubwa sana!! Na ndio maana bado utakuta daraja la tatu limejaa sana!! Hata ije hiyo sgr umwambie masikini kuwa dar to dodoma ni tsh. 15,000, wakati kwenye lile li ngwalangala iwe 12000!! Lazima tu watu wajae kwenye hilo la muda mrefu, masikini anawahi nini?? Hizo ndege wakati zinakuja kulikuwa na punguzo la bei dar to mwanza ilikuwa hadi 160,000 kwa wenye uwezo ilikuwa ni kama bure hivi lakini kwa abiria wa NAJIMUNISA, ni vigumu kumpata, yeye atapigia hesabu nauli ya basi ni 40,000 anabakiza 120,000!!mfukoni,hata alale barabarani siku mbili, wewe tumia saa. Moja na nusu hana habari. Leo unamsikia kiongozi anasema baada ya muda kidogo sgr ikifika mwanza, mtu atakuwa anaishi dar anafanya kazi mwanza/kigoma(hahahaha) kwa mshahara gani utakao muwezesha kuweza iyo nauli ya kila siku hata iwe kwenda na kurudi ni 40,0000??
 
Raisi anahujumiwa vipi !?
Kwani hiyo treni ni mali ya raisi !?
Umeandika vya maana, vyema uweke title inayoeleweka. Wanaohujumiwa ni mm na wewe. Bila mimi na wewe kulipa kodi hata hiyo treni ingekuwa hadithi.
Kila kitu raisi, raisi, miaka yote hakukuwa na maraisi hadi sasa hv !? Au huyu wa sasa hivi ni muwekezaji na sisi ni assets zake !?
Anatajwa rais sababu ndiye mwenye maamuzi ya mwisho.sio kwa sababu train ni ya kwake.

Wewe kama mhujumiwa unatakiwa uchukue hatua kama za mleta mada,sio kujisifu kwa kodi unayolipa ambayo kwa maelezo ya mleta mada kama inatolewa kwa mfumo huo,inapotea bure.
 
Wakuu, wiki hii nilifanya safari kwenda Tabora kwa kutumia usafiri wa treni (delux ama wengine huiita express). Nilishangaa kuona mabehewa karibu yote ya daraja la pili yakiwa matupu na baadhi tu yakiwa na abiria wachache mno!! Nikajua labda ni tofauti ya bei, kwani daraja la tatu mpaka Tbr kwa mfano ni tshs 20,000 wakati daraja la pili kukaa ni tshs 25,000. Tofauti ya tshs 5,000 ni kubwa sana kwa maisha ya sasa.

Nikiwa naendelea na safari niliamua kuhamia kwenye mojawapo ya behewa lililokiwa tupu kabisa, nikakaa humo, kufika dodoma waliingia watu kama wanne hivi tukajumuika. Basi alipokuja TT akikagua tiketi, kumbe wale watu waliukwa na tiketi za daraja la tatu, wakatakiwa kuongeza pesa ili wakae humo kihalali. Watu wale walilalama sana kwa sababu kumbe tangu awali walitaka kukata tiketi za daraja la pili lakini waliambiwa treni imejaa, hivyo wakate daraja la tatu kusimama bila siti. Walichukizwa kukuta mabehewa yakiwa tupu huku abiria wengi wakiwa wameahirisha safari kwa kukosa siti. Inasemekana huu ni mchezo wa kila mara.

Tulisafiri mpaka Tabora niliposhuka wala asiongezeke abiria hata mmoja. Nakumbuka Dar kuna behewa liliachwa kwamba ni la abiria wa Dodoma, hivyo tiketi kuwa ngumu kupata, lakini hakukuwa na abiria wowote kwa mabehewa yote manne.

Naomba TRL wawe wazalendo, kwani usafiri huu ni msaada mkubwa kwa watu wenye kipato cha chini na kwa wasafiri wengine wanaopenda kusafiri kwa starehe.View attachment 1242747
hakika hizo ni hujuma sana
 
Due kazi kweli kweli kupambana na watu,yasijirudie ya zamani tiketi zote kununuliwa na madalali ukienda upati hadi uwapate madalali,hio ni hujuma kutouzia watu tiketi kwamba zimejaa,hio ni michezo ya rushwa
 
Wala haiwezi kuwa suluhisho hiyo, kwa jamii ambayo ni masikini wao muda mrefu wa safari sio inshu sana!! Hata hiyo express , utofauti wa nauli kati ya second, na third ni mdogo sana lakini kwa masikini hiyo tofauti ni kubwa sana!! Na ndio maana bado utakuta daraja la tatu limejaa sana!! Hata ije hiyo sgr umwambie masikini kuwa dar to dodoma ni tsh. 15,000, wakati kwenye lile li ngwalangala iwe 12000!! Lazima tu watu wajae kwenye hilo la muda mrefu, masikini anawahi nini?? Hizo ndege wakati zinakuja kulikuwa na punguzo la bei dar to mwanza ilikuwa hadi 160,000 kwa wenye uwezo ilikuwa ni kama bure hivi lakini kwa abiria wa NAJIMUNISA, ni vigumu kumpata, yeye atapigia hesabu nauli ya basi ni 40,000 anabakiza 120,000!!mfukoni,hata alale barabarani siku mbili, wewe tumia saa. Moja na nusu hana habari. Leo unamsikia kiongozi anasema baada ya muda kidogo sgr ikifika mwanza, mtu atakuwa anaishi dar anafanya kazi mwanza/kigoma(hahahaha) kwa mshahara gani utakao muwezesha kuweza iyo nauli ya kila siku hata iwe kwenda na kurudi ni 40,0000??
Hata Moro dar hakuna atakaemudu kusafiri asubui kazini jioni kurudi labda nauli iwe 500 au 1000 kwa ruti dar moro
 
Wala haiwezi kuwa suluhisho hiyo, kwa jamii ambayo ni masikini wao muda mrefu wa safari sio inshu sana!! Hata hiyo express , utofauti wa nauli kati ya second, na third ni mdogo sana lakini kwa masikini hiyo tofauti ni kubwa sana!! Na ndio maana bado utakuta daraja la tatu limejaa sana!! Hata ije hiyo sgr umwambie masikini kuwa dar to dodoma ni tsh. 15,000, wakati kwenye lile li ngwalangala iwe 12000!! Lazima tu watu wajae kwenye hilo la muda mrefu, masikini anawahi nini?? Hizo ndege wakati zinakuja kulikuwa na punguzo la bei dar to mwanza ilikuwa hadi 160,000 kwa wenye uwezo ilikuwa ni kama bure hivi lakini kwa abiria wa NAJIMUNISA, ni vigumu kumpata, yeye atapigia hesabu nauli ya basi ni 40,000 anabakiza 120,000!!mfukoni,hata alale barabarani siku mbili, wewe tumia saa. Moja na nusu hana habari. Leo unamsikia kiongozi anasema baada ya muda kidogo sgr ikifika mwanza, mtu atakuwa anaishi dar anafanya kazi mwanza/kigoma(hahahaha) kwa mshahara gani utakao muwezesha kuweza iyo nauli ya kila siku hata iwe kwenda na kurudi ni 40,0000??
Anadai nyongeza yake ya mshahara siyo ya kitoto, ngoja nijipange hapa kuhamia morogoro niwe nakuja daily kufanya kazi dar
 
Raisi anahujumiwa vipi !?
Kwani hiyo treni ni mali ya raisi !?
Umeandika vya maana, vyema uweke title inayoeleweka. Wanaohujumiwa ni mm na wewe. Bila mimi na wewe kulipa kodi hata hiyo treni ingekuwa hadithi.
Kila kitu raisi, raisi, miaka yote hakukuwa na maraisi hadi sasa hv !? Au huyu wa sasa hivi ni muwekezaji na sisi ni assets zake !?
Huyu jamaa ameandika kuhusu jambo la muhimu tatizo Heading!
 
Back
Top Bottom