Je, Rais anahujumiwa Shirika la Reli?

Je, Rais anahujumiwa Shirika la Reli?

Wakuu, wiki hii nilifanya safari kwenda Tabora kwa kutumia usafiri wa treni (delux ama wengine huiita express). Nilishangaa kuona mabehewa karibu yote ya daraja la pili yakiwa matupu na baadhi tu yakiwa na abiria wachache mno!! Nikajua labda ni tofauti ya bei, kwani daraja la tatu mpaka Tbr kwa mfano ni tshs 20,000 wakati daraja la pili kukaa ni tshs 25,000. Tofauti ya tshs 5,000 ni kubwa sana kwa maisha ya sasa.

Nikiwa naendelea na safari niliamua kuhamia kwenye mojawapo ya behewa lililokiwa tupu kabisa, nikakaa humo, kufika dodoma waliingia watu kama wanne hivi tukajumuika. Basi alipokuja TT akikagua tiketi, kumbe wale watu waliukwa na tiketi za daraja la tatu, wakatakiwa kuongeza pesa ili wakae humo kihalali. Watu wale walilalama sana kwa sababu kumbe tangu awali walitaka kukata tiketi za daraja la pili lakini waliambiwa treni imejaa, hivyo wakate daraja la tatu kusimama bila siti. Walichukizwa kukuta mabehewa yakiwa tupu huku abiria wengi wakiwa wameahirisha safari kwa kukosa siti. Inasemekana huu ni mchezo wa kila mara.

Tulisafiri mpaka Tabora niliposhuka wala asiongezeke abiria hata mmoja. Nakumbuka Dar kuna behewa liliachwa kwamba ni la abiria wa Dodoma, hivyo tiketi kuwa ngumu kupata, lakini hakukuwa na abiria wowote kwa mabehewa yote manne.

Naomba TRL wawe wazalendo, kwani usafiri huu ni msaada mkubwa kwa watu wenye kipato cha chini na kwa wasafiri wengine wanaopenda kusafiri kwa starehe.View attachment 1242747
Kunguni siku hizi hamna tena ?
 
Nilienda mbeya pale kutaka kupakiza mzigo wa tani mbili kutoka Mbeya kuja Dar kwa treni. Naambiwa tani moja ni Tsh 220,000, laki mbili na ishirini. Ina maana tani mbili nitatakiwa kulipia shillingi laki nne na arobaini.

Wakati katika gari kubwa ya mzigo tani moja ni kuanzia elfu sabini hadi laki. Nikajua ni kwann watu hawatumii usafiri wa reli kuzafirishia ambao ndio ulitakiwa kuwa cheap kuliko usafiri wowote wa mizigo.

Sasa natamani kulifikisha hili swala wizarani tupatiwe ufumbuzi.
Mzee baba we pandisha mzigo kwny roli endelea na inshu zsko nyingine.

Kwani si uliona hata clip za yule Ole Sabaya akizingua kule hai uliona amefanywa chochote?
 
Raisi anahujumiwa vipi !?
Kwani hiyo treni ni mali ya raisi !?
Umeandika vya maana, vyema uweke title inayoeleweka. Wanaohujumiwa ni mm na wewe. Bila mimi na wewe kulipa kodi hata hiyo treni ingekuwa hadithi.
Kila kitu raisi, raisi, miaka yote hakukuwa na maraisi hadi sasa hv !? Au huyu wa sasa hivi ni muwekezaji na sisi ni assets zake !?
Kaleta ujumbe kwa kujimwambafai
 
Andika lugha inayoeleweka.
Nani anabishana na wewe ?
Acha kujistukia.
Unajadili kitu hata hukifahamu, majukumu ya raisi wasome watoto wa primary na secondary leo useme hakuna anayefahamu majukumu ya raisi.
Wacha niuonyeshe ujinga wako. Rais amekuwa akiongoza mapambano dhidi ya wazembe, wavivu, wala rushwa, wahujumu uchumi n.k. Iko wazi wako ambao hawafurahishwi na hatua zinazochukuliwa hivyo kumwona rais kama sio mtu sahihi kukalia kiti cha uongozi.

Wakati wewe una mtazamo wa mkondo mmoja tu (linear thinking) wenye upeo hutazama mambo kwa upana. Kitendo cha kuhujumu idara mbalimbali hakikusudiwi kuhujumu raia ama uchumi kwa ujumla wake, wananchi wanakuwa ni collateral, lakini nyuma yake kunaweza kuwa na political agenda, vita vya madaraka, n.k. Jifunze kufikiri nje ya box.
 
Ndo maana katika usafiri wa ndege kuna low season na high season kwa hiyo hata katika usafiri wa mabasi na train sio siku zote abiria watakuwa wanasafiri kwa wingi e.g. Wakati wa xmass mabasi yote yanakuwa yanajaa pamoja na train therefore don't exaggerate things for your own and your bosses for mileage
Sasa kwanini abiria waachwe kwa kisingizio cha treni kujaa wakati ipo tupu?!
 
Mkuu kuna mambo ya ajabu, daraja la tatu wanakata tiketi bila kujali idadi. Ukipata siti shukuru, ila siti zikiisha wanaendelea kukata ivyo hivyo bila kuandika siti no. Hawa wanakaa makoridoni na kufanya msongamano mkubwa.

Malalamiko niliyoyasikia mimi ni kwa abiria kwamba wanaambiwa daraja la pili limejaa hivyo wanalazimika kukata tiketi za daraja la tatu bila siti. Wakiwa ndani ya treni wanashangaa mabehewa yako tupu, ila wanatakiwa waongeze nauli ifikie ya daraja la pili, wanapewa namna ya risiti kisha wanaruhusiwa kusafiri kwenye daraja hilo. Sasa sijui kama hizo genuine kwa sababu zinaandikwa wa mkono.
Basi hapo ndipo ulipo upigaji. Yaani wafanyakazi wa reli kitengo cha tiketi wako tayari behewa la daraja la pili liende tupu ili wapate mshiko. Mshiko wanaupata kwa kuandika hizo risiti ''fake'' na kuhamishia wasafiri daraja la pili. Hili ni tatizo la menejimenti. Uongozi wa juu pengine wanashirikiana nao au wamejifungia ofisini na hawatoki kujua uendeshaji wa shirika. Aisee sina cha kusema. Kweli nchi yetu imeoza. Mwanzisha thread kudos sana kwa kufichua hii hujuma. Hawa ndiyo wanatakiwa washtakiwe kwa uhujumu uchumi na utakajishaji fedha.
 
Mzee usafir wa train Kwa mambo hayo tumeshazoea kabisa Kuambiwa hakuna siti na kukuta behewa zipo tupu ni kawaida sana
Wakuu, wiki hii nilifanya safari kwenda Tabora kwa kutumia usafiri wa treni (delux ama wengine huiita express). Nilishangaa kuona mabehewa karibu yote ya daraja la pili yakiwa matupu na baadhi tu yakiwa na abiria wachache mno!! Nikajua labda ni tofauti ya bei, kwani daraja la tatu mpaka Tbr kwa mfano ni tshs 20,000 wakati daraja la pili kukaa ni tshs 25,000. Tofauti ya tshs 5,000 ni kubwa sana kwa maisha ya sasa.

Nikiwa naendelea na safari niliamua kuhamia kwenye mojawapo ya behewa lililokiwa tupu kabisa, nikakaa humo, kufika dodoma waliingia watu kama wanne hivi tukajumuika. Basi alipokuja TT akikagua tiketi, kumbe wale watu waliukwa na tiketi za daraja la tatu, wakatakiwa kuongeza pesa ili wakae humo kihalali. Watu wale walilalama sana kwa sababu kumbe tangu awali walitaka kukata tiketi za daraja la pili lakini waliambiwa treni imejaa, hivyo wakate daraja la tatu kusimama bila siti. Walichukizwa kukuta mabehewa yakiwa tupu huku abiria wengi wakiwa wameahirisha safari kwa kukosa siti. Inasemekana huu ni mchezo wa kila mara.

Tulisafiri mpaka Tabora niliposhuka wala asiongezeke abiria hata mmoja. Nakumbuka Dar kuna behewa liliachwa kwamba ni la abiria wa Dodoma, hivyo tiketi kuwa ngumu kupata, lakini hakukuwa na abiria wowote kwa mabehewa yote manne.

Naomba TRL wawe wazalendo, kwani usafiri huu ni msaada mkubwa kwa watu wenye kipato cha chini na kwa wasafiri wengine wanaopenda kusafiri kwa starehe.View attachment 1242747
 
Hilo ni wazo zuri, ticket zikiisha kila kitu kinakuwa wazi..
Unajua nimesoma hii habari nikagundua kuna watu wana roho katili sana. Wako tayari kufanya hujuma ili tu wanufaike. Jambo jingine la kujiuliza: Kwa nini mabehewa ya daraja la pili yaende matupu na daraja la kwanza wabanane wakati kwa kutumia logic ndogo kabisa uongozi wa shirika ulitakiwa upunguze mabehewa ya daraja la pili na kuongeza ya daraja la tatu? Yes, kama daraja la pili hakuna abiria wa kutosha basi punguza mabehewa na ongeza ya daraja la tatu.
 
Wakuu, wiki hii nilifanya safari kwenda Tabora kwa kutumia usafiri wa treni (delux ama wengine huiita express). Nilishangaa kuona mabehewa karibu yote ya daraja la pili yakiwa matupu na baadhi tu yakiwa na abiria wachache mno!! Nikajua labda ni tofauti ya bei, kwani daraja la tatu mpaka Tbr kwa mfano ni tshs 20,000 wakati daraja la pili kukaa ni tshs 25,000. Tofauti ya tshs 5,000 ni kubwa sana kwa maisha ya sasa.

Nikiwa naendelea na safari niliamua kuhamia kwenye mojawapo ya behewa lililokiwa tupu kabisa, nikakaa humo, kufika dodoma waliingia watu kama wanne hivi tukajumuika. Basi alipokuja TT akikagua tiketi, kumbe wale watu waliukwa na tiketi za daraja la tatu, wakatakiwa kuongeza pesa ili wakae humo kihalali. Watu wale walilalama sana kwa sababu kumbe tangu awali walitaka kukata tiketi za daraja la pili lakini waliambiwa treni imejaa, hivyo wakate daraja la tatu kusimama bila siti. Walichukizwa kukuta mabehewa yakiwa tupu huku abiria wengi wakiwa wameahirisha safari kwa kukosa siti. Inasemekana huu ni mchezo wa kila mara.

Tulisafiri mpaka Tabora niliposhuka wala asiongezeke abiria hata mmoja. Nakumbuka Dar kuna behewa liliachwa kwamba ni la abiria wa Dodoma, hivyo tiketi kuwa ngumu kupata, lakini hakukuwa na abiria wowote kwa mabehewa yote manne.

Naomba TRL wawe wazalendo, kwani usafiri huu ni msaada mkubwa kwa watu wenye kipato cha chini na kwa wasafiri wengine wanaopenda kusafiri kwa starehe.View attachment 1242747
Mkuu, kwa upande mwengine sio kama kuna hujuma hapo kati, kwa sababu c jukumu la wafanyakaz wa shirika kuforce watu wapende treni baada ya kukata tiket. Na nukuu kuwa ticket zilikuwa zimekwisha, yani kwenye vitabu vyao nikiwamabehewa yalikuwa yamejaa na mpunga shirika lishavuta tayari.
 
Sidhani, mabehewa zaidi ya manne wasisafir wote! Pia wale wasafiri walidai tiketi wamekata watu wachache tu wa mwanzo kisha wakatangaziwa kuwa zimekwisha.
 
Hapo kuna hujuma ya uchumi,inatakiwa mkurugenzi wa Trc aswekwe ndani ili akili imkae sawa
 
Dawa yake ni kuweka e ticketing system, mtu anunue ticket kwa mtandao ili wakatisha ticket wakapangiwe kazi nyingine
Hii ni nzuri ila huko vijijini ambako huu usafiri ndio unahitajika sana itabidi wawekewe njia mbadala maana e ticketing system inaweza kuwa ni tatizo zaidi kwao
 
Wacha niuonyeshe ujinga wako. Rais amekuwa akiongoza mapambano dhidi ya wazembe, wavivu, wala rushwa, wahujumu uchumi n.k. Iko wazi wako ambao hawafurahishwi na hatua zinazochukuliwa hivyo kumwona rais kama sio mtu sahihi kukalia kiti cha uongozi.

Wakati wewe una mtazamo wa mkondo mmoja tu (linear thinking) wenye upeo hutazama mambo kwa upana. Kitendo cha kuhujumu idara mbalimbali hakikusudiwi kuhujumu raia ama uchumi kwa ujumla wake, wananchi wanakuwa ni collateral, lakini nyuma yake kunaweza kuwa na political agenda, vita vya madaraka, n.k. Jifunze kufikiri nje ya box.
Acha umandemba.
Basi unajiona mjanjaaa.

Hivi unaishi nchi gani!?
Kuna awamu iliyojaa chuki, unafiki, unyanyasaji, mauaji, visasi, ukosefu wa amani na uovu zaidi ya hii?

Mf:
Vita ya vyeti Bashite hadi leo ni mwana wa mfalme.
Kununua viongozi - mnyeti

Jina lako sawa na pumba zako
 
Hii ni nzuri ila huko vijijini ambako huu usafiri ndio unahitajika sana itabidi wawekewe njia mbadala maana e ticketing system inaweza kuwa ni tatizo zaidi kwao

Kwa mfumo wa simu ya mkononi ni rahisi kuliko manual
 
Back
Top Bottom