Je, Rais anahujumiwa Shirika la Reli?

Je, Rais anahujumiwa Shirika la Reli?

Asante kumbe sio mbaya
Njiani hakuna wizi katika vituo vyao ?
Nilishawahi kusikia kuwa katika treni kuna kunguni ni kweli?
Inayozungumziwa hapa ni treni ya deluxe, sio yale mabehewa ya mkoloni.
pic%2Btreni.jpg
TRL.jpg
 
Watu wale walilalama sana kwa sababu kumbe tangu awali walitaka kukata tiketi za daraja la pili lakini waliambiwa treni imejaa, hivyo wakate daraja la tatu kusimama bila siti. Walichukizwa kukuta mabehewa yakiwa tupu huku abiria wengi wakiwa wameahirisha safari kwa kukosa siti.

]

Hebu nieleweshe taratibu hapa, hivi ni kwamba DARAJA la 3 hakuna siti ni KUSIMAMA..?
 
"..alipokuja TT akikagua tiketi, kumbe wale watu waliukwa na tiketi za daraja la tatu, wakatakiwa kuongeza pesa ili wakae humo kihalali. Watu wale walilalama sana kwa sababu kumbe tangu awali walitaka kukata tiketi za daraja la pili lakini waliambiwa treni imejaa, hivyo wakate daraja la tatu kusimama bila siti..."

Mkuu mleta mada asante kwa kudadavua, hapo nilipokuqute ndipo "uhujumu" ulipo hiyo hela ya kujazia ili ukae daraja husika ndipo upigaji ulipo.....watanzania tu wabadhlifu hadi kwenye DNA!
 
Heri umenena wewe maana tumechoka na kila kitu kumtanguliza Magufuri as if before him no one did anything. Urais ni taasisi siyo mali ya mtu na yeye alichaguliwa humohumo. Nyimbo vulizoimba kuhusu Nyerere zinatosha sasa basi.
Watu wanajitoa ufahamu, utafikiri hilo jina ni cheo.
Ana mamlaka kama raisi ila sio kila kitu ni yeye. Aseme tunahujumiwa wananchi maana sisi ndio tunaumia, walionyimwa na kuminywa haki zetu ndio wanaumia. Sio watu ambao hizi kero wanazisikia na kuambiwa tuu.
Kila mtu ana haki ya kuwa na maoni ila kuna mahali watu wanaitumia hii haki vibaya.
 
Mtazamo wwko, m oppose everything. Wenye ufahamu wameelewa, by the way halikuwa lengo langu kubishana bali kufikisha ujumbe. Unaweza kujadili contents ama kushikilia kubisha kuhusu title, ndio ufahamu wetu ulipoishia.
Andika lugha inayoeleweka.
Nani anabishana na wewe ?
Acha kujistukia.
Unajadili kitu hata hukifahamu, majukumu ya raisi wasome watoto wa primary na secondary leo useme hakuna anayefahamu majukumu ya raisi.
 
Asante kumbe sio mbaya
Njiani hakuna wizi katika vituo vyao ?
Nilishawahi kusikia kuwa katika treni kuna kunguni ni kweli?
Ilikuwa zamani mkuu, siku hizi mambo yameboreshwa. Treni ni safi na wizi sio kama awali. Wahudumu wa mgahawa wanapita kuwa leteeni vyakula kama msafiri hahitaji kwenda restaurant. Pia kuna socket nyingi tu za kuchaji simu ama laptop, hivyo safari haichoshi. Maeneo mengi yana 3G internet. Vyoo ni visafi na vina maji. Kifupi treni ya Delux wameiboresha sana.
 
Safi sana.

Tanzania ya sasa ujinga mtupu.

Rais amegeuka Mungu au Yesu Kristo.

Pambaf kabisa.
Ujinga mzigo. Kama hujui ni kwa jinsi gani rais anaweza kuhujumiwa sina cha kukusaidia. Endelea na siasa zako za bendera fuata upepo. Mimi siongelei siasa hapa, naongelea uhalisia. Mengine nawaachieni wanasiasa
 
Vipi mkuu wakati wa kukata tiketi hawakukuomba kitambulisho pamoja na barua kutoka serikali ya mtaa?
Kuna ujinga mwingi sana unaofanywa kwenye hii treni ya delux,
Hujuma nyingine kwenye treni hii ni kuondoa route ya Dar - Mwanza kwa madai kua hamna abiria wa kutosha.
Management nzima ya TRL inapaswa iwajibishe na ikiwezekana wafungulie kesi ya uhujumu uchumi kwa mambo wanayoyafanya.
Mkuu, nilitumia kitambulisho, ila nilishuhudia wasio na vitambulisho wakirudishwa wakatafute barua za serikali za mtaa.
 
Hebu nieleweshe taratibu hapa, hivi ni kwamba DARAJA la 3 hakuna siti ni KUSIMAMA..?
Mkuu kuna mambo ya ajabu, daraja la tatu wanakata tiketi bila kujali idadi. Ukipata siti shukuru, ila siti zikiisha wanaendelea kukata ivyo hivyo bila kuandika siti no. Hawa wanakaa makoridoni na kufanya msongamano mkubwa.

Malalamiko niliyoyasikia mimi ni kwa abiria kwamba wanaambiwa daraja la pili limejaa hivyo wanalazimika kukata tiketi za daraja la tatu bila siti. Wakiwa ndani ya treni wanashangaa mabehewa yako tupu, ila wanatakiwa waongeze nauli ifikie ya daraja la pili, wanapewa namna ya risiti kisha wanaruhusiwa kusafiri kwenye daraja hilo. Sasa sijui kama hizo genuine kwa sababu zinaandikwa wa mkono.
 
Shirika la reli ndio shirika pekee limebaki linafanya kazi ki-analojia. Mimi ningeshauri waweke an online bookings na kukata tickets ili halafu anachagua siti na kulipia moja kwa moja. Haya ya kwenda kukaa kwenye mstari mara siti zimeisha ,naona ni ngumu.Wale wanaouza ticket wanafanya mambo awe magumu sana . Sidhani kama hata management inaweza kujua ni tickets ngapi zimeuza na zipi zimebaki. Hiyo system iwe na system ya report kwa manager kuona level ya mauzo. Maana sidhana kwa mfumo wa sasa kama kuna njia ya kuangalia faster kama imejaa au la.
Last hii nchi ni yetu ,ndio tutakaoijenga ,usitegemee wageni kuna mwingine atakuja kuiendeleza tofauri na wewe ulieajairiwa. So tufanye kazi kama tunafanya yetu. Serekali nayo ijaribu kuwawekea motisha kwa kiasi fulani especially wale wanaofanya kazi kwa kujituma
 
"..alipokuja TT akikagua tiketi, kumbe wale watu waliukwa na tiketi za daraja la tatu, wakatakiwa kuongeza pesa ili wakae humo kihalali. Watu wale walilalama sana kwa sababu kumbe tangu awali walitaka kukata tiketi za daraja la pili lakini waliambiwa treni imejaa, hivyo wakate daraja la tatu kusimama bila siti..."

Mkuu mleta mada asante kwa kudadavua, hapo nilipokuqute ndipo "uhujumu" ulipo hiyo hela ya kujazia ili ukae daraja husika ndipo upigaji ulipo.....watanzania tu wabadhlifu hadi kwenye DNA!
Inawszekana mkuu, wanapewa risiti (tiketi) za kuandikwa kwa mkono hapo hapo ndani.
 
Watu wanajitoa ufahamu, utafikiri hilo jina ni cheo.
Ana mamlaka kama raisi ila sio kila kitu ni yeye. Aseme tunahujumiwa wananchi maana sisi ndio tunaumia, walionyimwa na kuminywa haki zetu ndio wanaumia. Sio watu ambao hizi kero wanazisikia na kuambiwa tuu.
Kila mtu ana haki ya kuwa na maoni ila kuna mahali watu wanaitumia hii haki vibaya.
Siwezi kusema hivyo, ila wewe pia una huo uhuru. Chuki zako usilete hapa
 
Nilienda mbeya pale kutaka kupakiza mzigo wa tani mbili kutoka Mbeya kuja Dar kwa treni. Naambiwa tani moja ni Tsh 220,000, laki mbili na ishirini. Ina maana tani mbili nitatakiwa kulipia shillingi laki nne na arobaini.

Wakati katika gari kubwa ya mzigo tani moja ni kuanzia elfu sabini hadi laki. Nikajua ni kwann watu hawatumii usafiri wa reli kuzafirishia ambao ndio ulitakiwa kuwa cheap kuliko usafiri wowote wa mizigo.

Sasa natamani kulifikisha hili swala wizarani tupatiwe ufumbuzi.
 
Dawa yake ni kuweka e ticketing system, mtu anunue ticket kwa mtandao ili wakatisha ticket wakapangiwe kazi nyingine
Hivi kwann serikali haitoi fursa kama hizi kwa makampuni binafsi yajiwekeze ili tushare keki ya taifa.
 
Back
Top Bottom