Je, Prof. Kabudi amewajibu Wazungu kwa niaba ya Watanzania ama CCM?

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
4,553
2,000
Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kiamataifa, Prof. Kabudi aliongea na vyombo vya habari kuhusu Tanzania kujadiliwa na Kamati ya Bunge la Ulaya kuhusu kuminywa kwa demokrasia na matumizi ya pesa kutoka Jumuiya ya Ulaya kwa ajili ya virus vya korona.

Prof. Kabudi alitamba kuwa Tanzania ni nchi huru. Asichokijua Prof. Kabudi ni kuwa duniani kote hakuna nchi yenye uhuru wa kuua watu wake huku Jumuiya ya Kimataifa ikiangalia. Hakuna uhuru wa aina hiyo asilani. Katika ngazi ya familia, pia iko hivyo. Hakuna baba anayeweza kuua watoto wake huku akidai kuwa familia yake iko huru. Prof Kabudi aelewe kuwa baba anayeua watoto wake, anatenda kosa la mauaji kwa mujibu wa sheria za nchi. Nchi inayokandamiza watu wake na kuua inafanya kosa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Prof Kabudi, macho yakiwa kodo, alitamba kuwa “Watanzania” wanathamini sana utu na uhuru wao na hawatatishwa kwa vile hawajawahi kushindwa vita. Swali langu ni kuwa ni “Watanzania” wapi wanaoongelewa hapa? Je, anawazungumzia Watanzania wa kweli waliojitokeza kupiga kura zao tarehe 28 Okt 2020 ama kile kikundi cha mafia kilicho chafua uchaguzi huo kwa makusudi?

Je, ni kweli kuwa Watanzania wanaunga mkono kuporwa haki yao ya kuchagua viongozi wanao wataka? Ni kweli kuwa Watanzania milioni 60 walifurahia kitendo cha wagombea wa upinzani kuporwa fomu na kukamatwa na vyombo vya dola ili wagombea wa CCM akiwemo Kabudi, wapiti bila kupingwa? Je, ni kweli Watanzania walipenda uchaguzi uamuliwe na wapigakura wale wa tarehe 27 Okt 2020 kule Zanzibar? Je, ni kweli Watanzania milioni 60 walipenda mawakala wa vyama vya upinzani kufukuzwa katika vituo? Je, ni kweli kuwa Watanzania walifurahia kitendo cha kura kupigwa nyumbani na mahotelini na baadae kupenyezwa katika vituo zikiwa ziemebebwa kwenye mabegi na vikapu? Hawa “Watanzania” anaowaongelea Kabudi ni wapi.

Prof. Kabudi amejazwa kiburi na JWTZ, polisi na TISS kiasi cha kuona kuwa ni sawa kwa kikundi kidogo cha kimafia cha CCM kuamua matokeo ya uchaguzi kwa manufaa yao na kusema “Watanzania” wameamua. Na kwamba Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa wanatakiwa kutabasamu tu kana kwamba hakuna kitu kimetokea!

Prof. Kabudi ajue kuwa Watanzania wa kweli tunaililia haki yetu ya kuchagua viongozi tunaowataka wenyewe kupitia sanduku la kura. Kabudi asichanganye CCM na Watanzania. CCM ni kundi dogo sana miongoni mwa Watanzania milioni 60 ila tu lina majeshi yenye silaha za moto. Kama vikwazo vitaleta haki ya Watanzania milioni 60 kupiga kura na kuchagua viongozi wanao wataka bila ya kuamualia na jeshi, polisi, TISS, NECCM, Msajili wa Vyama, nk, na vije. Tunavisubiri kwa hamu kubwa.

Kweli huu ndio utu wa Mtanzania anaongelea Prof. Kabudi na kutoa macho kiasi kile huku akinyeshea microphone na mvua ya mate vile? Kwa hakika huu siyo utu wa Mtanzania. Ni utu wa CCM:

1606069474327.png

1606069550707.png
 
Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,600
2,000
Mebeberu yanastahili kujibiwa vile, yasitake kutupangia. Tz ni nchi huru, hatutalamba miguu ya wazungu, nimependa majibu murua kabisa kutoka kwa Prof Kabudi. Sasa hivi yamepoa kama maji ya kwenye mtungi, chezea tz tuna msimamo tangu enzi za Hayati Mwl. Nyerere. Mabeberu ukiwalegezea watatuchezea wanavyotaka.
 
Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
4,553
2,000
Watanzania wa kweli wamenyimwa haki yao ya kuchagua viongozi kwa njia za kikatiba. Wasilaumiwe kwa kuitafuta kwa njia ambazo ziko nje ya katiba.

Hakuna aliyenyimwa hiyo unayodai ni haki ya kikatiba. Mbona kule Nkasi wameshinda, Mtwara vijijini wameshinda. Upinzani wenyewe umeshajifia kitambo tu.
 
mchichapori

JF-Expert Member
Aug 5, 2017
744
1,000
Mebeberu yanastahili kujibiwa vile, yasitake kutupangia. Tz ni nchi huru, hatutalamba miguu ya wazungu, nimependa majibu murua kabisa kutoka kwa Prof Kabudi. Sasa hivi yamepoa kama maji ya kwenye mtungi, chezea tz tuna msimamo tangu enzi za Hayati Mwl. Nyerere. Mabeberu ukiwalegezea watatuchezea wanavyotaka.
Kuna kiongozi Africa alikuwa anawatukana whites kama Gaddafi? sasa yupo wapi? wananchi wa Libya wana hali gani? hivi Tanzania inaifikia nini Libya kwa wakati ule?
Acha kutumia makalio kufikiri.
 
Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,745
2,000
Hahaha lile ni tatizo la ccm sio la Tanzania, yote anayojibu ni majibu ya ccm, lakini ukimsikiliza analazimisha liwe tatizo letu watanzania.

Wao ndio waliiba kura, wao ndio wametwaa madaraka kwa nguvu, wao ndio wanashutumiwa, sio wananchi wala sio watanzania.

Hitimisho, hili ni tatizo lao ccm hivyo anaongea kwa niaba ya ccm.
 
IPECACUANHA

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
3,144
2,000
Mebeberu yanastahili kujibiwa vile, yasitake kutupangia. Tz ni nchi huru, hatutalamba miguu ya wazungu, nimependa majibu murua kabisa kutoka kwa Prof Kabudi. Sasa hivi yamepoa kama maji ya kwenye mtungi, chezea tz tuna msimamo tangu enzi za Hayati Mwl. Nyerere. Mabeberu ukiwalegezea watatuchezea wanavyotaka.
Unawatendea watu wako "uhuni" kwa kuiba haki yao ya kuchagua viongozi halafu unawaita wanaohoji vitendo vyako visivyo vya kistaarabu wahuni. Ajabu la kiwango cha STANDARD GARGE RAILWAY
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,419
2,000
Mebeberu yanastahili kujibiwa vile, yasitake kutupangia. Tz ni nchi huru, hatutalamba miguu ya wazungu, nimependa majibu murua kabisa kutoka kwa Prof Kabudi. Sasa hivi yamepoa kama maji ya kwenye mtungi, chezea tz tuna msimamo tangu enzi za Hayati Mwl. Nyerere. Mabeberu ukiwalegezea watatuchezea wanavyotaka.
Uliwahi kuwalegezea mabeberu wakakuchezea mgongoni nini? Hauta wasahau maishani mwako.
 
elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,419
2,000
Kauli za Kabudi hazina tofauti na za Sirro akiwabeza watanzania wasio wanaccm, wanaccm wanajiona kuwa wao ndiyo wenye nchi nz hii inatokana na viongozi wao kusema ukimpiga mwanaccm aliyevaa sare utakiona chamoto! Naye huwabagua wasio wanaccm.
 
Bayyo

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,600
2,000
Mnaweza wadanganya Wazungu ambao mliwanyima kibali cha kuleta waangalizi hapa ili wizi wenu usishuhudiwe lakini Watanzania tuliona kila kitu. Kubishana na wewe ni kupoteza muda wangu.
Kw hiyo unawaamini hao wazungu kuliko mawakala wenu, kipindi kingine wawekeni hao wazungu wenu wawe mawakala kabisa, kumbe ndo maana mnawalamba miguu!
 
goodluck5

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
4,423
2,000
Kabudi mwenyewe alipita bila "kupingwa"...unategemea atasema nn juu ya uchaguzi wa juzi?!.

ni miongoni mwa wanufaika wa kubwa wa uchafuzi wa majuzi.

ikiwa vikwazo vitaleta haki, na vije tu hakuna namna!.
 
mwekundu

JF-Expert Member
Mar 4, 2013
21,850
2,000
Pale hatujawakilishwa kabisa,Nina wasiwasi ni mawazo yake binafsi hata boss wake hajamuwakilisha
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom