Je, Ofisi ya Taifa ya Takwimu ina wajibu wa Kutoa Tamko kuhusu Usambazaji wa Takwimu zilizo bandikwa mitandaoni?

SYLLOGIST!

JF-Expert Member
Dec 28, 2007
7,101
6,708
Wakuu, Wahusika,
Ni matumaini yangu mmejaa rehema na amani Asubuhi hii katika kukabiliana na majukumu yenu. Nawaombeni muda wenu mchache kutathmini Uzi huu ili kuweza kulinusuru Taifa.

Mada: Katika kile nilchokiona kamaa ni ukiukwaji wa Sheria ya Takwimu, Statistics Act (revised 2019) Sehemu ya 26(2)(3) sehemu ndogo C inayompa/enye matakwa ya kuwa msambazaji wa Takwimu kuhakikisha anatoa takwimu hizo kwa Usawa na kutopendelea katika, kuripoti, kuwakilisha, na kusambaza matokeo ya Taarifa za Takwimu.

Siku ya Jumatano tarehe 22/2/2023 mnamo saa kumi na moja Jioni jamvini, mwanahudhuri mmoja ali bandika uzi unaodai "Hivi ndivyo Hayati Magufuli aliharibu uchumi wa Tanzania. Takwimu hazidanganyi"

Katika maudhui yake ambayo inaweza kutafsiriwa kuwa ilijengwa kuchafua Serikali ya Tanzania ya Awamu ya Hayati Raisi John Pombe Magufuli ambamo amedai ushahidi wake amedadavua kutokana na Taarifa zilizochapishwa katika jarida linaloitwa Tanzania Business Insight ambayo 'ilinukuu' taarifa za Benki Kuu Tanzania(BOT) na Ofisi ya Takwimu Tanzania. NBS au National Bureau of Statistics.

Alidai, Takwimu hizo zinabainisha awamu za mwanzo za marais wa tatu kati ya 1995 mpaka 2015. Tanzania na kuonyesha Uchumi 'uliharibiwa' na Hayati Rais J.P Magufuli... kwa maoni yangu hii ni slandering!

Walakin, kwa kile alichokiita "Majigambo" ya Serikali iliyoongozwa na Hayati Raisi na kubaini yanayodhihirisha kuwa ni upotoshaji wa Umma na Wananchi wa Tanzania na Dunia kwa Ujumla kuwa Serikali ilitunga sheria za Kidikteta ambazo zilileta changamoto kwa yeyote yule anayetaka Ku Challenge Taarifa ambazo anadai(mwanahudhuri) ni za kupikwa na Uongo, kitendo ambacho nimekiona kana Upotoshaji kana hizo taarifa ambazo zilinukuliwa BOT na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuwa zilipikwa na za uongo na ndio kulipeleka Serikali kutunga sheria kuficha uovu.... yaani takwimu za uongo na za kupika kwa kile nilichokiona ni kuwa ni ukiukwaji wa sehemu ya 26(2)(3) sehemu ndogo C. ya Sheria ya Takwimu(2019) na kuichafua Serikali.

Wakuu/Wahusika,

Sheria ya Takwimu inatoa na kuwapa Wajibu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Licha kuwapa majukumu mengine, pia inawapa haki ya kupinga matumizi mabaya au tafsiri potofu ya taarifa za takwimu zinazosambazwa na mtu yeyote (hapa ni mwanhudhuri mwenzetu)ikiwa maelezo hayo ya takwimu yana makosa ya msingi au hayafuati kanuni zilizoainishwa chini ya sehemu 26(3).C

Kwa hayo, Wakuu/Wahusika utaona kuwa memba mwenzetu amekiuka siyo miongozo ya Jamvi bali hata Sheria za Nchi kwa kusambaza Matokeo ya Taarifa zilizojaa upotoshaji na za upendeleo wa Serikali na Rais aliyoko madarakani sasa. Kimsingi tafsiri potofu ya Matokeo ya Takwimu hizo.

Nawasilisha

Je, kulingana na Ukiukwaji wa sehemu ya 26(3).C pamoja na wajibu wa Idara na kifungu cha 27(1) na 27(2).b Ofisi ya Taifa ya Takwimu ina jukumu la kulitolea tamko Uzi huo? au Litoe mwongozo?
 
Ofisi ya Takwimu ya Taifa ina mambo mengi muhimu zaidi ya kufanya kuliko kujibu malumbano ya mtandaoni. Huu uzi wako hapa ni uchafu mtupu unaosukumwa na hulka za kidikteta za kupenda kufunga watu midomo au kutaka waseme yale unayopendea kusikia tu.
 
Usiipe NBS majukumu ya kijinga kama DIKTETA alivyo badili Sheria ya Takwimu kubariki uhayawani wake. Wala huhitaji NBS ndiyo ikuambie uchumi uliporomoka kiasi gani. Kama una afya nzuri ya akili angalia yafuatayo:-

1. Biashara ya Korosho Lindi na Mtwara ilivurugwa
2. Kumfilisi Yusuf Manji kuliathiri biashara ya ufuta na mbaazi
3. Alifunga mipaka tusiuze mahindi, mchele na maharage nje ya Tanzania
4. Biashara ya mbao na wanyama hai ilipigwa marufuku
5. Wafanyabiashara wa Kichina waliondoka Kariakoo na kuhamia Zambia na nchi zingine jirani
6. Hatukupata mitaji mingine (Foreign Direct Investments) kama ile ya DANGOTE Cement, baada ya DANGOTE kuwa harassed
7. Wawekezaji walisumbiliwa sana kwa kutupwa ndani kwa madai ya Kodi hewa walizokwepa kama Halotel, Vodacom etc
8. Mgogoro na Kenya ambaye ndiye ana makampuni mengi yaliyowekeza nchini
9. Kufungwa kwa mabenki mengi kama M- Bank, TwigaBancop, Tanzania Women Bank etc
10. Kunyang'anya fedha za wafanyabiashara kupitia Task forcce
 
Unasomeka, ila haukujibu hoja. Huu uzi hauna uchafu wowote zaidi ya kutaka kubaini kama sheria zimekiukwa au lah.

Siwezi kupenda upotoshaji wa aina yeyote ule, hususani unaoenda Kuishambulia au kulenga Serikali ya Jamhuri ya Muingano wa Tanzania .
 
Acha Watu Wateme Nyongo Zama Za Uwimbombo Na Ulindi (Kupekecha Moto Kwenye Gogo) Zimepitwa
Hakuna tabu kutapika nyongo, kwani ni afya.

Walakin unakuja pale nyongo hizo zilizojaa upotoshaji na visasi kutuondoa kujadiliana yale yenye mustakabhali wa nchi kama mada inavyouliza.

Nina Uhakika hao unaodai ni 'watema nyongo' ni wale wanaotaka Katiba Mpya, na kama ulivyosoma nimetaka mwongozo au tamko kutoka chombo kilicho na(katiba yake) majukumu kisheria kuchakata, kuratibu, n.k yale yanayohusiana na Takwimu za Nchi ikiwa na pamoja na zile Uchumi kama zilivyoletwa hapa na mwanahudhuri wa jamvi hili.

Kwa wale wanaodai tuwe na 'Taasisi zenye kufanya kazi kwa weledi, Taasisi zinazosimama zenyewe, basi itakuwa vizuri kutizama hoja, na kama hoja inasimama basi wawe na wajibu wa kuchagiza Taasisi tajwa ili kupata mwongozo au litolee tamko, badala ya kutupiana nyongo/vijembe.

Karibu
 
Usiipe NBS majukumu ya kijinga kama DIKTETA alivyo badili Sheria ya Takwimu kubariki uhayawani wake.

HuiHui tu, Sina uwezo kuipa NBS majukumu yaliyoainishwa kisheria na Sheria ya Takwimu 2019 ila kama Mwananchi niliyeipa Serikali na Taasisi zake dhamana, ni wajibu wangu kama raia wa nchi hii kuitii katiba na sheria za nchi. Hivyo basi siwezi kuitelekeza wajibu wangu alimradi ametokea mtu au watu au makundi kushindwa kuipa sheria ya nchi kipaumbele stahiki.
Wala huhitaji NBS ndiyo ikuambie uchumi uliporomoka kiasi gani.
Ni kweli, sihitaji iniambie uchumi ukoje. Vipimo vipo vingi visivyohitaji takwimu, lakini hapa, mwanahudhuri huyo au uzi huo niliozungumzia ulielekea kupotosha, kudhihaki na hata kukiuka kanuni/sheria za utoaji na usambazaji wa Takwimu
Kama una afya nzuri ya akili angalia yafuatayo:-
1. Biashara ya Korosho Lindi na Mtwara ilivurugwa...
Huihui, nikiri mengi hapo uliyoorodhesha mengi nimeyasikia aidha kutoka kwako , na kwingineko hatahivyo siwezi nikajadili hayo kwani nitakuwa natoka nje ya mada. Naamini wapo ambao watayachukua hayo na kuyafanyia kazi.

Nikuulize tu kama ulisoma uzi tajwa? na una maoni kuhusu hoja zangu kuhusiana nao....Je Ofisi ya Taifa ya Takwimu ina wajibu wa Kutoa tamko au mwongozo kuhusiana na ukiukwaji wa sheria ya nchi?
 
Wakomunisti ndio huwa wana tabia za kupekua pekua na kufanya patrols za vitu vinavyoitwa upotoshaji na uchochozi. Huu ni mfumo mbaya sana wa kuwatisha wakosoaji na watu wenye mawazo mbadala.

Ni ujima na udikteta wa hali ya juu kufikiria serikali na watawala pekee ndio chanzo cha taarifa sahihi na haiwezu kudanganya, kufanya propoganda au kupika taarifa.

Unasomeka, ila haukujibu hoja. Huu uzi hauna uchafu wowote zaidi ya kutaka kubaini kama sheria zimekiukwa au lah.

Siwezi kupenda upotoshaji wa aina yeyote ule, hususani unaoenda Kuishambulia au kulenga Serikali ya Jamhuri ya Muingano wa Tanzania .
 
Wewe ni msumbufu tu kwa sababu legacy imepopolewa. Katika karne hii haiwezekani tena kuwaweka watu wote kwenye chungu kimoja wasubirie taarifa kutoka kwa watawala tu, hizo zama zilishapitwa na wakati.
Hakuna tabu kutapika nyongo, kwani ni afya.

Walakin unakuja pale nyongo hizo zilizojaa upotoshaji na visasi kutuondoa kujadiliana yale yenye mustakabhali wa nchi kama mada inavyouliza...
 
Ukiona kimya hakuna fafanuzi elewa ngoma ina ukwel!! Kwahiyo vumilia tu hakuna namna.
Kama kutakuwa hakuna Tamko sawa, lakini watoe mwongozo hata katika majamvi kuhusiana na utii wa sheria za Nchi katika masuala kama hayo yakijitokeza. Tusiipe mwanya utofauti wetu kuharibu mustakabhali moana wa Nchi yetu.

Nadhani kwa nyakati hizi za vidubwasha vya (akil bandiya) itakuwa ni sahihi kwa NBS kutolea ufafanuzi,au kutoa tamko n.k ili kuondoa sintofahamu katika taarifa za baade. Ni naamini aliyeleta uzi ule ana malengo yake, naomba tu isije ikawa ni kuilisha akil bandiya ili ziweze...."kutapika nyongo" baadae.

Asante kwa uangalizi
 
Wakuu, Wahusika,
Ni matumaini yangu mmejaa rehema na amani Asubuhi hii katika kukabiliana na majukumu yenu. Nawaombeni mda wenu mchache kutathmini Uzi huu ili kuweza kulinusuru Taifa...
Ile Sheria Haina tofauti na Sheria ya kuminya mitandao,ni Kati ya Sheria za hovyo za Mwendazake na bahati nzuri ilishakuwa ignored..

Mwisho kwamba hutaki watu walinganishe au? Mapovu kawatolee The Business Insight..

On top of that Jana Mbowe akiwa Sumbawanga amesema Mwendawazimu mmja alitokea from no where na kuzuia Mikutano akaleta laana Juu Nchi na Mungu akaamua 😜😜😜😜
 
Ile Sheria Haina tofauti na Sheria ya kuminya mitandao,ni Kati ya Sheria za hovyo za Mwendazake na bahati nzuri ilishakuwa ignored..
Hayo ndio nimesikia hapa, kwamba sheria niliyonukuu na kutungwa na Bunge la Jamhuri wa Muungano lishatelekezwa.
Mwisho kwamba hutaki watu walinganishe au? Mapovu kawatolee The Business Insight..

Fanya ulinganishi wako vyovyote inavyokufaa, weka takwimu zezote kwa namna inayokufaa, Fuata taratibu, kanuni na Sheria za Nchi. Tanzania ni Nchi inayoongozwa na Sheria....huwezi kudai sheria zilikiukwa na hivyo basi na wewe ukiuke sheria. No two wrongs make a right.Ulis
On top of that Jana Mbowe akiwa Sumbawanga amesema Mwendawazimu mmja alitokea from no where na kuzuia Mikutano akaleta laana Juu Nchi na Mungu akaamua 😜😜😜😜
Hicho ulichowasilisha hapo juu haijalishi na ndio nilicho jengea hoja, kuwa, umetafsiri takwimu without objectivity, umetafsiri matoke yale with malice towards the Government of Tanzania. We kisasi binafsi sawa, unaeleweka lakini usiweke Takwimu na nyongo pamoja.
Usipotoshe.

Usijali, nimewasilisha tunasubiri ya NBS.
 
Zikiwa za kusifia zinafaa ila kinzani zinavunja Sheria si ndio? 😜😜😜😜

Hayo ni yako, Sheria iko wazi na yale yaliyoainishwa katika sheria hizo, kulingana na ulivyowasilisha uzi ule ni dhahiri kuna ukiukwaji wa sehemu za Sheria ya Takwimu na mtazamo.

Ninacho kitafuta ni Serikali kutoa Tamko kama ulikiuka au la na vilevile itoe mwongozo kuhusiana na uwasilishaji wa taarifa kama zile ulizowasilisha. Hakika umefuata kanuni nyingi za kiuandishi lakini unakinzana na matakwa yake ikiwa na pamoja na kuondoa bias.

Ile ni Sheria ya hovyo iko mbioni kufutwa ndio ilisababisha serikali kunyomwa mabilioni na imf
Naheshimu maoni yako Ni haki yako kuwa na maoni, hatahivyo haibadilishi kuwa umekiuka kipengele cha Usambazaji na uwasilishaji wa taarifa za matokeo ya Takwimu.

Binafsi sioni u Hovyo wake kwani ikinibidi nitoe taarifa zezote ni tatafuta mwongozo kutoka NBS na sio kujibwatukia tu.
 
Kati ya mambo maovu yanayorudisha maendeleo katika nchi nyingi za Africa ni "WEAPONIZATION OF LAW".

That statement is False!

Clearly the reversal is the truth. That Europeans and its Sister States have weaponised the laws to advance there own agendas and therefore hinder progress being made by African Countries.

Yoda, I would love if you could open a thread to discuss just that. What a psycho-babble!

...ni kawaida pale mnapoona hoja zimesimama no mkaanzisha mjadala mwingine ndani just to deflect on the pending arguments.
 
Ofisi ya Takwimu kila mwezi wakati wa Mwendakuzimu ilikuwa inaripoti kuwa mfumuko wa bei kushuka na kupaa kwa uchumi kufikia takriban 9.5% kumfurahisha Magu
Kitu ambacho kilipingwa na taasisi zote za kifedha na uchumi kimataifa
Nilihoji hapa kwa taarifa zao za kupungua mfumuko kuna siku watadai Tanzania hakuna mfumuko kabisa.
Ndio hao unataka ufafanuzi kwao?
 
Nadhan unajua fika kuhusu tawala zetu kuhusu kusema ukwel au kutoa matamko. Hata kipind cha nyuma kitu ukwel hakikutakiwa kbs even vyombo vya hbr ilikua marufuku kutoa hbr ambayo ni sahihi kwa upande Taifa lkn kwa upande wa utawala hakikutakiwa kujulikana!! Huu ndio utawala wetu.
Kama kutakuwa hakuna Tamko sawa, lakini watoe mwongozo hata katika majamvi kuhusiana na utii wa sheria za Nchi katika masuala kama hayo yakijitokeza. Tusiipe mwanya utofauti wetu kuharibu mustakabhali moana wa Nchi yetu.

Nadhani kwa nyakati hizi za vidubwasha vya (akil bandiya) itakuwa ni sahihi kwa NBS kutolea ufafanuzi,au kutoa tamko n.k ili kuondoa sintofahamu katika taarifa za baade. Ni naamini aliyeleta uzi ule ana malengo yake, naomba tu isije ikawa ni kuilisha akil bandiya ili ziweze...."kutapika nyongo" baadae.

Asante kwa uangalizi
 
Usiipe NBS majukumu ya kijinga kama DIKTETA alivyo badili Sheria ya Takwimu kubariki uhayawani wake. Wala huhitaji NBS ndiyo ikuambie uchumi uliporomoka kiasi gani. Kama una afya nzuri ya akili angalia yafuatayo:-

1. Biashara ya Korosho Lindi na Mtwara ilivurugwa
2. Kumfilisi Yusuf Manji kuliathiri biashara ya ufuta na mbaazi
3. Alifunga mipaka tusiuze mahindi, mchele na maharage nje ya Tanzania
4. Biashara ya mbao na wanyama hai ilipigwa marufuku
5. Wafanyabiashara wa Kichina waliondoka Kariakoo na kuhamia Zambia na nchi zingine jirani
6. Hatukupata mitaji mingine (Foreign Direct Investments) kama ile ya DANGOTE Cement, baada ya DANGOTE kuwa harassed
7. Wawekezaji walisumbiliwa sana kwa kutupwa ndani kwa madai ya Kodi hewa walizokwepa kama Halotel, Vodacom etc
8. Mgogoro na Kenya ambaye ndiye ana makampuni mengi yaliyowekeza nchini
9. Kufungwa kwa mabenki mengi kama M- Bank, TwigaBancop, Tanzania Women Bank etc
10. Kunyang'anya fedha za wafanyabiashara kupitia Task forcce
11. Kunyanganya watu mashamba yao na viwanda
 
Back
Top Bottom